:

Nini kifanyike baada ya Hija?

     Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ}

Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.

Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, peke yake asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana Wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mswalie, marehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila mwenyekuufuata mwongozo wake kwa wema mpaka siku ya mwisho.

Na baada ya Utangulizi huu.

Hakika mzingativu wa sunna ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika uumbaji wake, ataona kasi ya kutoweka kwa masiku na miezi na Miaka. Masiku yenda na miaka inapita, na Maisha ya Duniani si lolote isipokuwa pumzi chake zenyekuhesabika, na nyakati finyu, na katika hili kuna mazingatio kwa atakayeangalia na kufikiri na kuwaidhika.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِمَنْ أَرَادَ أَنْ يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا}

Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anaye taka kukumbuka, au anaye taka kushukuru.

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anafuta madhambi kwa Hija njema, na mwenyekuhiji anareja akiwa kama siku aliyezaliwa na mama yake mzazi, ambapo Mtume S.A.W anasema: yoyote atakaye hiji na akawa hakutoa maneno machafu na hakufanya vitendo viovu basi atarejea kama siku aliyozaliwa na mama yake. Kwa hiyo, ni juu ya  mwenye akili kuzitumia fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake, akaachana na maasi yote yaliyobakia na anamwelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa moyo safi na nina njema ya kiwango kikubwa. Na mwenyekuhiji analazimika kuihisi neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake yeye, kwa kumuwafikisha akaitekeleza ibada hii ya Hija. Na atambue kwamba hilo linawajibisha kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kudumisha kazi njema. Kwani aina zote za utiifu wa Mja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hauna muda maalumu, au sehemu maalumu bali huendelea daima muda wote wa kuendelea kuwepo maisha ya mwanadamu na kufikia Masharti ya kupewa majukumu. Na hivyo ndivyo Mtume S.A.W alivyokuwa akifanya. Kwa hiyo, kudumisha ibada na aina mbalimbali za Utiifu ni utekelezaji wa tamko lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ}

Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.

Na katika utekelezaji wa Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{ فَإِذَا فَرَغْتَ فَانْصَبْ *وَإِلَى رَبِّكَ فَارْغَبْ}

Na ukipata faragha, fanya juhudi.Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.

Kwa maana ya kwamba: unapomaliza ibada na utiifu wa Mwenyezi, basi jishughulishe na Utiifu wa Mwenyezi Mungu. Wewe jishughulishe Kumtii yeye pamoja na ibada nyingine kwa kukusudia kwa ibada hizo, radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kudumisha kazi mbalimbali njema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni katika matendo ayapendayo Mwenyezi Mungu, na dalili mwisho mzuri. Na kutoka kwa Aisha R.A, alisema: Mtume S.A.W aliulizwa: Ni kazi gani ambayo inampendeza zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema ni ile yenyekudumu hata kama itakuwa kidogo. Pongezi nyingi kwa yule aliyefanikishiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kumtii yeye, na akaboresha matendo yake, na akajiweka vizuri yeye mwenyewe, na akapupia katika kuwakidhia watu haja zao, na kuwaondoshea mazito walo nayo na akaeneza Kheri katika Jamii yake na Nchi yake.

Na ikiwa muumini amewafikishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuitekeleza ibada ya Faradhi ya Hija, basi huo sio mwisho wa aina mbalimbali za utiifu bali ana mtu huyu mengi miongoni mwa matendo mema ambayo kwayo huyatumia kwa ajili ya kujisogeza Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile kuzidisha ibada na swala za Sunna; kama vile kuswali na kufunga na kuyahangaikia maslahi ya waja na Nchi pia na kuwalea mayatima, kuwatembelea wagonjwa, na nyingine nyingi ambazo humnyanyua mtu daraja na hadhi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kutoka kwa Abu Huraira R.A, Amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, S.A.W:  Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: …na hanikurubii mja wangu kwa chochote nikipendacho mno miongoni mwa nilivyomfaradhishia na akawa anaendelea mja huyu kunikurubia kwa Swala za Sunna mpaka nikampenda, na ninapompenda basi mimi huwa ndio sikio lake analosikilizia, macho yake anayoonea, mkono wake anayoutumia na mguu wake anaoutembelea. Na iwapo ataniomba kitu basi nitampa. Na lau angelitaka mimi nimuepushe na jambo lolote basi ningelimuepusha nalo.

Mwenyekuhiji pia anapaswa kuonesha athari nzuri za hija yake latika uzuri wa tabia zake, na Usamehevu wake katika kutangamana na Watu. Na hii ni miongoni mwa alama za kukubalika kwa Hija yake. Anawatendea Watu tabia njema na kutangamana nao kwa Wema, na anajirekebisha kasoro zake alizokuwa nazo kabla ya kuhiji, kwa kuonekana katika mienendo yake kwa Watu wake, kama Baba, Mama, Mke, Mtoto, na yoyote aliye na undugu naye, lakini pia na aina nyingine za Wema kwa Watu wote.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {لَيْسَ الْبِرَّ أَنْ تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَى حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ أُولَئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ }

Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.

Hija lazima iache athari njema za kimaadili katika mwenendo wa aliyehiji. Hija sio vitendo vya inada vinavyotekelezwa tu bila ya uwepo wa lengo na upeo wake, bali ni ibada iliyofaradhishwa ili impandishe daraja binadamu na tabia zake ziboreke. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {الْحَجُّ أَشْهُرٌ معْلُومَاتٌ فَمَنْ فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّهُ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى وَاتَّقُونِ يَاأُولِي الْأَلْبَابِ}

Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!

Na anasema Mtume S.A.W: Atakaeijia Nyumba hii akawa hakutoa maneno machafu na hakufanya maovu, atarejea akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.

Hasani l Basrii aliambiwa: Hija nzuri Malipo yake ni Pepo. Akasema: Alama yake ni mtu kurejea akiwa emeupa nyongo ulimwengu, mwenye utashi wa Pepo. Na akaambiwa: Malipo ya Hija ni Msamaha.akasema: Alama yake ni kuacha ovu alilokuwa nalo katika matendo yake.

Kwa hiyo ibada kama haiathiri Tabia ya mtu na kumfunza Maadili, basi haina faida yoyote hapa Duniani na hata kesho Akhera. Anasema Mtume wetu S.A.W: Je? Mnamjua ni nani aliyefilisika? Wakasema Maswahaba: Aliyefilisika kwetu sisi Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni yule asiye na fedha au mali yoyote.  Mtume akasema: Aliyefilisika katika Umma wangu ni yule ambaye atakuja siku ya Kiama akiwa na swala zake, na funga zake, na zaka zake, na akaja hali ya kuwa amemtusi huyu, amemtuhumu uzinzi yule, amekulia mali ya huyu, amemwaga damu ya yule, amempiga huyu, atakaa chini kisha huyu akapunguza katika mema yake, na yule katika mema yake, na iwapo Mema yake yatakwisha basi atabebeshwa makosa ya wale aliyowadhulumu kisha kutupiwa yeye na kutupwa motoni. Mtume S.A.W aliulizwa. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Hakika fulani anatajwa sana kwa wingi wa swala zake, funga zake, na Sadaka zake, isipokuwa anamuudhi jirani yake kwa maneno yake. Akasema: Huyo ataingia Motoni. Akaulizwa tena: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika fulani anatajwa kuwa na uchache wa funga yake, Sadaka zake, na Swala zake.na kwamba yeye hutoa sadaka za kila aina na hamuudhi jirani yake kwa ulimi wake. Mtume S.A.W akasema: Huyo ataingia Peponi.

