:

Fadhila za masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie)
na mifano ya historia yao njema
16 Jamad Akhar 1437H. sawa na 25/3/2016

awkaf-

Kwanza: vipengele

 1. Nafasi za masahaba na kupanda vyeo vyao.
 2. Fadhila za masahaba ndani ya Qurani Tukufu.
 3. Kuwapenda masahaba ni katika imani.
 4. Mahimizo ya kuwaiga masahaba watukufu.
 5. Makatazo ya kuwatusi au kuwasema vibaya.
 6. Mifano katika historia yao.

Pili: dalili

Ndani ya Qurani Tukufu

 1. Mwenyezi Mungu anasema { Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wana hurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao katika nyuso zao,  kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katikaTaurati. Na mfano wao katika Injili ni  kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.}(Alfathi. 29)
 2. Mwenyezi Mungu anasema { Na wale walio tangulia, wa kwanza, katikaWahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema,Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake,wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.}(Atawba. 100).
 3. Mwenyezi Mungu anasema {Na wa mbele watakuwa mbele. 11. Hao ndio watakao karibishwa 12. Katika Bustani zenye neema. 14. Na wachache  katika  wa mwisho. 13. Fungu kubwa katika wa mwanzo, }(alwaqia. 10-14)
 4. Mwenyezi Mungu anasema { Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye – hao ndio wenye kufanikiwa.}(Alaaraf. 157).
 5. Mwenyezi Mungu anasema {Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari waliomfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye kuwarehemu}(Atawaba.117)
 6. Mwenyezi Mungu anasema {Lakini Mtume na wale walio amini pamoja naye waliwania Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa.89. Mwenyezi Mungu amewatengenezea Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa.}(Atawaba.88-89)
 7. Mwenyezi Mungu anasema { Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa ushindi wa karibu.}(Alfathi.18)
 8. Mwenyezi Mungu anasema {Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli. 9. Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao,wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake,basi hao ndio wenye kufanikiwa.} (Alhashri.8-9)

Ndani ya hadithi

 1. Kutoka kwa Abdala bin Masud (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “bora ya watu ni waliopo katika wakati wangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia, kisha watakuja watu shahada ya mmoja wao itatanguliwa na kiapo na kiapo chake kwa shahada yake.” (Muslim na Bukhari).
 2. Kutoka kwa Abi hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amaesma Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie): “ Msiwatusi masahaba zangu, msiwatusi masahaba zangu, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake lau kama mmoja wenu angelitoa dhahabu mfano wa jabali la Uhud basi asingelifikia kwa utoaji huo wala nusu yake.” (Bukhari na Muslim).
 3. Mtume (rehma na amani zimshukie) anasema: “Tahadharini, tahadharini kuhusu masahaba wangu. Tahadharini, tahadharini kuhusu masahaba wangu. Msiwavunjie heshima baada yangu, mwenye kuwapenda basi kwa mapenzi yangu nitampenda, na mwenye kuwachukia basi kwa chuki yangu nitamchukia, na mwenye kuwakera basi kwa hakika amenikera mimi, na anikeraye hakika huwa amemkera Mwenyezi Mungu, na amkeraye Mwenyezi Mungu pana wasiwasi wa kuchukuliwa.” (Ahmad).
 4. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) nani kaamka hali ya kuwa amefunga? Abu Bakar akasema: “Mimi”. Akasema: “Ni nani kati yenu aliyeshindikiza jeneza?” Abu Bakar akasema: “Mimi” akasema: “Ni nani kati yenu aliyelisha masikini?” Abu Bakar akasema: “Mimi” akasema: “Ni nani kati yenu aliyetembelea mgonjwa?” Abu Bakar akasema: “ Mimi” Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema mambo haya yakikusanyika kwa mtu basi ataingia peponi.” (Muslim).

Tatu: maudhui

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemchagulia Mtume wake (rehma na amani zimshukie) watu wasafi, masahaba walio wema, waliomuamni na kumuunga mkono na kumnusuru, waliosoma na kupasi kutoka katika chuo cha Nabii Muhammad (rehma na amani zimshukie), waliolelewa katika mikono yake, waliokunywa kinywaji cha chemuchemu safi ambayo inatoa maji ya imani, wakawa watu wenye imani ya kweli, na wenye elimu kubwa, na ufahamu wa kina, na matendo mema zaidi. Waliibeba bendera ya dini katika ulimwengu wote, hawakuwa wakiogopa lawama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili hiyo, wakafanikiwa kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Naye akawasifu ndani ya Qurani Tukufu kwa kusema { Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema,Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhikanaye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake,wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.}(Atawbah. 100). Hao ndio masahaba wa Mtume (rehma na amani zimshukie) ambao Mwenyezi Mungu amewateua kwa Mtume wake wa mwisho.

   Kizazi kilichoweza kubadilisha mwenendo wa maisha, waliibeba nuru aliyokuja nayo bwana wetu, Mtume Muhammad (rehma na amani zimshukie) kwa ulimwengu wote. Na kadiri tutakavyojaribu kuwafukuzia basi hatutaweza, na inatosha kuelewa kuwa lau kama tutatoa sadaka ya dhahabu kila siku mfano wa jabali la Uhudi hatofikia mmoja wenu thamani ya kile walichokitoa masahaba wala nusu yake. Hivi ni kama alivyoashiria Mtume (rehma na amani zimshukie) aliposema… “Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake lau kama mmoja wenu angelitoa dhahabu mfano wa jabali la Uhud basi asingelifikia kwa utoaji huo wala nusu yake.” (bukhari na Muslim). Na hii ni kwa sababu walihimili matatizo ya kueneza hii dini na kufikwa yaliyowafika, wakajitolea kinafsi zao, roho zao na mali zao katika njia ya kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu na kumnusuru Mtume wake (rehma na amani zimshukie), akasema Mwenyezi Mungu { Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu – wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur’ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,}(Atawbah.111).

Na iwapo ni katika haki zetu kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) kuisoma historia yake na mwenendo wake na kufuata uongofu wake na kutenda kwa mujibu wa sheria yake, basi pia katika haki zetu kwa upande wa masahaba ni kuelewa ubora wao na nafasi zao na kusoma historia zao ili tuweze kufanana nao katika kuwa na maadili mazuri, katika kumtii na kumuabudu Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu wote, na tuchukue mazingatio na mawaidha katika maish yao. Kwani wao wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu ili wawe pamoja nae (rehma na amani zimshukie) na kueneza ujumbe baada ya kuondoka kwake, kwani wao ni watu bora katika umma huu kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewasifu kwa sifa za ukamilifu na kuwasafisha, hakuna katika watu aliyeweza kuelewa mfano wa uchaji Mungu kama walivyokuwa hawa wakimcha Mungu . Mwenyezi Mungu amewasifu na akaweka wazi ni kipi alichowaandalia katika malipo makubwa, akasema { Na wa mbele watakuwa mbele. 11. Hao ndio watakao karibishwa 12. Katika Bustani zenye neema. 14. Na wachache katika wa mwisho. 13. Fungu kubwa katika wa mwanzo,}(Alwaqiah. 10-14).

    Na kwa kuweka wazi nafasi zao na kupanda kwa cheo chao Mwenyezi Mungu akawapa sifa miongoni mwa sifa zake ndani ya Qurani Tukufu, si hivyo tu, bali pia wamesifiwa katika Taurati na Injili akasema { Muhammad ni  Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wana hurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katikaTaurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa} (Alfathi.29). Mwenyezi Mungu akawasifu kuwa wao ni wenye nguvu mbele ya makafiri pasi na kudhulumu na weney kuoneana hurumu kati yao, wakimuabudu Mwenyezi Mungu mmoja bila ya kumshirikisha na chochote, wakirukuu na kusujudu, hawatafuti fadhila na radhi isipokuwa zitokazo kwa Mwenyezi Mungu, na ibada imewaathiri mpaka ikadhihiri alama zake katika viungo vyao, ukimuona mmoja wapo basi utaelewa tu ni katika wale wamuogopao Mwenyezi Mungu na kumcha. Hivyo, masahaba (radhi ziwe juu yao) ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, akasema { Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu.}(Alfathi 18) .

