Habari

Unafiki na Hiana na hatari zake kwa Watu na Nchi

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote. Mwenyezi Mungu Mtukufu anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُمْ مِنْ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمُنْكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ نَسُوا اللَّهَ فَنَسِيَهُمْ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ هُمُ الْفَاسِقُونَ}

{Wanaume wanaafiki na wanawake wanaafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na huyakataza mema, na huifumba mikono yao. Wamemsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia amewasahau. Hakika wanaafiki ndio wapotofu}.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, peke yake asiyekuwa na Mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu, Mtume wetu na Kipenzi chetu Muhammad, ni Mja wake na Mtume Wake, anaesema katika Hadithi Tukufu

     : ” آية المنافق ثلاث:إذا حدث كذب,وإذا وعد أخلف ,وإذا ائتمن خان” Alama za Mnafiki ni tatu: anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huvunja ahadi, na anapoaminiwa hufanya hiana. Ewe Mola wetu mswalie na umrehemu na umbariki Bwana wetu Muhammad, na Jamaa zake na Maswahaba wake, na kila mwenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.أما بعد

Na baada ya hayo:

Jambo ambalo halina shaka ndani yake ni kwamba unafiki ni ugonjwa hatari, na ni janga linaloshambulia, na ni angamizi kwa watu na mataifa. Ni katika magonjwa hatari ya moyo ambayo hushambulia Imani ya kweli na hubomoa misingi yake na kuziangusha nguzo zake. Na ni janga la kijamii na la kimaadili lililo hatari mno ambalo huibomoa jamii, amani na utulivu wake; na kwa ajili hii, hakika hatari yake ni zaidi ya ukafiri na ushirikina; kwani ugonjwa wa Unafiki unapoingia katika mwili wa Umma huinyonya na kuikongoa mifupa yake, na huligawa neno la pamoja la Umma.

Vile vile silaha ya haini na kutumiwa ndivyo hatari zaidi vinavyoendelea kutishia mfumo mzima wa nchi na uwepo wake katika kipindi chote cha historia ambayo inazingatiwa kuwa ni ushahidi mzuri wa kwamba nchi zote zilizozorota na kuvunjika vunjika hadi kuteketea kabisa ukweli ni kwamba ziliangamizwa kwa ndani, na wahaini wote na watumiwa na mamluki walitoa mchango mkubwa dhidi ya nchi zao katika kipindi chote cha historia ya mwanadamu. Kwa hivyo, daima hatari zinazozitishia nchi kutokea ndani ya nchi hizo ni hatari zaidi kuliko hatari ambazo zinazitishia nchi hizo kwa nje.

Sisi tunapaswa kutambua kwamba Unafiki uko wa aina mbili: Unafiki Mkubwa na Unafiki Mdogo. Katika aina hizi mbili, Unafiki Mkubwa ni hatari zaidi, nao ni wa Itikadi ambapo aliyenao hudhihirisha Uislamu na huficha ukafiri alionao ndani yake. Na aina hii, aliye nao hudumu milele Motoni, bali huwekwa katika daraja la Chini zaidi la Motoni. Na Unafiki wa aina ya Pili: Unafiki Mdogo: Nao ni ule wa kivitendo ambao ni kukengeuka katika mwenendo. Na kujivesha kitu chochote ni katika alama za wanafiki. Nako ni mtu kudhihirisha Uzuri na kuyaficha yote yaliyo kinyume na hivyo, na aina hii haimtoi mtu kikamilifu katika Dini; isipokuwa ni njia ya  kuelekea katika Unafiki Mkubwa ikiwa Muhusika hatatubu.

Hakika Qurani tukufu imetuhadithia, na Sunna ya Mtume S.A.W iliyotwaharika imetuhaidithia kuhusu wanafiki na sifa zao pamoja na tabia zao na sumu zao. Hatujawahi kuziona sifa hizo zinabadilika katika zama zozote, au kutofautiana kwa tofauti ya nchi. Na miongoni mwa alama muhimu zinazowatambulisha wanafiki ni:

* الكذب، وخلف الوعد، وخيانة الأمانة، والفجور في الخصومة

Uongo, kwenda kinyume na ahadi au miadi, na kufanya hiana katika kuaminiwa, na ukorofi katika ugomvi: Nazo ni sifa mbaya mno katika sifa za Wanafiki ambazo Mtume S.A.W amewasifu kwazo Wanafiki, nayo ni katika unafiki wa vitendo alioufafanua Mtume S.A.W, pale aliposema  : حيث قال : (أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ

 مُنَافِقًا خَالِصًا ، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا :

إِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ ، وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ).

