Habari

Uislamu ni utendaji na Mwenendo. Mifano itokanayo na Maisha ya Taabiina

Sifa zote njema ni zake yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَالَّذِينَ جَاءُوا مِنْ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ}

Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na kwamba Bwana na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Mlezi wetu, tunakuomba umswaslie, umpe Rehema na umbariki Bwana wetu, yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakayewafuata kwa wema mpaka siku ya Mwisho.

Na baada ya Utangulizi huu,

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huwachagua katika waja wake, watakaoitumikia Dini yake na kuwa na moyo mkunjufu kwake na kwa Ujumbe wake. Na Mtume S.A.W, amesema kwamba chaguo la Uma huu ni Maswahaba wake R A, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia waliowafuatia Maswahaba R.A. Kutoka kwa Abdillahi bin Masoud R.A, amesema: anasema Mtume S.A.W: Watu walio bora zaidi ni wa Karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia…

Kwa hiyo hawa ndilo chagua la Mwenyezi Mungu Mtukufu waliosifika kwa Kheri nyingi, na walioibeba Amana ya Elimu, wakiisafisha kutokana na kauli za wapotoshaji na mwenendo wa walio batili, na tafsiri potofu za wajinga. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu na akawajumuisha na Maswahaba wa Mtume S.A.W, na kuwapa wasifu wa Ihsani, na akawaridhia wote, na akawaahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu Pepo yenye kupita Mito chini yake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ}

Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Muhahajirina na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Na Taabiina (waliowafuatia Maswahaba) ni Watu walio karibu zaidi na zama za Mtume S.A.W, kwani wao ni Kizazi cha Maswahaba wa Mtume R.A, na waliowafuatia wao ni Kizazi cha pili cha Waliowafuatia Maswahaba wa Mtume S.A.W, na walijifunza mikononi mwao R.A.

Na wote wamechukua elimu zao kutoka kwa Mtume S.A.W, na waliambatana na Maswahaba wa Mtume R.A, kwa fadhila na kwa elimu; na katika hili tunaupata Ushahidi wa Bin Omar R.A, kwa Saiid bin Musiib R.A, kwa kauli yake: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakika yeye ni miongoni mwa Watoa Fatwa. Na alikuwa anasema: Muulizeni Saiid bin Musiib; hakika yeye aliketi na Wema. Na Saiid bin Musiib alikuwa akitoa Fatwa na Maswahaba wakiwa hai. Na Atwaau bin Abuu Rabaah alikuwa akiketi na wavulana akiwa Makkah baada ya kufariki kwa Mtaalamu wa Uma Abdullah bin Abas R.A, na Bin Omar R.A, alipokuja Makkah wakamuuliza akasema: Enyi Watu wa Makkah mnanikusanyia mimi masuala mbalimbali wakati mnae Abu Rabaah?

Taabiina walikuwa wakijulikana mno kwa ukweli wa mapenzi yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hasanil Basriy Mola Mlezi amrehemu, alikuwa anapoizungumzia Hadithi ya Kipande cha Mti – na kumuinamia Mtume S.A.W – analia na akasema: Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Kipande cha Mti kinamnyenyekea Mtume S.A.W, kwa kuwa na shauku nae, na kwa hivyo nyinyi mna haki zaidi katika hili, na muwe na shauku ya kutaka kukutana naye. Na Imamu Malik R.A, aliwahi kuulizwa: ni lini ulimsikia Ayubu Sakhtiyaaniy akizungumza?  Akasema:  Alihiji Hija mbili na mimi nikawa ninamfuatilia na wala sisikii lolote kuka kwake, isipokuwa yeye alikuwa pindi Mtume S.A.W anapotajwa hulia mpaka nikamhurmia, na alikuwa amefikia kiwango cha juu mno cha unyenyekevu wao kw Mtume SAW, wakawa wao hawaungumzii Hadithi yake isiokuwa wanapokuwa katika hali ora abisa, na wauasi wao walileleka katika malezi hayo. Anasema Abu Salamahl Jazaaii Mola amrehemu: Malik bin Anas alikuwa anapotaka kutoka kwenda haja hutawadha udhu wake kwa ajili ya Sala, na huvaa nguo nzuri zaidi, na huchana ndevu zake, na mpaka akaambiwa kuhusu jambo hilo, akasema: Ameyachukua ayo kutoka katika Hadithi ya Mtume S.A.W.

Na katika Taabiina, wapo ambao Mtume S.A.W aliwataja kwa wema, kama vile Uweisil Qarniy ambaye alikuwa akimtendea wema mama yake, na Mtume S,A,W, amemtaja  na  akawaambia Maswahaba kuwa Dua yake ni yenye kupokelewa. Kutoka kwa Omar bin Khatwab R.A, amesma: hakika mimi nimemsikia Mtume S,A,Wm , anasema: Hakika Mbora wa Taabiina ni Mwanaume mmoja anaitwa Uweis, na ana mzazi wake wa kike  na alikuwa na uweupe basi mwamrisheni akuombeeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Na Omar alipowaendea watu wa Yemen akawa anamuulizia mtu huyo na alipomwona mwambia: Niombee, akasema: Wewe kwakweli ndio wa kuniombea mimi. Wewe ni Swahaba wa Mtume S.A.W. Omar aliendelea kumwomba hivyo hivyo mpaka Uweis akamwombea Dua Omar…

Na Taabiina walijifunza Dini sahihi kutoka kwa Maswahaba wa Mtume S.A.W.  aliyeijua Dini vizuri. Na tunaona ya kwamba Imamu Hasanil Basriy Mwenyezi Mungu amrehemu, yeye ni katika Taabiina wakubwa, aliulizwa: Je? Wewe ni Muumini? Akasema: Imani ipo ya aina mbili; ikiwa wewe unaniuliza mimi kuhusu kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake, na Pepo, na kufufuliwa, na Malipo, basi mimi ni Muumini, na ikiwa unaniuliza kuhusu Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

{إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَاناً وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ * الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ * أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً}

Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi.

Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba mimi sijui kama ni miongoni mwao au sivyo. Amesema Baihaqiy akitoa maelezo juu ya jambo hili: Haani hakusita katika asili a maniyake hapo hapo, bali alisimamia katia ukamilifu wake ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaahidi watu wa weponi katika Kauli yake Tukufu:

 {لَهُمْ دَرَجَاتٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ}

Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi

     Vile vile wao waliujua vyme wepesi na wakautekeleza ipasavyo karika maisha yao. Anasema Sifiyani Thauriy Mola amrehemu: Hakika Mambo yalivyo, Elimu kwetu sisi ni kibali cha uaminifu, na ama ukali wa mambo kila mmoja wetu anauweza. Na Azraq bin Qais akasema: Tulikuwa katika kingo za Mto huko Ahwaaz na majili yalikuwa yamejaa akaja Abou Barzat akiwa juu ya farasi akawa anasali na akamwacha farasi wake, na Yule farasi akaondoka, Yule bwana akaiacha sala yake na akamfuata farasi wake mpaka akamfikia alipo akamchukua kisha akarejea na kuilipa sala yake. Na kuna mtu mmoja aliyekuwa nasi aliyeona tukio hilo, akaja na akasema: Mwangalieni huyu Sheikh, ameiacha sala yake kwa ajili ya Farasi wake! Akaja na akasema: Hakuna mtu yoyote aliyenikanya tangu Mtume S.A.W, afariki Dunia, na akasema: Hakika nafasi yangu inaniruhusu, kama ningelimwacha farasi wangu nisingeliwafikia watu wangu isipokuwa Usiku. Na hakika Mtu huyu alifunza jambo hilo kutoka kwa Mtume S.A.W, ambaye hakuwahi kuchagulishwa baina ya mambo mawili isipokuwa alichagua lililo jepesi kati ya mawili hayo kama halikuwa na dhambi yoyote kwa kulifanya kwake. Na Mtume S.A.W, anasema: Rahisisheni mambo na wala msiyatie ugumu, na mpeane habari njema na wala msipeane habari mbaya. Na kauli yake Mtume S.A.W: Hakika upole ahuwi katika kitu chochote isipokuwa hukipendezesha, na hauondoshwi katika kitu chochote isipokuwa hukifanya kiwe kibaya.