Na tukiusoma mwenendo wa Mtume (rehma na amani zimshukie) tutaona kuwa umejaa masimulizi yenye kuonyesha ubora wao na kukuwa kwa nafasi zao, kwa mfano, kukiri kwake Mtume (rehma na amani zimshukie) kuwa wao ni katika watu wa karne (wakati) bora na bora ya umma. Kutoka kwa  Abdala bin Masud (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “bora ya watu ni waliopo katika wakati wangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia, kisha watakuja watu shahada ya mmoja wao itatanguliwa na kiapo na kiapo chake kwa shahada yake.” (Muslim na Bukhari). Na wamekuwa watu bora kwa kuwa walimuamini Mtume (rehma na amani zimshukie) wakati watu wengine walipomkanusha, na kumsadiki wakati wengine walipomuona muongo, na kumnusuru kwa mali zao na nafsi zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu . imepokewa katika kitabu cha imam Ahmad, kutoka kwa Abdalla bin Masud (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: “Mwenyezi Mungu ameangalia katika nyoyo za waja akaona moyo wa Muhammad (rehma na amani zimshukie) ni bora kati ya nyoyo za waja, akamchagua yeye, na akampa ujumbe wake, kisha akaangalia nyoyo za waja baada ya moyo wa Muhammad akaona nyoyo za masahaba ni nyoyo bora kati ya nyoyo za waja, akawafanya kuwa ni mawaziri wa Mtume wake (rehma na amani zimshukie) wenye kuipigania dini yake, na kile waonacho waisilamu ni jema basi na kwa Mwenyezi Mungu pia ni jema, na walionalo kuwa si jema basi kwa Mwenyezi Mungu pia si jema.”

   Pia katika ubora wa masahaba ni kama alivyosema Mtume (rehma na amani zimshukie) kuwa wao ni amana ya umma, Mtume (rehma na amani zimshukie) anasema: “nyota ni amana kwa mbingu, na nyota ziondokokapo basi mbigu huleta kile kilichoahidiwa, na mimi ni amana kwa masahaba zangu nikiondoka basi masahaba zangu wanaleta kile walichoahidiwa, na masahaba zangu ni amana kwa umma wangu wakiondoka basi umma wangu wataleta kile walichoahidiwa.” (Muslim) . Ikawa kuwepo kwa masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) ni amana kwa umma ya kutokuwepo kwa uzushi, lakini pia kutokana na Baraka zao zimeenea na kufika hadi katika kizazi cha pili baada yao. Kutoka kwa Saad Alkhudriy (rehma na amani zimshukie) kwamba Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “watakuja watu watawapigana vita na kundi jengine, watasema: “yupo katika nyie aliyekuwa na Mtume (rehma na amani zimshukie)?” watasema: “ ndio” basi watafunguliwa. Kisha watakuja watu watapigana vita na kundi jengine, itasemwa ““yupo katika nyie  aliyekuwa na waliokuwa na Mtume  (rehma na amani zimshukie)? Watasema: “ndio” watafunguliwa. Kisha watakuja watu watapigana vita na kundi jengine, itasemwa, “yupo katika nyie aliyekuwa na waliokuwa pamoja na waliokuwa na Mtume  (rehma na amani zimshukie)? Watasema “ndio” watafunguliwa. (Bukhari naMuslim).

Pia Mwenyezi Mungu amewashuhudia kuwa ni watu waliokuwa na moyo wa kujitolea, ukarimu na juhudi za kutafuta radhi na mafanikio kwa Mwenyezi Mungu. Naye akawaandalia kutokana na hili pepo ya milele yenye neema. Akasema {Lakini Mtume na wale walio amini pamoja naye waliwania Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa 89. Mwenyezi Mungu amewatengenezea Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa. }(Atawbah88-89). Umar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) anasema: “siku moja Mtume (rehma na amani zimshukie) alituamrisha tutoe sadaka, ikawa ninazo mali, nikasema: “ leo nitamshinda Abu Bakar nikishindana naye, nikaja na nusu ya mali yangu. Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema: “ watu wako umewabakishia kitu gani? Nikasema: “mfano wake. Akasema: “akaja Abu Bakar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) na kila alichonacho, Mtume akamwambia. “watu wako umewabakishia kitu gani? Akasema: “nimeaachilia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nikasema (Umar) siwezi kushindana na wewe kwa kitu chochote milele..” (Tirmidhi).

Na iwapo hii ndio nafasi ya masahaba wa Mtume (rehma na amani zimshukie) basi kuwapenda kwao (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie ) na kukiri ubora wao kuliko wengine ni katika imani ya lazima juu ya kila muisilamu. Kwani ni ishara ya kumpenda Mtume (rehma na amani zimshukie) ambaye aliwapenda na kuwachagua kuwa ni masahaba wake. Muumini hupenda kila apendacho Mtume (rehma na amani zimshukie) wakiwemo masahaba zake. Imepokewa na Abdalla bin Mugh-qal (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “tahadharini, tahadharini kuhusu masahaba wangu. tahadharini, tahadharini kuhusu masahaba wangu. Msiwavunjie heshima baada yangu, mwenye kuwapenda basi kwa mapenzi yangu nitampenda, na mwenye kuwachukia basi kwa chuki yangu nitamchukia, na mwenye kuwakera basi kwa hakika amenikera mimi, na anikeraye hakika huwa amemkera Mwenyezi Mungu, na amkeraye Mwenyezi Mungu pana wasiwasi wa kuchukuliwa.” (Ahmad). Na katika kitabu cha imam bukhari na muslim kutoka kwa Bara`a ibn A`zib, kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema kuhusu Maanswar; hawapendi hao (Maanswar) isipokuwa ni muumini, na wala hawachukii isipokuwa ni mnafiki, atakaewapenda basi atapendwa na Mwenyezi Mungu, na mwenye kuwachukia atachukiwa na Mwenyezi Mungu. Kuwapenda ni dalili ya imani na ni kumtii Mwenyezi Mungu, na kuwachukia ni unafiki na uasi. Imepokewa na Anas bin malik (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “dalili ya imani ni kuwapenda Maanswari, na dalili ya unafiki ni kuwachukia Maanswari.” (Bukhari).

Uisilamu umeharamisha kuwasema vibaya masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) kwani aliowachagua ili wawe na Mtume –naye ni Mwenyezi Mungu – amewasifu na kuwaridhia. Na kama alivyotukataza Mtume (rehma na amani zimshukie) juu ya kuwatusi. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie), hakika ya Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: Musiwatusi masahaba wangu, musiwatusi masahaba wangu naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake lau kama mmoja wenu angelitoa dhahabu mfano wa jabali la Uhud basi asingelifikia kwa utoaji huo wala nusu yake.” (Muslim). Na kutoka kwa Abdalla bin Umar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema. Musiwatukane masahaba wa Mtume Muhammad (rehma na amani zimshukie), kwani kisimamo cha ibada ya mmoja wao cha saa moja ni bora kuliko ibada ya miaka arobaini ya mmoja wenu.” (ubora wa masahaba, Imam Ahmad). Kwa ajili hiyo ni wajibu wetu kuwapa heshima na kuelewa vyeo vyao.

Na mwenye kuangalia maisha ya masahaba (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) ataona kiwango kikubwa sana cha imani waliyokuwa nayo, na kufuata amri za Mwenyezi Mungu na Mtume wake (rehma na amani zimshukie), atakutia kuwa kuna ufasiri wa kiuhakika wa utendaji matendo mazuri, walikuwa ni viongozi wema walioonyesha mfano wa utoaji, elimu, utendaji, kujitolea muhanga kwa ajili ya kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, mpaka wakateremshiwa aya { Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli.}(Alhashri.8) .

Na mfano wa wazi kabisa ni, sahaba Ali bin Abi Twalib (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) alipojitolea kulala katika kitanda cha Mtume (rehma na amani zimshukie) usiku wa kuhama kwa Mtume ili ajitoe muhanga kwa nafsi yake na roho yake hali ya kuelewa kuwa washirikina wanamsaka kwa mapanga kwa ajili ya kumuua.

Pia sahaba Suhayb Ruumi alijitolea muhanga wa mali zake kwa ajili ya kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, na kumnusuru Mtume (rehma na amani zimshukie) wakati alipotaka kuhamia Madina. Makafiri wa kikuraish wakamwambia: “ulikuja kwetu huna kitu, ukaupata utajiri kutoka kwetu, na kufikia ulipofikia kisha unataka kutoka wewe na nafsi yako, hiyo haiwezekani. Akawaambia: “Mnaonaje iwapo nitakupeni mali zangu mutaniachia? Wakasema: “ ndio” akasema: “ninakuwekeni mashahidi kuwa mali yangu nimewaachilia nyinyi.” Ikamfika hilo Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema: Suhayb amepata faida, suhayb amepata faida.” (Ibn Haban).

Mfano mwengine ni Abu bakar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) anatupa mfano mzuri wa maadili mema, na sifa nzuri mpaka akawa ni kigezo cha kila jema. Na Mtume akamshuhudia kwa hili kuwa ni katika watu wa peponi. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) nani kaamka hali ya kuwa amefunga? Abu Bakar akasema: “mimi”. Akasema: “ni nani kati yenu aliyeshindikiza jeneza?” Abu Bakar akasema: “mimi” akasema: “ni nani kati yenu aliyelisha masikini?” Abu Bakar akasema: “mimi” akasema: “ni nani kati yenu aliyetembelea mgonjwa?” Abu Bakar akasema: “ mimi” Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema mambo haya yakikusanyika kwa mtu basi ataingia peponi.” (Muslim).