Na katika mambo ambayo mja anapaswa kuyapupia ni mwisho mwema. Na Uhakika wake: ni Kuwafikishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kabla ya kufa kwa kuepushwa na yale yanayochukiza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamrahisishia njia za toba kutokana na madhambi na maasi aliyoyafanya na kuelekea katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na matendo mema, kisha baada ya hapo, mauti yake yatakuwa katika hali nzuri.

Kwa kuwa mwanadamu hapa duniani anaambatanishwa na vitendo vyake, basi kuwafikishwa kwake katika kutenda mema na kudumu nayo mpaka umauti umkute ni katika alama za mwisho mwema. Kama alivyotuambia Mtume S.A.W: Hakika mambo yalivyo zingatio la Matendo ni mwisho wake. Na katika Mapokezi mengine: Hakika ya Matendo ni kama chombo, kinapokuwa kizuri chini yake huwa kizuri juu yake, na kinapoharibika chini yake huharibika pia juu yake. Kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu ajitahidi kuuboresha mwisho wake na ajiandae kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa matendo Mema.

Kama inavyotuelekeza Qurani Tukufu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلاً صَالِحًا وَلاَ يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا}

Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.

Na atakayemcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akazitii amri zakena kuyaacha aliyoyakataza, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwafikisha katika kutenda mema na kisha akamfisha akiwa katika mema hayo. Kama alivyobainisha Mtume S.A.W kwa kauli yake: Mwenyezi Mungu Mtukufu anapomtakia mja wake Kheri basi humtumia. Pakasemwa: anamtumiaje ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema: Humuafikisha katika kutenda mema kabla ya kufa kwake. Na katika Mapokezi mengine: Mwenyezi Mungu Mtukufu anapomtakia mja wake Kheri basi humpa ladha. Pakasemwa: Naana yake? Akasema S.A.W: Mwenyezi Mungu Mtukufu anamfungulia matendo Mema kabla ya kufa kwake, kisha anamfisha katika hali hiyo. Kwa hiyo zingatio hapo ni katika Matendo ya Mja na Mwisho wake. Na yule atakaye wafikishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Utiifu na Ibada na kudumu katika kufanya mema basi atamwandalia mwisho mwema na atakuwa miongoni mwa wenye furaha na waliofanikiwa kuipata Pepo.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ}

Na ama wale walio bahatika, wao watakuwamo Peponi wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisicho na ukomo.

Na katika mafunzo yanayopatikana katika Hija, ni iwe ni aliyehiji au asiyehiji, ni kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kufuata njia za riziki, na mtu kuamini kwamba kila kitu ni cha kuachiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba kadari yake ipo na haikwepeki.

Ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلالا مُّبِينًا}

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {مَّا يَفْتَحِ اللَّهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ}

Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana wa kuipeleka isipo kuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ  وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ}

Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea hayo ila Yeye. Na ikiwa akikugusisha kheri, basi Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu. Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake, na ndiye Mwenye hekima na Mwenye khabari zote.

Kwa hiyo, kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni katika dalili za Imani, na hilo ni katika mambo thabiti ya Uislamu. Na ili hayo yafanikiwe lazima mja mdhanie vyema Mola wake Mlezi. Atakaporidhika na Majaaliwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na akajisalimisha kwake, basi kwa hakika ataneemeka na ridhaa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na atauhisi Utulivu na Usalama.

Ninaisema kauli yangu hii na ninajiombea na kukuombeeni nyinyi Msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

*        *        *

     Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, peke yake asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana Wetu na Mtume Wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake, ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mswalie, mrehemu, na umbariki, yeye pamoja na Jamaa zake, na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu Waislamu:

      Aliyehiji amesharejea kutoka katika Ibada yake ya Hija kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa amesamehewa dhambi zake zote, juhudi zake zikiwa zimepokelewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akiwa amelipwa kwa kazi yake na kwa hivyo, anatakiwa ajihadhari kwa nguvu zake zote asije akadanganyika kwa kusifiwa  na Watu. Kwani Hija sio sifa anayoipata Mja wala sio sababu ya kujifakharisha na kutambiana baina ya watu, bali mtu aliyehiji baada ya kurejea kwake, anapaswa awe mnyenyekevu na mwenye moyo wa woga. Hija ni faradhi iliyo tukufu aliyoikadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu, Hija ina thawabu nyingi. Atakayeitekeleza Ibada hii, na akavumilia tabu zake basi ataipata ladha yake katika moyo wake na athari yake itaonekana katika Maisha yake kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu na ataonja ladha yake kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Haingizi kiburi ndani ya nafsi yake, wala utiifu wake haukinzani na kujidanganya kwake. Hakuna utiifu wowote anaoutekeleza mja muumini kwa nia safi na ya kweli isipokuwa humpelekea katika utiifu mwingine wa juu zaidi, na Ibada ya juu zaidi na ataendelea kupanda daraja za juu za ibada na kutoka katika utiifu kuelekea katika mwingine, mpaka akakifikia kiwango cha Wema. Na hii ni miongoni mwa alama za Utiifu.

Na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu asemaye kweli, amesema kwamba watu wa imani wanaoharakisha kuelekea katika mambo ya Kheri huwa wanasimama kisimamo cha mtu mwenye kuogopa kutokubaliwa matendo yake mema, na kutarajia pamoja na kuwa na tamaa ya kupokelewa kwa Matendo hayo na kupata thawabu zake.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {إِنَّ الَّذِينَ هُمْ مِنْ خَشْيَةِ رَبِّهِمْ مُشْفِقُونَ * وَالَّذِينَ هُمْ بِآيَاتِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ *وَالَّذِينَ هُمْ بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُونَ * وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوْا وَقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَى رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ* أُولَئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ}

Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea, Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini, Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi, Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi,Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.

Anasema Ibnu Kathiir Mwenyezi Mungu amrehemu: kwa maana kwamba wao pamoja na wema wao na Imani yao na matendo yao mema wanahuruma kutokana kwake na wanamuogopa Mwenyezi Mungu, wanaogopa hali zao zisije zikabadilika. Na kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R.A, amesema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

 {والَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوْا وَقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَى رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ}

Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi,

Huyu ni yule anaeiba, anazini, anakunywa pombe, na anamuogopa Mwenyezi Mungu? Akasema: Hapana ewe Bintiye Abu Bakar. Bali ni yule ambaye anaswali, na anafunga, na anatoa sadaka, na huku yeye anamcha Mwenyezi Mungu Mtukufu

Muumini wa kweli hajali wingi wa ibada na Swala za Sunna kwa kiasi ambacho anajali kukubaliwa na kutokukubaliwa kwa amali zake na kwa kiasi kinachoonekana katika maisha yake kutokana na Ibada hizo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amemwamrisha Mtume wake S.A.W, kuhangaika na kujitahidi katika Kumtii. Basi asiidogeshe kazi yoyote na akaiacha na wala asizidishe kazi yoyote mpaka ikamshangaza, na Mtume S.A.W ametuambia kuwa kushangazwa huko ni katika yaangamizayo na kuyaporomosha Matendo yetu. Kutoka kwa Ibnu Abas R.A, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Yaangamizayo ni matatu: Mtu kuhadaika na nafsi yake, na Mchoyo anaenyenyekewa, na mwenye Matamanio akawa mfua

Ewe Mola wetu tusaidie sisi katika kukutaja wewe na kushukuru na tuwe waja wako wema, na utuwafikishe katika msimamo wa njia ya kukutii na kufanya Ibada

 

Tunayojifunza kutokana na Hotuba ya Kuaga ya Mtume S.A.W.