Taabiina pia walitekeleza katika maisha yao, tabia ya Upole na Kuleana na kuwahisi wengine, kwa vitendo. Tunaona kwamba Ali bin Huseina bin Ali, R.A, alikuwa akiwasaidia Mafukara wengi mno kwa siri, na hakuna mtu aliyekuwa akijua/ na alipofariki Dunia walimkosa wa kuwasaidia, na walipomkosha walikuta mgongoni mwake na begani mwake athari za kuwabebea mizigo wanawake waliofiwa na waume zao na masikini na kuwafikishia majumbano mwao, na wakati huo wakajua kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiwajia nyakati za usiku kwa vitu alivyokuwa akiwaletea. Na inasemekana kwamba: alikuwa akiwalea mana Ahlu baiti, huko Madina. Na kuhurumiana na kuleana hakuishii kwa Waislamu tu, bali kunawakusanya pia waislamu na wasio waislamu. Tunaona kwamba Bwana wetu Omara bin Abul-Aziiz, R.A, anamwandikia mfanyakazi wake huko Basrah akisema: Na umwaangalie alie kabla yako miongoni mwa Watu wa Dhimma, hakika mama huyo amezeeka sana, na hana nguvu tena, na hana tena uwezo wa kujitafutia riziki, kwa hiyo uwe unampa kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu kile kinachonfaa. Na hapo Bwana wetu Omar anaiga mfano wa Bwana wetu Omarl Khatwaab R.A, alipomwona mtu aliyezeeka miongoni mwa Watu wa Kitabu anawaomba omba watu, akasema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hatukumtendea haki mtu huyu, kwani tumeutumia ujana wake na tukampoteza katika uzee wake. Kisha akawa anampa kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu kiasi kinachomtoshelezea mahitaji yake. Na vile vile tuna mfano mwingine wa Bwana wetu Khalid bin Walid R.A, katika mkataba wake kwa ajili ya watu wa Alheerah:

Na nimewaandalia wao, pale mtu anapozeeka na kukosa nguvu za kufanya kazi, na anapopatwa na janga lolote miongoni mwa majanga, au alikuwa tajiri kasha akafilisika, nimemwandalia usaidizi kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu. Na wote hao, walikuwa wakimfuata Mtume S.A.W, na walikuwa wakiitekeleza Dini sahihi ya Uislamu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{لا ينهاكم اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ}

Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.

Huruma hii haikuishia kwa Watu tu bali iliwajumuisha pia Wanyama na Ndege na viumbe wengine. Omar bin Abdul-Aziiz, Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu, alimwandikia Mfanyakazi wake wa Misri akimuusia kuwahurumia ngamia, akasema: Hakika nimefikiwa na habari ya kwamba Misri kuna ngamia wabeba mizigo, na kwamba ngamia hubebshwa mizigo mizito mno ya ratili elfu moja, ukifikiwa na ujumbe wangu huu, basi sitaki kujua kuwa ngamia wanabebeshwa zaidi ya kiwango cha mzigo wa ratili mia sita. Vile vile aliusia kuwahurumia ngamia bila kulipuuzia jambo hili, wala wasipigwe pigwe. Na alijifunza jambo hili kutoka kwa Mtume S.A.W, pale alipomuusia mwenye ngamia kwa kusema: Je huwezi kumcha Mwenyezi Mungu na kumuogopa kwa ajili ya ngamia huyu ambaye umeruzukiwa naye? Hakika ngamia huyu amenilalamikia ya kwamba wewe unamnyima chakula na unamtesa.

Ninaisema Kauli yangu hii na ninamwomba msamaha Mwenyezi Mungu na kukuombeeni nyinyi.

* * *

     Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika yoyote. Na ninashuhudia ya kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, mswalie na umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika sifa za kipekee walizokuwa nazo Taabiina, ni Usamehevu kwa kwatu wote. Na kuwa wapole kwao. Walikuwa ni watu wenye usamehevu wa ali ya juu sana na ulaini pia katika kuishi na watu. Kutoka kwa Qataadah, amesema: Tuliingia kwa Hasanul Basriy, hali ya kuwa akiwa amelala, na kichwani kwake kuna kikapu, tukakivuta kikapu kile, tukakuta kuna mkate na tunda, na tukawa tunakula. Kasha yeye akazinduka, na akatuona, na akafurahishwa na kitendo kile, akatabasamu hali ya kuwa anaisoma kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {أَوْ صَدِيقِكُمْ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ}

Au rafiki yenu basi hapana ubaya wowote juu yenu…

            Na kutoka kwa Jurair bin Haazim R.A, amesema: Tulikuwa kwa Hasan, na ilikuwa katikati ya mchana, mwanae akasema: Mpumzisheni Sheikhe kwani hakika nyinyi mmemtaabisha mno, kwani yeye hajala wala hajanywa, akasema Hasan: Waache. Hakika mimi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna kitu kinachoyatuliza macho yangu kama kuwaona wao.

Na katika haya ndani yake kuna kujikana na kutambua uzito wa elimu na kuiheshimu na kubainisha cheo cha Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Nafsi za watu. Na huwenda likawa hilo ni somo kwa mwenyekujitanguliza kwa watu ili aizungumzie Dini ya Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na Elimu nayo, akapotoka na akawapotosha watu. Anasema Mtume S.A.W: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu haondoshi Elimu kwa kuiondosha kwa Waja wake, bali huindosha Elimu kwa kuwaondosha Wanachuoni, mpaka asibakie hata mwanachuoni mmoja, na hapo watu wakawafanya wajinga kuwa viongozi wao, wakaulizwa na wkatoa fatwa bila ya kuwa na Elimu, wakapotea na wakawapoteza watu.

Hakika Tabiina walikuwa Ruwaza njema kwa waliokuja baada yao miongoni mwa Maimamu. Tunaona kwamba Imamu Malik bin Anas R.A – naye ni miongoni mwa waliowafuatia Taabiina – anaombwa na Abu Jaafarl Mansour Mwenyezi Mungu amrehemu, akisambaze kitabu chake cha Muwatwau katika Miji mbali mbali ya Kiislamu, akisema: Mimi nimekusudia kuamrisha vitabu vyako hivi ulivyoviandika – kwa maana ya Muwatwau –  vichapishwe kwa wingi kasha nipeleke  chapa moja moja  katika kila mji miongoni mwa miji yote ya Waislamu, niwaamrishe wayafanyie kazi yaliyomo ndani yake, na wasikikwepe na kuelekea katika kingine na wakalingania kinyume na hayo kwa elimu hii iliyozuka. Kwani hakika mimi nimeliona Chimbuko la Elimu hii ni Mapokezi ya watu wa Madina n Elimu yao. Akasema Imamu Malik: Ewe Amiri wa Waumini, usifanye hivyo. Hakika watu wametanguliwa na maneno mengi, na wamesikia Hadithi nyingi, na wamepokea Riwaya nyingi, na kila watu wamechukua kutoka kwao kwa yale yaliyowafikia hapo kabla, na wakayafanyia kazi, na wakayajongelea kwayo kutokana na hitilafu za watu na wengine wao, na hakika kuwarudi kwa yale waliyokwishayaamini ni kuwalazimisha, kwa hivyo waache watu na hali zao walizo nazo, na walichokichagua watu wa kila mji miongoni mwao kwa ajili yao. Akasema: hakika ninaapa, kama ungeliniunga mkono katika jambo hili basi ningeliamrisha litekelezwe.

