Habari Muhimu Zilizotufikia

Haki za Vijana na Wajibu wa kila Mmoja wao

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Viumbe vyote anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آَمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى}

Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye peke yake asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake.Ewe Mola wetu tunakuomba umswalie na umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika kipindi cha Ujana ni katika vipindi Muhimu mno kwa Umri wa Mwanadamu; Ni kipindi cha nguvu za kimwili na ukomavu na uchangamfu, na kutoa, Matumaini Mapana, na kuwa wazi kimaisha. Hapana shaka Kwamba vijana ni Nguzo Kuu ya Uma na ni Moyo wake unaodunda na ni mkono wake wenye nguvu na hakuna yoyote anaeweza kuukana mchango wao muhimu katika ujenzi wa Mataifa na katika Maendeleo ya Uma na Kuimarika kwake.

Na Qurani Tukufu imekielezea kipindi hiki cha Ujana kama ni kipindi cha nguvu kati ya unyonge wa aina mbili, unyonge wa utotoni na unyonge wa Uzeeni. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اللَّهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْ بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِنْ بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً}

Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe.

Utume na Risala vilikuwa wakati wa umri wa Ujana. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kisa cha Bwana wetu Yusufu A.S:

{وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ}

Na alipo fikilia utu uzima tulimpa hukumu na ilimu. Na kama hivi tunawalipa wanao tenda mema.

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Bwana wetu Musa A.S:

{وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَى آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا  وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ}

Na Musa alipo fika utu-uzima baraabara, tulimpa akili na ilimu. Na hivi ndivyo tunavyo walipa walio wema.

 Ibnu Abas R.A, amesema: Mwenyezi Mungu Mtukufu hajawahi kumtuma Mtume isipokuwa Kijana, na wala hajawahi kupewa Elimu Mtu isipokuwa akiwa katika umri wa Ujana.

Tunamuona huyu kipenzi cha Mwenyezi Mungu Mtukufu Nabii Ibrahim A.S, alipambana na Watu wanaoyaabudu Masanamu akiwa Kijana. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ}

Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.

Qurani Tukufu vilevile imeashiria juu ya Utambuzi na Akili pevu ya Bwana wetu, Mtume Suleiman A.S, tena akiwa katika kipindi cha Ujana wake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَفَهَّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ وَكُلًّا آتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا}

Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Musa A.S, alipewa Utume na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipokuwa katika kilele cha Ujana wake, nguvu na uaminifu ambavyo vilipelekea Binti wa Mja Mwema wavielezee kwa baba yao, kama isemavyo Qurani Tukufu:

{قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ}

Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba yetu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amemsemesha Yahya A.S, ili asimame kwa amana ya Elimu na kulibeba jukumu la Ulinganiaji, kwa nguvu zote na azma ya Vijana, akasema:

{يَا يَحْيَى خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا}

Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto.

Na kutokana na umuhimu wa kipindi hiki cha Ujana, Mtume S.A.W, amebainisha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atamuuliza Mja Wake swali maalumu Siku ya Kiama mpaka ajitahidi mtu kunufaika na Ujana wakena kuutumia vizuri kwa manufaa yake na ya Watu wote. Akasema Mtume S.A.W: Miguu ya Mja wangu siku ya Kiama haitapumzika mpaka aulizwe mambo manne; Aulizwe kuhusu Umri wake na ameumalizaje? Ujana wake aliumalizaje? na Mali yake aliichumaje na akaitumiaje? Na Elimu yake aliifanyia nini?

Na Uislamu umewahimiza sana vijana kwa himizo kubwa, na ukawajaalia majukumu, kwani wao wana haki ya kusomeshwa, Kuongozwa na kuandaliwa vizuri. Na Qurani Tukufu imelizungumzia jambo hili kwa yale aliyoyasema Luqmaani mwenye Hekima na Busara alipokuwa na mwanae. Ambapo yeye alipandikiza ndani ya kijana wake pande mbalimbali za Kidini na akamuasa awe mwema na mwenye kujitolea na ajipambe na Maadili mema. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ }

Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا بُنَيَّ إِنَّهَا إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِي صَخْرَةٍ أَوْ فِي السَّمَاوَاتِ أَوْ فِي الْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا اللَّهُ إِنَّ اللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ * يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَى مَا أَصَابَكَ إِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ * وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ * وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِن صَوْتِكَ إِنَّ أَنكَرَ الْأَصْوَاتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ}

Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, Mwenye khabari za yote. Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha. Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.

Na hivyo ndivyo alivyokuwa Mtume S.A.W, anafanya anapokuwa na vijana. Akawa Mtume S.A.W, ana hima kwao kwa kiwango kikubwa mno na anapupia katika kuwawezesha kielimu na kuwaandaa vilivyo na alikuwa anapandikiza nyoyoni mwao na katika akili zao Misingi ya Dini Tukufu ya Uislamu na kupenda Elimu na Kujiwekea Sifa maalum. Kutoka kwa Ibnu Abas R.A, amesema: Nilikuwa nyuma ya Mtume S.A.W, Siku moja, akasema: Ewe kijana, mimi ninakufundisha maneno haya; Mlinde Mwenyezi Mungu Mtukufu naye atskulinda. Mlinde Mwenyezi Mungu Mtukufu utamkuta upande wako. Unapoomba basi mwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na unapotaka msaada mwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ujue kwamba kama Uma wote ungelikusanyika ili ukusfae kwa kitu chochote usingeliweza kukufaa isipokuwa kwa kitu alichokuandikia Mwenyezi Mungu Mtukufu na kama wangelikusanyika ili wakudhuru kwa kitu chochote wasingeliweza kukudhuru isipokuwa kwa kitu alichokuandikia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kalamu zimekwisha nyanyuliwa, na vitabu vimekwisha kauka.