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote, asemaye katika Kitabu chake Kitukufu:

{الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الإِسْلامَ دِينًا}

Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume Wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu mswalie, mrehemu na umbariki Mtume Wetu na Jamaa zake, na Maswahaba wake na kila mwenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakika mwenyezi Mungu Mtukufu amemtuma Mtume wake S.A.W, kwa Uongofu ili awatoe Watu katika giza na kuwapeleka katika vyao mwanga na awachukue kwa nywele zao za mbele ya vichwa vyao kutoka katika upotofu na kuelekea katika uongofu na anawapitisha katika njia ya Uokovu na Furaha Duniani na Akhera. Mtume S.A.W ameyalingania Maadili bora na Ruwaza ya hadhi ya juu, na ameufikisha Ujumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika sura ya ukamilifu wake na iliyotimia, na akawa katika zama za Uhai wake anaweka misingi imara ya kibinadamu kwa maneno yake, vitendo vyake na upitishaji wake wa yale anayoyaona kuwa yanafaa

   

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomuidhinishia Mtume Wake S.A.W, utekelezaji wa Nguzo ya Tano katika Nguzo za Uislamu, Mtume S.A.W alisimama katika eneo la Milima ya Arafaat katika Mawe, katika Mjumuiko mkubwa wa watu kwa wakati huo, akizichambua Ibada mbalimbali za Hija kwa Maswahaba wake na kwa umma ujao baada yao, na akiweka misingi imara ya Maadili ya Kibinadamu na ya Kitabia ambayo aliendelea kuyalingania katika maisha yake yote, huku akihisi kukaribia kifo chake na kumalizika kwa umri wake. Na kwa hivyo, hotuba yake ilikusanya mambo mengi muhimu ya kujifunza na mazingatio ya hali ya juu ambayo yanazingatiwa kuwa ni Mfumo wa Maisha ya Watu wote

Na miongoni mwa mafunzo ya hotuba yake ni: Kujenga Misingi imara ya Uadilifu na Usawa baina ya Watu wote. Anasema Mtume S.A.W: Enyi Watu:Hakika Mola wenu Mlezi ni Mmoja. Na Hakika Baba yenu ni Mmoja. Tambueni kwamba hakuna ubora wowote wa mwarabu kwa muajemi, wala muajemi kwa mwarabu, wala mwekundu kwa mweusi, wala mweusi kwa mwekundu, isipokuwa kwa Uchamungu. Hakika Mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mchamungu…

Mtume S.A.W aliufanya Uchamungu na Matendo mema kuwa ni kigezo cha mtu kuwa bora zaidi ya mwingine kwa kuitekeleza kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ}

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari

Kwa hiyo, Watu wote ni sawa kwa upande wa haki na wajibu bila ya kumbagua yoyote kimatabaka, kasumba ya kikabila, na haya yanatokana na Uadilifu ambao ndio kipimo cha kusimamisha haki na Uuwianifu wa Mataifa.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُواْ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى}

Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُواْ بِالْعَدْلِ}

Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلاَ يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلاَّ تَعْدِلُواْ اعْدِلُواْ هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى}

Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu.

Na katika faida hizo pia: ni Ulinzi wa Maisha na Mali pamoja na Heshima za watu. Kutoka kwa Abdurahman bin Abuu Bakra R.A, kutoka kwa Baba yake anasema: Mtume S.A.W alikuwa ameketi juu ya ngamia na mtu mmoja alikuwa ameushika utepe wa kumswagia ngamia kisha akasema S.A.W: Leo ni siku gani? Tukanyamaza mpaka tukadhani kwamba Mtume aipa siku hiyo jina jingine. Akasema Mtume S.A.W: Je leo sio siku ya kuchinja? Tukasema: Ndio. Akasema: Kwani huu ni mwezi gani? Tukanyamaza mpaka tukadhani kwamba Mtume S.A.W, ataupa mwezi huu jina jipya. Akasema Mtume S.A.W: Je mwezi huu sio wa Dhulhijah? Tukasema: Ndio. Akasema: Hakika Damu zenu, Mali zenu na Heshima zenu ni Haramu kama ilivyo Haramu ya siku yenu hii katika mwezi wenu huu na katika Mji wenu huu. Aliyekuwepo amfikishie asiyekuwepo. Kwani huwenda aliyekuwepo akamhadithia aliye mtambuzi zaidi kuliko yeye.

Katika jambo hili, Mtume S.A.Waliwazindua Maswahaba wake na akaziamsha zaidi akili zao kwa maneno haya bobezi ambayo yamekusanyika katika mwenendo huu wa Mtume S.A.W wenye mtazamo wa kina unaoonesha uzito wa kuyaheshimu maisha ya binadamu, mali na heshima yake na Ulinzi wake, na kwamba haiwi halali kumshambulia mtu kwa ushambuliaji wa aina yoyote. Uislamu unalingania Usalama na Amani, Utulivu na Salama. Na Uislamu unawataka Watu wote waishi maisha ya utulivu bila ya ubaguzi au utofautishaji baina ya mtu na mwingine bila kujali jinsia yake, rangi yake au hata Dini yake kwani Sheria ya Uislamu imemlindia yote haya kila mtu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ}

 Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekufanya kuiua nafsi moja bila ya haki ni sawa na kuwaua Watu wote. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {مَن قَتَلَ نَفْساً بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأرض فَكَأَنَّمَا قَتَلَ الناس جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا}

Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.

Kwa kuthibitisha uharamu wa kuua na kumtia hatiani muhusika, Mtume S.A.W ameonya onyo jingine katika hotuba yake hii, onyo ambalo linahusika na uharamu wa kuua ambapo anasema Mtume S.A.W: Msirejee tena kwenye Ukafiri baada yangu mimi, mkauana wenyewe kwa wenyewe. Kama ambavyo Uislamu umeharamisha kuishambulia nafsi, umeharamisha pia kushambulia mali za Watu kwa aina yoyote ya mashambulizi, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَنْ تَكُونَ تِجَارَةً عَنْ تَرَاضٍ مِنْكُمْ}،

Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.

 Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

 {وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ}

Wala msiliane mali zenu kwa baat’ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua.

Kwa ajili ya kuzilinda Mali za Mali kwa ujumla, Sheria ya Kiislamu imeuharamisha wizi na kuuwekea adhabu kali ikemeayo.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِنَ اللَّهِ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ}

Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Na Sheria ya Uislamu imeharamisha pia upokonyaji wa aina zote wa Ardhi za Watu, ambapo Mtume S.A.W, anasema: Mtu yoyote atakayedhulumu kiasi cha upana wa vidole kumi na mbili moja ya ardhi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamtwisha shingoni kwa ardhi hiyo siku ya Kiama uzito wa ardhi saba.

    Na vile vile Uislamu umeharamisha uadui wa heshima za Watu au hata kuzigusa vyovyote iwavyo, na hakuna tofauti kati ya mwislamu na asiye mwislamu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا}

Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.

Uislamu pia umeharamisha kuwatuhumu uzinzi Wanawake wenyekujiheshimu na ukazingatia kuwa hili ni katika Madhambi Makubwa. Na Mtume S.A.W anasema: Jieousheni Mambo saba yaangamizayo. Akaulizwa: Ni yepi hayo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema: … Kuwatuhumu uzinzi Wanawake wanaojiheshimu, walioghafilika, Walio Waumini…. Na Mtume S.A.W amekataza Matusi na kutukana kwa ujumla na akaiita Tabia hii ya kutukana kama Uovu akasema Mtume S.A.W: Kumtukana Mwislamu ni Uovu na kupigana nae ni Ukafiri.

Na miongoni mwa ya kujitunza ni: Ulinganiaji wa Umoja na kuonya juu ya migawanyiko ambapo anasema Mtume S.A.W katika hotuba yake ya kuaga: Hakika Shetani amekata tamaa ya kuabudiwa katika Nchi yenu hii, katika zama za mwisho. Na amekuridhieni kutoka kwenu matendo maovu basi tahadharini nae katika Dini yenu… Kwa hiyo tuungane na tushikamane kwa kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Sisi sote, kwa kuiitikia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anaposema:

 {وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ}

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَأَطِيعُواْ اللّهَ وَرَسُولَهُ وَلاَ تَنَازَعُواْ فَتَفْشَلُواْ وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ}

Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.

