:

Sababu za Wazi na za Siri za kuondoshewa Janga, na Ulazima wa kumtii Kiongozi wa Nchi

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{رَبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ}

Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume Wetu Muhammad S.A.W, Ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata kwa Wema, mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu,

Kupatwa na Majanga ni katika alama za utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Waja wake, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا}.

Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.

Na katika kuondosha janga lolote, Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia uwepo wa sababu za Wazi na za Siri; Sababu za Wazi ambazo lazima zitumike kwa Kiwango cha Juu, ni kama vile – kutumia kitu chochote – nazo ni sababu za Sayansi na aina za tahadhari zinazotolewa na wataalamu bobezi pamoja na utekelezaji wa maagizo yanayotolewa na taasisi rasmi za Dola. Na kumtii Kiongozi wa Nchi na yule anaempa majukumu, au anakaimu kazi zake kupitia taasisi mbalimbali za Dola, kumtii ni jambo la lazima. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَأَطِيعُوا اللهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الأَمْرِ مِنْكُمْ}

 Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَاسْئَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لا تَعْلَمُونَ}

Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.

Na wenye elimu hapa ni wale waliobobea katika kila nyanja; na kwa hivyo ni lazima kisheria kutoiingilia taasisi yoyote miongoni mwa taasisi za Dola katika nyanja zake.

Na miongoni mwa sababu hizo za Wazi ni: kujihimiza na Usafi. Uislamu unasisitiza sana Usafi kwa ujumla, na unaufanya Usafi huo kuwa ni jambo la dharura kisheria kwa ajili ya kumlinda Binadamu kutokana na maradhi mbalimbali na madhara. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}

Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.

Na Mtume Wetu S.A.W, anasema: Usafi ni Nusu ya Imani…

Na anasema Mtume Wetu S.A.W: Visafisheni viwanja vyenu. Na hapa vinakusudiwa viwanja vya nyumbani, Shuleni, Viwandani, Barabarani, na Maeneo ya umma ya wazi, na kadhalika. Uislamu vile vile unahimiza sana kuosha mikono kwa kuipa kinga maalumu kila unapowadia wakati wa kutawadha. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا}

Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni.

Kwa hiyo kuosha mikono miwili pamoja na vifungo viwili ni moja ya faradhi za Udhu, ukiongezea na kuwa inasuniwa kuanza kutawadha kwa kuosha mikono miwili mara tatu kisha kunafuatiwa na kusukutua Kisha kuvuta maji puani na kisha kuosha uso. Baada ya hapo ni kuosha mikono kwa mara nyingine pamoja na vifundo viwili kwa kuzingatia kuwa ni faradhi. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Pindi anapoamka mmoja wenu kutoka Usingizini basi asiuingize mkono wake katika chombo isipokuwa mpaka atakapouosha mara tatu.

Vilevile ni Sunna kuosha mikono kabla ya kula na baada ya kula; na katika kufanya hivyo kuna uthibitisho mkubwa wa kwamba hakuna ukinzani baina ya Elimu na Dini. Kuilinda Afya ya Mtu ni katika malengo yenyewe ya Dini zote za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Hakuna kujidhuru au kuwadhuru wengine.

Kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu kuchukua hatua za kinga zitakazozuia kuenea magonjwa na majanga au magonjwa ya mlipuko. Na kwa ajili hiyo, kuna kuzuiliwa kukumbatiana, na kubusu, na kupunguza kupeana mikono pamoja na kujitenga na mikusanyiko ya Watu.

Na tunathibitisha ya kwamba Migogoro na Hali tete ndivyo vinavyofichua tabia za Watu na Uhalisia wao wa Maadili. Kwa hiyo sisi sote tunapaswa tuhurumiane na tujiepushe kwa kila njia na kujipendelea na uchoyo, na kila aina za ulanguzi na magendo katika biashara kwa lengo la kuongeza bei za bidhaa husika, au Shari ya Mtu katika kununua na U ndani yake kwa upande wa mnunuzi, kwa namna ambayo inapindisha uuwiano mahitaji ya soko na kiwango cha bidhaa. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Halangui isipokuwa mkosa. Na kulangua ni kufanya magendo. Na anasema Mtume Wetu S.A.W: Mlanguzi amelaaniwa.

Na anasema Mtume Wetu S.A.W: Hawi mmoja wenu muumini wa kweli mpaka ampendelee nduguye kile anachokipendelea kwa nafsi yake.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee asiye na mshirika wake na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume Wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na watakaowafuata kwa wema.

Ndugu zangu Waislamu,

Tukiziangalia sasa sababu za siri ambazo kila mmoja wetu anapaswa daima azingatie, ni kama vile: Uzuri wa Kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 }فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ{،

 …basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.