Na baada ya Elimu bora na Mafunzo yaliyokamilika, inafuatia haki ya vijana katika kuwawezesha na kuwapa msukumo – kila mmoja kwa mujibu wa uwezo na Sifa alizonazo – katika maeneo ya kazi au Uongozi na Majukumu. Na hivi ndivyo Mtume S.A.W, alivyofanya ampo aliwaajiri vijana wenye nguvu mbali mbali. Na akawasukuma ili waingie katika vita vya maisha; Mtume S.A.W, alimwamini kijana wakati wa Ulinganiaji wake, ambae Umri wake hauzidi miaka ishirini, nae ni Arqam R.A, ambae nyumba yake ilikuwa Makao Makuu yenye Usalama kwa Mtume S.A.W, na Maswahaba wake mwanzoni mwa Ulinganiaji wa Uislamu. Mtume vilevile, alimpa uongozi wa Jeshi la Waislamu, Usama bin Zaid R.A, na Umri wake Wakati huo ukiwa haujavuka miaka kumi na nane.

Omar bin Khatwab R.A, alikuwa akiwaita vijana katika makao yake pamoja na wazee katika kila jambo, na anasema: Hakatazwi yoyote miongoni mwenu kwa udogo wa Umri wake kutoa maoni yake, kwani hakika ya Elimu haimo kwa wadogo wala kwa wakubwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaiweka atakapo. Na kwa hivyo katika Makao yake walikuwapo vijana akiwamo Abdullahi bin Abas R.A, ambaye Omar R.A, alikuwa akimzungumzia kwa kusema: Hakika Kijana huyu ana ulimi wenye kujitambua na moyo wenye akili.

Na jambo hili halijawahi kuishia kwa vijana wa kiume tu, bali na wa kike pia wana mchango wao usiopingika wa Ujenzi wa Ustaarabu wa Kiislamu, wao walikuwa na mchango wao Wakati wa amani na wakati wa vita. Miongoni mwao ni Bi Asmaa Binti Abuu Bakar Sidiiq, R.A, na mchango wake wa wazi katika Hijra ya Mtume S.A.W, na baba yake R.A, ambapo yeye Asmaa alikuwa anawaandalia chakula na vinywaji  Mtume na Baba yake Abu Bakar Wakati wa Hijra tukufu, bali wanawake walikuwa na mchango katika nyakati nzito na ngumu kuliko zote. Na Katika viwanja vya mapigano, Wanawake walikuwa wakiwanywesha maji wapiganaji na wakitoa huduma ya kwanza kwa wenye kujeruhiwa, na katika hilo ni kama ilivyokuwa katika siku ya vita vya Uhudi. Anasema Anas R.A: Nilimwona Aisha binti Abu Bakar R.A, na Umu Sula8m wakisambaza viriba vya maji migongoni mwao kisha wanavimaliza kwa kuwagawia watu maji hayo kisha wakarejea tena na kuvijaza viriba hivyo kisha kuja navyo na kuwagawia watu maji.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Viumbe vyote, na ninashudia ya kwamba hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake asiye na mshirika wake, na ninashudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu mswalie, marehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika vijana wana majukumu mengi. Na la Kwanza: Kujiimarisha kielimu na kitamaduni, pamoja na kuendeleza kujielimisha huko kwani Elimu daima inasonga mbele kila dakika na hapana budi kwa vijana wetu kwenda sambamba na maendeleo na matukio ya Ulimwengu huu na kuchunga mahitaji ya soko la kazi, na mahitaji ya taifa, na kwa hivyo kujiongezea elimu kwa njia za mipango ya masomo na mafunzo na zoefu zinazohitajika mpaka vijana hawa wawe na uwezo wa kupambana na changamoto zilizopo. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumuamrisha Mtume wake S.A.W, kujiongezea chochote katika vitu vya duniani isipokuwa Elimu ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akimwambia Mtume wake S.A.W:

{وَقُلْ رَبِّ زِدْنِي عِلْمًا}

Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu

Tatu: Kujihimiza katika kunufaika na zoefu mbali mbali na kujihadhari na kudanganyika. Vijana wanapaswa wanufaike na hekima na uzoefu wa watangulizi wao wenye uzoefu kwani uhusiano baina ya vizazi vinavyofuatana sio uhusiano wa kupuuziana au kukinzana; bali ni uhusiano wa kushirikiana kikamilifu na Kunasihiana, na vijana wetu wajihadhari na majivuno ambayo huwa yanabomoa na wala hayajengi, bali humuangamiza muhusika. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake Kitakatifu:

{وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا إِنَّكَ لَن تَخْرِقَ الْأَرْضَ وَلَن تَبْلُغَ الْجِبَالَ طُولً}

Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima.

Anasema Mtume wetu S.A.W: Mambo matatu huangamiza: Uchoyo wenye kunyenyekewa, na matamanio ya nafsi yanayofuatwa, na mtu kupendezwa mno na maoni yake, kupindukia.

Tatu: Kuweka nia upya kwa ajili ta kuitumikia Dini na Nchi. Mwanadamu hulipwa kwa mujibu wa Uzuri wa nia yake katika Kazi yake, na ukweli wa nia yake. Anasema Mtume S.A.W: Hakika matendo hutokana na Nia, na kila Mtu hukipata kile alichokinuia…

Nne: Ni Kuitumia fursa kwa kuongeza juhudi zaidi na kutambua kuwa Njia ni ndefu na Amana ni Nzito sana, kwa kuwa sisi tunaishi katika jamii inayoendelea kwa kasi kubwa mno na hakuna nafasi ya kwa wale wasio na bidii na wasiozijali kazi zao, na hasa katika kutekeleza kazi walizopewa wazitekeleze. Ili tuweze kufanikisha matarajio yetu na kuifikia nafasi yetu, ambayo sisi wenyewe tunaitarajia na kwa ajili ya taifa letu hapana budi tujitume kwa nguvu zote na juhudi zetu kwa mapana zaidi katika Kazi Zeru.

Tano: Kuurejesha wema kwa Taifa ambalo limetulea na sisi tukakulia ndani yake likatusomesha na kutuwezesha; Taifa lina haki kwa wananchi wake ambao wameishi ndani yake na wakalelewa na kujipatia uzoefu wake na wana wao ndani ya Taifa hilo kumbukumbu na historia zao na iwe nguvu yetu ni kuwa na msimamo na kuwa na nia isiyotetereka, na silaha yetu iwe Elimu na Ubunifu, na kauli mbiu yetu iwe Uzalendo na Kujitolea; kwa ajili ya kulitumikia taifa letu hili na kulilinda.