Nae sahaba Umar (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) siku moja alikuwa akitembea usiku, tahamaki kuna mwanamke ana watoto na chungu kipo motoni na watoto wamejikunyata. Umar akasema: Amani juu yenu enyi watu wa mwangani, alichukia kusema enyi watu wa motoni, mwanamke  akasema: “nawe amani iwe juu yako”. Akasema (Umar) je nikaribie? Akasema (mwanamke) ikiwa kwa heri karibia na kama kwa shri usikaribie, akakaribia, akasema: “ muna nini? Akajibu: “usiku umekuwamfupi kwetu pamoja na baridi. Akasema: “na hawa watoto wana nini mbona wamejikunyata? Akasema: ‘ni njaa. Akasema: “ndani ya chungu hiki muna kitu gani?” Akasema: “cha kuwadanganyia mpaka walale, na Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi juu ya Umar. Akasema “Mungu akurehemu, munamjuaje Umar?” akasema: “Umar unatuongoza kisha anatusahau.” Zaid – mpokezi wa hadithi- anasema: “ akanikabili kisha akaniambia tuondoke, tukaondoka huku tunakazana mpaka tukafika nyumba ya unga (nyumba ya hazina), akatoa kiwango cha unga na kopo la mafuta, akasema: “ nibebeshe: “ nikamwambia: “ mimi nitakubebea: “je nawe utanibebe mzigo wa madhambi yangu siku ya kiyama? Nikambebesha, akaondoka nami nikaondoka nae hali yakukazana. Tulipofika kwa Yule mwanamke tukautua akampa unga, akawa anamwambia tupa juu yangu na ninakutetemeka mimi mwenywe,  akawa anapuliza chungu. Akasema: “ nipe kitu chochote (cha kupakulia) akapewa na kupakuwa ndani yake huku akisema: “walishe na mimi nitawashikia, akawa katika hali hiyo mpaka wakashiba, na baadae wakamuacha akaondoka nami (Zaid) nikaondoka nae. Naye Yule mwanamke akawa nasema Mungu akulipe kila la kheri, jambo hili ulilolifanya ni jema kuliko afanyavyo kiongozi wa waumini: ‘nikamwambia “ sema mema pindi kiongozi wa waumini atakapokujia, na nisimulie kuhusu yeye akipenda Mungu, kisha akajiweka upande na baadae akamsogelea na kukaa  kitako ,na kumpokea tukamwambia: “ tuna jambo jengine lisilo hili na akawa hatuzungumzishi mpaka nilipowaona watoto wamelala na kutulizana, akasema : amani, hakika njaa imewafanya wasilale na kuwafanya walie na nilipendelea kuwa nisiondoke mpaka nione niliyoyaona. (ubora wa masahaba, imamu Ahmad).

Na hata masahaba wa kike (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) nao wana fadhila na misimamo ya kujitolea muhanga kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu, kwa mfano: –

Msimamo wa Mama wa waumini Khadija (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) alivyokuwa na msimamo wa kueneza dini ya Mwenyezi  Mungu pale aliposimama wima na mumewe na kujitolea muhanga kwa mali zake na nafsi yake, na kumtuliza kutokana na hofu aliyokuwa nayo (rehma na amani zimshukie) wakati alipoteremshiwa wahyi katika jabali la Hiraa,na kumwambia kwa kujiamini, na wala kutetereka: “ hakika Mwenyezi Mungu hakuhuzunishi katu, wewe utaunga ukoo, na kubeba yote na kumpata asiyekuwepo, na kumtuliza mgeni na kusaidia kwenye haki. (Bukhari) akawa ni katika wake wema sana mwenye kujua wajibu wake na haki. Vilevile Mtume (rehma na amani zimshukie) alikuwa akimtaja sana na kumsifia, kutoka kwa Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu) amesema: Mtume (rehma na amani zimshukie) alikuwa akitajwa Khadija huwa anamsifia,, akasema: “ nikawa na wivu siku moja, nikasma: “mbona unamtaja sana huyu mwenye uso mwekundu  yaani khadija ,na Mwenyezi Mungu amekubadilishia mbora kuliko yeye. Mtume akasema (rehma na amani zimshukie) Mwenyezi Mungu hajanibadilishia mbora zaidi yake, kwani yeye aliniamni wakati watu wakinipinga, na kuniona ni mkweli wakati watu wakiniona ni mwongo, na kuniliwaza kwa mali zake wakati watu walinitenga, na Mwenyezi Mungu amenipatia kutoka kwake watoto wakati sikupata watoto kutoka kwa wanawake wengine.” (Ahmad)

Na mfano mwengine mwema na wa kuigwa wa masahaba wa kike (radhi za Mwenyezi Mungu  ziwashukie) ni Mama Umarah nasiybah bint Ka`ab Al answari ambaye Mtume (rehma na amani zimshukie ) alisema kuhusu yeye: “ mimi katika vita ya Uhud sikuwa nikigeuka upande wa kulia wala wa kushoto isipokuwa nilikuwa nikimuona Umu Umarah akipigana pamoja nami.”  Mpaka  mtu akitaka kumuua Mtume (rehma na amani zimshukie) anamuona Umu Umrah yupo mbele yake, na hupigana naye kwa panga mpaka bega lake likajawa na damu kutokana na mapigo ya mapanga. Mtume akamwambia: “ ni adhabu gani uipatayo ewe umu umarah, akajibu”: “lakini ninaweza kuivumilia, ninaweza, ninaweza ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Mtume (rehma na amani zimshukie) niombe ewe Umu Umarah” akasema: “naomba niwe nawe peponi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema sio wewe peke yako bali na watu wa nyumba yako pia. Akasema (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) sijali kwa yanipatayo duniani.” Kitabu cha Siyra A`alam Anubalaa)

Na iwapo tunataka kuendelea na kuokoa na matatizo na kufanikiwa kwa kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu hapa duniani na kesho akhera, basi hatuna budi tufuate mwangaza tuliomurikiwa kwa nuru ya masahaba wa Mtume (rehma na amani zimshukie) na kufuata mwenendo waona tabia zao, wao ni kigezo cha waumini na waislamu wote. Mtume (rehma na amani zimshukie ) katuhimiza kuwafuata na kushikamana na mwenendo wao pia, kutoka kwa Urbaadh bin Sariyah kuwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “ jilazimisheni kufuata mwenendo wangu na mwenendo wa makhalifa walioongoka, na chukueni kwa kukaza magego, na tahadharini na yenye kuzuka, kwani kila la uzushi ni upotofu.” (Ibn Majah).

Na juu yetu kujifunza na watoto wetu na wake zetu juu ya mwenendo wa masahaba watukufu, ni namna gani walikuwa wakimfuata Mtume (rehma na amani zimshukie) na kujitolea kwao muhanga kwa ajili ya kuinusuru dini na kumnusuru Mtume (rehma na amani zimshukie) kwani waliziuza nafsi zao kwa ukweli na kwa uyakini hii yote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Uhusiano wa kifamilia ulio bora
23 Jamad Akhir 1437 H. sawa na 1 Aprili 2016 AD

awkaf-

Vipengele

 1. Nafasi ya familia katika uisilamu.
 2. Njia za uongofu katika kuwepo kwa utulivu wa kifamilia.

  1. Uchaguzi bora
  2. Kuchunga ya haki na yaliyo lazima
  3. Kuwepo kwa upendo na huruma
  4. Kuishi kwa salama
  5. Uadilifu kati ya watoto.
 3. Athari za kuwepo kwa utulivu wa familia katika jamii.

Pili: dalili

Ndani ya Qurani Tukufu.