Na katika unyenyekevu wenye ukarimu na ufahamu mkubwa na Elimu ya Fiqhi, ni tukio la Imamu Shafi aliposigana na Mwanafunzi wake Yunus bin Abdul Aalaa, na akasimama hai ya kuwa na hasira, na ulipofika Usiku, Yunus akasikia mtu anagonga mlango wa nyumba yake, akasema: ni nani aliye mlangoni? Akasema: Muhammad bin Idris, Yunus akasema: nikawa ninafikiria kila mtu anayeitwa kwa jina hilo la Muhammad Idris nikakuta ni Imamu Shafi peke yake, akasema: Na nipoufungua Mlango nikakutana nae uso kwa uso akasema: Ewe Yunus, mamia ya masuala yanatukutanisha pamoja na suala moja linatutenganisha?! Ewe Yunus, usijaribu kushinda katika hitilafu zetu zote, kwani baadhi ya nyakati kujipatia ushindi wa nyoyo ni bora kuliko kujipatia ushindi wa Mambo mbali mbali, Ewe Yunus, usiyabomoe madaraja uliyokwishayajenga na kuyavuka, kwani huwenda siku moja ukayahitaji kwa ajili ya kaurejea, daima lichukie kosa lakini usimchukie mkosa, na uyachukie maasi kwa moyo wako wote, lakini msamehe na umhurumie Mtu aliyemwasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, Ewe Yunus, ikosoe kauli ya mtu, lkini muheshimu msemaji, kwani jukumu letu sisi ni kuyaangamiza maradhi na sio mgonjwa.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu Imamu Shafi kwa kauli yake hii:

Ninawapenda Wema nami si katika wao

huwenda nikaupata uombezi wao

Na ninamchukia ambaye biashara yake ni maasi

Hata kama bidhaa zetu zinalingana.

Na Wanachuoni wetu watukufu wakaufuata Mwenendo huo huo na wakawa Ruwaza njema kwetu sisi katika kuibeba Amana ya Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ya Uislamu na kuielewa kwa mweleweko sahihi, na kujipamba na Tabia zake pamoja na uzuri wa kuufikisha kwa Watu, kwa hekima na Mawaidha Mazuri.

Ewe Mola wetu tujaalie tuwe miongoni mwa wenye kuisikia Kauli na wakaifuata iliyo bora zaidi, haowee ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaongoa na haowee ndio wenye kuzingatia.

Sura angavu za Maisha ya Maswahaba R.A

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

 {وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ}

Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewachagua Manabii na Mitume wake, A.S, miongoni mwa viumbe vyake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اللَّهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ}

Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawachagulia Mitume wasaidizi wao katika kuzifikisha risala za Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Msema Ukweli, amemchagulia Mtume Muhammed, watu walio wasafi, na Maswahaba wateule, waliomwamini yeye na wakawa wanamuheshimu na kumnusuru na wakaifuata nuru aliyoteremka nayo. Anasema Abdallah bin Masoud R.A: amesema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameziangalia nyoyo za waja wake na akamchagua Muhammad S.A.W, na kumpa ujumbe wake na alimchagua kwa Kujua kwake kisha akaziangalia nyoyo za watu baada ya Muhammad na akamchagulia Maswahaba na akawajaalia wakawa ni wenye kuinusuru Dini yake na wakawa Mawaziri wa Mtume wake S.A.W. kwa hiyo wanachokiona Waumini kuwacni kizuri basi hata mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kizuri pia, kile ambacho Waumini wanakiona kuwa ji kibaya basi hata mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kibaya.

Walikuwa R.A, ni wakweli wa Imani katika watu, ba wenye ujuzi zaidi kielimu katika Watu, na wenye fahamu ya ndani zaidi, na wenye kazi bora katika Watu, waliibeba bendera ya Dini na kupeperusha katika maeneo mbalimbali Ulimwenguni, kwa hekima na Mawaidha Mazuri, na wakaifikisha risala ya Mola wai Mlezi kwa ufikishaji  ulio bora zaidi, wakastahiki wawe ni chaguo la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume S.A.W. Kutoka kwa Ibnu Abas R.A, amesema katika Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {قُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلامٌ عَلَى عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَى}:

Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa.

Kwamba Maswahaba wa Mtume S.A.W, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemteulia Mtume wake S.A.W, kwani wao ndio waliofuata Mfumo wa Uislamu kutoka katika chanzo chake cha asili na kisafi na hawakutoka katika njia yake iliyonyooka.

Hakika Maisha ya Maswahaba yalijaa sura nyingi angavu ambazo ziliunda utekelezaji wa kivitendo wa Uislamu Sahihi, na miongoni mwazo ni: Rehma. Mtume S.A.W, alipandikiza kwa Maswahaba wake Maadili ya rehma, na kwa hivyo, Ayina bin Husnu alipomwona Omar R.A, siku moja akimbusu mmoja wa watoto wake, na akiwa amempakatia, Ayina akasema: Unabusu Wakati wewe ni Amiri wa Waumini? Kama mimi ningelikuwa Amiri wa Waumini nisingelimbusu mtoto. Omar R.A, akamwambia: Mimi nifanye nini ikiwa Mola wako Mlezi amekuondoshea rehma na upole moyoni mwako? Hakika mambo yalivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu huwarehemu waja wake walio wapole wenye kuwahurumia wengine. Na katika tukio hili, Bwana wetu Omar amejifunza kutokana na tukio lililomtokea Mtume Muhammad S.A.W, alipokuwa na Aqrau bin Haabis; ambapo Mtume S.A.W, alimbusu Bwana wetu Husein bin Ali R.A, mbele ya Aqrau, na Aqrau akasema: Hakika mimi nina watoto kumi na sijawahi kumbusu yoyote kati yao. Mtume S.A.W akamwangalia kisha akasema: asiyehurumia watu na yeye hahurumiwi.

Maswahaba R.A, walikuwa pia ni mifano mizuri ya kuigwa katika kusamehe na Usamehevu. Na katika sura zenye ubora wa hali ya juu ni ile ya Bwana wetu Abu Bakar Swiddiq katika Usamehevu wake kwa Musatwah bin Athaathah. Abu Bakar alikuwa akimpa pesa za matumizi kwake kutokana na ukatibu wake na ufakiri wake. Na Musatwah alikuwa miongoni mwa watu waliomzungumzia vibaya Bi Aisha R.A. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha aya za kuonesha kuwa Bi Aisha hana yoyote.hatia yoyote, Abu Bakar akataka kumnyima Musatwah pesa za matumizi, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha Kauli yake:

{وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَالسَّعَةِ أَنْ يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَى وَالْمَسَاكِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا أَلَا تُحِبُّونَ أَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ}

Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

Akasema Abu Bakar Swiddiq R.A: Ndivyo hivyo. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, miki ninapenda Mwenyezi Mungu anisamehe. Na akarejesha tena kumpa nduguye Musatwah pesa za Matumizi, huku akisema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kamwe mimi Sitazisitisha pesa za matumizi kwa Musatwah.

Na miongoni mwazo ni: Ari ya hali ya juu na ushindani katika kutenda mambo ya Kheri. Hakika Maswahaba R.A,  walijifunza kutoka kwa Mtume S.A.W, jinsi ya kuwa na ari ya haoi ya juu pamoja na ushindani katika kutenda mema na kuyatafuta mambo yaliyo juu ambapo anasema Mtume S.A.W: Mbapo mwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mwombeni Pepo ya Firdaus. Kwani pepo hiyo ndio ya kati katika Pepo na ni ya Daraja la juu – ninaona – juu yake kuna Arshi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutokea hapo Mito ya Peponi huwa inaanzia, na jambo hili ndilo lililowafanya Maswahaba watukufu watazamie Mambo ya juu katika kila jambo. Anasema Bwana wetu Omar R.A: Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu alituamrisha tutoe sadaka, na jambo hilo likaenda sambamba na mimi kuwa na fedha, na nikasema: Leo  nitamshinda Abou Bakar ikiwa kuna uwezekano wa kumtangulia leo. Nikaja na nusu ya Mali yangu kwa Mtume S.A.W, na Mtume akasema: Umewaachia kitu gani watu wako wa nyumbani? Nikasema: Nimewaachia mfano wa mali hii. Akasema: Na Abu Bakar R.A, alikuja hapa na mali yake yote aliyonayo, na Mtume S.A.W, akamwambia: Umeiachia kitu gani familia yako? Akasema: nimeiachia Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake. Nikasema: Kamwe siwezi kushindana na wewe katika kitu chochote.