Ewe Mola wetu Mlezi wabariki vijana wetu, na uwalinde na kila ovu, na uwawafikishe katika Ujenzi na Uimarishaji wa nchi, na uwaongoze katika mambo yenye masilahi kwa Nchi yao na kwa. Watu wake, na Uilinde Nchi yetu na nchi zote Duniani.

 

Uma wa Soma, ni Uma wa kutekeleza Majukumu yake Ipasavyo Baina ya Wanachuoni wa Uma na Wanachuoni wa Fitina

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Viumbe vyote anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ}

Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.

Na ninashuhudia ya kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliye peke yake na wala hana mshirika wake, na ninashuhudia ya kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu, tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Na baada ya Utangulizi huu:

Uislamu umehimiza utafutaji wa Elimu na umehikiza pia bidii na jitihada katika kujipatia hiyo Elimu, na hakuna dalili bora zaidi kuliko aya ya kwanza kuteremshwa katika Quran tukufu nalo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ * خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ * الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ * عَلَّمَ الْإِنْسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ}

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.

Kwa hiyo amri ya Kwanza ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyoteremshwa katika Wahyi ni Kusoma ambako ndio mlango wa kwanza katika milango ya Elimu. Kisha baada ya hapo ikaja ishara ya kalamu ambayo ndiyo njia ya kuandikia Elimu na kuinukulu kwake. Na katika hili kuna msisitizo kwa Watu wote juu ya ubainishaji

Hakika ya Wanachuoni Wakweli wa Uma huu, wautumia Wakati wao wote na juhudi zao, na wakatuletea Elimu yao wakiitumikia Dini na Nchi yao, na wakawapitisha Watu njia ya Ukati na Uuwiano, Usamehevu na Huruma, na Ulinganiaji wao ukaleta Matunda makubwa yenye manufaa kwa vizazi na vizazi, vizazi vinavyojenga na wala havibomoi, vinatengeneza na haviharibu, vinayaweka juu Maadili ya Kibinadamu, na kuinyanyua juu Heshima ya Mwanadamu, na amani na usalama. Na hii ndio Elimu yenye manufaa ambayo inakuwa akiba kwa mwenye nayo anapofariki. Anasema Mtume wetu S.A.W: Mtu anapofariki, matendo yake yote hukatika usipokuwa Mambo Matatu: Sadaka endelevu, ay Elimu inayowanufaisha Watu, au Mtoto Mwema atakayemwombea.

Na Mtume S.A.W: alikuwa anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amuepushe na Elimu isiyokuwa na Manufaa, na wala haijengi wala haifundishi maadili na mwenendo Mzuri, na Mtume S.A.W, alikuwa anasema: Muombeni Mwenyezi Mungu Mtukufu, akupeni Elimu yenye manufaa, na mjikinge kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Elimu isiyokuwa na Manufaa.

Na moja ya Dua zake Mtume S.A.W: Ewe Mola wangu ninajikinga kwako na Elimu isiyokuwa na Manufaa, na Moyo usio kuwa na uchamungu, na nafsi isiyotosheka, na Dua isiyojibiwa.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni na nyinyi.

* * *

Sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliye peke yake na wala hana mshirika wake, na ninashuhudia ya kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu, tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata kwa Wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ndugu zangu Waislamu.

Hakika Wanachuoni wenye moyo msafi ndio watu wa Mwongozo Mwema, Mwenendo Mwema, na Nia njema na Uuwianifu, Watu ambao wanaibeba bendera ya Ukati katika kila zama na wanaiepusha Dini Tukufu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Uvurugaji wa Wenye misimamo mikali, na tafsiri potofu pamoja na kuwaiga wapotoshaji.

Kwa upande wa Wanachuoni wa Fitina ambao wameifanya Dini kama njia ya kuyafikia malengo yao na kufikia wanayoyakusudia, basi hao ndio waliothubutu dhidi ya Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakarusha makombora ya Fatwa ambayo yanadhuru na wala hayanufaishi, na yanawagawa watu na wala hayawaunganishi, na yanabomoa na wala hayajengi, na yanaufungulia Uma mlango wa kukufurisha ambao Uislamu umetutahadharisha tusiuingie mlango huo. Anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakaemwambia nduguye: Ewe Kafiri, basi mmoja wao atakuwa katika hali hiyo, ikiwa kama alivyosema ni vizuri, ni ikiwa kinyume na alivyosema basi kauli hiyo itamrejea yeye mwenyewe.

Wanachuoni wa Fitna wameufanya Ukali wa kutoa Fatwa, Ubishi Kuwabana watu, kama ni Mfumo wao; na huu ni Mfumo ulio mbali sana na Uislamu wenye Usamehevu na Ukati wa Mambo. Uislamu umewaondoshea Watu kila aina ya Uzito na ukawaowekea mbali aina zote za Ugumu wa Mambo.

Ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ}

Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini.

Na anasema Mtume S.A.W: Peaneni habari njema na wala msipeane habari mbaya, na mrahishiane na wala msisababishiane uzito.

Kwa hiyo ukali wa kutoa Fatwa unakwenda kinyume na Ukati wa Uislamu wenye Usamehevu na ambao Dini Tukufu ya Uislamu inajipambanua kwayo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ}

a vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu…

Na Ukati una maana ya Uadilifu, Uwastani na kujiepusha na Kujikweza ambako ni sababu ya kuangamia kwa Mataifa. Mtume S.A.W, anasema: Enyi Watu, jiepusheni na kujikweza katika Dini, hakika mambo yalivyo, huko kujikweza katika Dini kuliwaangamiza waliokuwa kabla yenu.

Na amesema Sufiyani Thauriy R.A: Hakika elimu kwetu sisi ni kibali cha Fiqhi na ama ukali katika Dini kila mmoja wetu anauweza vizuri sana.

