Makala na Yaliyochaguliwa

Miji mikuu, mipaka na ujenzi wa taifa

Mokhtar-300x198

Uhusiano kati ya miji mikuu na mipaka yake ni uhusiano wa kukamilishani na si wa kugombana na wala haitakikani iwe hivyo, kwa kuwa hakuna taifa lolote ambalo linaweza kujitosheleza kufanya kuwa mji mkuu ndio kitovu na kusahau pande nyengine za taifa kwani bila ya mipaka taifa haliwezi kusonga, isipokuwa tu mataifa mengi huifanya miji mikuu kuwa ni kituo kikubwa walichokipa kipaumbele na mifano ya kihistoria inaweka wazi ushahidi wa jambo hili. Isipokuwa kuna tafauti kati ya mataifa yaliyoendelea na mataifa yasiyoendelea katika kutoa umuhimu wa miji mikuu. Mataifa yaliyoendelea haiwezekani kuzembea hata kidogo kuhusu hata kipande cha ardhi, jengo au sehemu na kuiacha ikiharibika au kufanyia uharibifu au hata fikira tu za kutaka kujitenga (kama ni maeneo). Mshairi mmoja alikwenda kwa Umar bin Abdul Aziz (Mungu amwie radhi) akamsomea shairi akasema: Iwapo unahifadhi unaowamiliki basi elewa Wafanyakazi wa ardhi yako ni mbwa mwitu Hawajaitikia wito wako uliowaita Mpaka wapigwe viboko na kukatwa shingo Na kwa kuwa ukuaji wa maeneo na sehemu za mipakani si jukumu la serikali pekee au viongozi wa kisiasa, kwani hifadhi na umuhimu pamoja na kazi za ukuzaji ni jukumu linalokusanya taasisi zote za nchi, sawa na iwe taasisi rasmi au mashirika ya kijamii, wafanyabiashara, watega uchumi, sekta za elimu, sekta za afya, za ujenzi, za tamaduni, wizara ya wakfu, na wizara nyengine na mashirika pia, pamoja na jumuiya za huduma za kijamii. 2 Wote hawa inabidi watilie umuhimu mkubwa na hasa maeneo ya mipaka. Na walipe kipaumbele na kuona kuwa ni suala linalohusu usalama wa taifa kwa upande mmoja na la ukuzaji kwa upande wa mwengine. Na inatakikana sote kwa pamoja tuyageuze maeneo ya mipakani iwe ni maeneo ya kuvutia na si ya kukimbiwa. Na inapotokezea taifa kutojali maeneo haya basi huwa ni nafasi kwa makundi kufika katika maeneo haya na kufanya kambi zao na kusababisha msongamano usio wa kawaida kwa vituo vya huduma za kijamii na kupatikana uwepo wa ujenzi wa kiholela, na hata kusababisha kukuwepo kwa maisha ya kitabaka, maradhi na matatizo mengine ya kijamii ambayo yatahitaji udhibiti usio wa kawaida ili kuyatatua. Ama kwa upande wa taifa kujali na kutoa umuhimu wa maeneo haya ya mipakani kwa upande wa vitega uchumi, ni kule kuweka huduma za lazima kwa wananchi wake: makazi, afya, elimu, utamaduni, na huduma nyenginezo ambazo zinahitajika kuendeleza maisha katika ardhi yao. Pamoja na kuwepo kwa nafasi za kazi na uzalishaji. Hayo yote yatapelekea kwa wananchi kuipenda ardhi yao (taifa lao) na kuhifadhi chembe ndogo ya mchanga ili isipotee pamoja na kuwafanya wawe wazalendo. Na panapokuwepo kwa vivutio na ushajiishaji wa kazi katika maeneo haya na kuwepo kwa vitega uchumi madhubuti kama nchi inayotilia mkazo ilivyo hivi sasa katika maeneo ya Sinai, Matruh na Ismailia mpya, Halayib, Shalatin na Wadi Jadid, na maeneo mengine kama yale ya jangwani. Maeneo haya karibuni yatabadilika na kuwa ya kuvutia. Kitu ambacho kitapelekea kuwepo kwa ugawaji sawa wa kijiografia, kimakazi na pia utawezesha kuwepo kwa maisha mazuri kwa wananchi wa maeneo hayo. Na kupunguza msongamano wa utoaji wa huduma kwa wakazi wa maeneo hayo, au kupatikana huduma kama zile zipatikanazo katika miji sawa huduma za kisiasa au za kiuchumi. Na kuwepo kwa vivutiaji vitakavyowezesha kuvutia watalii na kuushangaza ulimwengu na kuonyesha ukubwa na upevu wa wanachi wa ukuaji wao.