 1. Mwenyezi Mungu anasema {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika  haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri} (Aruum. 21).
 2. Mwenyezi Mungu anasema { Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni mwake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?}(An hahl. 72)
 3. Mwenyezi Mungu anasema { Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua.}(An nuur 32)
 4. Mwenyezi Mungu anasema { Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. }(Al baqara 228)
 5. Mwenyezi Mungu anasema { Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.}(Anisaa 19.)
 6. Mwenyezi Mungu anasema {Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume,na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari}(Anisaa 35)

Mwenyezi Mungu anasema { Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa. }(Atalaak.7)

Dalili katika hadithi

 1. Kutoka kwa Abdallah bin Masuud (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “ enyi vijana mweneye kuweza miongoni mwenu kuoa basi na aowe, kwani hivyo ni kuinamisha macho na kuhifadhi tupi. Na asiyeweza basi afunge kwani hiyo ni kinga.” (Bukhari na Muslim).
 2. Na kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) : “mwanamke huolewa kwa mambo manne; kwa mali yake na nasaba (ukoo) yake na uzuri wake na dini yake, chagua aliye na dini ili ubarikiwe mikono yako.” (Bukhari).
 3. Kutoka kwa Anas (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: Wageni watatu walikuja katika nyumba za wake wa Mtume (rehma na amani zimshukie) kuja kuuliza kuhusu ibada ya Mtume (rehma na amani zimshukie) na walipoelezwa wakawa kama kwamba wamejiona ni wadogo wakasema: “tuko wapi sisi na Mtume? Amekwishasamehewa madhambi yaliyotangulia na yaliyochelewa. Na mmoja wao akasema: “ ama mimi nitasali sala za usiku milele. Mwengine akasema: “ mimi nitafunga na wala sitofuturu. Na wa mwisho akasema: “ama mimi  nitajiepusha na wanawake na sitaoa milele. Mtume (rehma na amani zimshukie) akawaendea akasema: “ni nyinyi muliosema hivi na hivi, ama mimi naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ninamuogopa Mweneyzi Mungu kuliko nyinyi nyote lakini ninafunga na kufuturu, ninasali na kulala na ninaoa wanawake, na mwenye kujiweka mbali na mwenendo wangu basi hayuko nami.” (Bukhari.)
 4. Kutoka kwa Abi hatim Almuzaniy amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie): atakapokujieni Yule munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, na musipofanya hivyo itakuwa ni fitina duniani na ufisadi. Wakasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na akiwa naye? “ akasema: “atakapokujieni Yule munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, mara tatu. (Tirmidhi) na katika kitabu cha Bayhaqi (atakapokuja yule munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, na musipofanya hivyo itakuwa ni fitina katika dunia na ufisadi mkubwa mno.)
 5. Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari)
 6. Kutoka kwa Abdallah bin Amru bin Al`as (Radhi za mwenyezi Mungu ziwe juu yao) amesema: nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “inatosha mtu kuwa na madhambi kwa kukizembea kile anachokilisha.”(Ahmad). Na katika mapokezi ya  Hakim (inatosha mtu kuwa na madhambi kwa kukizembea kile anachokilea.)

 Maudhui

Uisilamu umejali sana familia kwani ni nguzo ya kwanza ya kujenga,  jamii familia ikitengemea na jamii nayo hutengemea na ikiharibika na jamii pia huharibika. Kwa ajili hiyo uisilamu ukaweka shuruti na vipimo vitakavyosimamia jambo hili, kwa ajili ya kuwepo na utulivu na usalama kwa lengo la kuhifadhi watu na jamii nzima, kwani utulivu wa familia ni utulivu wa jamii.

***********************

Uisilamu umefuatilia uhumimu wa familia hata kabla ya makutano (ndoa) katika wa wanajamii kwa kutaka kuwepo upendo, huruma na ushirikiano na kupunguza kila kinachopelekea uharibifu wa jengo hilo. Na ukawataka wafuasi wake kutengeneza familia kwa njia zinazokubalika zenye kuhifadhi utu na heshima ya mwanadamu yenye kwenda sambamba na maumbile yake na njia hiyo ni ya kuozana ambayo ni mojawapo ya mwenendo wa Mwenyezi Mungu kwa  viumbe vyake vyote. {na kila kitu tumekiumba viwiliviwili ili mupate kukumbuka} (Adhariyat. 49). Na anasema pia {utukufu ni wake aliyeumba kike na kiume katika vile viotavyo katika ardhi na katika nafsi zenu na katika vile musivyovijua} Yaasin. 36). Ndoa ni mwenendo wa kimaumbile. Na mwenyezi Mungu akaifanya kuwa ni mojawapo ya ishara za utukufu wake na nguvu zake na miujiza yake mikubwa yenye kushangaza, akasema { Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.}(Ruum. 21).

Na kama uisilamu ulivyopendekezesha kutengeneza familia na utulivu wake kuwa ni kuijenga ardhi na kuleta masilahi kwa jamii na ujenzi wa taifa na kuwa ni njia ya kufikia katika lengo lililokusudiwa: nalo ni kueneza heshima na utu na kuilinda jamii kutokana na aina zote za uchafu na maovu, na kuunganisha familia kwa njia ya kuozana, pamoja na hekima nyengine na malengo yaliyo mazuri. Mwenyezi Mungu anasema { Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri, Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua. 33. Na wajizuilie na machafu wale wasio pata chakuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu.Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye  kurehemu.} (Anuur 32.33). bali pia Mtume (rehma na amani zimshukie) amewahimiza vijana wafikie lengo la kuona kwa kuweka wazi manufaa yake na faida zake akasema: ““ enyi vijana mwenye kuweza miongoni mwenu kuoa basi na aowe, kwani hivyo ni kuinamisha macho na kuhifadhi tupi. Na asiyeweza basi afunge kwani hiyo ni kinga.” (Bukhari na Muslim).

Kinyume na hivyo, uisilamu umekataza mambo yenye kupingana na uimarishaji wa ulimwengu, mfano kukaa bila ya kuoa na kujiweka mbali na wanawake (kukataa kuoa), mtme (rehma na amani zimshukie) amekataza kukaa bila ya kuoa, Saad bin abi Waqas (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema, hali ya mtume (rehma na amani zimshukie) kumjibu Othman bin Mad ghun kuhusu kuacha kuoa, na lau kama angeruhusiwa basi nasisi tungelihusika pia.” (Muslim). Na kutoka kwa Anas (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema wageni watatu walikuja katika nyumba za wake wa Mtume (rehma na amani zimshukie) kuja kuuliza kuhusu ibada ya Mtume (rehma na amani zimshukie) na walipoelezwa wakawa kama kwamba wamejiona ni wadogo wakasema: “tuko wapi sisi na Mtume? Amekwishasamehewa madhambi yaliyotangulia na yaliyochelewa. Na mmoja wao akasema: “ ama mimi nitasali sala za usiku milele. Mwengine akasema: “ mimi nitafunga na wala sitofuturu. Na wa mwisho akasema: “ama mimi  nitajiepusha na wanawake na sitooa milele. Mtume (rehma na amani zimshukie) akawaendea akasema: “Ni nyinyi muliosema hivi na hivi, ama mimi naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ninamuogopa Mweneyzi Mungu kuliko nyinyi nyote lakini ninafunga na kufuturu, ninasali na kulala na ninaoa wanawake, na mwenye kujiweka mbali na mwenendo wangu basi hayuko nami.” (Bukhari.)

Na ilivyokuwa  utulivu wa familia ni kitu kitakiwacho kisheria na hata kidunia basi usilamu ukaweka nguzo madhubuti na misingi imara ili ukoo na familia idumu kati ya wanandoa na upatikane utulivu unaotakiwa, na miongoni mwa misingi hiyo ni:-

 • Uchaguzi mwema kwa kila mwanandoa kwa mwengine, Mtume (rehma na amani zimshukie) aliusia wakati wa kuchagua mke kuwa uchaguzi uwe mwema kwani una masilahi na unahifadhi mali na heshima na ni starehe nzuri duniani. Kutoka kwa Abdalla bin Amruu (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie): “ dunia ni starehe na starehe iliyo bora zaidi ni mke mwema.” Na familia inapojengwa kwa uchaguzi uliobora basi ndipo utulivu, mapenzi ya kudumu, kuoneana huruma kunapatikana, na hapo tena ndoa inakuwa ni yenye Baraka na kuwa na athari.

Na katika uchaguzi hakuna budi iwe ni kwa misingi ya dini na tabia, imepokewa na Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) : “mwanamke huolewa kwa mambo manne; kwa mali yake na nasaba (ukoo) yake na uzuri wake na dini yake, chagua aliye na dini ili ubarikiwe mikono yako.” (Bukhari). Na katika mapokezi ya Imam Ahmad kutoka kwa Abi Saad Alkhudriy (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema: amasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “mwanamke huolewa kwa moja ya mambo matatu; huolew mwanamke kwa mali zake, huolewa mwanamke kwa uzuri wake, na huolewa mwanamke kwa dini yake, chukua mwenye dini na tabia ubarikiwe mkono wako. (Ahmad)

Mke ana nafasi kubwa katika kulea familia, akiwa mwema basi nayo huwa njema na jamii itakuwa na utulivu na kama si mwema basi familia huporomoka.

Mshairi anasema:

Mama ni shule pindi ikiandaa * itaandaa watu weney asili njema.

Pia Mtume (rehma na amani zimshukie) ameusia wakati wa kuchagua mke kuwa uchaguzi uambatane na dini na tabia. Kutoka kwa Abi Hatim Almuzaniy (radhi za mwenyezi Mungu zimshukie) amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie): atakapokujieni Yule munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, na musipofanya hivyo itakuwa ni fitina duniani na ufisadi. Wakasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na akiwa naye“ akasema: “atakapokujieni Yule munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, mara tatu. (Tirmidhi). Mtume akafanya kuwa dini na tabia kuwa ndivyo sifa muhimu za ndoa njema, kwa ajili hiyo, uchaguzi sahihi ni misingi ya dini ambayo utulivu wa familia utapatikana ambao utakuwa ni sababu ya kuendelea kwa jamii.