Na wanaoandamana na Wanachuoni wa Fitna ni Wanachuoni wa kupotosha wanaozungumza bila ya kuwa na Elimu, na wala hawajazinduka na kuijua haja ya Uma ya kufuata njia bora kabisa a za maendeleo na hawajatambua ya kwamba Ujenzi wa Dunia ni katika Malengo Makuu ya Dini zote, na kwamba Watu hawataiheshimu Dini yetu kama hatutafanikiwa katika Dunia yetu. Na tukifanikiwa katika Dunia yetu basi watu wataiheshimu Dini na Dunia yetu kisha akawarahisishia wale wasioutambua hivyo, Mawaidha kwa ajili ya tahadhari ya wazi kutokan na Dunia yao kwa kuwasababishia wengi katika Watu kuangukia katika Ufahamu wenye Makosa wa Uhusiano wa Dini na Dunia na Umuhimu wa kutumia njia za mafanikio, wakaelewa maana potofu ya kuupa nyongo Ulimwengu Kwamba eti ni kujitenga kabisa na Maisha, na huku wakiwa wameghafilika na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anayosema:

{رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ}

Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto

Hakika sisi tunasisitiza kwamba uthubutu wa kutoa Fatwa kwa wasio kuwa na sifa ya kufanya hivyo Kielimu ni upotofu na upotoshaji. Wingu ulioje wa Fatwa zilizotolewa bila ya Elimu na kusababisha madhara makubwa sana kwa Maisha ya watu. Kutoka kwa Jabir bin Abdillah R.A, amesema: Tulikuwa safarini na mmoja wetu akaumizwa na jiwe lililompiga kichwani na likamuumiza, kisha akaota ndoto ya kuingilia mwanamke, na akawauliza wenzake: Je mnaniruhusu nitayamamu? Wakasema: Hatuwezi kukuruhusu wakati Wewe una uwezo wa kuoga, basi mtu yule akaoga na akafa. Na tilipofika kwa Mtume S.A.W, tukamweleza juu ya tukio lile, na akasema: Wamemuua, na Mwenyezi Mungu atawaua. Kwanini wasiulize wasichokijua, kwani hakika mambo yalivyo, tiba ya ujinga ni kuuliza, ilimtosha mtu yule Kutayamamu na kukamua kidonda chake, au akafunga kitambaa juu ya jeraha lake kisha akapangusa juu yake na akaosha sehemu ya mwili iliyobakia. Haja iliyoje kwa kila mmoja wetu kufuata ubobezi wake, na ajitahidi katika yale anayoyaweza vizuri, kwa ajili ya kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa ajili ya kuiheshimu Elimu, na kwa kuijali hatari ya Neno. Ni maneno mangapi yaliyosemwa na mtu bila ya Elimu, na ikawa sababu ya uharibifu, maangamizi, na Ufisadi. Kwani kunyamaza ni bora zaidi kuliko kuzungumza maneno yanayosababisha madhara kuliko kunufaisha, na kama mtu asiyejua angenyamaza basi pasingelikuwapo hitilafu. Mtume wetu Muhammad S.A.W, anasema: …na anaemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Siku ya Mwisho basi na aseme maneno mazuri au anyamaze.

Ewe Mola wetu tunakuomba utuoneshe Ukweli na uturuzuku kuufuata, na utuoneshe batili na uturuzuku jinsi ya kujiepusha, na utufundishe mambo yanayotunufaisha na utunufaishe kwa uliyotufundisha, na utuzidishie Elimu, na uilinde nchi yetu na nchi zote Duniani.

 

 

 

Miongoni mwa Mifumo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Ulimwengu ni kutumia njia zinazounda Sababu

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Viumbe vyote anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ}

 Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na hana mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu msalie na marehemu na umbariki Bwana wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Na baada ya Utangulizi huu:

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameujaaoia Ulimwengu huu aina mbalimbali za mifumo na misingi inayouongoza Ulimwengu huu, na inayouendesha, hakuna kinachokitangulia kingine, kilicho mbele kiko mbele na kilicho nyuma kiko nyuma. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake Kitukufu:

 {لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ}

Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّهِ تَبْدِيلًا وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّهِ تَحْوِيلًا}

Basi hutapata mabadiliko katika mtindo wa Mwenyezi Mungu. Wala hutapata mageuko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameijaalia mifumo hii kuwa ni kama vipimo vya kupimia Misingi ya Maisha na kupitia mifumo hiyo Ulimwengu huu unajengeka na unalindwa kwayo, ambapo hili ni moja ya Malengo Makuu ya Kuumbwa kwetu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا}

Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا}

Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa.

Hakuna shaka yoyote kwamba Mataifa ambayo yameutambua ukweli wa mifumo hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufuna yakaifanyia kazi ipasavyo, yakefanikiwa kuongoza hata kama sio ya kiislamu, bali hata kama hayana Dini; kwani mifumo hii haimpendelei mtu yoyote na kukisifia kiumbe chochote.

Na katika Mifumo ya Mwenyezi Mungu ya Ulimwengu huu ni: kutumia njia au sababu za mafanikio; Mwenyezi Mungu Mtukufu ameziumba Sababu na visababishaji vyake, na akatuamrisha tuzitumie Sababu hizo, na  kwa hivyo, zinapopatikana sababu hizo  mafanikio nayo hupatikana. Na hii ni kanuni kuu inayofanya kazi katika Ulimwengu wote, wakati wowote na sehemu yoyote. Kila kitu kina sababu yake. Moto kwa mfano, ni sababu ya kuungua, na kuua ni sababu ya kifo, na kulima na kupanda mbegu ni sababu ya kulima, na kula ni sababu ya kushiba, na kufanya Kazi kwa juhudi na bidii ni sababu ya kufanikiwa, na uvivu, uzembe na upuuziaje ni sababu za kushindwa kuendelea. Na hivyo ndivyo ilivyo.

Hakika Amri ya kufanya juhudi Duniani na kufanya Kazi ni Faradhi katika Dini ya Uislamu. Na ni Wajibu wa Kisheria na wa Kitaifa. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu jambo hili:

{هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ}

Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّهِ وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}

Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.