Kisa cha masanamu na ubomoaji wa ustaarabu

Mokhtar-300x198

Kwa kuanzia, hakuna muisilamu duniani mwenye kuabudu sanamu. Au hata kuamini jambo hilo pia hata kulingani kuabudiwa au kufikiria tu jambo hilo, si muisilamu tu mwenye kuamini hivi lakini pia hata wale wa dini zilizoteremshwa. Na iwapo uisilamu umekataza kutengeneza masanamu mwanzoni mwa uisilamu basi hili lilikuwa kwa sababu mbili; Ya kwanza. Watu walikuwa bado ni wapya katika uisilamu na walikuwa wameacha kuabudu masanamu kwa muda mchache (tangu kuingia kwao katika uisilamu) kwa kudhania kuwa yanawaweka karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu. Kama iliyoeleza kurani tukufu kwa ndimi zao pale Mwenyezi Mungu aliposema { Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu }. Sababu ya pili:Iwapo masanamu haya hutengenezwa kwa ajili ya kuabudiwa au kutengenezwa kwake ni kwa ajili ya kumfananisha na Mwenyezi Mungu. Na kati ya yenye kuthibitisha hayo na kuwa tukiachilia mbali kuondosha masanamu yaliyokuwa yakiabudiwa ndani ya Alkaaba kwa ajili ya kuisafisha haikuthibiti kuwa kuna sahaba yeyote aliyevunja sanamu au athari yoyote ile ya sanamu katika nchi yoyote katika zile walizozifungua. Hii ni kwa kuwa walifahamu malengo ya makusudio ya uisilamu ufahamu ulio sawa na wala hawakusita kusimamia ufasiri wa aya kijuujuu. Lakini waliangalia kwa undani zaidi juu ya makusudio na malengo kwa dalili ya kuwa walijua madhumini ya aya, hata sayidna umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) pale alipozuia fungu la sadaka kwa wale wanaozoweshwa nyoyo zao 2 katika uisilamu pamoja na kuwa imethibiti ndani ya kurani, Mwenyezi Mungu aliposema { Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika njia ya Mwenyezi Mungu,) na alipoulizwa Umar( Mwenyezi Mungu amwie radhi) iweje unasimamisha fungu ambalo Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akilitoa? Akasema: “ tulikuwa tukiwapa na uisilamu ni dhaifu na kwa lengo la kuwazowesha lakini sasa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameupa nguvu uisilamu kwa fadhila zake kwa ajili hili fungu hili halina kazi tena. Na zaidi ya haya, alizuia kutimizwa hukumu ya wizi katika mwaka wa njaa pale alipomwandkia mmoja wa wafanya kazi wake, utafanya nini akikujia mwizi (mtu kaiba)? Akasema: nitamkata mkono wake.” Akasema: “ mimi akinijia mwenye njaa basi nitaukata mkono wako. Isipokuwa umma wetu wa kiisilamu umefikwa na mitihani mikubwa akili za watu wake zikasimama wakaanza kuhalalisha na kuharamisha bila ya elimu, ufahamu na wala kujua, wakajidhatiti kwa nafsi zao na za wanafunzi na wafuasi wao kwa yale wasiyo kuwa na elimu nayo kwa kutoa fatwa, wakapotea na kupoteza wengine, pia kufungua mlango mpana wa kuwapa mwanya watawala na mabeberu kufuta athari za ustaarabu wetu sawa ustaarabu wa kiarabu, kiisilamu, kikiristu, kifirauni, kiashuri, kibabeli, kiyunani, kirumi na ustaarabu mwengine. Hii ni kwa kufuta utajo wa waarabu na pia ustaarabu wake na ustaarabu wa kiisilamu na pia wa kikiristu. Kwa kuwa wao ni wajinga wa tabia na 3 wasio na dini na wala maadili. Kwao wao ni kufikia malengo yao pasi na kutizama sababu na hata kama kuangamiza wanadamu na majengo na kila kikavu na kibichi pia hata kubomoa ustaarabu wa kibinaadamu. Mbaya zaidi ni kuwa haya yanatendeka kwa jina la dini na baadhi ya watu huidhania dini vibaya na kuona ni ya kiadui kumbe dini ipo mbali sana na mambo haya. Na hata kama watajidanganya wenyewe na kuwahadaa wahanga wao (wafuasi wao) katika vijana wenye kujiunga nao kwamba wao wapo sawa. Hao ni kama wale aliosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, {na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu. Kwa hakika hao waliwafanya mashet’ani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka} na anasema {Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri} {. Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu. 205. Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.} Na kiongozi mkuu wa Al Azhar Profesa Ahmad Al-Twayib amesisitiza kama alivyosisitiza waziri wa wakfu na Dar Al-Iftaa ya Misri, kuwa haifai kuharibu alama hizi za ustaarabu kwa namna yoyote ile sawa iwe kwa kuzivunja, kuziharibu 4 mkuziuza, kuziiba au kuzibomoa na kuziharibu ni sawa na kuharibu ustaarabu wa mwanadamu. Na katika jambo lenye kuhitaji mazingatio na lenye kuleta hisia na mshangao na kuleta masuala mengi ni msimamo wa nchi za magharibi na mashirika ya kimataifa juu ya kimya chao kikubwa juu ya makosa haya ambayo lau kama yangelitokea sehemu yoyote hapa ulimwenguni ukiachilia mbali eneo la mashariki ya kati (ukanda wa kiarabu) basi ulimwengu wote ungelijua. Basi hii ndio tabia ya maadui zetu ambao wanatushajiisha katika vita visivyo vya sheria, na lenye kuuma zaidi ni zile Fatwa ambazo hutilia mkazo matendo ya aina hii, hivyo basi tunahakikisha na kuthibitisha tena na tena kuwa kuna haja kubwa ya kuweka sheria ambazo zitazingatia utoaji wa Fatwa kwa kutolewa na wale tu wenye ujuzi nazo na si wengine.