Na tumtazame Swahaba huyu hapa, Kaab bin Aslamiy R.A, amesema: Nilikuwa ninalala na Mtume S.A.W, nikamletea baadhi ya vitu vyake akaniambia S.A.W: Omba utakacho. Akasema: ninaomba niwe nawe Peponi, akasema au kuna ombi jingine?. Nikasema: ni hicho hicho. Basi Mtume S.A.W, akasema: basi nisaidie mimi kwa kusujudu kwako kwa wingi.

Na miongoni mwayo: Ni kujinyima na kutokuwa na tamaa. Maswahaba wa Madina walikuwa ni mifano bora zaidi katika hili la kujinyima. Kutoka kwa Abu Huraira R.A, amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu S.A.W, Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika mimi nimekumbwa na njaa. Mtume akampeleka kwa wakeze na hakukuta chakula chochote. Akasema S.A.W: Ajitokeze mtu wa kuwa mwenyeji wa huyu kwa usiku huu, Mwenyezi Mungu atamrehemu? Mtu mmoja katika Watu wa Madina akasimama na akasema: Mimi hapa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akaenda kwa watu wake nyumbani na akamwambia mkewe: Tuna mgeni wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, usiache kumpa kitu chochote tulichonacho. Akasema yule mke wake: Ninaapa ya kwamba mimi sina chochote isipokuwa chakula cha watoto. Akasema Mume: watoto watakapo chakula cha usiku uwalaze na uje, kisha uzime taa, na yuyapumzishe matumbo yetu usiku wa leo. Mke wake akafanya hivyo. Kisha Mume akaenda kwa Mtume S.A.W, na Mtume akasema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amestaajabishwa au – amefurahishwa – na fulani pamoja na fulani. Na hapo ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha Kauli yake:

{وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ}

bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.

Na katika tukio zuru linalokusanya baina ya hali ya upendeleo kwa mwingine waliokuwa nayo Maswahaba wa Madina R.A, na hali waliyokuwa nayo Maswahaba wa Makkah ya kujizuia na tamaa, Bwana wetu Saad bin Rabiigh anapendekeza kwa Bwana wetu Abdulrahmaani bin Aufi R.A, ampe nusu ya mali zake, akakutana na Bwana wetu Abdulrahmaani R.A, akiwa na kila aina ya kujizuia na tamaa, alichokifanya ni kumwomba amjulishe sehemu lilipo soko, na akafanya biashara na akajitahidi mpaka akawa ni miongoni mwa matajiri wakubwa wa Madina.

Na miongoni mwayo ni: Kurejea katika Haki. Maswahaba R.A, walikuwa na hima kubwa katika Haki, hawawi na kiburi katika kurejea kwenye haki. Kutoka kwa Abu Masoud Answaariy R.A, alisema: nilikuwa nikimpiga kijakazi wangu, nikaisikia sauti ikitokea nyuma yangu: Tambua ewe Abu Masoud kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye uwezo zaidi juu yako kuliko uwezo wako juu ya kijakazi huyu. Nikageuka na kuangalia nikamwona Mtume S.A.W, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu kijana ni huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akasema: Kama usingelifanya hivyo basi Moto ungekutafuna. Au Moto ungekukamata.

Na miongoni mwayo ni: Kutekeleza ahadi. Mtume S.A.W, alipandikiza thamani ya kutekeleza ahadi katika nyoyo za Maswahaba wake na akawahikiza kuwajibika na Jambo hili. Tunamwona Bwana wetu Muawiya bin Abu Sufiyani R.A, ambapo baina yake na Warumi palikuwa na Ahadi na Muawiya R.A, akafikiria kutoka na kuelekea karibu na Mipaka ya Urumi, ili muda wa ahadi ukimalizika awavamie. Akajiwa na mtu katika Maswahaba wa Mtume S.A.W, huku akisema Mtu huyo, Allahu Akbar, Allahu Akbar, ni utekelezaji wa Ahadi na sio kinyume chake. Watu wakamwangalia alikuwa ni Amru bin Absa R.A, Muawiya akamtumia mtu na akamuuliza: akasema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu S.A.W, anasema: Mtu yoyote mwenye ahadi baina yake na wengine basi asiuongeze ugumu wake, wala asiifungue ahadi mpaka itakapoumaliza muda wake au akakata nao ahadi kwa mujibu wa vitendo vyao. Muawiya akarejea nyuma na hakuchukua hatua aliyotaka kuichukua.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Hana mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad ni Mja na Mtume wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake Wote, na yoyote atakaewafuata mpaka Siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika Maswahaba wa Mtume S.A.W, walikuwa ruwaza njema katika ujenzi wa Dunia kwa Dini, kwani kila mmoja wao alikuwa na kazi anayoifanya, na anaijua vizuri na kuitekeleza ipasavyo. Miongoni mwao alikuwamo Mfanyabiashara, Kiongozi, Mbeba Elimu, na wengine wengi. Anasema Mtume S.A.W: aliye mpole zaidi wa Uma wangu katika umma wangu huu ni Abu Bakar, na aliye Mkali zaidi katika Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ji Omar, na mwenye haya zaidi ni Othman, na Mjuzi zaidi wa Halali na Haramu ni Muadh bin Jabal, na msomaji zaidi wa Kitabu chake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Ubayu. Na Mjuzi zaidi wa Elimu ya Mirathi ni Zaidu bin Thabit. Na kila Umma una mwaminifu wake zaidi, na Mwaminifu zaidi wa Umma huu ni Abu Ubaidah bin Jarraah.

Na kazi za Maswahaba R.A, zilikuwa na matunda yake mazuri. Na Mtume S.A.W, alikuwa akiwahimiza na kumkumbusha kila mmoja wao kile anachoweza kukifanya vizuri zaidi kwa ajili ya kuonesha kumjali Swahaba huyo na kazi yake anayoifanya. Na katika hayo ni yale yaliyokuwapo kwa Bwana wetu Othman bin Afaan siku ya Vita vya Tabuk, ambapo aliingia alipo Mtume S.A.W, akiwa na Dinari elfu moja na akamkabidhi Mtume S.A.W. Na Mtume S.A.W, akasema: Baada ya kitendo chake hichi, kamwe hakuna Kitu chochote atakachokifanya Othman kikamdhuru.

Na miongoni mwayo ni kuichunga halali, na kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kila Jambo. Na katika hili ndivyo alivyokuwa Bwana wetu Jurair bin Abdillah R.A, ambapo Mtumishi wake alimwamuru amnunulie farasi na akamnunulia farasi kwa dihamu mia tatu. Na akaja na farasi pamoja na mwenye farasi ili amlipe na Jurair akamwambia mwenye farasi: farasi wako ni bora kuliko dirhamu mia tatu, je unaweza kumuuza kwa dirhamu mia nne? Akasema: hiyo ni juu yako wewe. Akasema: Farasi wako ni bora zaidi ya hiyo. Je unaweza kumuuza kwa dirhamu mia tano? Kisha akaendelea kuongeza mia mia mpaka akafikia dirhamu mia nane, na akamnunuackwa bei hiyo. Na akasemwa katika hilo akasema: Hakika mimi nimempa Mtume S.A.W ahadi ya utiifu juu ya kumnasihi kila mwislamu.