Na hii ndio maana halisi ya Juhudi na Bidii na Jitihada, na Ujenzi wa Ardhi, katika Dini ya Uislamu. Hatuna hoja yoyote pale tunapoachwa nyuma kimaendeleo, chini ya Madai yoyote yasiyokuwa na uhusiano wowote na Dini yetu Tukufu. Hakika ukweli wa Miito hiyo ni ya uvivu na uzembe na kuachwa nyuma kimaendeleo.

Na mtu yoyote mwenye kuizingatia Sira ya Mitume na Watu wema, atakuta kuwa wao walijitahidi katika kuzitumia njia au sababu za mafanikio katika mambo yote ya Maisha yao. Tunamwona Mtume wetu Nuhu A.S, alikuwa fundi seremala, na baada ya umri mrefu wa kuwalingania Watu wake, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuamrisha atengeneze Meli. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ}

Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usinisemeze kuwatetea walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.

Na ilikuwa inawezekana kuokolewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa uwezo wake bila ya sababu au kazi yoyote, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuonesha na kutufundisha jinsi ya kutumia sababu, na Mtume Nuhu A.S, akaiitikia amri ya Mola wake Mlezi, na akawa anatengeneza Meli na wala hakuzembea hata kidogo ingawa watu wake walimdharau na kukebehi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلأٌ مِنْ قَوْمِهِ سَخِرُوا مِنْهُ قَالَ إِنْ تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنْكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ}

Na akawa anaunda jahazi, na kila wakipita wakuu wa kaumu yake wakimkejeli. Yeye akasema: Ikiwa nyinyi mnatukejeli na sisi tunakukejelini kama mnavyo tukejeli.

Na aliendelea na kazi yake na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamlipa kwa kukuokoa yeye na Waumini katika Watu wake. Na Mtume wetu Daudi A.S, alikuwa Mhunzi, alifundishwa kazi hiyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kazi ambayo athari na manufaa yake yanarejeakwake na kwa watu wake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ * أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ}

Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, (tukasema): Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia. Na tukamlainishia chuma

(Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayo yatenda.

Na anasema Mtume S.A.W: Hakuna Kamwe Mtu yoyote aliyekula chakula kilicho bora zaidi kuliko kula Mtu huyo kutokana na kazi ya mikono yake, na kwamba Mtume Daudi A.S, alikuwa anakula chakula kinachotokana na kazi ya mikono yake.

Na katika Kisa cha Nabii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Yusuf A.S, matumizi ya njia au sababu pamoja na mipango mizuri vilikuwa ndio sababu ya yeye kuiokoa nchi na watu kutokana na njaa inayoangamiza na hatari ya wazi iliyokuwa inawanyemelea. Mtume Yusufu A.S, alitumia njia au sababu na akauandaa mkakati wake mrefu ulioudurusiwa, kwa ajili ya kuiokoa nchi kutokana na njaa kali iliyoenea Duniani kwa wakati huo, na nchi yake ikajipatia utajiri na maisha Mazuri, ulinzi na nguvu za kiuchumi, na ikawapokea watu kutoka pande mbalimbali za Dunia ili wajipatie heri iliyomo Misri. Na Qurani Tukufu imetueleza hayo kupitia Ulimi wa Nabii Yusufu, katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِي سُنبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ * ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ * ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ}

Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Mtacho vuna kiwacheni katika mashuke yake, isipo kuwa kidogo mtacho kula. Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayo kula kile mlicho iwekea isipo kuwa kidogo mtacho kihifadhi. Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watasaidiwa, na watakamua.

Na tunamwona Bi Maryam A.S, aliyekuwa anajiwa na riziki nyingi kwa namna ya iliyomshangaza Nabii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Zakariya A.S, na akamwambia Bi Maryam, kama inavyotuambia Qurani Tukufu:

{كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّى لَكِ هَذَا قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ}

Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.

Na katika tukio jingine, pamoja na udhaifu wake na maumivu makali,  Bi Maryam anaamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, autikise ule mtende ili matunda yake yapate kumdondokea, na kama Mwenyezi Mungu Mtukufu angetaka Matunda hayo yadondoke bila ya Bi Maryam kufanya kitu chochote, basi angelifanya hivyo, lakini yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu, anatufundisha jinsi ya kuutumia njia au sababu na kujitahidi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا}

Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.

Anasema Mshairi:

Mtegemee Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kila kitu

Wala usipende kushindwa hata siku moja kumwomba

Je huoni asemavyo Mwenyezi Mungu kwa Bi Maryam

Na utikise mti huo ili ukudondoshe tende mbivu

Na kama Mungu, angelitaka Maryamu azipate bila kutikisa mti

Angelizichuma lakini kila kitu kina sababu yake.

Na Mtume wetu Karimu ametutolea mifano mizuri sana ya kutumia njia au sababu za kufanikisha mambo yetu, na hasa katika Hijra yake iliyobarikiwa ya kuelekea Madina, kwa namna ambayo aliufundisha Uma wake jinsi ya kuweka mikakati iliyopangwa kwa kina kwamba ni muhimu sana yanayoleta mafanikio, na kuivuka migogoro mbalimbali. Mtume S.A.W, aliandaa safari mbili, na akamteua Mwenza Mwaminifu, akapanga wakati na sehemu ya kutokea inayofaa, wakiondokea nyumbani kwa Abuu Bakar R.A, na akamchagua Mwongozaji mwenye umahiri mkubwa kwa Imani yake Mtume S.A.W, ya kuwatanguliza Wenye Elimu ya mambo, na kuwekeza katika Nishati, bila kujali tofauti za kifikra au mitazamo au hata Akida za watu. Kisha Mtume S.A.W, akampa Aamir bin Fuhairah R.A, jukumu la kufuatilia nyayo zao na kuzificha kama njia au sababu, huku akitambua fika kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mlezi kwake yeye na Mwenzake. Isipokuwa Mtume S.A.W, alikuwa anataka kutufundisha jinsi ya kutumia njia au sababu, kisha kumwachia jambo hilo Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha kwa ajili yangu na kwa ajili yenu.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na hana mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu msalie na marehemu na umbariki Bwana wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata mpaka siku ya Malipo..