) Mtu ambaye atakuwa na sifa hizi nne basi atakuwa Mnafiki Mtupu. Na atakayekuwa na yoyote katika hizo basi atakuwa na sehemu ya unafiki mpaka aiache: Anapoaminiwa hufanya hiana, na anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huvunja ahadi yake, na anapogombana na mtu hufanya uovu).

 Mtu yoyote ambaye sifa hizi nne zitamkusanyikia, au moja kati yake, basi anakuwa Mnafiki mtu huyo, na sifa hizi zote huyavuruga masilahi ya Umma na hulenga katika kuyabomoa kabisa.

Mara nyingi huwa tunaona Mtu Mnafiki anasema Uongo ili amfikirishe mwingine kuwa yeye ni mkweli katika kauli na kvitendo vyake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّهَ عَلَى مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ}

{Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu}.

Unapotajwa Unafiki, Udanganyifu na Hiana ya kuaminiwa katika Qurani tukufu, hutajwa pamoja na Uongo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَالَّذِينَ آَمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ * فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّهُ مَرَضًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ}،

{Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo}.

Mtume S.A.W ametuonya kuhusu Uongo kwa kutuwekea wazi athari zake mbaya aliposema:

  (وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللَّهِ كَذَّابًا)

( Uepukeni Uongo, kwani hakika ya Uongo hupelekea katika Uovu, na hakika ya Uovu hupelekea Motoni, na Mtu huendelea kudanganya na kujipamba na uongo mpaka kaandikiwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye ni Mwongo).

Na Mtume S.A.W aliulizwa: Je Muumini anaweza kuwa mwoga? Akasema: ndio. Akaambiwa: Je Muumini anaweza akawa Bakhili? Akasema: Ndio. Akaulizwa: Je Muumini anaweza akawa mwongo? Akasema: Hapana. Na Abu Bakari R.A ameupa uongo sifa ya hiana, katika kauli yake: Ukweli ni Uaminifu na Uongo ni Hiana

 Pia Uhaini na Utumiwaji (الخيانة والعمالة) ambavyo hupelekea kukata mahusiano ya upendo, na kubaguana hupelekea migogoro na migawanyiko, na kuvurugika kwa mahusiano. Na Mtume S.A.W amebainisha kuwa hiana ya kuaminiwa huwa fedheha kwa muhusika siku ya Malipo: Pindi Mwenyezi Mungu atakapowakusanya wa Mwanzo na wa Mwisho pamoja, Siku ya Kiama, kila aliyevunja ahadi atavuliwa vazi na patasemwa: Huu ni uvunjaji wa ahadi wa Fulani bin Fulani. Na Mtume S.A.W atakuwa Mgomvi wake Siku ya Kiama, ambapo amesema:

حيث قال : (ثَلَاثَةٌ أَنَا خَصْمُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ، وَمَنْ كُنْتُ خَصْمَهُ خَصَمْتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ : رَجُلٌ أَعْطَى بِي ثُمَّ غَدَرَ ، وَرَجُلٌ بَاعَ حُرًّا فَأَكَلَ ثَمَنَهُ ، وَرَجُلٌ اسْتَأْجَرَ أَجِيرًا فَاسْتَوْفَى مِنْهُ وَلَمْ يُوفِهِ أَجْرَهُ)

 (Watu watatu mimi ni Mgomvi wao Siku ya Kiama, na yule mimi nitakayekuwa Mgomvi wake basi nitamfanyia ugomvi Siku ya Kiama: Mtu aliyeniahidi kisha akavunja ahadi yake, na mtu aliyemuuza Muungwana na akala thamani yake, na mtu aliyemwajiri mwajiriwa akatekeleza wajibu wake lakini hakumlipa ujira wake).

Na miongoni mwa aina hatari mno za Uhaini, ni uhaini wa nchi na kuziuza kwa thamani ya chini na kwa ajili ya lengo la Dunia lenye kutoweka kwa mfano wa yafanyavyo makundi yenye misimamo mikali ya kidini na wanaowafuata au wanaopita katika mkumbo wao na mfumo wao katika kuziuza nchi zao kwa thamani duni.

Na miongoni mwa sifa mbaya ambazo Uislamu umetuonya nazo: Ni Uovu katika ugomvi: الفجور في الخصومة. Nao ni mkusanyiko wa aina zote za shari, na ni asili ya kila jambo baya, na ni njia ya kumtoa mtu katika haki, na huifanya haki ikawa batili na batili ikawa haki. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameusifu Uovu katika ugomvi kama ukubwa wa Ugomvi au uhasimu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{ وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّهَ عَلَى مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ}

{Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu}.

Na kutoka kwa Bi Aisha R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W, amesema:

(إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللَّهِ الأَلَدُّ الخَصِمُ).