Uzuri, furaha na hisia njema

Mokhtar-300x198

Uisilamu ni dini ya ustaarabu na upendo, dini ya furaha na maelezo yake na njia zake zote zinathibitisha hili na hata kurani tukufu na hadithi za mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) pia zinathibitisha hili. Mwenyezi Mungu anasema katika kurani { Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. 6. Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na mnapo-   wapeleka malishoni asubuhi.}

 Na anasema pia { Ambaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na akakupitishieni humo njia, na akakuteremshieni kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za mimema.} na kuendelea kusema { na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.} {, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.} na kusema pia {17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?19. Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?} na anasema pia { Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema.}ama kuhusu mbingu zilizo juu anasema { na tumezipamba kwa wenye kuangalia.} { Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa,}

Kurani tukufu imetuamrisha kujipamba kwa mapambo mazuri na tuchukue mapambo yetu kila tuendapo misikitini (tusalipo). Mwenyezi Mungu anasema { Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu 32. Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.} Na Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliposema: “ haingii peponi mtu mwenye chembe ndogo ya kiburi (dharau). Mtu mmoja akasema: “kuna mtu hupendelea nguo yake iwe nzuri na viatu vizuri.” Mtume akasema: “ Mwenyezi Mungu ni mzuri hupenda uzuri, kiburi ni kukana ukweli na kudharau watu.” (muslim). Na sayidna Mughira bin Shuuba (Mungu awie radhi) alipomueleza kuwa yeye amemchumbia mwanamke, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akamwambia: “mwangalie kwani itapelekea kudumu kati yenu.” (Tirmidhiy).