Na Kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu hakupingani na utumiaji wa sababu. Mtu mmoja mmoja alimwambia Mttum S.A.W, Ewe Mtume Wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, je mimi nimfunge kamba mnyama wangu na kisha nimtegemee Mwenyezi Mungu Mtukufu au nimwache huru kisha nimtegemee Mwenyezi Mungu Mtukufu? Mtume S.A.W, akamjibu na akamwambia: Mfunge kamba na umtrgemee Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kwa hiyo ni wajibu kwetu na hasa katika zama zetu hizi, tutumie sababu za kutuweka katika Afya njema, na hatua za kujikinga kielimu kunakozingatiwa, kisha yulirejeshe jambo letu lote kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye katika mikono yake kuna uwezo wa kufanya kitu chochote, na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunamtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu ipasavyo na tutakuwa tumejiweka mbali na uzembe.

Na miongoni mwa sababu za Siri ni: Dua na Unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا}

Kwa nini wasinyenyekee ilipo wafika adhabu yetu?

Haja iliyoje Kwetu ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ukweli ili atuondoshee janga katika nchi yetu na Watu wake pamoja na Watu wote Duniani! Na hii iwe ni fursa kwa kila mmoja wetu auangalie uhusiano wake na Mola Wake.

Na miongoni mwa sababu hizo za Siri ni: Mtu kujiwekea ngao kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Hakuna Mja yoyote atakayesema asubuhi ya kila siku na jioni ya kila usiku: Bismillahi ladhii laa yadhurru maa ismihi shaiun fil-ardhi walaa fi-Samaai wahuwa Samiiul Aliim.

بِسْمِ اللهِ الَّذي لا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الأَرْضِ وَلا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ العَلِيمُ.

Aseme hivyo Mara tatu tatu halafu kitu chochote kimdhuru.

Na anasema Mtume Wetu S.A.W: Mtu yoyote atakayefika nyumbani kwake, kisha akasema: Auudhu bikalimaati llaahi Taamat min Sharri maa khalaqa.

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ.

Basi hakitamdhuru Mtu huyo kitu chochote mpaka aondoke nyumbani kwake.

Na miongoni mwa sababu za Siri: anasema Mtume S.A.W: Ziwekeeni kinga Mali zenu kwa kutoa Sadaka, na waponyeni wagonjwa wenu kwa kutoa sadaka, na jiandaeni kwa Dua mnapofikwa na janga lolote.

Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba utujaalie afya njema tuwe miongoni mwa uliowajaalia afya, na tunakuomba utuongoze katika mambo yetu na utukinge na shari ya yale uliokwisha yaamua na Uilinde Nchi yetu na nchi zote za Waislamu Duniani.

Katika makaribisho ya Suratul Israa

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote ambaye  alimchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali. Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume Wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo. Na baada ya Utangulizi huu,

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiunga mkono Mitume yake A.S, kwa Miujiza, na miongoni mwa Miujiza hiyo: Ni ule Muujiza wa Israa na Miiraji kwa Mtume Wetu Muhammad A.S.W, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آَيَاتِنَا إِنَّه هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ}.

 Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Na yoyote atakaezingatia akilini mwake Muujiza huu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuta kuwa unabeba mafunzo mengi, na katika hayo ni:

Kuubainisha Uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu usio na mipaka, kwani Utashi wake hauendani na kanuni zozote za Sababu, na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَنْ يَقُولَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ}.

Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. 

Na miongoni mwake ni:  Wepesi baada ya Ugumu na Faraja baada ya Dhiki, na baada ya kuvumilia Mtume S.A.W, aina mbalimbali za maudhi ya Washirikina, akiwa katika njia ya Ulinganiaji na Ufikishaji wa Risala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ukaja Muujiza wa Israa na Miiraji kama ni kumkirimu na kumuunga mkono Mtume S.A.W, na ni Kigezo cha kumfariji Mtume baada ya kuwa na Mazito, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا *إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا}.

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi, Hakika pamoja na uzito upo wepesi.

Na miongoni mwake ni: Utukufu wa Cheo cha Uja, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَأَوْحَى إِلَى عَبْدِهِ مَا أَوْحَى}

Na  (Mwenyezi Mungu) akamfunulia mja wake alicho mfunulia.

Kwa hiyo, Uja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Utukufu na Heshima nalo ni lengo lake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Waja wake, na Risala ya Manabii wote.

Na miongoni mwake ni: Ubainifu wa Nafasi ya Msikiti wa Wasaa, kwani huko ndiko alikopelekwa Mtume S.A.W, na huko ndiko alikopandishwia Mbinguni katika Miiraji, na Msikiti huo ni moja ya Kibla mbili za Waislamu, na ni wa Tatu kwa Utukufu baada ya wa Makkah na wa Madina. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape msimamo wenye kuulinda Msikiti huo na aurejeshe kwa Waislamu kwa Wema.