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika matumizi ya Sababu au njia hayapingani na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakika mwenyekuujua ukweli wa kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu atajitahidi sana katika kuzitumia njia au sababu za mafanikio. Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu kweli kweli, ni yule anaye zitumia njia au sababu za kuleta mafanikio yake, akaitumia nishati aliyo nayo pamoja na juhudi pevu kisha naoirejesha suala lake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Muwafikishaji na Mwenye Fadhili na Msaada. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ}

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada

Katika utekelezaji wa maana ya Kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa vitendo, anasema Mtume S.A.W: Kama mngelimtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu ukweli wa kumtegemea, angelikuruzukuni kama anavyowaruzuku Ndege. Wao huruka wakiwa na njaa na hurejea hali ya kuwa matumbo yao yakiwa yamejaa.

Kwa kawaida ndege huwa hawalimbikizi chakula au maji, lakini pia wao sio wazembe wa kuhangaika na kuitafuta riziki yao. Wao huanza asubuhi na mapema, kuhangaika na kutoka na kutafuta riziki, na hurejea wakiwa wameruzukiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na fadhili zake, riziki inayowatosha. Kwa hiyo ndege hutoka na kurejea. Na jambo hili ni Silika na maumbile sambamba na harakati za maisha. Kama angelikuwa ana chakula cha kumtosha umri wake wote asingezembea na kuwa mvivu kwa kuomba dua tu, bali angeendelea na juhudi zake pamoja na utafutaji wa riziki yake kwa kutoka kila siku asubuhi.

Mtume S.A.W, alikua anajua Maana halisi ya kuzitumia sababu katika mambo yote na alikuwa anazuia uzembe na utegemezi ambao kwa kawaida unadhuru na hauna faida yoyote, na wala hatuzidishi tunaposema kwamba: Hakika sisi tunapata madhambi na tunajidhulumu sisi wenyewe na watoto wetu pale tunapoacha kuzitumia sababu za Maendeleo na maisha bora. Kwa hiyo Dini yetu ni Dini ya Elimu na Maisha bora na Ustaarabu na Uzuri na Manufaa kwa Watu wote. Kuna mtu mmoja alimwambia Mtume S.A.W: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Je mimi nimwache huru ngamia wangu na kisha nimtegemee Mwenyezi Mungu anilindie? Mtume S.A.W, akamwambia: Mfunge Mnyama wako kisha umtegemee Mwenyezi Mungu Mtukufu. Yule Mtu akamfunga Mnyama wake akiitumia njia au sababu ya kutompoteza Mnyama wake huyo, kwani kutomfunga ni jambo linaloweza kupelekea kuibiwa kwa mnyama huyo au kumpoteza.

Ewe Mwenyewe Mungu Mtukufu, tunakuomba utufanikishie Mambo yanayoifaa Dini yetu na kuwainua watu wetu na kuimarika kwa maendeleo ya nchi zetu na zote Duniani.

 

Haki za Wazazi Wawili na Ndugu

.

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَقَضَى رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا * وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا}

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu mjaalie rehma na amani na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Na baada ya Utangulizi huu:

Uilsamu umekuja kwa risala ya usamehevu, inayowalingania watu tabia njema, na kuwawekea misingi mizuri na kuwaongoza katika kila mwenendo ulionyooka, na kuyafanya maadili na ruwaza za hali ya juu kuwa ndio mfumo wa maisha, unaodhibiti kipimo cha kuishi pamoja baina ya watu wote, kwa uadilifu, huruma, upendo na utu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَى وَيَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ}

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.

Na miongoni mwa alama za Utukufu wa Uislamu ni kwamba wenyewe umeweka misingi na masharti na haki za kuwatendea wazazi wawili na ndugu; kwani wazazi wawili wana haki zaidi ya kuheshimiwa katika watu, na kuwajali na kuwatunza. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha katika Kitabu chake Kitukufu kuwatendea wema wazazi wawili, na kuwa mwema kwao, na Mwenyezi Mungu Mtukufu, akakusanya baina ya hili na amri ya kumwabudu yeye na kutomshirikisha na kitu chochote, ambapo anasema:

 {وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا  وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا}

Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili.

Kama ambavyo ameamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kumshukuru yeye kwa neema zake, na akaambatanisha kuwashukuru wazazi wawili na kumshukuru yeye, kutokana na fadhila zao na nafasi ya juu waliyonayo wazazi wawili, na kiwango cha juu cha uzito wao. Anasema Bwana wetu Abdullahi bin Abas R.A: Aya tatu zimeteremka zikiambatana na mambo matatu, hakuna chochote kinachokubaliwa bila ya kinachoambatana nacho, na miongoni mwa aya hizo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{أَنْ اُشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ}

(Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio.

Na yoyote atakayemshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akawa hajawashukuru wazazi wake, basi hatakubaliwa.uislamu umenyanyua juu heshima ya wazazi wawili na kuamrisha watendewe wema, na kulelewa vyema, na kuwa nao kwa upole. Kutoka kwa Abdullahi bin Amru R.A, anasema: Mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W, anamwomba idhini ya kwenda kupigana Jihadi. Mtume S.A.W, akamwambia: Je? Wazazi wako wako hai? Akasema: ndio. Basi kwao wao kapigane jihadi.

Na mabinti wawili wa Mtu Mwema katika Kisa cha Nabii Musa A.S, walikuwa ni mfano mzuri katika kumtendea wema na kumlea vyema baba yao. Kwani baba yao alikuwa Mtu mzima hajiwezi, na hana uwezo wa kufanya kazi, wao wawili wakawa wanafanya kazi badala ya baba yao, bila ya kunung’unika au kuchoshwa. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّى يُصْدِرَ الرِّعَاءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ}

Na alipo yafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta karibu yao wanawake wawili wanawazuia wanyama wao. Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao wachunga. Na baba yetu ni mzee sana.

Na kutoka kwa Jabir R.A, anasema: Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika mimi nina mali na watoto, na baba yangu anataka kuivamia mali yangu. Mtume S.A.W, akasema: Wewe pamoja na mali yako ni mali ya baba yako.