Mtume (rehma na amani zimshukie alikuwa kipenda uzuri, na alilingania pia uso wa bashasha akasema: “jambo jema lolote usilidharau hata kama utakutana na mwenzio basi iwe kwa uso wa bashasha.” (Muslim). Na  kusema kuwa kuingiza furaha kwa watu ni kitu kimuwekacho mtu karibu na Mwenyezi Mungu akasema: “ mwenye kuingiza furaha katika nyoyo ya muisilamu basi ni haki ya Mwenyezi Mungu kumridhisha siku ya kiyama.” Na akasema “ amali zipendwazo sana na Mwenyezi Mungu ni furaha uiingizayo kwa muisilamu.” Na akawataka masahaba zake kuvaa nguo nzuri wakati wanapokutana na katika sherehe na minasaba

Pamoja na kuwa uzuri wa kweli haupo katika mandhari ya muonekano na uzuri wa vitu lakini unavuka mipaka zaidi nao ni uzuri tabia na mwuonekano. Mustafa Saadiq Rafii (Mungu amrehemu) anasema: “ mwanamke mbora ni yule mwenye sura nzuri kama tabia zake na akili yake ikawa uzuri wake wa tatu. Mwanamke huyu akiwa na mwanamke mwenye kuendana nae basi atamfurahisha na kumfurahisha na kumfurahisha. Mshairi anasema

Mtu iwapo hajalaumiwa kwa heshima yake

Basi nguo yoyote aivaayo huwa nzuri

Tunaelewa kuwa kidogo huwa ni kingi

Nikasema kuwa ukarimu huona kidogo

Sikudhurika kwa kidogo na jirani yetu

aliye mwema ni mwenye nguvu

na jirani mwenye wengi ni  dhalili

Inatulazimu sote kujipamba kwa tabia za kiisilamu katika muonekano wetu, mazingira yetu, mashule yetu, vhuo vyetu, bustanini mwetu, matembezini mwetu na katika sehemu zote. Na wala tusifanye yenye kuondosha  furaha na ucheshi.

Na katika alama kubwa sana za ucheshi na ziletazo furaha ni neno zuri lililo jema, sayidna Umar bin Khatab (Mungu amwie radhi) alipita kwa watu waliokuwa wakiota moto akachukia kuwasalimia kwa kusema “amani iwe juu yenu enyi watu wa motoni” isipokuwa akasema”  amani iwe kwenu enyi watu wa kivulini”. Na kama ulivyotulingania uisilamu kuwa tuchague majina yenye maana nzuri na kujiepusha na majina mabaya yasiyoendana na hisia za kiutu, kwani kurani imetuamrisha kufanya kila lililo zuri na jema na kusema kila lililo jema. Mwenyezi Mungu anasema { nasemeni na watu kwa wema,} Albaqara 83. Na akasema { Waambie waja wangu waseme maneno mazuri,} Israa 53. Basi kauli mbiu yetu ni “hisia njema na uzuri”. Hisia nzuri ni kigezo cha kujua uzuri na kuueneza kwa waliotuzunguka katika wanajamii.

Mfano mzuri wa kugawanya mali ya zaka

Hapana shaka kuwa iwapo zaka itagaiwa kama itakiwavyo kisheria basi itaziba pengo  kubwa la mahitajio ya mafakiri na wenye shida sana na masilahi ya taifa zima. Pindi nafsi za matajiri na  wenye uwezo wakifanya  ukarimu na kutenda wajibu wao wa kuwalisha wenye njaa, kuwavesha wasio na nguo, kuwatibu wagonjwa, kuwasaidia wenye kuhitaji na kutoa mchango wa kuboresha na kudumisha kwa  taifa basi ni lazima nchi ibadilike. Na hapatakuwa na raia ambaye atakuwa anahitajia na kuomba, imamu Ali (mwenyezi Mungu amwie radhi) anasema: “Hakika ya Mwenyezi Mungu Mtukufu amegawa chakula cha masikini katika mali za matajiri, na katu masikini hatokuwa na njaa isipokuwa tajiri atakuwa ameshiba, na akipatikana masikini mwenye njaa, tambua kuwa pana tajiri dhalimu na hakutoa haki ya Mwenyezi Mungu katika mali yake, na hakutekeleza wajibu wake kwa upande wa jamii yake.”