 • Na miongoni mwa utulivu ni; kila mmoja katika wanafamilia achunge wajibu na haki. Kwani Uisilamu umetoa haki na wajibu ulio sawa kwa wanandoa wote, Mwenyezi Mungu akasema { Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao.}(Al baqara 128). Mwanafamilia hatotakiwa kutekeleza haki ya mwengine kabla ya kutekeleza haki aliyonayo yeye kwanza ili upendo na utulivu upatikane vitu ambavyo vinaituliza familia.

Uisilamu ukaweka wazi wajibu na haki hizi, na ukazigawa kwa wanandoa na kutaka kila mmoja kujilazimisha na kuzihifadhi, kwani kuna haki za kimali na za kiroho na kimalezi, pia kuna haki za kushirikiana katika ujenzi wa kutekeleza majukumu. Na umuhimu wa kusaidiana kati ya wanafamilia kutokana na mahitajio ya maisha. imepokewa katika hadithi ya Abdallah bin Amru (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) kwamba yeye amemsikia Mjumbe wa Mweneyzi Mungu akisema nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari). Na kutoka kwa Abdallah bin Amru bin Al`as  (Radhi za mwenyezi Mungu ziwe juu yao) amesema: nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “inatosha mtu kuwa na madhambi kwa kukizembea kile anachokilisha.”(Ahmad).

Mmoja wa masahaba alimuuliza Mtume (rehma na amani zimshukie) akasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni ipi haki ya mke wa mmoja wetu kwake?” akasema: “kumlisha unapokula, kumvisha unapovaa au unapopata, usimpige usoni, wala usimnange (usimwambie kama ni mbaya) na wala usimkimbie isipokuwa ndani ya nyumba.” (Abi Daudi).

Mfano huu wa Asmaa bint Yazid Al ansareyyah anamuuliza Mtume (rehma na amani zimshukie) anasema: “ Kwa hakika sisi wanawake kuna wengi  wetu wamefungwa na kuwekwa ndani katika misingi ya nyumba zenu na kumaliza matamanio yenu na kubeba mimba za watoto wenu. Nyinyi wanaume mumefadhilishwa sana kuliko sisi kwa kusali sala ya Ijumaa na sala za pamoja, kuwatembelea magonjwa, kushindikiza jeneza, kuhiji tena na tena, na bora kuliko yote ni kuwa munapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mtu yeyote miongoni mwenu akitoka na kwenda kuhiji au kufanya umra tunakuhifadhieni mali zenu na kukutengeeni nguo na kuwalea watoto wenu, hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hatushirikiani nanyi katika malipo? Akasema: “Mtume  (rehma na amani zimshukie) akawageukia sawa sawa (kwa uso wake) masahaba zake kisha akasema: “ mmesikia masuala ya mwanamke hakuna mazuri kama hayo katika masuala ya dini yaliyoulizwa, ni nani muulizaji?wakasema: “ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hatukuwa tukidhani kwamba mwanamke angeweza kuuliza kama hivi. Mtume (rehma na amani zimshukie) akamgeukia mwanamke na kisha akasema: “ ondoka ewe mwanamke, na waeleze wanawake walio nyuma yako kuwa, mwanamke akiwa mwema kwa mumewe na kutaka radhi zake na kumtii basi hupata malipo sana na hayo yote.” Akasema: “mwnamke akaondoka hapo hali ya kusema  “Lailahailla llah na Allahu Akbar, hali ya kujibashiria mema. (Mlango wa sehemu ya imani).

Kwa ajili hiyo kufanikiwa kwa familia ya kiisilamu ipo katika kuhifadhi haki na wajibu kati ya wanandoa na kujiepusha na uzembe na kukiuka mipaka.

 • Na miongoni mwa mambo yenye kusaidia kuleta utulivu ndani ya familia; ni kuenea kwa upendo kati ya wanafamilia, kwani upendo ni nguzo muhimu ndani ya nyumba na ni chanzo cha mafanikio yote ndani ya familia yenye njema. Nao ni muhimili mkubwa ambao unapaswa kwa kila mwanafamilia kuwa nao ili familia ineemeke kwa utulivu, upendo na msimamo, Mwenyezi Mungu anasema { Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri} (Ruum.21). Upendo kwa wanajamii wote umewekewa rehani kwa kuwepo katika familia. Na tuna kigezo kizuri kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) kwani alikuwa ni mfano wa upendo kwa watu wa familia yake wote bila kubaguwa, wake zake, watoto wake na hata wajukuu wake na mtumishi wake kwani yeye (rehma na amani zimshukie) alikuwa ni mbora kwa watu wake.

Na iwapo nyumba haina upendo basi maisha ya familia huwa ni mabaya na magumu, hivo, ni wajibu wa kila mwanafamilia awe makini katika kuhakikisha kuna upendo.

 • Na miongoni mwa utulivu wa familia: ni kuishi kwa wema, na hili nalo ametuamrisha Mola wetu na Mtume wetu nae ametuusia. Mwenyezi Mungu anasema Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.}(Anisaa 19.) kila mwanandoa anahitajika kuwa na mawasiliano na mwengine ili upendo uenee na ushirikiano uzidi hapo ndipo lengo la ilaka-uhusiano- litapatikana. Mwenyezi Mungu anasema { Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.}(Al baqara 187) na akasema pia { Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao.Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.}(Ruum. 21). Na akasema { na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. } (al araaf. 189).

Na katika yaletayo uhusiano mwema ni pamoja na maneno mazuri vitendo vyema, kusameheana, kusaidiana, kuheshimiana, kushauriana, kulinda siri, kujiepusha na mzozo na matatizo na mambo mengineyo yaliyo mazuri.

Na Mtume (rehma na amani zimshukie) pamoja na masahaba zake wametuwekea mifano mizuri kuhusu uhusiano wa kuishi na familia zao. Imepokewa kutoka kwa Aswad, amesema,: nimemuuliza Aisha (rehma na amani zimshukie) Mtume alikuwa akifanya nini nyumbani kwake? Akasema: “alikuwa akifanya kazi za watu wake- yaani alikuwa akiwasaidia wakeze – muda wa sala ukifika alikuwa akitoka na kwenda kusali. (Muslim). Na kutoka kwa ibn Abbas (radhi za Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: Mimi ninapenda kujipamba kwa mwanamke (mke wangu) kama nipendavyo yeye ajipambe kwa ajili yangu, kwani Mwenyezi Mungu anasema { Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu }(Al baqara 228). Na nipendalo ni usafi kwa haki zangu zote, kwani Mwenyezi Mungu anasema { Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao.} (Albaqara 228) (kitabu cha Ibn Abi Shayba).

Na miongoni mwa uhusiano mwema kati ya wanandoa; ni kumuachilia mmoja wapo matatizo yote ya ndani ya ndoa, uhusiano mwema unakusanya maana zote zinazoshikamana na uhai wa wanandoa. Hakina ya uisilamu unahimiza sana kuwepo kwa uhusiano wa mapenzi, kufahamiana na kuwa pamoja na hii ni hatua nzuri ya kujenga jamii.

Na miongoni mwa mambo ambayo yatasaidia kuendeleza familia: ni kushauriana kati ya wanandoa, kwani katika kushauriana kunaleta upendo kati yao. Hata katika mambo ambayo yataonekana kwa baadhi ya watu kuwa ni madogo mfano suala la kumnyonyesha mtoto miaka miwili, Mwenyezi Mungu anasema {Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao.} (Al baqara. 233). Mashauriano kati ya wanandoa na hata wanafamilia hujenga muongozo wa maisha ya dini yetu tukufu ya kiisilamu. Na amri iliyokuja katika aya hii ni kwa ujumla aliposema { Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa }(Ashuraa.38).  na jambo hili ndilo alilolofanya Mtume (rehma na amani zimshukie) kimatendo. Na katika mienendo mengine ya kushauriana kwake na wakeze, mfano; kama ilivyotokea kati yake (rehma na amani zimshukie) na mkewe bibi Umu Salama (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) siku ya Hudaibiya. Baada ya Mtume kumaliza kuweka ahadi za suluhu kati yake na watu wa Makka, akawaambia masahaba zake: “ simameni na chinjiyeni kisha nyoeni”. Mpokezi wa hadithi akasema: naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hajasimama mtu yeyote mpaka akarudia kusema tena hivyo mara tatu. Na ilivyokuwa hajasimama yeyote Mtume (rehma na amani zimshukie) akaingia hemani kwa Ummu salama akamueleza yaliyotokea kati yake na watu wake. Ummu salama akamwambia: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unataka wakusikilize kuhusu hilo? Toka kisha usizungumze na yeyote mpaka utakapochinja mnyama wako na kumuita kinyozi wako na kukutaka nywele. Mtume akatoka na hakumsemesha yeyote mpaka akachinja mnyama akamwita kinyozi na kumnyoa, na watu walipomuona wakasimama na kunyoa na wengine wakanyoana mpaka wakakaribia kusongamana.) (Muslim) Hassan Basriy (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) amesema; “ijapokuwa Mtume hakuwa na ulazima wa kufuata ushauri wa Ummu Salama isipokuwa amefanya hivyo ili watu wapate kumfuata na wala mwanamme asihisi kuwa kuna kasoro katika kufuata ushauri wa mwanamke.