Kila mmoja wao akawa anatambua wajibu wake na anautekeleza ipasavyo na wala hapundukii katika majukumu yake. Na Bwana wetu Abu Bakar R.A, alimpa Bwana wetu Omar R.A, Majukumu ya Ukadhi, na Bwana wetu Omar akakaa kiasi cha mwaka, hakuna mtu yeyote anayemwendea, na hapo ndipo alipomtaka Bwana wetu Abu Bakar amtoe katika Ukadhi huo, akasema: Je unataka uondoshwe kwenye Ukadhi kutokana na ugumu wa kazi ewe Omar? Omar R.A, akasema: Hapana ewe Khalifa wa Mtume S.A.W; baoi ni kwa sababu ya kutohitajika kwangu kwa Waumini, kila mmoja wao anaijua haki yake, na wala hahitaji zaidi ya hivyo, na anaujua wajibu wake na wala hazembei katika utekelezaji wake, kila mmoja wao anampendelea ndugu yake kile anachokipenda yeye mwenyewe, na pindi mmoja wao anapokuwa haonekani wao humtafuta, na anapoumwa wao humtembelea, na anapoishiwa wao humsaidia, na anapohitaji wao hukidhi mahitaji yake, na anapokuwa na msiba wao humhani na kumliwaza, Dini yao ni Kunasihiana, na Tabia zao ni kuamrishana Mema na kukatazana Mabaya. Watu wa aina hii ni kipi watakachokigombania?

Tutambue kwamba sisi tunahitaji zaidi kurejea katika Maadili ya Mifano hii mema ya Maswahaba wa Mtume S.A.W, na kujipamba kwa Tabia zao pamoja na kuionesha sura sahihi ya Dini yetu ya Uislamu, Dini ya Rehma, Usamehevu, Utu, na Amani kwa Watu wote.

Ewe Mola wetu tulindie nchi yetu, wananchi wake, na Majeshi yake ya Ulinzi na Usalama, na Uijaalie Maendeleo, na Maisha Mazuri, pamoja na Nchi zote Duniani.

Maisha ya Mtume S.A.W kama mfano wa kiutendaji wa kuigwa wa Uislamu Sahihi

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا}

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakika mwenyezi Mungu Mtukufu amemtuma Mjumbe wake Muhammad S.A.W, kama mwongozaji, mtoaji wa habari njema, na Mlinganiaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa idhini yake Mola, akiwa pia ni taa iangazayo, kwa risala ya mwisho na ya kimataifa inayofaa na kurekebisha kwa zama zote na popote, inapelekea Mtume S.A.W, awe Mfano wa kuigwa kwa vitendo, kauli na hali zote, kwa ajili ya kuutekeleza Uislamu Sahihi na hakuna jambo lolote la kushangaza katika hilo, kwani Mtume S.A.W, alikuwa ni Mfuasi wa Mfumo wa Quran Tukufu katika Mahusiano yake na Mola wake, na mahusiano yake na Watu wote, bila kujali jinsia, rangi au itikadi zao; na kwa hivyo, Mama wa Waumini, Bi Aisha R.A, alipoulizwa kuhusu tabia ya Mtume S.A.W, akasema: Tabia yake ilikuwa Qur-ani.

Na mwenye kuizingatia Sira ya Mtume S.A.W, ataona kuwa Mtume S.A.W, alikuwa Ruwaza njema na Kiigizo chema katika kila hali, kwa maneno na vitendo vyake. Na kutokana na hali hiyo, kwa ukweli wake na uaminifu wake, alikuwa Mtume S.A.W, Msema kweli, na Mwaminifu katika Maisha yake yote, mpaka watu wake wakampa jina la Msema Kweli Mwaminifu, kabla ya kupewa kwake Utume. Na kutokana na hali hiyo anasema Shauwqiy:

Mmemwita Mwaminifu wa watu udogoni mwake.

Na wala Mwaminifu hatuhumiwi kwa kauli yoyote. 

Na pindi Mfalme wa Warumi, Hirakli alipomwita Abu Sufiani bin Harbi kabla ya kusilimu kwake ili amuulize kuhusu Mtume S.A.W, yalijiri baina yao mazungumzo marefu ambapo Hirakli alimwambia Abu Sufiani: Je mlikuwa mkimtuhumu kwa uongo kabla hajayasema aliyoyasema? Akasema Abu Sufiani: Hapana. Na je huwa anavunja ahadi? Akasema Abu Sufiani:  Hapana. Na sisi tuko nae kwa muda mrefu katika ahadi na hatujui anachoweza kutufanyia katika hilo. Kisha akasema: Na sipati maneno yoyote mengine ya kumuelezea Mtume huyu isipokuwa maneno haya, Msema kweli Mwaminifu.

Na hakika palionekana Tabia za Uaminifu wazi wazi katika sura zake za daraja la juu na maana zake katika Utu wa Mtume S.A.W, Usiku wa Hijra iliyobarikiwa (Kuhama kwake), ambapo Mtume S.A.W, aliamwamrisha Ali bin Abu Twalib R.A, alale katika kitanda chake na asubiri ili azirejeshe kwa wenyewe amana zote walizoziacha kwa Mtume S.A.W, ingawa wao walimfanyia uadui, na wakamtoa kwake, wakamuudhi, na wakawaudhi Maswahaba wake R.A, na wakachukua kutoka kwao kila walichokimiliko; kwa sababu Khiana haiswihi kwa Muumini wa kweli hata kwa maadui zake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:

{وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِنْ قَوْمٍ خِيَانَةً فَانْبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَى سَوَاءٍ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ}

Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini.

Na anasema Mtume S.A.W: kuwa mwaminifu kwa anaekuamini, na wala usimfanyie khiana aliyekufanyia khiana.

Katika uaminifu wake, Mtume S.A.W, alikuwa ni Mbora wa uaminifu, na hajawahi kumkana mtu yoyote na wala hajawahi kusahau fadhili za mtu yoyote, na alikuwa akimtendea Mazuri kwa kila mtu. Alisema Mtume S.A.W, kabla ya kufa kwake: hakuwahi kutusogezea mkono wake mtu yoyote isipokuwa tulimpa wema, isipokuwa Abu Bakar, kwani hakika yeye kwetu sisi ana mkono ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye atakaempa mazuri hayo Siku ya Kiama.

Na katika Mionekano ya Uaminifu wake S.A.W, ni jinsi alivyokuwa akimfanyia Mama wa Waumini Bi Khadija R.A; Mtume alikuwa anampenda na alikuwa anamjali na alikuwa mwaminifu kwake alipokuwa hai na hata alipofariki. Katika kuiweka wazi nafasi ya Bi Khadija, Anasema S.A.W: Mwenyezi Mungu hajawahi kunibadilishia Mwanamke aliye Mbora kuliko Bi Khadija, aliniamini pale watu waliponikufuru na kunikana, na aliniamini pale watu waliponikadhibisha, na alinikiwaza kwa pesa zake pale watu waliponinyima, na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliniruzuku watoto wake aliponinyima watoto kwa wake wengine.

Na anasema Bi Aisha R.A: Sijawahi kuwa wivu mkubwa kwa wakeze Mtume kama nilivyomwonea wivu Bi Khadija, na wala sijawahi kumwona kwa macho. Lakini Mtume S.A.W, alikuwa akimtaja Bi Khadija kwa wingi sana, na baadhi ya nyakati alichinja mbuzi kisha akamkatakata vipande na kuvipeleka kama sadaka kwa ajili ya Khadija.