Na sisi tuna ruwaza njema kwa Bi Fatuma R.A, katika mapenzi yake, na heshima yake, na kuwa kwake mpole na baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, S.A.W; Bi Fatuma alikuwa Mtume S.A.W, anapoingia pale alipo, alikuwa Bi Fatuma akinyanyuka alipokaa, akambusu na kumkalisha baba yake pale alipokuwa ameketi yeye, kwa ajili ya kuwa mpole kwa baba yake na kwa furaha alio nayo, na pia kwa ajili ya kumpa cheo chake S.A.W.

Uislamu vile vile umetuamrisha tuwanyenyekee wazazi wawili na tusiwaudhi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا}

Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkataza Mwanadamu kusema hata neno dogo mno linaloashiria kukemea, hata kama ingekuwa kuna neno dogo kuliko neno “ah” basi Mwenyezi Mungu angelilizuia na kulikataza lisisemwe, kwa hivyo, ni bora kwa mtu kutosababisha maudhi kwa wazazi wawili, au kuwafanyia vitendo vibaya vya aina yoyote iwayo. Bwana wetu Abu Hurairah R.A, alimwambia mtu mmoja – alipokuwa akimpa mawaidha – Usitembee mbele ya Baba yako, na wala usikae kabla yake, na wala usimwite kwa jina lake, na wala usimsababishie kutukanwa. Kwani haifai kwa Mwislamu kuwasababishia wazazi wake maudhi ya aina yoyote. Anasema Bwana wetu Muhammad S.A.W: Hakika miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kuwalaani wazazi wake. Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, vipi mtu annawalaani wazazi wake? Akasema: Mtu anamtukana mtu mwingine, kasha mtu huyo aliyetukanwa, anamtukana baba yake, na Mtu anamtukani mtu mwingine mama yake, kasha aliyetukaniwa mama yake nay eye anamtukana mama yake.

Na Uislamu umeusia kuwatendea wema wazazi wawili na kuwa nao kwa wema, hata kama watakuwa kinyume na Uislamu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَى أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا}

Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat’ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani.

 وهذا ما كان من سيدنا إبراهيم (عليه السلام) في دعوته مع أبيه ،  وفي ذلك يقول الحق سبحانه:

Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Ibrahim A.S, katika kumlingania Baba yake, na katika hili, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا * إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا * يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا * يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَنِ عَصِيًّا * يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا}

Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii. Alipo mwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyo sikia, na visivyo ona, na visivyo kufaa chochote? Ewe baba yangu! Usimuabudu Shet’ani. Hakika Shet’ani ni mwenye kumuasi Mwingi wa Rehema. Ewe baba yangu! Hakika mimi naogopa isikupate adhabu inayo toka kwa Mwingi wa Rehema ukaja kuwa mwenziwe Shet’ani.

Tunaona kuwa Mtoto wa Abu Bakar R.A, Bi Asmaau binti Abu Bakar R.A, anajiwa na mama yake – akiwa mshirikina – anataka kuonana nae: Bi Asmaau akamuuliza Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mama yangu alinijia akitaka kuonana na mimi, je? Ni unge nae undugu? Mtume S.A.W, akasema: Ndio. Unga undugu na Mama yako.

Hakika wema kwa wazazi wawili una athari nyingi na una faida kubwa na fadhila nzuri anazozipata mja Duniani na Akhera; miongoni mwa faida hizo ni: Sababu ya kupata radhi za Mola wake. Amesema Mtume S.A.W: Radhi za Mwenyezi Mungu ziko katika Radhi za Wazazi wawili, na hasira za Mwenyezi Mungu ziko katika kuwakasirisha wazazi wawili.

Na miongoni mwa matunda hayo ni kwamba hii ni sababu ya kuondoshewa magumu na mazito. Mtume S.A.W, ametutajia kisa cha Watu watatu ambao mvua ilipelekea wakimbilie pangoni kwenye jabali. Na jiwe kubwa likaangukia kwenye mlango wa Pango hilo na likauziba. Wakasema: Hakika mambo yalivyo, hakuna wa kukuokoeni na hili jiwe isipokuwa kumwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mema katika Matendo yenu. Akasema mmoja wao: Ewe Mola wangu Mlezi, hakika mimi nilikuwa nina wazazi wangu wawili waliozeeka mno, na nina watoto wadogo na nilikuwa nikiwachungia wanyama, na nilikuwa ninapowaendea nilikamua maziwa, na nikaanza kwa kuwapa Wazazi wangu, nikawa ninawanywesha maziwa hayo kabla ya watoto wangu, na Siku moja mimi nilichelewa na sikwenda kwao isipokuwa baada ya kufikiwa na jioni nilienda na nikawakuta wamelala, na nikakamua maziwa kama kawaida na nikasimama upande wa kichwani kwao nikichelea kuwaamsha na nikawa ninachukia kuwanywesha watoto wangu huku watoto wakilia kutokana na njaa huku wakiwa miguuni kwangu mpaka alfajiri ikachomoza. Ewe Mola wangu Mlezi ikiwa mimi nilifanya hivyo kwa ajili kutafuta radhi zako, tunakuomba utufungulie hili jiwe kiasi cha kuiona mbingu. Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafungulia. Na wakaiona mbingu… hadi mwisho wa Hadithi. Kwa hiyo wema wake kwa wazazi wake ukawa ndio sababu ya kuondoshewa uzito na kuokoka kwake.