Na tutambue kwamba Dni ya Uislamu haina uhusiano wowote na mparaganyiko pamoja na mgawanyiko.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُواْ دِينَهُمْ وَكَانُواْ شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ }

Hakika walio igawa Dini yao na wakawa makundi makundi, huna uhusiano wowote nao. Kwa hivyo, Uislamu unalingania Umoja na unaharamisha Gomvi na Mgawanyiko.

Na katika tunayonufaika nayo: Ni Wajibu wa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunna ya Mtume S.A.W, ambapo anasema Mtume S.A.W: Na hakika nimekuachieni ambapo hamtapotea kamwe iwapo mtashikamana nacho, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na nyinyi ndio mnajukumu la kunifikishia…

Na kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Muujiza kudumu Milele, haujiwi na Batili kwa mbele au kwa nyuma yake, haubadiliki wala haugeuki miaka na miaka inayopita. Na karne na karne ziendazo. Mwenyezi Mungu ameondosha kwayo na kwa Sunna ya Mtume S.A.w, Matamanio, na kumaliza kwavyo aina zote za hitilafu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنْكُمْ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا}

Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.

Na kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunna ya Mtume S.A.W ni alama ya Imani na ni Dalili ya Uchamungu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجًا مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا}

La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili yangu na kwa ajili yenu.

*        *        *

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Bwana Mlezo wa viumbe vyote, na ninashuhudia na kukiri kuwa hapana mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na Mshirika wake, na ninakiri na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu mswalie, mrehemu na Umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote. Hapana Shaka kuwa Hotuba ya Hija ya Kuaga aliyoitoa Mtume S.A.W, ndio kumbukumbu ya kwanza na azimio la kimataifa la ulinzi wa Haki za Binadamu, kutokana na maadili iliyoyakusanya ndani yake ambayo yanaulinda utukufu wa Mwanadamu na kumletea udalama na amani yake. Na katika faida muhimu za mafunzo zinazopatikana ndani ya Hotuba hiyo: ni ubainifu wa sheo cha mwanamke na nafasi yake katika Sheria ya Uislamu. Mtume S.A.W ameusia kuhusu Mwanamke kwa kumpa uzito wake, na akaweka wazi nafasi yake. Wanawake ni ni ndugu wa wanaume, na Haki na Majukumu ni ya pande mbili baina yao. Anasema Mtume S.A.W: Hakika mna nyinyi juu ya wanawake wenu Haki na wao wana juu yenu haki. na Uislamu umempa heshima kubwa Mwanamke, awe ni mama, dada, binti au mke. Na kumfanya awe na Haki zinazoidhamini furaha yake ya Duniani na Akhera, na kumlinda pamoja na kuuhifandhi utukufu wake wa kibinadamu. Na Mtume S.A.W alipoulizwa: Ni nani mwenye haki zaidi ya kuwa naye katika watu? Mtume S.A.W akasema: Ni mama yako. Kisha akasema yule muulizaji: Kisha nani? Mtume akasema: kisha Mama yako. Akasema yule muulizaji: kisha nani? Mtume akasema: kisha mama yako. Kisha akasema tena yule muuliza: kisha nani? Akasema Mtume S.A.W; kisha Baba yako. Na anasema Mtume S.A.W: Mtu atakayekuwa na watoto wa kike watatu na akawavumilia, akawalisha na kuwanywesha, akawavisha kwa jasho lake, basi sisi tutakuwa kwake yeye siku ya Kiama kizuizi cha Moto. Na katika mapokezi mengine. Anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakayewalea watoto wawili wa kike,  au watatu, au dada zake wawili au watatu, mpaka watakapoolewa  au akafariki dunia na kuwaacha, basi mimi nay eye tutakuwa kama vidole hivi, akaashiria kwa vidole viwili; cha tatu na cha shahada. Na kutoka kwa Abu Huraira R.A, amesema: Anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Usianeni juu ya wanawake, kwani mwanamke ameumbwa kwa mbavu ya mwanaume, na hakika kitu kilichopinda zaidi katika mbavu ni kilicho juu yake, na utakapoenda kutaka kuinyoosha utaivunja, na ukiiacha itaendelea kuwa imepinda, basi usianeni wema juu ya wanawake. Neno kheri katika Hadithi hii ya Mtume ni neno linalokusanya maana pana zaidi ambapo linaashiria uwajibu wa kujipamba kwa maana bora za uwanaume pale wanaume wanapotangamana na wanawake. Haja iliyoje kwetu sisi ya kuyatekeleza maadili haya yenye thamani kubwa ambayo yamezikusanya kheri nyingi kwa ajili ya ubinadamu.

 Hakika Maadili haya yamekuja yakizitangulia zaka katika historia ya Ubinadamu na ya Kitabia ambayo kama watu watayazingatia vyema na wakayaingiza akilini mwao na wakayafanyia kazi ipasavyo, basi hapana shaka kwamba hiyo itakuwa ndiyo sababu ya furaha yao Duniani na Akhera.

Ewe Mola wetu Mlezo tukubalie sisi hakika wewe ni Msikivu Mjuzi, na tunakuomba utupokelee toba zetu hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea Toba na Mpole mno.

  َّ

 

Jinsi ya kuitumia Misimu ya Ibada na Kheri

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, anayesema katika Kitabu chake Kitukufu:

  {وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ * الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ}

Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu, Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema;

Na ninashuhudia kuwa hapana mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu msalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametenga katika masiku ya mwaka mzima, misimu ya kufanya ibada ambayo ndani yake malipo huongezeka kwa wingi mkubwa, na huzidi kheri ndani ya misimu hiyo, na daraja hupandishwa kwa ajili ya kuhimiza watu wadumu katika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lakini pia na kuipokea misimu hiyo vyema. Na mwenye akili ndiye anayeweza kuitumia misimu hiyo vilivyo na akaisafisha nia yake na akatenda mema ndani ya misimu hiyo kwa uzuri wa kutenda na akamwelekea Mola wake Mtukufu kwa kuongeza mambo ya kheri na akapata tunu na rehma zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo anasema Mtume wetu Muhammad S.A.W: Hakika Mola wetu Mtukufu ana yeye katika masiku ya mwaka wenu masiku ya tunu, basi yapateni masiku hayo, huwenda mmoja wenu akaipata moja kati ya hizo tunu na baada ya tunu hiyo hawi mwovu milele.

Na katika mambo yasiyokuwa na shaka ni kwamba sisi tunaishi katika masiku haya msimu miongoni mwa misimu mitukufu ya kulipwa kwa wingi, na yenye uzito mkubwa, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia thawabu za mema ndani ya masiku haya kuwa nyingi mno, na malipo makubwa ya kazi ndani ya masiku haya ni tofauti na masiku mengine, kwani haya masiku ni matukufu, na ni nyakati zilizotukuzwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amezinyanyua daraja, na Mtume S.A.W amefafanua nafasi ya masiku haya, na kwa ajili hiyo: Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa katika Qurani tukufu ambapo anasema:

 {وَالْفَجْرِ* وَلَيَالٍ عَشْرٍ * والشفع والوتر}

(Naapa kwa alfajiri, Na kwa masiku kumi, Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja.)

Na rai wanayoifuata wanazuoni wote ni kwamba Masiku haya kumi ni ya mwanzo wa mwezi wa Dhulhijja, na Mwenyezi Mungu Mtukufu haapi isipokuwa kwa kitu kitukufu, na kiapo kilichopo hapa ni kwa lengo la kuyatukuza masiku hayo na kuonesha nafasi yake, na kuwazindua waja kuyahusu masiku haya, na kuweka wazi fadhila zake, na kuwaongoza katika umuhimu wake.