 • Pia miongoni mwa misingi ya utulivu wa familia: ni kutoa mahitajio kwa wanafamilia wote, kwani ni haki ambayo sheria ya kiisilamu imewajibisha. Mwenyezi Mungu anasema { Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. }(Anisaa 34). Na kusema { Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. }(Albaqara 233). Na akasema pia {7 Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenyedhiki atoe katika alicho mpa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa.} (Atalaq. 7).
 • Na miongoni mwa mambo yenye kusaidia kuwepo kwa utulivu ndani ya familia: kuwepo kwa uadilifu kwa wanafamilia, malezi mema ya kidini kwa watoto na kuwafundisha mambo ya dini. Uadilifu ni nguzo muhimu sana katika kuendelea kwa familia, Mtume (rehma na amani zimshukie) ametuhadharisha kuwatafautisha watoto katika kuwa nao kwa ajili ya kuhifadhi ushirikiano na kuwa pamoja kwa wnafamilia. Imepokewa na Nuuman bin Bashiir (radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie) amesema: baba yangu alinitolea sadaka kwa baadhi ya mali zake. Ummu Umra bint Rawaha akasema: “ sikubali mpaka tumuweka Mtume kuwa ni shahidi, baba yangu akaondoka mpaka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) ili awe ni shahidi wa sadaka yangu. Mtume (rehma na amani zimshukie) akamuuliza, je, umefanya hivyo kwa wototo wako wengine? Akasema: “hapana” akasema: “ Muogopeni  Mwenyezi Mungu na wafanyieni uadilifu watoto wenu.” Baba yangu akarudi na kuirudisha ile sadaka. (Muslim).

Uisilamu umeiangalia familia kwa mtazamo wa heshima na kuitukuza, kwani ni mfungamano uliosafi na ni malengo yaliyo matakatifu, na ukataka familia ibakie kuwa ni madhubuti yenye kushikamana. Ifikie malengo yake na isimame imara penye matatizo. Kwa ajili hii, uisilamu ukaiangalia kwa umakini zaidi na kuweka adabu ambazo zitakuwa ni msingi wa kujenga familia iliyoshikamana na yenye nguvu. Na yenye kuhifadhi utulivu wa jamii na kuweko mbali na aina zote za kiugaidi na utumiaji wa nguvu.

Jamii itakapokuwa na utulivu wa watu wote watahisi usalama katika nyanja zote, kinafsi, kimwili kijamii na kiuchumi, kitu ambacho kitaakisi jamii ya kiisilamu na uwepo wake wa amani na utulivu. Uisilamu umezingatia utulivu wa familia ni njia mojawapo ya kuhakikisha usalama wa kijamii kwa kuepukana na ufisadi na mizozo, mwanzo wa usalama wa jamii unatokana na familia, kisha shuleni na baadae katika jamii nzima.

Familia ni shule ya kwanza ambayo mtoto huelimishwa zuri na baya, kheri na shari, na kujifunza kutimiza majukumu na uhuru wa maoni. Familia ndio imjengayo mtoto na kujulikana nini akitakacho na iwapo atakuwa ni raia mwema ndani ya jamii yake.

Usalama hauletwi kwa nguvu, hutetwa na wanajamii weneywe, kupitia dhamiri zao na kwa nafasi kuu ya familia katika kutengeneza dhamiri na kuikuza katika nafasi za watu wake.

Na kwa hili nimeandika beti zifuatazo:

Mokhtar-300x198

Misri tukufu iliyohifadhika Kitabu kitukufu kimetaja amani yake Na ikidhoofisha siku moja itapona haraka haraka Na uisilamu utarudi hali ya kuenea Na umma wa kiarabu utakuwa na nguvu zake Atakaekuja kwa amani atapokewa Na atakaekuja kwa vita basi sisi ndio wenyewe Hatufanyi uadui na wala haturidhii khiyana Nguzo yeu ni ujanadume Moja ya mawili ndio tutakacho Ushindi mkubwa au kuonekana mashahidi Iulizeni historia kuhusu mashujaa wake Na lieleweni jeshi la mtume Jeshi bora ni jeshi la Misri, liheshimuni Ardhi bora ni haki yake na ni cheo chake

Sifa za waumini ndani ya kurani
17 jamad uwla 1437 H. 26/22016

awkaf-

Kwanza: vipengele

 1. Kumjua Mweneyzi Mungu ni njia ya imani
 2. Imani na matendo mema ni mambo yenye mshikamano

  Sifa za waumini

  1. Kumuogopa Mwenyezi Mungu.
  2. Kumtegemea Mwenyezi Mungu ipasavyo.
  3. Kuhifadhi sala na kunyeyekea ndani yake.
  4. Kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  5. Ukweli, uaminifu, kutimiza ahadi, haya na tabia njema.
 3. Neema alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa waumini.

Pili: Dalili:

Dadili ndani ya Kurani tukufu

 1. Mweneyzi Mungu Mtukufu anasema {1. Hakika wamefanikiwa Waumini,2. Ambaoni wanyenyekevu katika Sala zao, 3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi, 4. Na ambao wanatoa Zaka. 5. Na ambao wanazilinda tupu zao, 6. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamilikimikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. 7. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndiowarukao mipaka. 8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao, 9. Na ambao Sala zao wanazihifadhi Hao ndio warithi,} Almuuminun 1-10.
 2. Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa MwenyeziMungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zakehuwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 3. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku 4. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira,na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi. }Al anfal, 2-4.
 3. Mwenyezi Mungu anasema: {Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mleziwananyenyekea, 58. Na wale ambao Ishara za Mola wao Mleziwanaziamini, 59. Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,60. Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, 61. Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo yakheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.} Almuuminun 57-61.
 4. Mwenyezi Mungu anasema {Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.160. Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wakukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yakeYeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu} Al imran. 159-160.
 5. Mwenyezi Mungu anasema: {Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemezahujibu: Salama! 64. Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. 65. Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata tuhaimwachi. 66. Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya. 67. Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.} Alfurqan 63-67.
 6. Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli} Atawba,119.
 7. Mwenyezi Mungu anasema: { Enyi mlio amini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwawanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa. Lakinimsihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. HakikaMwenyezi Mungu anahukumu apendavyo} Almaida,1.

Dalili ndani ya hadithi.