  ومنها: وفاؤه (صلى الله عليه وسلم) مع غير المسلمين، ففي يوم بدر قال (صلى الله عليه وسلم): (لَوْ كَانَ الْمُطْعِمُ بنُ عَديٍ حَيًّا، فَكَلَّمَنِي فِي هَؤُلَاءِ الأسْرَى لَأَطْلَقْتُهُمْ) ، وكان للمطعم جميل عند رسول الله (صلى الله عليه وسلم)، حيث دخل (صلى الله عليه وسلم) مكة في جواره بعد عودته من رحلة الطائف .

ومنها –أيضا- وفاؤه (صلى الله عليه وسلم) مع أعدائه حتى في وقت الحرب، فعن حُذَيْفَة بْن الْيَمَانِ (رضي الله عنه) ، قَالَ : مَا مَنَعَنِي أَنْ أَشْهَدَ بَدْرًا إِلَّا أَنِّي خَرَجْتُ أَنَا وَأَبِي، فَأَخَذَنَا كُفَّارُ قُرَيْشٍ ، قَالُوا : إِنَّكُمْ تُرِيدُونَ مُحَمَّدًا ، فَقُلْنَا : مَا نُرِيدُهُ ، مَا نُرِيدُ إِلَّا الْمَدِينَةَ ، فَأَخَذُوا مِنَّا عَهْدَ اللهِ وَمِيثَاقَهُ لَنَنْصَرِفَنَّ إِلَى الْمَدِينَةِ ، وَلَا نُقَاتِلُ مَعَهُ، فَأَتَيْنَا رَسُولَ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ، فَأَخْبَرْنَاهُ الْخَبَرَ ، فَقَالَ (صلى الله عليه وسلم) : (انْصَرِفَا ، نَفِي لَهُمْ بِعَهْدِهِمْ ، وَنَسْتَعِينُ اللهَ عَلَيْهِمْ) .

كما كان (صلى الله عليه وسلم) أنموذجًا فريدًا ، وأسوة طيبة في تعامله مع أزواجه ، فقد عاش النبي (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مع أزواجه حياةً طيبة، تجلت فيها كل مظاهر المودة، والرحمة ، والتواضع ولِين الجانب ، فلَم يتعالَ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  على أزواجه، ولم يترفَّع عليهن ، بل أحسن معاملتهن جميعًا، منطلقًا في ذلك كله من قول الله (عز وجل) :

 {وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ}

Na kaeni nao kwa wema,

Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, anasema:

{وَمِنْ آياتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْواجاً لِتَسْكُنُوا إِلَيْها وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذلِكَ لَآياتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ}.

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri

Mtume S.A.W, alikuwa Mume Mpole kwa wakeze, na katika moja ya matukio ya upole wake yaliyo mazuri na kiutu, ya Mume Mtaratibu anapokuwa na wakeze, Mtume anampangusa machozi Mkewe Bi Swafiyah R.A, mikono yake miwili inatumika kuyafuta machozi hayo na kumtuliza kwa utukufu wa mikono yake miwili. Anasema Anas bin Malik R.A: Bi Swafiya alikuwa na Mtume S.A.W, safarini, na hiyo ilikuwa siku yake Bi Swafiyah na akapunguza mwendo wake, na Mtume S.A.W, akamwelekea huku Bi Swafiyah akiwa analia na anasema: Umenibeba kwa ngamia asiye na kasi. Kauli yake hiyo inamfanya Mtume ampanguse macho yake kwa mikono yake miwili na kumnyamazisha.

Vilevile, Mtume S.A.W, alikuwa Ruwaza njema katika kutangamana na Watoto pamoja na Wajuu zake.

Ubora na Uzuri ulioje wa Baba na Babu Mtaratibu, ansewabeba wanae na Wajukuu zake, kwa kila maana za Upendo na Upole. Anasema Mama wa Waumini Bi Aisha R.A: Sijawahi kumuona Mtu anaefanana na Mtume S.A.W, kwa wema na uwelewa na uongofu kuliko Binti yake Mtume S.A.W, Bi Fatuma R.A. Na akasema: Na alikuwa anapoingia ndani alipo Mtume S.A.W, Mtume alikuwa akimsimamia Bi Fatuma, kisha anambusu na kumkalisha pale alipokaa yeye.

Na kutoka kwa Abu Huraira R.A, amesema: Mtume S.A.W, alimbusu Hassan bin Ali na alikuwepo hapo Akrau bin Haabis Tamiimiy akiwa ameketi. Akasema Al-akrau: Mimi nina watoto kumi na sijawahi kumbusu yoyote kati yao. Mtume S.A.W akamwangalia kisha akasema: Mtu asiyewahurumia wengine na yeye hahurumiwi. Na siku Moja Mtume S.A.W, alisujudu na akarefusha sijida yake, na alipomaliza Sala yake, watu wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika umesujudu sijida ambayo hukuwa ukiisujudu, je hicho ni kitu ulichoamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu? Umemsujudia Mwenyezi Mungu au ulikuwa ukiteremshiwa Wahyi? Akasema Mtume S.A.W: Hayo yote hayakuwa, lakini mwanangu wa kiume ameniondoka nikakarahika nisijenikamuharakisha mpaka akidhi haja yake.

Sisi tunasisitiza kwamba jambo hili halikuwa Maalumu kwa watoto na wajukuu zake tu; bali ulikuwa Mfumo wake anaoutekeleza yeye mwenyewe kwa watu wote hambagui yoyote kati yao na akawa anamfanyia wema kila mtu. Na kutoka kwa Usama bin Zaid R.A: kutoka kwa Mtume S.A.W, amesema: Kwamba Mtume alikuwa akimchukua yeye na Alhassan, na anasema: Ewe Mola wangu hakika mimi ninawapenda Wote wawili basi na uwapende wote wawili.

Na Anas bin Malik R.A, anasema: Mimi nimemtumikia Mtume S.A.W, kwa miaka kumi, hata siku moja hajawahi kuniambia lolote baya hatadogo, na wala hajawahi kuniambia mimi kwa kitu chochote nilichokifanya, kwanini nimekifanya, au kwa kitu chochote nilichokiacha kwanini nilikiacha?

Mtume alikuwa vile vile mfano wa kuigwa wa uzuri wa kutangamana na Maswahaba wake. Mtume alikuwa akishirikiana nao katika furaha na huzuni zao na anamtafuta yoyote aliyepotea katika wao na anamtembelea mgonjwa miongoni mwao na anayajali mambo yao, na anazichunga hisia zao katika masuala ya Maisha yao. Kutoka kwa Simaki bin Harbi R.A, amesema: Nilimwambia Jabir bin Samurah R.A, amesema: Je ulikuwa unaketi na Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu S.A.W? Akasema: Akasema: Ndio. Mara nyingi sana. Alikuwa hasimami katika mswala wake anaouswalia katika swala ya Asubuhi mpaka Jua linapochomoza, na linapochomoza tu husimama. Na walikuwa wanazungumza, wakigusia zama za Ujahili kisha wanacheka, na Mtume S.A.W, anatabasamu. 

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu:

Kwa kuwa Mtume S.A.W, alikuwa Ruwaza njema, kivitendo, kwa kuutekeleza Uislamu Sahihi katika Utu na Ubinadamu wake yeye Mwenyewe, alikuwa pia Ruwaza njema kwa Ukati na Uadilifu wake. Mtu yoyote mwenye kuzizingatia Hukumu za Sheria ya Uislamu aliyoilingania Mtume S.A.W, ataona Mfumo wa Uadilifu na Ukati wa Wazi Katika nyanja zote. Anasema Mama wa Waumini, Bi Aisha R.A: Mtume S.A.W, hajawahi kuchagulishwa baina ya Mambo Mawili isipokuwa alichaguliwa kilicho chepesi (kati ya viwili hivyo), kama kitu hicho hakina dhambi yoyote, na kama kitu hicho kingelikuwa na dhambi yoyote basi Mtume aliwa wa kwanza kuwa mbali nacho. Na anasema Mtume S.A.W: Hakika Dini ya Uislamu ni nyepesi, na hakuna yoyote mwenye kuikazia isipokuwa humshinda.