Na miongoni mwa fadhila zake: ni kuwa masiku haya yanajulikana kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu anaposema:

 {وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ عَلَى مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ}

(… na walitaja jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama yao alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri). Kwa hiyo masiku haya ndani yake humkusanyikia Mwislamu aina mbali mbali za ibada, ambapo yeye huwa na nafasi ya kutekeleza ibada hizo kama vile swala, sadaka, swaumu, na Hija, na ibada hizi haziji hivyo katika masiku mengine kinyume na haya.

Na katika fadhila za masiku haya ni kwamba: Ni masiku ayapendayo mno Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kazi yoyote nzuri ndani ya masiku haya inapendwa mno na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko katika masiku mengine. Huu ni msimu wa mapato, na ni njia ya uokovu na ni uwanja wa kushindana katika mazuri ambapo anasema Mtume S.A.W: Hakuna masiku ambayo kazi njema inapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu kama katika masiku haya. Kwa maana ya masiku kumi. Maswahaba wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake na hakurejea kutokana na hicho kilichomtoa. Kwa hivyo kila Mwislamu anapaswa kuyatumia masiku haya yenye fadhila kubwa mno, na malipo makubwa sana kwa kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila aina za ibada na kumtii yeye.

Na miongoni mwa matendo yaliyo bora na ya kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya masiku haya, ni kuhiji Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu mtukufu kwa mwenye kuweza kufanya hivyo.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَعْلُومَاتٌ فَمَنْ فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ}

Hijai ni miezi maalumu. Na anayekusudia kufanya Hijai katika miezi hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala sibishane katika Hija.

Na Hija ni nguzo ya tano ya Uislamu ambayo kwayo jambo hili hutimia, na dhambi husameheka, na Mja huandikiwa mazazi mapya ambapo Mtume S.A.W anasema: Mtu yoyote atakayehiji na akawa hakufoka maneno machafu na wala hajafanya mabaya yoyote, basi atarejea na kuwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.

Na Hija ni mnasaba Mkubwa kwa ajili ya kujifunza fadhila nyingi na Maadili mema, ambapo mwislamu analeleka ndani yake katika kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujilinda na misukumo na matamanio ya nafsi yake pamoja na kujipamba na tabia njema na mazuri yake kwa kuwapendelea watu na sio kujipendelea, na kutosheka na kutotamani vya watu, sio kuomba omba wala kufanya israfu. Mwislamu pia anajifunza ndani ya masiku haya uhakika wa maneno na vitendo vyake, pamoja na kukufuata sheria na kujidhibiti. Kwa hivyo, Mtu anayehiji ni wajibu kwake ndani ya masiku ya Hija kutekeleza kivitendo yale yanayolinganiwa na Uislamu miongoni mwa Maadili mema, na Tabia Njema; ili atoke katika chuo cha Hijai akiwa amenufaika na madhumuni yake ya kimaadili na kimwenendo.

Sisi tunathibitisha kwamba Ibada ya Hijai ni Ujumbe wa Amani kwa Ulimwengu wote. Hijai ni Amani kwa ujumla, na Usalama kwa Ujumla. Kwani Mwenyekuhiji hagombani na yoyote, wala hamwindi mnyama wala hamuudhi au hata kumuua.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنْتُمْ حُرُمٌ}

Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija.

Na wala haiishii katika kuwa na amani na Watu na Wanyama tu bali hali hii inaelekea na kutanda pia kwa mimea. Mwenye kuhiji anaamrishwa awe na amani hata kwa mimea ambapo anasema Mtume S.A.W: Hakika Nchi hii Mwenyezi Mungu ameharamisha ndani yake kutokatwa hata mwiba, na wala mnyama yoyote asibughudhiwe, na mnyama aliyepotea asiokotwe isipokuwa na mtu anayemjua. Na hapana shaka kwamba katika hayo yote kuna mafunzo na maandalizi kwa mwislamu ili Watu, Miti, na hata Mawe visalimike na maudhi yake baada ya kurejea kwake kutoka katika utekelezaji wa Ibada ya Hijai. Na Mtume S.A.W ametuambia kuwa Mwislamu wa kweli ni yule ambaye Watu watasalimika na Ulimi wake na Mkono wake. Ambapo anasema Mtume S.A.W katika Hotuba yake ya Kuaga: Je nikujulisheni kuhusu Muumini? Ni yule ambaye watu wamemwamini kwa mali na nafsi zao, na Mwislamu: ni yule ambaye Watu wamesalimika na Ulimi pamoja na Mkono wake. Na Mpiganaji Jihadi: ni yule ambaye anapambana na Nafsi yake katika Kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Muhaajir (Mhamaji): ni yule aliyehama makosa na Madhambi.

Na katika vitendo vyenye fadhila nyingi ambavyo inapendeza kwa Mja kujisogeza kwa Mwenyezi Mungu kwa vitendo hivyo katika masiku haya, ni: Swaumu. Swaumu ni katika vitendo bora vya kumtii Mwenyezi Mungu na ni njia bora ya kujikurubisha kwake. Na Mwenyezi Mungu ameiongeza ibada hii kwake yeye kutokana na uzito wa hadhi yake na utukufu wa hceo chake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Qudsiy: Kila kitendo cha Mwanadamu ni chake yeye isipokuwa Swaumu ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa.

Na Mtume S.A.W anasema: Mja yoyote atakayefunga siku moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atauepusha Uso wake na Moto kwa kiasi cha miaka sabini. Na kwa hivyo inapendeza kwa Mwislamu afunge siku Tisa za Mwezi wa DhulHijai kiasi awezacho. Na kuzifunga siku hizo ni katika vitendo avipendavyo mno Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hasa Siku ya Arafa kwa siyehiji. Mtume S.A.W ametenga swaumu ya siku hii ya Arafa miongoni mwa masiku kumi ambapo anasema S.A.W: Swaumu ya Siku ya Arafa humwa ninamtegemea Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu ya Mwaka mzima ulio kabla yake na mwaka mzima ujao baada yake. Na siku ya Arafa ni katika masiku ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yanayoshuhudiwa kujitokeza kwa Utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake, kwa Rehma, Kusamehe makosa yao na kuwaacha huru na Moto. Ni siku ambayo ndani yake hujibiwa Maombi ya waja na makosa madogo madogo husamehewa, na Mwenyezi Mungu hujigamba kwa viumbe vya Ardhini na Mbinguni. Anasema Mtume S.A.W: Hakuna siku ambayo Mwenyezi Mungu kwa wingi humuepusha ndani yake mja wake na Moto kuliko siku ya Arafa, na hakika yeye Mwenyezi Mungu huwajongelea waja wake kisha kisha akajigamba kwa malaika, nayo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliikamilisha Dini yake ndani ya siku hii, na kuikamilisha neema yake. Kutoka kwa  Omar bin Khatwaab R.A: kwamba kuna mtu mmoja katika Mayahudi alisema: Ewe Amiri wa Waumini, kuna aya moja imo ndani ya Kitabu chenu mnaisoma, kama tungekuwa tumeteremshiwa sisi Mayahudi basi siku hiyo ya kuteremshwa kwake tungeifanya ikawa Sikukuu. Akasema: Ni aya ipi hiyo? Akasema yule Myahudi:

{الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا}

Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.

Akasema omar R.A: Tumejua hivyo leo, na sehemu ilipoteremshiwa kwa Mtume S.A.W, hali ya kuwa amesimama Arafa, siku ya Ijumaa.

Inapendeza pia kwa Mwislamu kukithirisha utajo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika masiku haya, kwani kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ni uhai wa Nyoyo, na kwa utajo wa Mwenyezi Mungu hupatikana Utulivu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ}

Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!