 1. Kutoka kwa Ibn Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: siku moja tulipokuwa tumekaa pamoja na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akatutokezea mtu amevaa nguo myeupe sana ana nywele nyeusi haikuonekana athari yoyote ya safari na hakuna yeyote kati yetu aliyemjua mpaka akakaa mnele ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akakutanisha magoti yake na magoti ya mtume na kuweka bega lake katika bega la mtume kisha akasema: “ewe Muhammad nieleze kuhusu uisilamu.” Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ uisilamu ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na hakika Muhammad (rehma na amani zimshukie juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha sala, na kutoa zaka na kufunga ramadhani na kuhiji nyumba ukiwa na uwezo. Akasema: “umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu imani.” Akasema: “kumuamini Mwenyezi Mungu na malaika wake na vitabu vyake na siku ya mwisho na kuamini kadari kheri yake na shari yake. Akasema: “ umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu ihsani. Akasema: “ni kumuabudu Mwenyezi kama kama kwamba unamuona na iwapo humuoni basi yeye anakuona. Akasema: “Umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu kiama. Akasema: “huenda muulizaji akawa anaelewa zaidi kuliko anaeulizwa. Akasema: “ nieleze ishara zake” akasema: “ mtumwa kuzaa bwana wake na kuwaona wachungaji watembeao miguu peku wanashindana katika ujenzi wa majumba makubwa. Akasema, kisha akaondokam nikabaki hali ya kufikiria, kisha nikamuuliza ewe Umar unamjua ni nani huyo muulizaji? Akasema: “ Mwenyezi Mungu na mtume wake wanaju. Akasema Yule ni Jibrilu amekujieni kukufundisheni dini yenu.” (Muslim)
 2. Kutoka kwa Anas bin Malik (Mwenyezi mungu amwie radhi)hakika ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake siku moja alitoka na akakutana na kijana wa kianswar anaitwa Haritha bin Nuuman, akamwambia: “ umeamkaje ewe Haritha? Akasema: nimeamka hali ya kuwa ni muumini wa kweli. Akasema mtume wa Mweneyzi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) angalia usemacho, kwani kila haki ina kithibitisho, basi ni upi huo uthibitisho wa imani yako? Akasema: Najizoea nafsi yangu kujiepusha na ya dunia, nikakesha usiku wangu na kufunga mchana wangu, nami kama kwamba naagalia Arshi ya Mola wangu iliyo wazi na kama kwamba naagalia watu wa peponi namna wanavyotembeleana, na kama kwamba naangalia watu wa motoni na namna wanavyofanyiana uadui ndani yake. Mtume rehma na amani ziwe juu yake akamwambia. Umeona (umesema kweli) basi jilazimishe. Kasema hivi mara mbili, mja Mwenyezi Mungu amenawirisha imani ndani ya moyo wake.” (sehemu ya imani).
 3. Kutoka kwa Abi Hurayra (mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema mjumbe wa Mweneyzi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) imani ni sehemu sabini au sitini ya mafungu na bora ya (mafungu haya) ni kauli ya “Lailaha illa llahu” (hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuondosha uchafu njiani na kuona haya ni sehemu ya imani.” (Muslim)
 4. Kutoka kwa Umar (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema, nimemsikia mjumbe wa Mweneyzi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “ lau kama mungelimtegemea Mwenyezi Mungu kama ipasavyo basi angelikupeni riziki kama ampavyo ndege, huondoka asubuhi ana njaa na kurudi jioni ameshiba.” (Tirmidhi).
 5. Kutoka kwa Ibn Abbas (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) amesema, mtume alikwenda kwa Umar alipokuwa yupo na masahaba zake, akasema: “je nyinyi ni waumini?” hawakujibu. –akawauliza mara tatu- kisha mwishoni Umar akasema. “ndio, tunaamini kile ulichotuletea, na kushukuru juu ya hali nzuri na kusubiri juu ya balaa, na tunaamini kadari. Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) Akasema: “hakika mumeamini kwa jina la Mola wa Alkaba.” (Tabari).

Tatu: maudhui

Miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu ni na upendo wake kwa waja wake ni kuwapelekea mitume ili wawaongoze katika njia ya haki, na katika njia iliyonyooka, ili isije ikapatikana hoja kwa mja yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema { Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watuwasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewaMitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima }Anisaa 165.

Kumuamni Mwenyezi Mungu ni katika ilaka kubwa walizokuja nazo mitume, ikiwa na maana kuthibiti imani ya Mwenyezi Mungu –itikadi- ndani ya moyo wa mja, na kuamini malaika wake, vita  vyake, mitume wake, na siku ya mwisho na kadari kheri zake na shari zake. Na waumini itawalazimu watimize wajibu wa imani nao ni kutimiza yale waliyokalifishwa ambayo yana uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu yaliyoletwa kutoka kwa mtume wetu (rehma na amani zimshukie) katika makatazo na mahimizo.

Na kumjua Mwenyezi Munguni njia ya kwanza ya imani, Mwenyezi Mungu anasema { Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pakukaa.} Muhammah, 19.

Na kitu kijulikanacho ni kuwa imani ya Mwenyezi Mungu imeshikamana na matendo mema, na wala havitengani, imekuja katika kurani tukufu ndani ya aya nyingi, kwa mfano, { Na wale walio amini na wakatenda mema, hao ndiowatu wa Peponi, humo watadumu }Albaqara 82. Na { Hakika walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itakuwa inapita mito kati yao katika Mabustani yenye neema }Yunus 9. Na aliposema { Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi }kahf 107. Na aya nyeginezo zilizo tukufu.

Imani huzidi kwa kutii na hupungua kwa maasi, na kuna  sehemu (makundi) tafauti za waumini kwa mujibu wa imani zao kwa Mwenyezi Mungu. Kutoka kwa Abi Hurayra amesema: amasema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake)  imani ni sehemu sabini au sitini ya mafungu na bora ya (mafungu haya) ni kauli ya “Lailaha illa llahu” (hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuondosha uchafu njiani na kuona haya ni sehemu ya imani.” Na matendo mema ni sehemu ya imani.

Na imekuja katika hadithi ya Jibrilu – juu yake rehema- iliyo mashuhuri inayoweka wazi ukweli wa imani ambayo inapaswa kuwepo ndani ya nyoyo ya kila muumini, hadithi yenyewe, anasema umar (Mweneyzi mungu amwie radhi) amesema: siku moja tulipokuwa tumekaa pamoja na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akatutokezea mtu amevaa nguo myeupe sana ana nywele nyeusi haikuonekana athari yoyote ya safari na hakuna yeyote kati yetu aliyemjua mpaka akakaa mnele ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akakutanisha magoti yake na magoti ya mtume na kuweka bega lake katika bega la mtume kisha akasema: “ewe Muhammad nieleze kuhusu uisilamu.” Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ uisilamu ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na hakika Muhammad (rehma na amani zimshukie juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha sala, na kutoa zaka na kufunga ramadhani na kuhiji nyumba ukiwa na uwezo. Akasema: “umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu imani.” Akasema: “kumuamini Mwenyezi Mungu na malaika wake na vitabu vyake na siku ya mwisho na kuamini kadari kheri yake na shari yake. Akasema: “ umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu ihsani. Akasema: “ni kumuabudu Mwenyezi kama kama kwamba unamuona na iwapo humuoni basi yeye anakuona. Akasema: “Umesema kweli.” Akasema: “ nieleze kuhusu kiama. Akasema: “huenda muulizaji akawa anaelewa zaidi kuliko anaeulizwa. Akasema: “ nieleze ishara zake” akasema: “ mtumwa kuzaa bwana wake na kuwaona wachungaji watembeao miguu peku wanashindana katika ujenzi wa majumba makubwa. Akasema, kisha akaondokam nikabaki hali ya kufikiria, kisha nikamuuliza ewe Umar unamjua ni nani huyo muulizaji? Akasema: “ Mwenyezi Mungu na mtume wake wanaju. Akasema Yule ni Jibrilu amekujieni kukufundisheni dini yenu.” (Muslim).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka wazi katika kitabu chake kitukufu sifa nyingi za waja wake waumini,kwa mfano, unyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa unyenyekevu ni vyeo vya juu kabisa, Mwenyezi Mungu anasema { Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa MwenyeziMungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zakehuwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 3. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku 4. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira,na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi.}Al anfal 2-4. Na anasema { Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mleziwananyenyekea, 58. Na wale ambao Ishara za Mola wao Mleziwanaziamini, 59. Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,60. Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, }Al muuminuun 57-60. Na anasema pia { Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, naakamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basimbashirie huyo msamaha na ujira mwema.} Yasini, 11.

Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake ametupigia mfano wa hali ya juu ya unyenyekevu. Kutoka kwa Mutarif  kutoka kwa baba yake amesema: nimemuona mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akisali na katika kifua chake kuna mgurumo kama mgurumo wa chombo .” (Ibn Khuzayma). Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akimuomba Mweneyzi Mungu ampe unyenyekevu, kutoka kwa Abi Mijlaz (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Umar alitusalisha sala, akaifupisha, na akapinga (kuwa hakufupisha) akasema, kwami sijatimiza rukuu na sujudu? Wakasema: ndio” akasema: “kwa kuwa mimi nimeomba kwakati wa sujudu na kurukuu dua aliyokuwa akiomba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akiomba “ewe Mola kwa elimu yako ya visivyojulikana na kudura zako kwa viumbe nihuishe iwapo uhai una kheri nami na unifishe iwapo kifo kina kheri nami, nakuomba unyenyekevu wako kwa nikionacho na nisichokiona na neno la kweli niwapo na hasira na kuridhia, na lengo wakati wa umasikini na utajiri, na kadha ya kuona uso wako na hamu ya kukutana nawe na najikinga kwako kutokana na madha yenye kudhuru na fitina zenye kupoteza, ewe Mola zipambe nyoyo zeteu kwa imani na utufanye katika walioongoka.” (Ahmad).

Mshairi anasema:

Muogope mola na tarajia kila zuri * usiitii nafsi kwa maasi utajuta.

Kuwa na khofu na matarajio * na jibashirie msamaha wa Mungu iwapo ni muisilamu.

Namiongoni mwa sifa za waumini ni kumtegemea Mwenyezi Mungu, ikiwa na maana kuufanya moyo umtegemee Mwenyezi Mungu katika kuleta masilahi na kuondoa madhara, na kumuachia mambo yote Yeye pamoja na kuitakidi kuwa hakuna atoaye wala azuiaye na anayedhuru na kunufaisha isipokuwa Yeye pekee. Muumini humtegemea  Mwenyezi Mungu na hutenda sababu zenye kupelekea kutimia matendo bila ya kutegemea matendo hayo. Kufanya sababu haina maana kuwa humtegemei Mwenyezi Mungu, kutoka kwa Umar (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema, nimemsikia mjumbe wa Mweneyzi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “ lau kama mungelimtegemea Mwenyezi Mungu kama ipasavyo basi angelikupeni riziki kama ampavyo ndege, huondoka asubuhi ana njaa na kurudi jioni ameshiba.” (Tirmidhi).