Na miongoni mwa matunda yake ni kwamba kuwatendea wema Wazazi wake ni kuwafanya watoto wake wamtendee yeye wema; kwani malipo hutokana na kazi iliyofanywa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alimzawadia Bwana wetu Ibrahim A.S, kwa Tabia zake njema kwa baba yake na kwa kumlingania kwake na kumtendea Wema, akajakutendewa wema na mwanae Ismail A.S. Na Qurani imetutajia hayo katika moja ya Sura za juu ya utiifu na Wema kwa Baba. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَى فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَى قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ}

Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

Kuwatendea wema Wazazi Wawili pia kuna matunda yake hapa hapa duniani, kwani huwa sababu ya kuleta furaha kwa Mwislamu na Kesho Akhera huwa sababu ya kuingizwa Peponi. Mtu mmoja alimjia Mtume S.A.W, akimwomba idhini ya kwenda kwenye Jihadi. Mtume S.A.W, akasema: Je wewe una mama? Akasema: Ndio. Mtume akamwambia: Basi endelea kuwa nae karibu kwani Pepo iko miguuni mwake. Na anasema Mtume S.A.W: Mzazi ni Mlango wa kati katika Milango ya Peponi, ukitaka basi ulinde mlango huo au upoteze. Na amesema Bin Omar R.A akimwambia mtu: Je Wewe unauogopa Moto na unapenda uingizwe Peponi? Akasema: ndio, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ninapenda. Je? Wazazi wako wako hai? Akasema: Nina mama. Akasema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, lau wewe ungeweza kuwa na kauli nzuri kwake, na ukamlisha chakula, basi hakika utaiingia Pepo iwapo utaendelea kujiepusha na Madhambi Makubwa.

Na sisi tunathibisha ya kwamba vyovyote vile mtu atakavyoweza kuwafanyia wazazi wake wawili katika wema basi hawezi kuwatoshelezea haki yao kamili na wala hawezi kuwalipa wema wao kwake. Anasema Mtume S.A.W: Mtoto hawezi kumlipa Mzazi wake isipokuwa labda akimkuta ni mtumwa akamnunua na kisha akwachoa huru.

Ninaisema kauli yangu hii, na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa Viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kuwa Hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, asiye na mshirika yoyote, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetuMuhammad, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu mswalie, mrehemu na umbariki Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila mwenye kuwafuata wao kwa wema mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu,

Uislamu umeusia juu ya Wazazi Wawili na Ukausia pia kuhusu Ndugu, nao ni wale ambao mtu ana mfungamano nao kiundugu, na akawawekea haki zao.

Kama ulivyousia juu ya wazazi wawili, Uislau umeusia pia juu ya ndugu. Na ndugu ni wale ambao mtu anakaribiana nao kiundugu. Mwenyezi Mungu amewawekea haki zao. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَى بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّهِ}

Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu

Na Mtume S.A.W, anasema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba Viumbe na alipomaliza kuviumba, Kizazi kilisimama na kikasema: Hii ni nafasi ya Kisimamo cha anayejikinga kwako kutokana na kuukata undugu, akasema: Ndio. Je wewe huridhiki mimi nikakuunganisha na aliyekuunga wewe na nikamkata aliyekukata wewe? Kizazi kikasema: Ndio. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi nimekupa Jambo hilo. Kisha Mtume S.A.W, akasema: Mkipenda isomeni aya hii:

 {فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ * أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ}

Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mfanye ufisadi katika nchi a mwatupe ndugu zenu? Hao ndio Mwenyezi Mungu aliowalaani, na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao.

Na anasema Mtume S.A.W: Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

Mimi ni Mwenyezi Mungu, na Mimi ni Rahmani, nimekiumba kizazi na nikakipa jina kutoka katika Majina  yangu, na yoyote atakaeunga undugu na mimi nitamuunga yeye, na atakaeukata undugu na mimi nitamkata.

Na kuunga undugu kinapatikana kwa kuwatembelea, na kuzijua hali zao, na kuwasaidia. Anasema Mtume S.A.W: Sadaka kwa Masikini ni Sadaka, na kwa ndugu ni maradufu; kuunga undugu ni Sadaka. Vilevile hupatikana kwa kuukubali mwaliko wao, na kumtembelea mgonjwa wao na kuhudhuria mazishi yao na pia kumuheshimu mkubwa wao na kumhurumia mdogo wao, na kusalimika na kuwa na nia njema kwa ajili yao, na kuwaombea dua.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia kuunga undugu kama ni sababu ya baraka katika Umri, na Ongezeko la riziki ambapo anasema Mtume wetu S.A.W: Anaependa kuongezewa Umri wake au aongezewe riziki yake basi awetendee wema Wazazi wake na aunge undugu.

Mtume S.A.W, ametuambia kwamba kuunga undugu ni sababu ya kusamehewa madhambi. Mtu mmoja alimjia Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakika mimi nimefanya dhambi kubwa, je ninaweza kutubu? Mtume S.A.W, akamwambia: Je wewe una mama? Akasema: Hapana. Sina mama. Mtume akasema: Je wewe una Mama mdogo? Akasema yule Mtu: Ndio. Ninae Mama mdogo. Mtume akasema: basi mtendee wema.

     Kila mtu anapaswa kujihadhari na kukata undugu na asilipe ovu kwa ovu, bali asamehe na alipuuzie ovu alitendewa. Anasema Mtume S.A.W: Mwenye kuunga Undugu sio mtoa zawadi lakini muunga Undugu ni yule ambaye undugu wake unapokatika yeye huuunga.

Mtu mmoja alimjia Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika mimi nina ndugu huwa ninawaunga na wao hunikata, na huwatendea wema na wao hunitendea mabaya, mimi ninawajali na wao hawanijali. Mtume S.A.W, akasema: Ukiendelea kuwa kama ulivyo basi utakuwa kama vile umewamwagia majivu nyusoni mwao na Mwenyezi Mungu Mtukufu ataendelea kukunusuru kama utaendelea kufanya hivyo.

Uislamu umekataza kuukata undugu na ukatoa onyo kali juu ya mwisho wake mbaya Duniani na Akhera, ambapo anasema Mtume S.A.W: hakuna dhambi mbaya inayomfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe kutoa adhabu kwa muhusika hapa hapa Duniani, pamoja na adhabu anayomwekea Akhera kuliko dhuluma na kukata undugu. Na anasema Mtume S.A.W: Haingii Peponi mtu mwenye kuukata undugu.

Tumche Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Wazazi wetu wawili, na tuunge undugu na tuwafanyie wema Watu wote.

Ewe Mola wetu Mlezi tuwafikishe katika kuwatendea wema wazazi wetu, na utujaalie tuwe ni wenye kuunganisha Undugu wetu, na uwalinde Watu wetu, na uijaalie Nchi yetu iwe na Amani, Utajiri na Maisha bora, salama Amani, pamoja na Nchi zote Duniani.