Na Mtume wetu S.A.W anasema: Hakuna masiku yaliyo bora zaidi kwa Mwenyezi  Mungu wala amali inayompendeza zaidi yeye ndani ya masiku hayo kuliko masiku haya kumi. Zidisheni ndani yake utajo wa Mwenyezi Mungu wa tahliili (Laa ilaaha illa Llaahu), na utajo wa Takbiiraa (Allaahu Akbar), na utajo wa Tahmiid (alhamdulillah). Na Bwana wetu Omar R.A alikuwa akitoa Takbiira katika eneo la mbele la msikiti na watu wakawa wanamsikia na wao wanatoa Takbiira kwa kusema: Allaahu akbar. Na watu wa Masokoni nao wanatoa Takbiira mpaka eneo lote la Mina linatikisika kwa Takbiira. Na Omar R.A alikuwa anatoa Takbiira katika anapokuwa Mina ndani ya masiku hayo kbla ya kila swala na hata akiwa kitandani kwake, anapoketi, au anapotembea, na kwa ajili hiyo inapendeza kwa Mwislamu atoe Takbiira kwa sauti katika masiku haya kwa ajili ya kuutangaza na kuudhihirisha utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume wetu S.A.W: Je nikujulisheni kilicho bora katika matendo yenu, na kilicho na daraja za juu zaidi, na kilicho takasika mbele ya Mola wenu Mfalme wa Ulimwengu, na ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ni bora zaidi kwenu kuliko kukutana na adui zenu na mkazikata shingo zao? Wakasema: ndio. Akasema: Ni kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na kutoka kwa Muaadh bin Jabal R.A, Hakuna kazi bora ya mwanadamu inayomwokoa zaidi na adhabu ya Mwenyezi Mungu kuliko kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ninayasema maneno yangu haya, na ninamwomba Msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili yangu na kwa ajili yenu

*        *        *

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ninashuhudia kuwa hapana mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu msalie, mrehemu na umbariki yeye Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu Waislamu. Hakika miongoni mwa matendo yanayomkurubisha zaidi Mja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika masiku haya: Ni kichinjo. Kichinjo ni moja ya Alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nayo ni alama ya Dini ya Ibrahim A.S. Na ni dalili ya Sunna ya Muhammad S.A.W.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَـائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوب}

Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.

Mtume S.A.W alipoulizwa: Nini hivi vichinjo? Akasema: Ni Sunna ya Baba yenu Ibrahim. Na anasema Mtume S.A.W: Hakuna siku ya mwanadamu katika siku ya kuchinja inampendeza zaidi Mwenyezi Mungu kuliko kuchinja. Na hakika mambo yalivyo, kichinjo kitakuja siku ya Kiama kikiwa na mapembe yake, na manyoya yake na kwato zake, na kwamba damu yake itadondokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika sehemu kabla ya kudondoka kutoka ardhini, basi zipambeni nafsi zenu kwa vichinjo.

Kuchinja ni sura miongoni mwa sura za kuleana kijamii ambazo huleta mapenzi, na kuhurumiana, na kufungamana baina ya wanajamii wote. Na Mtume S.A.W alipoona watu wana utapia mlo, akawaambia: yoyote atakayechinja miongoni mwenu basi asipambazukiwe hadi siku ya tatu akiwa amebakiza kitu katika kichinjo chake

Na uliwadia mwaka mwingine wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, tufanye kama tulivyofanya mwaka uliopita? Akasema: Kuleni na wekeni akiba, kwani mwaka jana watu walikuwa na njaa sana na nikakutakeni msaidie ndani ya Mwaka huo.

Maisha yanapokuwa mazuri na Watu wana uwezo basi hutumika kauli ya Mtume S.A.W isemayo: Kuleni, toeni sadaka na wekeni akiba. Na pindi Watu wanapokuwa na haja zaidi au wakiwa na utapia mlo basi itumieni kauli ya Mtume S.A.W isemayo: Yoyote miongoni mwenu atakayechinja basi asipambazukiwe baada ya siku ya tatu hali ya kuwa nyumbani kwake kuna kitu chochote katika kichinjo.

 

Kwa kujua kuwa kama ambavyo kichinjo kunapatikana kwa kuchinja, kinatikana pia kwa kununua kununua kwa wingi, na hakuna shaka yoyote kuwa kufanya hivyo ni katika kuleta manufaa ya kuchinja na hasa kwa yule asiyekuwa na chombo cha ugavi kwa njia nzuri zaidi, jambo ambalo hukifanya kichinjo kifika kwa njia ya kununua kwa wingi hadi kuwafikia walengwa wenyekustahiki, jambo ambalo huongeza manufaa ya Kichinjo na thawabu zake kwa wakati huo huo, na pia huchangia katika kuifikisha kheri kwa wenyekustahiki, kwa hadhi na heshima yao, na nia uzuri ulioje wa mwenye kuweza tena mwenye mali kukutanishwa na mambo mawili ya kuchinja kichinjo kwa ajili ya kupanua zaidi kwa Jamaa zake na nduguze, pamoja na kununua kwa wingi kama ni upanuzi kwa mafukara wote katika maeneo yenye kuhitaji zaidi

Mwislamu anapaswa kuzidisha kwa wingi aina mbali mbali za kheri ambazo zinaweza kuwanufaisha watu wote. Azidishe kutoa sadaka ili aingize faraja na furaha katika nyoyo za mafukara na wenyekuhitaji.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu, ametuasa sisi kuifanya ibada ya kutoa, akasema:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَنفِقُواْ مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لاَّ بَيْعٌ فِيهِ وَلاَ خُلَّةٌ وَلاَ شَفَاعَةٌ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ}

Enyi mlio amini! Toeni katika tulivyo kupeni kabla haijafika Siku ambayo hapatakuwapo biashara, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhaalimu.

Na katika Hadithi ya Mtume S.A.W: Haipungui mali ya mja kwa kutoa sadaka.

Tuna hitaji kwa kiasi kikubwa mno Kuleana na Kuhurumiana, na kila mmoja kumuhisi mwingine, kwa kutekeleza kauli ya Mtume wetu S.A.W aliposema: Mwislamu ndugu yake ni Mwislamu; hamdhulumu, wala hamdhuru. Na yoyote atakayemsaidia ndugu yake basi Mwenyezi Mungu atamsaidia yeye. Na yoyote atakaemwondoshea jambo zito ndugu yake Mwislamu, katika mambo mazito basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwondoshea yeye jambo zito siku ya Kiama. Na yoyote atakayemsitiri mwislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu naye atamsitiri Siku ya Kiama.

Na anasema Mtume S.A.W: Kila Mwislamu ana sadaka. Maswahaba wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kama mtu hakupata cha kukitoa sadaka je? Akasema: basi afanye kazi kwa mikono yake, na ajinufaishe yeye na kisha atoe sadaka. Wakasema Maswahaba: Na ikiwa hakupata je? Akasema: atamsaidia mwenye shida aliyekwama. Wakasema: na kama hakupata je? Akasema: basi atende mema na ajizuie na shari, kwani hayo kwake ni sadaka.

Ewe Mola wetu tunakuomba utusaidie sisi tuwe ni wenye kukutaja, na kukushukuru na kukuabudu vyema

 

Manufaa ya Umma katika Kipimo cha Sheria

Ndugu zangu waislamu Afrika Mashariki na Kati na wanaozungumza Kiswahili dunia nzima. Hotuba yetu ya leo kwa anwan i:  Manufaa ya Umma katika Kipimo cha Sheria.

  Na hii ni kutoka wizara ya waqfu ya Misri,na mimi ni profesa\ Ayman Alasar,Chuo Kikuu cha Alazhar,Kitivo cha Lugha na Ufasiri,lugha za Kiafrika.

