Habari Muhimu Zilizotufikia

Utendaji wa dini kwa muonekano wa nje na wa kisiasa

أ.د/ محمد مختار جمعة وزير الأوقاف

D / Mukhtar Mohamed Juma Waziri wa Awqaf

Hapana shaka kuwa utendaji wa dini kwa muonekano wa nje na kwa muonekano wa kisiasa hii ni changamoto kubwa sana ambayo umma wa kiarabu na wa kiisilamu unakabiliwa nayo. Na iwe sawa kwa hawa ambao wanazingatia umbo au muonekano hata kama itakuwa ni kwa kuacha asili. Na kufanya kuwa muonekano ndio kila kitu, na hata kama mwenye kujidai muonekano huo hana utu wala tabia ambazo humfanya awe ni  kigezo na mfano wa kuigwa. Na hii inatokana na kuwa mwenye kujionesha huwa tabia yake haiendani sambamba na mafunzo ya kiisilamu na hii huzingatiwa kuwa moja ya uvunyaji na ukiukwaji wa dini, kwani iwapo muonekano wa wenye kujionesha ni tabia mbaya au uongo au kutengua ahadi au khiyana au kula mali za watu kwa dhuluma, hapa  jambo hili kwa hakika huwa ni hatari sana.

Isitoshe mwenye tabia hizi huwa ni katika wanafiki, kwani Mtume wetu (SWA) amesema : ”alama za mtu mnafiki ni tatu; akizungumza husema uongo, akitoa ahadi haitimizi na akiaminiwa hufanya khiyana. (imepokewa na Bukhari).

Vile vile kwa waichukuliao dini kuwa ni ibada na kufanya jitihada ambazo zitapelekea kuifahamu dini vibaya na kufikiria zaidi mambo yasiyohitajika na kubeba silaha na kujitenga na  watu wenzao, kama ilivyokuwa kwa madhehebu ya Khawarij ambao walikuwa wakisali sana, kufunga na kusali usiku isipokuwa wao hawajaisoma elimu ya sheria kama itakiwavyo ambayo ingeweza kuwakinga na umwagaji wa damu na kupelekea watu wawapinge kwa kutumia panga zao.  Lau kama wangetafuta elimu kwanza kama alivyosema imam shafii “Mwenyezi Mungu amrehemu”, wangejikinga na mengi, kwani uisilamu ni dini ya upole kabla ya chochote, na kila ambacho kitakuweka mbali na upole  basi hicho hukuweka mbali na uisilamu, na kinachozingatiwa ni tabia njema si maneno matupu. Kwani wamesema “Muungwana hujulikana kwa matendo na si kwa maneno.”

Na hakika ibada zote haziwezi kuleta matunda yake isipouwa tabia ya mwenyewe itakapokuwa njema, na yeyote ambae swala yake haitamkataza juu ya uovu na machafu basi huwa hana swala, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “hakika ya swala inakataza maovu na machafu, na utajo wa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, naye Mwenyezi Mungu anajua yote muyatendayo” (Ankabut, aya 45)

Na yeyote ambae funga yake haimzuii na maneno machafu basi huwa hana funga, kwani Mtume SWA anasema “asiyeacha maneno machafu na matendo machafu, basi hakika Mwenyezi Mungu huwa hana haja ya mja huyo kuacha chakula chake na kinywaji chake” (Imepokewa na Bukhari)

Mwenyezi Mungu huwa hakubali zaka wala sadaka isipokuwa kwa mali halali, Mtume wetu (SWA) anasema “Hakika Mwenyzi Mungu ni Mzuri na wala hakubali isipokuwa kizuri” (Imepokewa na Muslim).

Mtume (SWA) anasema “ Swala haikubaliwi bila ya tohara na wala sadaka haikubaliwi iwapo ina husuda (Imepokewa na Muslim).

Na hata ibada ya Hijja ili ikubaliwe itategemea kipato cha halali na tabia njema “Atakaehiji na akawa hajafanya uovu wala machafu basi hurejea (na madhambi yake hufutwa) kama siku aliyozaliwa na mama yake”. Na Mtume (SWA) ametaja “Mtu ametoka safari ya mbali amejaa vumbi kisha ananyosha mikono yake mbinguni anasema “Ewe Mola wangu ewe Mola wangu, hali ya kuwa chakula chake ni haramu kinywaji chake haramu, nguo zake ni haramu na amekula haramu iweje basi mtu huyu kujibiwa” (Imepokewa na Muslim).

Na utendaji ulio mbaya zaidi ni utendaji wa dini kwa muonekano wa nje kwa ajili ya kisiasa, hapa tunakusudia hili kundi ambalo wameifanya dini kuwa ndio njia ya kupitia kuelekea kwenye uongozi kwa kutumia upenzo wa dini na kuwapendezesha watu hasa wale wasiojua kitu kuhusu dini yao. Na kuwahadaa kuwa lengo la kushika madaraka ni kwa ajili ya kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu pekee na kuinusuru na kuifanya iwepo. Pamoja na kuwa sisi huwa hatuhukumu kupitia nia na wala hatuingilii chochote kuhusu nia ya mtu kwani nia ni kati ya mja na Mola wake, na kila mmoja wetu ana malengo yake (nia yake), lakini  ujuzi tulionao wa kuishi na kundi la kigaidi la Ikhiwani na kwa wale wenye mwenendo kama wao au kuwaunga mkono katika makundi mengine ya kiisilamu tumejihakikishia mambo mawili, nayo:-

  1. Tukio kwa upande wao si tukio la kidini hata kidogo isipokuwa ni kupigania uongozi kwa makeke na mabavu, hatukuwahi kuona mfano wake na kuwatendea wengine kwa kujeli, kiburi na maguvu, kitu ambacho watu wengi wakakipinga kwa kuwa ni mzigo katika dini, na ikawa hakuna budi isipokuwa kuifuta sura hii mbaya ambayo imeenea katika akili za wengi kati ya watu ambayo imefungamana na tabia za watu wa kundi hili pamoja na dini.
  2. Jambo la pili jingine ni kuwa, wao wameiharibu dini yao na kuipa sura mbaya pamoja na kuwa dini ina tamaduni nzuri na ya upendo, na wakajithibitishia kuwa wao si watu wa dini na wala hawawezi uongozi, kwa sababu, je ni dini gani inayowakhini watu wake na taifa lake na kutoa siri na kuuza hata nyaraka muhimu na kuwa wapelelezi wa nchi yao kwa wasioitakia manufaa. Na je kuna dini inayochochea vurugu, mauaji, ufisadi na kuunda vituo vyenye lengo la kueneza maovu kwa wafuasi wake pamoja na kufanya khiyana ambayo haijawahi kutokea, ikiwemo khiyana ya taifa na kutendeana na maadui wa nchi yake?

Imethibiti na ninazidi kuthibitisha kuwa kundi hili ambalo limeifanya dini kuwa ndio chombo cha kuwahadaa watu na kunufaisha malengo yao ya kuutaka uongozi si zaidi ya kuungana na shetani, ili kutekeleza na kuhakikisha malengo yao na tamaa zao za kutaka utawala na uongozi kwa kupitia dini, au nchi au kwa umma.