Basi saidianeni katika kufunika kasoro zenu, sogeleaneni, na mpeane habari njema na msaidiane katika ghadwa na rauha na sehemu ya dalja   

 بِالْغَدْوَةِ وَالرَّوْحَةِ، وَشَيْءٍ مِنَ الدُّلْجَةِ).

،التآسي

Na kwa ajili ya kuhifadhi Uwastani huu, Mtume S.A.W, ametutahadharisha na kila aina ya kujikweza katika Dini, na akamzuia yoyote katika Maswahaba wake R.A, kwa anaepindukia katika ufuasi wa Dini

Anasema Mtume S.A.W: Enyi Watu: Jiepusheni na kujikweza katika Dini, hakika kujikweza Kidini kuliwangamiza waliokuwa kabla yenu.

Ukubwa ulioje wa hitajio letu la kujiliwaza na Mtume S.A.W, na kuufuata Uongofu wake, na kufuata nyayo zake katika kueneza risala ya nuru ya ba Uongofu iliyo safi kama alivyoiteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Viumbe vyote, kwa ulaini, na upole, na urafiki, na kwa mjongeleano wa nyoyo, kwani risala ya Uislamu ndio Uadilifu kamili, ni Huruma Kamili, Usamehevu kamili, Manufaa kamili, na ni Utu Kamili. 

 Ewe Mola wetu Mlezi, tunakuomba uturuzuku kukupenda wewe, na kumpenda Mtume wako, S.A.W, na kila kazi inayotukurubisha katika kukupenda wewe na Uijaalie Nchi yetu iwe na Amani na Usalama, na isalimike kwa usalama, pamoja na Nchi zote Duniani.

Huu ndio Uislamu

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu.

{وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَاتَّخَذَ اللَّهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا}

Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo. Na baada ya utangulizi huu:

Na baada ya autanguli huu,

Hakika Uislamu wa kweli ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtii, na kumfuata yeye Mtukufu, na upendo, kufuata, na kumuiga Mtume wetu S.A.W, na kuwa na tabia njema, na kuwa mnyenyekevu,  na nafsi iliyo safi, na kuwa na uso mkunjufu katika kuonana na watu wote, na ulaini na upole, na uzuri pamoja na Ulimwengu wote, na kujenga na kuinua ujenzi miji, na ustaarabu na maendeleo miji, Uislamu ni mfumo wa maisha wanayoishi wafuasi wake katika harakati zao na utulivu wao na vitendo vyao vyote.

Hakika ya Uislamu, ni dini inayolingania Marekebisho na Utengemavu, na ujenzi wa Dunia kwa Dini, na wala sio kuibomoa Dunia kwa jina la Dini, na Dini ya Kiislamu inalingania Huruma, Usalama na Amani kwa Ulimwengu wote, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ}

Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.

Hakika ya mwenye kuzingatia Nguzo za Uislamu zilizotajwa katika Hadithi ya Jiburilu A.S, alipomuuliza Mtume S.A.W, akisema: Ewe Muhammad, niambie kuhusu Uislamu, Mtume S.A.W, akasema: (Uislamu ni kukiri kwa Moyo na kushuhudia kwa ulimi kwamba hakuna mungu mwingine apasae kuambudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ukasimamisha Sala tano, na ukatoa Zaka, na ukafunga Mwezi wa Ramadhani, na ukahiji Makkah kama utaweza kufanya hivyo…), atatambua kwamba huchangia kuujenga utu wa mtu uwe sawa. Mtu anapoamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na hana mshirika wake, na kwamba Bwana wetu Muhammad S.A.W, ni Mja wake na ni Mtume wake, atahangaikia kuifanyia kazi shahada hii kwa kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumnyenyekea, Mola wa viumbe vyote, akawa anafuata Maamrisho yake, na akajiepusha na Makatazo yake, na akasimama katika mipaka yake, na wala hayapuuzii yale aliyokalifishwa, na wala hahitaji kisichokuwa chake, vile vile anajitahidi katika kumfuata Mtume S.A.W, na kutangamana na watu kama vile Mtume alivyotangamana nao; kwa upole, huruma, unyenyekevu na ulaini.

Hakika Sala ndio Nguzo Kuu miongoni mwa Nguzo za Uislamu, na matunda yake humrejea mja huyu, kwa kumzuia na maovu na yaliyokatazwa, kuwa na msimamo katika njia ya Mwenyezi Mungu, na anaishi Mwislamu kwa amani na salama yeye na nafsi yake pamoja na Jamii yote kwa ujumla. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ}

SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.

Na utoaji Zaka kuna pande za kiimani na za kiutu; kwani zaka huinyoosha nafsi isiambatane zaidi na mali, mpaka mtu atambue kwamba Mali ni njia na wala sio lengo kuu la binadamu, na zaka pia ni mlango wa ushirikiano baina ya watu, kuhurumiana, kutoa, kujitoa, kuitoa nafsi, kuwapendelea wengine na wala sio kujipendelea, au kuwa bahili na mgumu wa kutoa. Kwani Muumini ni msamehevu, mtoaji na mkarimu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwasifu Maanswaar (Maswahaba wa Madina) R.A:

{وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِنْ قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ}.

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

Na vile vile Saumu, hii udhibiti maadili ya Mwislamu na kumfanya adumu katika katika kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na humzoesha mvumilivu na subira na kuiimarisha Nafsi yake na kuiweka zaidi kwa kuiepusha na kila kinachomkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mtume wetu Muhammad S.A.W, anasema: Saumu ni Kinga, na inapokuwa siku ya kufunga ya mmoja wenu, basi asitoe maneno machafu, wala asifoke foke, na iwapo mtu atamtukana au akamfanyia ugomvi, basi na aseme: Hakika mimi ni mtu niliyefunga.

 Na anasema Mtume S.A.W: Asiyeacha Uongo na kuutumia, basi hana yeye kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu haja yoyote ile ya kuacha chakula chake na kinywaji chake.

Vile vile Hija ni uwajibikaji wa kimwenendo na kimaadili kabla ya Hija, wakati wa Hija na baada ya kumaliza Idada zote za Hija. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّهُ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ}

Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!

Kutoka kwa Abu Huraira R.A, amesema: Nimemsikia Mtume S.A.W, anasema: Mtu yoyote atakayehiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajatoa maneno machafu, na wala hajafanya uovu wowte, basi atarejea kama siku alivyozaliwa na mama yake (kwa kutokuwa na kosa hata moja).

 Na hivi ndivyo ilivyo. Nguzo zote za Uislamu zina athari zinazoleta na kheri, Usalama na Amani zake kwa Jamii yote.

Hakika mtu anaeuangalia undani wa Dini yetu tukuzwa, atatambua ya kwamba hii ni Dini ya Tabia njema, na ni ujumbe uliokuja kutimiza Tabia hizi njema, ambapo anasema Mtume S.A.W: (Hakika mimi nimetumwa ili nije kukamilisha Tabia njema), ambapo Ukweli, Utekelezaji wa ahadi, Uaminifu, Wema, na kuunga undugu

Utoaji, ukarimu, Uokozi, Utu, Utambuzi, kujipamba na wema, na kuzuia maudhi kwa wengine, na kumnusuru mwenye matatizo, na kumwokoa mwenye kuomba uokovu, na kuwafariji wenye kukumbwa na matatizo, na kuwa mpole kwa wanyama, basi huo utakuwa Uislamu ulio sahihi na ndilo lengo lake kuu.