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa Viumbe vyote, anayesema katika Qurani Tukufu:

 {وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ}

Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

 

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye hana mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu, na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu, mswalie, na umrehemu na umbariki Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake, na atakayewafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.

 

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika mtu yoyote mzingativu wa Hukumu za Sheria ya Kiislamu, anakuta kwamba Sheria imekuja kwa ajili ya kuleta masilahi ya Nchi na Waja, na kumkuza mwanadamu kinafsi, na kumea hadi kufikia daraja za juu, na kwa hivyo kila kinachoyafikia masilahi ya watu wote kinaafikiana na Sheria ya Kiislamu, hata kama hakuna andiko la wazi ndani yake, na kila kinachogongana na masilahi ya watu na manufaa yao basi hakina asili yake katika Sheria tukufu.

 

Hakika Dini ya Uislamu iliyo tukufu, haitambui umimi na uchoyo au uhasi, na wala haitambui masilahi binafsi dhidi ya masilahi ya umma, bali inayatambua masilahi ya wote, masilahi ya umma, na upaji wa kweli na kusaidiana katika wema na uchamungu uliochanganyika na upendo na kumpendelea mwingine, mpaka jamii ikayafikia maendeleo yanayolinganiwa, na kuleana kwa wema, na juhudi ya kila mtu ikawa ni kwa ajili ya wote, na ikaleta heri kwa kila mtu na kwa wote, na kuingia zaidi ndani ya moyo wa wananchi na hisia za kuwa wamoja ambapo kila kiungo kikiwa na maumivu basi mwili mzima huwa na hisia za maumivu hayo, kwa kukesha na homa kali.

 

Anasema Mshairi wa Misri Ahmad Shawqy :

Nchi vijana wake wamekufa ili iendelee kuishi,

              na wakawa mbali na watu wao ili watu wao wabakie.

 

Na hapana shaka yoyote kwamba mzingativu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, anatambua fika kuwa Kusudio kuu na Jumla la uwekaji wa Hukumu mbali mbali kwa ajili ya watu, ni kwa sababu ya kuleta masilahi yao na manufaa pamoja na heri kwa wote, nao ni mfumo wa Mitume na Manabii wote, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtuma Mtume yoyote au Nabii yoyote alifanya hivyo kwa ajili ya kuwafurahisha watu wake na kuwaletea heri bila ya kusubiri malipo au manufaa ya kidunia.

 

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kauli ya Mtume wake Nuhu A.S:

{وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّهِ}

{Na enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali kwa ajili ya haya}.

 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia kauli ya Mtume wake Hud A.S:

 {يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي أَفَلَا تَعْقِلُونَ}

{Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa Yule aliye niumba. Basi hamtumii akili?}.

 

Na kipenzi huyu wa Mwenyezi Mungu, Mtume Ibrahim A.S, anamwomba Mola wake kwa Unyenyekevu Dua inayoonesha upeo wa ari yake ya kutaka watu wote wanufaike, na heri idumu kwao wote, anasema:

{رَبِّ اجْعَلْ هَذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُمْ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ}

{Ewe Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho}.

NDUGU ZANGU WAISLAMU

Inajulikana kwamba kusudio la nchi katika aya hii ni watu wake, kama alivyowaombea watu wake riziki inayowatosheleza na kuwaepusha kuwategemea wengine, kwa kuwa nchi inapokuwa na amani, na mahitaji ya watu katika maisha yao yakawepo katika hali ya kutosha, basi jambo hilo huwasaidia watu wake kuwa watiifu kwa Mwenyezi Mungu wakiwa na nafsi zilizotulizana, na nyoyo zenye matumaini, zenye kujihimiza katika kulifikia lengo alilolikusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu la kuumbwa kwao, ambalo ni kuijenga ardhi na kuiwekea mazingira bora ya kuishi. Jambo hili ni kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{هُوَ أَنْشَأَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا}

{Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo.}

Na katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anaposema:

 {وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا}.

{Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa}.

 Hakika Sheria ya Kiislamu imekuja kwa ajili ya kuiweka juu hadhi ya Msingi wa Kibinadamu na Kimarekebisho Ulionyooka na kuweka misingi ya kulinda utulivu kwa jamii na juhudi za kuimarika na kusonga mbele katika kutanguliza manufaa ya wote dhidi ya yale ya mtu mmoja mmoja, na kupangilia pia vipaumbele mpaka maisha yapangike na yawe na utulivu. Na Sira ya Mtume S.A.W iliyotwaharika, na maisha ya maswahaba watukufu vina matukio mengi yenye hadhi ya juu ambayo yanayathibisha haya:

Kutoka kwa Mama wa Waumini, Bi Aisha R.A, anasema: Kama tungelitaka kushiba basi tungeshiba, lakini Mtume Muhammad S.A.W alikuwa akiwapendelea watu wengine kuliko kujipendelea yeye mwenyewe. Mtume S.A.W alikuwa anawapendelea watu wengine kuliko nafsi yake na Watu wa nyumbani kwake pamoja kuwa na mahitaji mengi makubwa.

 Na kutoka kwa Abu Saidi Khudhwariy R.A, anasema: Tulipokuwa safarini pamoja na Mtume S.A.W, mtu mmoja alikuja akiwa juu ya kipando chake na anaendelea kusema: Mtu huyo akawa anaangalia kuliani na kushotoni kwake, Mtume S.A.W akasema: Yeyote mwenye kipando cha ziada basi na ampe yule asiyekuwa nacho, na mwenye chakula cha ziada basi na ampe yule asiyekuwa nacho. Akasema: akazitaja aina za mali ambazo hajawahi kuzitaja mpaka tukaona kuwa hakuna mtu yeyote katika sisi mwenye haki ya kuwa na kitu cha ziada.

 

Na katika Vitabu viwili vya Hadithi Sahihi  vya (Bukharin a Mulsim), kutoka kwa Bi Aisha R.A, anasema: Asikini wa kike alinijia huku akiwa amewabeba watoto wake wawili basi nikampa tende tatu ale, na yeye akampa kila mtoto tende moja na akaipeleka hadi mdomoni kwake tende moja ili aile, na akawalisha watoto wake tende hiyo, kisha akaipasua tente aliyotaka kuila na kuwagawia watoto wake, na kitendo hicho kikanifurahisha na nikakisimulia kwa Mtume S.A.W, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia kwa kitendo hicho pepo, au amemuachisha kwa kitendo hicho moto.  Kwa hiyo kama hayo ndio malipo ya mtu aliyewapendelea watoto wake kuliko nafsi yake, inakuwaje kwa yule mwenyekumpendelea mnyonge muhitaji aliye masikini?