Na iwapo (tajiri) ataekeza vitega uchumi kwa njia sahihi kwa ajili ya masilahi ya taifa lake jambo hili litapelekea  kuinuka kwa taifa letu zuri kama itakiwavyo. Bali pia huenda manufaa yakaenea katika nchi nyengine nyingi za kimasikiniambazo nasi tunahitajika kuzisaidia kwa mfano wa nchi za mto wa Nile ambazo inatubidi kuwa na mawasiliano nazo na kusaidiana kielimu, kitamaduni, kimanufaa na kiutu kwa kiwango cha kiserikali na cha kiraia na kwa taasisi zake za kitaifa ambazo tunaweza kufanya vitega uchumi vikubwa na imara katika nchi hizi na nyenginezo katika nchi za Afrika zilizo na umasikini, kama ni mojawapo ya mbinu na himaya ya usalama wa raia wetu. Na kwa jambo hili kuna mifano mingi inyoshukuriwa kwa upande wa taasisi za kiraia.

Zaka ni haki ya lazima katika mali

Nasisitiza juu ya ukweli, na wa kwanza ni: hakika ya zaka ni hali ya lazima katika mali na ni nguzo kuu kati ya nguzo za kiisilamu mfano wa sala na funga bila ya kutafautiana, na Sayidna Abdallah Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “Vitu vitatu ndani ya kurani tukufu vimeteremshwa kwa kuambatanishwa sambamba na vitu vitatu (vyengine) kimoja wapo hakikubaliwi bila ya chengine, navyo neno lake Mwenyezi Mungu “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtiini Mtume wake.” Na neno lake, “Na Simamisheni sala na toeni zaka” mwenye kuacha kutoa zaka pamoja na kuwa anajua kama ni lazima basis ala yake haitomnufaisha kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na neno lake, “na unishukuru mimi na wazazi wako wawili na kwangu ni marejeo.” Asiyewashukuru wazazi wake wawili kwa wema wao na matendo mazuri yao basi pia hatomshukuru Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema kuhusu wanaoweka hazina za mali na kujizuia na utoaji wa zaka {Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia yaMwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu. 35. Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, nakwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao namigongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwamkilimbika. }

Jambo la pili: hakika uisilamu umetoa wito wa kutoa sadaka kwa wingi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema     { Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia yaMwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punjemia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, naMwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.} ( Surat Albaqarah.Aya,261). Na Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake anasema) “ mali haipungui kwa kutoa sadaka.” Na anasema: “sadaka bora ni ile uitaoyo hali ya kuwa ni mzima kabisa, unataraji utajiri na kuogopa umasikini, usiicheleweshe hadi pale roho inafikia kooni kasha ndio unasema, Fulani apewe hiki na Fulani hiki na ilikuwa kwa Fulani (hiki) na ilikuwa kwa Fulani (hiki).” Na pia anaendelea kusema: “hakuna siku isipokuwa malaika wawili huita na mmoja wao husema “ewe Mola mpe kila atoe (mpe) ziada, ewe Mola mpe kila ajizuiaye uharibifu.”  Na anasema  Mwenyezi Mungu Mtukufu:{  Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi}. ( Surat Mhammad,Aya 38)  .

Huondosha na kutibu mwanya:

   Hapana shaka kuwa mwanya  utakuwa ima katika vyombo (taasisi)  vyenye kutoa zaka au vyenye kupokea zaka au vyombo vyenye kuunganisha na sawa iwe ni mtu, jumuiya au taasisi.

Mwanya unaopatikana kupitia vyombo vitoavyo zaka itakuwa ima kwa kutotoa hiyo zaka kabisa, au kwa kuipunja au itakuwa inatolewa lakini si kwa umakini kwa wahusika wake.

Hivyo basi, ni wajibu kuzingatia katika hutuba za dini juu ya ulazima wa kutoa zaka na umuhimu wake na madhambi makubwa ayapatayo mwenye kuzuia kutoa zaka mbele ya Mwenyezi Mungu, pamoja na kusisitiza ya kuwa tajiri hatoepukana na dhima yake kwa kuitoa mali yake kiholela. Na baadhi ya wasomi wa elimu ya sheria wameona ya kuwa iwapo tajiri amempa mali yake kwa anayedhania kuwa ni masikini kasha akaja kuelewa kuwa si masikini basi itamlazimu kutoa tena zaka. Ni wajibu wake ahakikishe kuwa anatoa kwa mujibu wa sheria na kwa amana na kwa uchunguzi na kwa vyombo vya kisheria ambavyo hupewa zaka ili dhima yake iondoke mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ili zaka yake ilete matunda mazuri ambayo yanapatikana kwa utoaji wa zaka.