Na miongoni mwake ni: Utukufu wa Cheo cha Sala, na ubainifu wa Fadhila zake na sifa zake maalumu, kwani Mtume Wetu S.A.W, alipopelekwa alifikishwa mpaka katika Eneo la Sidtstul Muntahaa; kwenye umbingu wa Sita… na akapewa mambo matatu: Sala tano, Aya za mwisho wa Suratul Baqarah, na kusamehewa kwa yule atakayekufa katika Umma wake bila kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na chochote.

Na miongoni mwake ni: Kubainisha Mafungamano ya pamoja baina ya Dini za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo anasema Mtume Wetu S.A.W: … Manabii ni ndugu wa baba mmoja mama mbalimbali na Dini yao ni moja. Na hakika Mitume na Manabii wote walikusanyika Usiku wa Israa na Miiraji na Mtume S.A.W, akawasilisha kama imamu wao na wakamkarobisha na kumwombea dua kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na miongoni mwake ni: Kutumia sababu au njia za kufanikiwa. Mtume S.A.W, alipowasili Baitul Maqdis alimfunga kamba mnyama wake ajulikanaye kwa jina la Buraqu. Anasema Mtume S.A.W: Nikamfunga mnyama yule pale wanapowafungia Mitume Wanyama wao.

Na miongoni mwake ni: Humtofautisha mtu mwenye Imani ya kweli na yule asiye na Imani ya kweli.

Walipomwambia Bwana Wetu Abu Bakari Swiddiiq R.A: Hivi unazionaje habari za rafiki yako? Yeye anadai kuwa eti alipelekwa Usiku huko Baitul Muqadas? Abu Bakari Swiddiiq Akasema: Je ni yeye ndiye aliyesema hivyo? Wakasema: Ndio. Akasema: ikiwa yeye ndiye aliyesema hivyo basi hakika amesema kweli. Wakasema: Je wewe unamwamini kuwa yeye alipelekwa Baitul Muqadas usiku, na akarejea kabla hapajakucha? Akasema: Ndio. Hakika mimi ninamwamini katika yale yaliyo zaidi ya hayo; Ninamwamini kwa Wahyi wa Mbinguni nyakati za mchana na jioni. Na kwa ajili hiyo, akaitwa Abu Bakari Swiddiiq.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote na rehma na amani zimfikie Mtume Wetu ambaye ni mwisho wa Mitume wote: Bwana Wetu Muhammad na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na wafuasi wake.

Ama baada ya Utangulizi huu:

Ndugu zangu Waislamu,

 Suratul Israa imeizungumzia safari hii ya Mtume Wetu S.A.W, iliyobarikiwa na imezungumzia jinsi ya kuwatendea wema wazazi wawili kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَقَضَى رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا}

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa mama nafasi kubwa zaidi kutokana na kazi yake kubwa pamoja na uvumilivu wake wa kubeba ujauzito, kunyonyesha na kulea. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَوَصَّيْنَا الانسَـانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّه وَهْنًا عَلَى وَهْنٍ}

Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu…

Na Mtu mmoja alipomuuliza Mtume Wetu S.A: Ni nani mwenye haki zaidi kwangu mimi katika Watu katika kumtendea Wema? Mtume akasema: Ni Mama yako. Akauliza yule Mtu: Kisha nani? Mtume akasema: Kisha mama yako. Akauliza tena Mtu: Kisha nani? Mtume akamwambia: Kisha mama yako. Akauliza tena kisha nani? Mtume S.A.W, akasema kisha baba yako.

Na Sheria tukufu imeujaalia wema kwa wazazi wawili kama ni moja ya sababu muhimu sana za kujipatia radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtu mmoja alimwendea Mtume Wetu S.A.W, kwa ajili ya kumwomba idhini ya kwenda kupigana Jihadi. Mtume S.A.W, akamuuliza: Je, mama yako yuko hai? Akasema: ndio. Mtume akamwambia: Rejea nyumbani ukamtendee Wema. Alipotaka kuendelea kumuuliza swali hilo hilo, Mtume S.A.W, akamwambia: Ole wako, ushike mguu wake kwani mguu wake ni Pepo.

Na kumtendea wema mama ni kumkirimu na kumfurahisha. Na Wema huo kwa mama unaendelea baada ya kufariki kwake Dunia, kwa Dua na kumwombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na pia kumtolea sadaka pamoja na kuwatendea wema wale anaowapenda. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Hakika Wema ulio na hadhi ya juu zaidi ni Mtoto kuwaunga vipenzi vya Baba yake.

Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu tunakuomba utujaalie msimamo katika Dini yako, na uwalinde wazazi Wetu na Nchi yetu, na Nchi zote .