Na huyu hapa Othmani bin Afaan R.A, katika mwaka wa janga ambapo ufakiri ulikuwa mkali kwa Waislamu pamoja na njaa, akaileta biashara yake kutoka Sham, akiwa na ngamia Elfu moja walibeba nafaka, mafuta, na zabibu na wakamjia wafanya biashara wa Mjini akawaambia: Mnataka nini? Wakasema: Hakika wewe unakijua tunachokitaka, tuuzie hicho kilichokufikia, kwani hakika wewe unajua jinsi watu wanavyohitaji bidhaa hizo. Akasema kwa mapenzi na kwa ukarimu, ni kwa kiasi gani cha faida mtakachonipa mimi kwa jinsi nilivyonunua? Wakasema: tukuongezee kwa kila Dirhamu moja dirhamu mbili? Akawaambia: mimi nimetoa zaidi ya hivyo. Wakasema: Nne, akasema: nimetoa zaidi ya hivyo, wakasema: Tano? Akawaambia: Mimi nimetoa zaidi ya hivyo. Wakamwambia: Ewe Baba Omar hawakubaki Madina wafanyabiashara isipokuwa sisi. Na hakuna yoyote katika sisi aliyetutangulia kuja kwako, basi ni nani aliyekupa kiasi hicho? Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu amenipa kwa kila Dirhamu moja, Dirhamu kumi, je nyinyi mna nyongeza yoyote katika kiwango hicho? Wakasema: Hakuna. Akasema: Hakika mimi ninatoa ushahidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa mimi nimekifanya hichi chote kilichobebwa na ngamia hawa kuwa ni sadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Masikini na mafukara Waislamu. Na pindi Mtume S.A.W alipoashiria kwa maswahaba wanunue kisima cha Rouma na kilikuwa chini ya myahudi na alikuwa akipandisha bei ya maji yake, Mtume S.A.W akasema: Ni nani anaweza kukinunua kisima hichi cha Rouma, na akachota maji ya kisima yeye pamoja na Waislamu? Othamni R.A akamjia yule Myahudi anayemiliki kisima na akajaribu kupatana nae kuhusu kukinunua kisima na yule Mtu akakataa kata kata,  kukiuza kisima chote, na akanunua nusu ya kisima hicho kwa Dirhamu elfu kumi na mbili, na akakifanya kuwa cha waislamu na Bwana wetu Othman A.S, akawa ana siku moja ya kuchota maji, na Myahudi ana siku moja za kuchota maji, Mtume S.A.W. na ikawa inapowadia siku ya Othman waislamu huchota maji yanayowatosheleza kwa siku mbili. Yule Myahudu=I alipoona hivyo, akasema: Umekifisidi kisima change, basi inunue nusu iliyobakia, Othman akainunua nusu iliyobakia kwa Dirhamu elfu nane na akakimiliki kisima chote. Na hili tukio lilikuwa ni uitikiaji wa Bwana wetu Othman R.A, wa amri ya Mtume S.A.W, na akakinunua kisima hicho kwa kuwa na shime ya masilahi ya waislamu wote.

Na katika zama zake Bwana wetu Omar bin Khatwaab R.A, pindi Msikiti wa Makka ulipokuwa mfinyu sana kwa watu, aliwalazimisha wenye nyumba za jirani zinazouzunguka msikiti huo waziuze nyumba zao na akawaambia: Hakikia yenu nyinyi ndio mlioteremka Kaabah na wala Kaabah haijawateremkia.

     

Kama ambavyo sisi tunathibitisha kuwa Ufahamu sahihi wa Dini ya Uislamu hupelekea kuiona sura kamili ya manufaa ya umma yaliyohimizwa na Dini yetu tukufu, na kukokotezwa ndani yake kuzichunga hali za watu na uhalisia wao, na kupangilia vipaumbele kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya msingi ya jamii. Ikiwa jamii ina hitaji ujenzi wa hospitali na kuziandaa kwa vifaa kwa ajili ya kuwatibu mafukara na kuwalea, basi hicho kinakuwa ndicho kipaumbele. Na kama jamii inahitaji ujenzi wa Shule na vyuo pamoja na na ukarabati wake pamoja na kulipia gharama za wanafunzi na kuwalea, basi hicho ndicho kipaumbele. Na kama jamii inahitaji urahisishaji wa ndoa kwa wenye uzito wan a kuwalipia deni wenye kudaiwa na kuwaondoshea mazito wenye kudaiwa, basi hicho ndicho kipaumbele.

 

Na ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu msamaha kwa ajili yangu na kwa ajili yenu.

*        *       

Ndugu zangu wa Islamu

      Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote. Rehma na amani ziwe juu ya Mtume wa mwisho katika Mitume wake na manabii. Na ninashuhudia kuwa hakuna Mola mwingine yoyote anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na Mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad ni Mja na Mtume wake S.A.W, na juu ya Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu waislamu: uislamu unachunga utaratibu wa vipaumbele mpaka katika matendo mema, na kwa hiyo unaamrisha wakati wa kuangalia ubora wa mambo, kuyatanguliza masilahi ya Umma dhidi ya Masilahi binafsi au maalumu, hasa kwa kuwa masilahi ya Umma manufaa yake yanawalenga wengi wakati ambapo masilaha binafsi manufaa yake hayazidi mtu mmoja. Kama mtu anafanya kazi katika taasisi Fulani na kwa kazi hiyo analipwa ujira wake, na anautumia usiku wake kwa ajili ya swala na kukesha kwa ajili ya ibada, kisha unapokuja mchana huenda kazini kwake hali ya kuwa amechoka taabani na akashindwa kuutekeleza wajibu wake wa kazi kama inavyotakiwa. Na masilahi ya taasisi yakazorota kwa sababu ya uzembe wake, na masilahi ya wale wanaohudumiwa na taasisi hiyo, je huko siko kupoteza amana? Na huo sio ulaji wa mali za watu kwa njia batili, na ni kuzembea majukumu aliyopewa mtu? Naye kwa njia hii anakuwa amepoteza mambo ya wajibu kwa kutekeleza Sunna, hapana shaka kwamba huko ni kutoyafahamu malengo makuu ya Dini. Na mfano hai ni wa Bwana wetu Abu Bakar siku alipolala katika kitanda cha umauti akamuusia Bwana wetu Omar R.A, kwa wasi ambao ndani yake kuna kauli hii: Na utambue kuwa Mwenyezi Mungu ana kazi za usiku ambazo hazikubali mchana, na ana kazi za mchana ambazo hazikubali usiku, na kwamba yeye hapokei Ibada za Sunna mpaka Ibada za Faradhi zitekelezwe   

Hakika uelewa sahihi wa Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa namna inayoendana na uhalisia wa zama hizi, na kuchunga hali za watu na mahitaji yao, huhukumia kutoishia kwa mipaka ya kuyafahamu baadhi ya mambo ya Fiqqhi ya Hukumu kwa njia ya kuambiwa au kujifunza bila kuzama zaidi au kutambua Fiqhi ya Makusudio makuu au vipaumbele au uhalisia au kilichopo kwa kile kinachopotea pamoja nacho ndio lengo kuu la kuweka sheria.

Kwa kuanzia katika ufahamu huu wa kimakusudio wa Maamrisho ya Dini hii tukufu, na kwa mpangilio wa Fiqhi ya vipaumbele, hakika sisi tunasisitiza juu ya utangulizaji wa kukidhi haja za watu na jamii ni bora zaidi kuliko kukariri Hija na Umra.  Kwani kukidhi mahitaji ya watu kama vile kumrahisishia aliye na magumu, au sadaka kwa fakiri na kumtoshelezea mahitaji yake, au kumwachia huru mfungwa mwenye deni, ni katika faradhi za kutoshelezeana na inajulikana kuwa utekelezaji wa faradhi za kutoshelezeana hutangulizwa mbele ya Ibada zote za Sunna ikiwemo kukariri Hija na Umra .

 

Ndugu zangu wa Islamu kwa hakika ,Ukubwa ulioje wa kuhitaji kwetu kuifahamu Dini yetu vizuri na kuutambua uhalisia wetu kwa utambuzi wenye mzinduko unaotufanya sisi tuwe na uwezo wa kutambua ukubwa wa hatari zinazotuzunguka, lakini pia kutuchukua na kutupeleka kuleta manufaa na masilahi ya umma dhidi ya masilahi binafsi kwa nia njema na iliyo safi kama ni utekelezaji wa Mafundisho ya Dini yetu tukufu, na kwa utashi wa kulisukuma mbele taifa letu na kuliinua na kuleta maendeleo pamoja na kulifikisha katika nafasi yake stahiki kwake na kwa Wananchi wake.

 

Ewe Mola wetu, tunakuomba uilinde nchi yetu, wananchi wake, na Majeshi yake ya Ulinzi na Usalama, kwa kila Jambo baya.