Katika jambo lisilo na shaka ni kwamba Kuujua Uislamu wenyewe, na kuzijua siri za ujumbe wake wa Usamehevu, na kusimama kidete katika Makusudio yake Makuu na Malengo yake Makuu, na kuyatekeleza yote kwa kuangazia mapya ya zama hizi, yanazingatiwa kuwa ni katika mambo ya lazima kwa ajili ya kupambana na changamoto za kisasa, na kuyazuia Makundi ya Kigaidi na ya Misimamo mikali, na kuizingira fikra iliyokengeuka na kuvunja mzunguko wake dumavu na uliojifunga, na Ufahamu mbaya, na Ufinyu wa peo, na kutoka katika Ufinyu huu kuelekea katika Ulimwengu unaokukribisha zaidi, mpana na ulio mwepesi, komavu na wenye mzinduko zaidi, na kuona na kuujua undani wa kitu, kwa ajili ya kuyafikia masilahi mapana ya nchi na Waja, na kusambaza Maadili ya Kibinadamu ambayo yanaleta usalama na amani, usalama, utulivu na furaha kwa binadamu wote.

Hakika miongoni mwa mambo ya wajibu mno na yaliyo muhimu zaidiambayo kila Mwislamu anapaswa kuyafanya ni kuwadhihirishia watu wote Utukufu wa Dini ya Uislamu ili ulimwengu mzima utambue kuwa Uislamu ni Dini ya Amani na inalingani Amani na inaiheshimu amani. Amani ni jina miongoni mwa Majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{هُوَ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ}

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama.

Na salamu ya Kiislamu ni Amani, na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَى إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا}

Wala msimwambie anayekutoleeni salamu; wewe sio Muumini

Na Maamkizi ya watu wa Peponi ni Salamu kwa maana ya amani, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ سَلَامٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ  فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ}

Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.

Na ilikuwa moja kati ya Dua zake Mtume S.A.W, baada ya kila Sala:

 (اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلاَمُ ، وَمِنْكَ السَّلاَمُ ، تَبَارَكْتَ يا ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ).

Ewe Mola wangu, wewe ni Amani, na amani inatoka kwako, umetukuka ewe Mwenye Utukuzo na Ukarimu.

Hakika Uislamu ni Dini inayoilinda heshima ya binadamu, inazuia kuteta na kusengenya uhasidi na kubaguana, kudharauliana na maudhi ya aina yoyote iwayo; iwe kwa kauli, kwa kitendo au hata kwa ishara, au hata kwa kudokezea, ambapo anasema Msema Kweli, Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَى أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَى أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَئكَ هُمُ الظَّالِمُون}

Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane heshima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kuamini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Mtu yoyote atakaemnyooshea nduguye chuma, hakika Malaika humlaani mpaka anapoacha kufanya hivyo, hata kama mtu huyo atakuwa ni nduguye wa mama mmoja na baba mmoja.

Na Mtume S.A.W, ametukataza Kupiga na kuchora usoni, na alipomwona mnyama amepigwa chapa usoni, akasema S.A.W: Mwenyezi Mungu amlaani aliyempiga chapa mnyama huyo usoni.

Na Mtume S.A.W, alipoulizwa kuhusu mwanamke anaefunga na kusali lakini anamuudhi jirani yake, akasema S.A.W: Huyo ni wa Motoni. Na anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote anayemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Siku ya Mwisho, basi asimuudhi Jirani yake, na mtu yoyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi amkirimu Mgeni wake, na yoyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi aseme maneno mazuri au anyamaze.

Ninaisema kauli yangu hii, na ninamwomba Mwenyezi Mungu anisamehe mimi na akusameheni na nyinyi. 

* * *

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ninashuhudia kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata wao mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu.

Mtume S.A.W, aliijenga misingi imara ya Mafunzo ya Uislamu wenye Usamehevu, na Tabia zake Njema, na Maadili Mema na Mazuri katika nyoyo za Maswahaba wake mpaka ukawa huo ndio Mfumo wa Maisha yao wanayoyaishi na kutangamana kwayo na watu wengine wote. Tunamwona Swahaba huyu, Jafar bin Abu Twaalib R.A, anasimama mbele ya Mfalme Najashi – Mfalme wa Uhabeshi, ambayo ni Ethiopia kwa sasa – akiweka wazi moja katika Maadili haya mema ya Uislamu, na hizo Tabia zake Njema kwa uweledi wa hali ya juu, na maneno ya kuaminika, anasema: Ewe Mfalme, sisi tulikuwa taifa la watu wa zama za Ujinga, tunayaabudu Masanamu, tunakula Mizoga, tunafanya Uzinzi, tunauvunja undugu, tunamtendea uovu ujirani, na Mwenye Nguvu anmmaliza Mnyonge miongoni mwetu, na tulikuwa hivyo hivyo mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, akatuletea Mtume miongoni mwetu, tunaijua nasaba yake, ukweli wake, uaminifu wake, Tabia yake njema, akatulingania tuelekee kkwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili tumpwekeshe, tumuabudu, na tujivule nay ale yote tuliokuwa tukiyaabudu sisi na baba zetu kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile Mawe na Masanamu, na akatuamrisha tuseme ukweli, tufikishe amana, tuunge undugu, tuwe na ujirani mwema, tuyaache yaliyoharamishwa na tusiuane, na akatuzuia uzinzi na Maneno ya uongo, na kula mali ya yatima, na kuwatuhumu uzinzi wanawake walioolewa, na akatuamrisha tumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu aliye peke yake, na wala tusimshirikishe na kitu chochote, na akatuamrisha kusali, kutoa Zaka, kufunga…

Kwa hivyo, Mwislamu wa kweli hadanganyi, hagushi, hafanyi uhaini, Mwislamu wa kweli ni yule ambaye Waislamu wenzake wamesalimika na Ulimi wake na mkono wake. Na Muumini wa kweli ni yule ambaye watu wote wamesalimika damu zao, heshima zao, Mali zao, na nafsi zao, Mwislamu wa kweli ni yule ambaye Tabia njema za Kiislamu huonekana wazi kwake, haiwafikii watu kutoka kwake isipokuwa kheri na wema, na kama tungelitaka kuweka maana halisi na ya kweli ya Mwislamu wa kweli na tusingeipata maana nzuri kuliko au ile jumuishi zaidi aliyoitoa Mtume S.A.W, kwamba: Mwislamu ni yule ambaye Watu wote wamesalimika kwa Ulimi wake na Mkono wake, ambapo anasema S.A.W: Je niwaambieni ni nani Muumini wa kweli? Ni yule ambaye watu wote wamemwamini kwa Mali zao na Nafsi zao, na Mwislamu ni yule ambaye watu wote wamesalimika kwa Ulimi wake na Mkono wake, na Mpiganaji wa Jihadi ni yule mwenyekupambana na nafsi yake katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mhamaji (Muhaajir) ni yule aliyoyahama Makosa na Madhambi yake.

Hakika risala ya Uislamu ni risala ya Ubinadamu, Hekima, Usamehevu, Huruma, Moyo mpana, Na ukubalifu, ni risala inayowakusanya watu na sio kuwatenganisha na kuwasambaratisha, Uislamu ni Uadilifu kamili, huruma kamili, usamehevu kamili, uwepesishaji kamili, utu kamili, na kila kila kinachozifikia maana hizi zenye hadhi ya juu nazo zimo ndani ya Uislamu, na mtu yoyote anayegongana au kujigonganisha na maana hizi zote; hakika mtu huyo atakuwa anajigonganisha na Uislamu, Malengo na Makusudio yake Makuu.

Ewe Mola wetu tuongoze katika Tabia zilizo bora zaidi, kwani hakuna wa kutuongoza katika Tabia bora zaidi isipokuwa wewe, na tunakuomba utuepushe na utukinge na tabia mbaya kwani hakuna wa kutuepusha na tabia mbaya isipokuwa wewe, na tunakuomba uzilinde nchi zetu na wananchi wake na majeshi yake ya ulinzi na ya usalama, na uyakinge na jambo baya, ewe Mpole wa wapole.