Ama kwa wale wanaodai kuwa kumtegemea Mwenyezi mungu bila ya kufanya kazi huku hakuitwi kumtegemea Yeye bali huko ni kuzembea na kuzembea ametukataza mtume (rehma na amani zimshukie) na pia kukataza sababu zinazopelekea kuzembea, kutoka kwa Muadh bin jabal ( Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema; nilikuwa nyuma ya punda wa mtume (rehma na amani zimshukie) akiitwa Ukayr. Akasema (mtume) ewe Muadh hivyo unafahamu haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja na haki za waja kwa Mweneyzi Mungu? Akasema: Mwenyezi Mungu na mtume wake wanajua. Akasema: “haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na wala wasimshirikishe na chochote na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutomwadhibu Yule asiyemshirikisha na chochote.” Akasema: ewe mjumbe wa Mwenyezi Munguje niwaambie watu hivyo? Akasema: “usiwaambie ili wasije kuzembea” (muslim). Kumtegemea kunakotakiwa kunashikamana na maisha ya muumini, manufaa hayatopatikana au madhara isipokuwa kwa utegemezi ulio mzuri.

Na miongoni mwa sifa za waumini ni kuhifadhi sala na kunyeyekea ndani yake. Mwenyezi Mungu anasema { Hakika wamefanikiwa Waumini,2. Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao,}. Sala ni alama ya uisilamu na imeamrishwa kupitia aya nyingi Mwenyezi Mungu anasema{Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanao inama}Albaqara 43. Na mtume (rehma na amani zimshukie) akaifanya ni moja ya nguzo tano za kiisilamu, kutoka kwa Ibn Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema; amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (reahma na amani zimshukie) “ uisilamu umejemngea juu ya nguzo tano: kushuhudia kuwa hapana Mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu nakusimamisha sala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba na kufunga Ramadhani.” (Bukharin a Muslim).

Na watu wametafautiana kidaraja za unyenyekevu ndani ya sala, wapo wapatao malipo kamili, na wengine hawana wapatacho zaidi ya kujihangaisha na tabu, kutoka kwa Abi Hurayra (Rehma na amani ziwe juu yake) amemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: “ huenda anaesimama usiku kusali fungu lake likawa ni kukesha tu usiku, na huenda anaefunga fungu lake likawa ni kukaa na njaa na kiu.” (Albaihaqi). Sala ni sababu za kuifunza nafsi tabia na nyendo na kujiweka mbali na yenye kuchukiza, mwenye kusali huwa yuko mbali sana na sababu za kuingia katika maasi na maovu. Mwenyezi Mungu anasema { na ushike Sala.Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu.}Al ankabuut 45. Na katika yenye kuthibitisha kuwa ni lazima sala iwe na unyenyekevu ni hadithi iliyopokelewa na Anas bina Malik (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)amesema; amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) inakuwaje watu hunyanyua macho yao juu (mbinguni) ndani ya sala zao, akasisitizaneno lake hili mpaka akasema: waache hivyo au Mwenyezi Mungu atapofua macho yao.” (Bukhari).

Na miongoni mwa sifa za waumini ni kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa maana ya utoaji wa zaka iliyolazimishwa na sadaka za kujitolea, kutoka kwa Ibn Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: “mkono wa juu (utoao) ni bora kuliko wa chini (usiotoa), na anza kwa unaowalisha, na sadaka iliyo bora ni ile itolewayo kwa kificho na anayeacha kuomba Mungu atamsaidia na anayejitosheleza basi Mungu atamtoshelezea.” (Bukhari). Kutoka kwa Ibn Masuud (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amepokea kutoka kwa mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ mtu akitoa kwa ajili ya watu wake huhesabiwa ni katika sadaka.” (muslim). Muumini huamini kuwa mali aliyonayo ni kama dhamana kwake, na fadhila zipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Kutoka wa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) kwamba mtume  (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ kijana mmoja alipokuwa akitembea jangwani akasikia sauti utoka mawinguni, nyoshelezea bustani ya Fulani, mawingu yale yakasogea kachota maji yake katika chombo, tahamaki kile chombo kikajaa maji chote, mara kuna mtu mwengine amemsimama kwenye bustani yake akijaribu kunyoshelezea maji, akamwambia: ewe mja wa Mweneyzi Mungu, unaitwa nani? Akasema, ni Fulani lile jina alililisokia kutoka katika mawingu, akamwambia, kwa nini unaniulia jina langu, akamwambia: “ nimesikia sauti kutoka mawinguni ambayo yamenipa maji yake, yakisema “ nyosheleza bustani ya Fulani kwa kutaja jina lako, wewe kwani unafanya nini ndani ya bustani hiyo? Akajibu: “kwa kuwa umeuliza basi mimi huwa matunda yakiwa tayari basi hutoa sadaka thuluthi na mimi mwenyewe na wanangu hula thuluthi najirudisha thuluthi yake.

Na kurani imeashiria sifa za waumini kama ifuatavyo kwa mfano, wanajiepusha nay a upuuzi, na huchunga amana, Mwenyezi Mungu anasema {1. Hakika wamefanikiwa Waumini,2. Ambaoni wanyenyekevu katika Sala zao, 3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi, 4. Na ambao wanatoa Zaka. 5. Na ambao wanazilinda tupu zao, 6. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamilikimikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. 7. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndiowarukao mipaka. 8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao, 9. Na ambao Sala zao wanazihifadhi  10. Hao ndio warithi, 11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo} Almuuninuun 1-11. Aya zikaweka wazi kuwa mafanikio na kufuzu ni kwa atakayesifika kwa sifa hizi za unyenyekevu ndani ya sala, kujiepusha na upuuzi, kutoa zaka, kuhifadhi tupu, kuhifadhi amana na kuzifikisha kwa wenyewe, kutimiza ahadi na yote hayo yametajwa ndani ya kurani kama ni sifa kwa waumini na tabia zao.

Kwa waumini ni lazima wawe na tabia ya kutimiza ahadi kama ilivyokuja ndani ya kurani ili ajidhaminie mafanikio duniani na akhera, ikipatikana imani ndani ya moyo wa mja kama itakiwavyo basi itamuhifadhi na chuki na itikadi kali na kutenda yaliyokatazwa na itamfanya ampendelee mwengine zaidi kuliko hata nafsi yake na atajiepusha na kauli za uongo na kukaa vikao vya kipuuzi, na atakuwa na pupa ya kufanya mema kwa ajili ya manufaa ya jamii na taifa lake. Ama kwa wanaojidai kuwa ni wauminina tabia zake zikawa ni mbaya na mwenendo wake ukawa si mzuri basi imani yake huwa ni pungufu. Kwani imani ahihi hujulikana, Kutoka kwa Anas bin Malik (Mwenyezi mungu amwie radhi)hakika ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake siku moja alitoka na akakutana na kijana wa kianswar anaitwa Haritha bin Nuuman, akamwambia: “ umeamkaje ewe Haritha? Akasema: nimeamka hali ya kuwa ni muumini wa kweli. Akasema mtume wa Mweneyzi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) angalia usemacho, kwani kila haki ina kithibitisho, basi ni upi huo uthibitisho wa imani yako? Akasema: Najizoea nafsi yangu kujiepusha na ya dunia, nikakesha usiku wangu na kufunga mchana wangu, nami kama kwamba naagalia Arshi ya Mola wangu iliyo wazi na kama kwamba naagalia watu wa peponi namna wanavyotembeleana, na kama kwamba naangalia watu wa motoni na namna wanavyofanyiana uadui ndani yake. Mtume rehma na amani ziwe juu yake akamwambia. Umeona (umesema kweli) basi jilazimishe. Kasema hivi mara mbili, mja Mwenyezi Mungu amenawirisha imani ndani ya moyo wake.” (sehemu ya imani).

Inatakiwa muumini asifike kwa sifa njema za ukweli, uaminifu, kutekeleza ahadi, ukarimu, haya, msimamo, upole, msamaha, unyeyekevu, uadilifu, hisani, kuathiri na tabia nyengine njema ambazo kurani imehimiza, Mwenyezi Mungu anasema {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli}At tawbah 119. Na akasema { Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao } Al maarij 32. Na akasema kuhusu alama za wakweli wacha Mungu. { na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; haondio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao } Al baqara 177.

Na Mwenyezi Mungu amewandalia waumini wenye kusifika kwa tabia njema kwa malipo mazuri na thawabu njema, akasema { Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi108. Watadumu humo; hawatataka kuondoka.} Kahf 107-108.