Na mwanya upatikanao kwa upande wa mpokeaji, unakuja kutokana na udhaifu wa ugawaji kwa baadhi ya wenye nia mbaya za kutaka kujilimbikizia mali kwa njia yoyote hata kama ni kwa kulaghai. Ni wajibu wetu kuwakumbusha muongozo sahihi wa kiisilamu na utu wa kibinaadamu ambao unakataza kwa mwenye uwezo  kulaghaia na kujidhalilisha. Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “haifai kuomba isipokuwa kwa Yule mwenye ufakiri uliopindukia mipaka, au mwenye madeni makubwa, au mwenye damu ya maumivu ”.  Na anasema; “Mwombaji ni kama pambo ambalo mtu hujipambia usoni mwake, akitaka huliacha usoni mwake na akitaka huliondoa.” Na ima Ali (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) anasema;

Ni afadhali kubeba kima cha jabali * kuliko kufadhiliwa na watu

Watu hunambia kazi ni aibu * nami huwambia “aibu ni kuomba watu”

Na mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “ katika mambo ambayo watu waliyapata kutokokana na maneno ya utume ya mwanzoni ni kuwa, usipokuwa na haya basa fanya utakacho.”

Lazima tuhakikishe ya kuwa uisilamu umekataza kuomba pasi na sababu ya msingi, na mtu mwenye heshima hawezi kuishusha nafsi yake kwa kuomba, na mkono wa juu (utaoa) wa juu ni bora kuliko wa chini (usiotoa). Pamoja na kuhakikisha umuhimu wa kufanya kazi na thamani yake na msisitizo wa uisilamu juu ya kazi. Na kuweka wazi ya kuwa anayekwenda mbio kwa ajili ya wajane na masikini ni sawa na apiganiaye jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mbora wa watu ni Yule alaye kwa mkono wake na si kwa kuomba kwa wengine.

Ama kwa upande wa mwanya wa tatu:  ni ukusanyaji na ugawaji, pamoja na imani yetu kwa baadhi ya taasisi za kijamii kuwa zinapunguza mzigo mkubwa kwa mafakiri na wasi na uwezo sawa kwa upande wa kuwapa mahitajio kwa kupitia vitega uchumi na hasa kwa upande wa matibabu, isipokuwa nionavyo kuwa taasisi hizi zinahitaji yafuatayo:-

  1. View chini ya uangalizi wa vyombo vya kiserikali, na vyombo hivi viwe vinafutilia na kuchunguza ipasavyo, na kuwe na uwazi wa kutangaza uwezo wake, mahitajio yake na mafao yake pamoja na kuwaongoza katika utendaji wa kiidara kadiri wawezavyo.
  2. Kuwe na ramani ya wazi juu ya taasisi hizi, na upeo wake wa kijiografia na  utendaji wake, ili ijulikane mipaka yake na kikomo chake na isije ikatokezea kupatikana uzembe kwa baadhi ya sehemu pengine zingelikuwa zinahitaji msada mkubwa zaidi.
  3. Kuwe na idara ambayo itashughulikia taasisi hizi kwa mfano Wizara ya Ushirikiano wa jamii. Kuwe na kiunganishi chenye kuwaunganisha watoaji na wapokeaji na taasisi za kijamii kwa mwelekeo wake wa kijiografia au mwelekeo wa kihuduma, ili pia wahusika wajulikane na iepukane kutowafikia walengwa halisi wanaohitajia zaka.
  4. Malengo na madhumuni yawe wazi yajulikane kwa wote, au kila chombo au jumuiya ijulikane ina dhumuni gani iwapo ni kuwalisha wasio na uwezo au kuwatibu wagonjwa, kulipia madeni ya watu, nahyo haya ni miongoni mwa malengo wanayoyaendea mbio Wizara ya Wakfu ya Misri.