( Hakika watu wasiopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni Wagomvi waliopindukia).

Kwa hivyo Unafiki uko karibu zaidi na wasifu wa hali zao kwa kuwa wao ni wenye nyuso mbili, bali tunawaona katika zama zetu hizi wamepindukia mipaka kwa kiasi kikubwa mno, wakawa sasa wana nyuso zaidi ya elfu moja, nao ni katika watu wa shari zaidi katika viumbe. Anasema Mtume S.A.W: Mtawakuta watu walio na Shari zaidi ni wale wenye nyuso mbili ambao huja kwa watu hawa kwa uso mmoja na huwenda kwa wengine kwa uso mwingine.

Na katika alama za Unafiki:                            الإفساد في الأرض وادعاء الإصلاح

Ni wao kufanya Ufisadi Duniani na kudai kuwa wanatengeneza:

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika jambo hili:

{وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَكِنْ لَا يَشْعُرُونَ}

{Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui}.

Na uharibifu au ufisadi una sura za aina mbali mbali, miongoni mwazo ni: Ni kuzua habari mbaya za kuvunja moyo katika nchi, na kueneza Udhaifu na Unyonge katika nafsi za waumini wa kweli, na kutumbukiza fikra potovu, na mieleweko iliyokengeuka, na kueneza fitina baina ya watu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, Msema Kweli:

{لَوْ خَرَجُوا فِيكُمْ مَا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا خِلَالَكُمْ يَبْغُونَكُمُ الْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّاعُونَ لَهُمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ}

{Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu}.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَقَالُوا لَا تَنْفِرُوا فِي الْحَرِّ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا لَوْ كَانُوا يَفْقَهُونَ}

{na wakasema: Msitoke nje katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto zaidi, laiti wangeli fahamu! }

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{قَدْ يَعْلَمُ اللَّهُ الْمُعَوِّقِينَ مِنْكُمْ وَالْقَائِلِينَ لِإِخْوَانِهِمْ هَلُمَّ إِلَيْنَا وَلَا يَأْتُونَ الْبَأْسَ إِلَّا قَلِيلًا}،

{Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua hao wanao zuilia, na wanao waambia ndugu zao: Njooni kwetu! Wala hawaingii vitani ila kidogo tu}. Na miongoni mwa sura za Ufisadi: ni kuwanyima watu haki zao, na kuwashusha hadhi.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ}،

{Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi}.

Na miongoni mwa sura zake ni: Kuvunja na Kubomoa, kuwaua wasiokuwa na hatia, na kuwatisha wenye amani, na kuzorotesha masilahi ya watu, na kutotekeleza majukumu ipasavyo, na vile vile rushwa, na upendeleo, na kula mali za watu kinyume na haki. Na uvivu wa kufanya ibada, kujionesha kwa watu\ mtu anapofanya ibada, na hasa katika tendo miongoni mwa matendo yaliyo bora zaidi na yenye kheri nyingi ambalo ni swala.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَى يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُون َاللَّهَ إِلَّا قَلِيلًا}

{Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kusali huinuka kwa unyong’onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu}.

*******

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَمَا مَنَعَهُمْ أَنْ تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ وَلَا يَأْتُونَ الصَّلَاةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَى وَلَا يُنْفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَارِهُونَ}

{Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala hawatoi michango ila nao wamechukia}.

Na Mtume S.A.W anasema: Hakuna Swala iliyo nzito kwa Wanafiki kuliko Swala yaAlfajiri na Isha, na kama watu wangejua yaliyomo ndani yake basi wangezienda swala hizi hata kwa kutambaa.

Na kutoka kwa Jabir bin Abdillah R.A, anasema: Mtume S.A.W alitoka akasema: Enyi watu. Jiepusheni na Shirki ya Siri, wakamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni ipi hiyo Shirki ya mambo ya ndani? Akasema: Ni Mtu kusimama na kuipamba swala yake kwa juhudi pevu kwa kuona watu wanamwangalia, na hiyo ndio Shirki ya Siri.

Ninaisema kauli yangu hii, na ninamwomba msamaha Mwenyezi Mungu kwa ajili yangu na kwa ajili yenu.

*       *       *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote. Na rehma na amani zimwendee Mtume wa Mwisho na Mjumbe wake, Bwana wetu Muhammad, S.A.W, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu Waislamu: Hakika miongoni mwa alama za Unafiki: Ni kuungana na Maadui na kuwasiliana nao dhidi ya Dini na Taifa, kufanya ujasusi, Kuwa Haini, kunukulu habari na maelezo, na kutoa siri za nchi. Kwa hiyo, mnafiki ni mtumiwa anayewasaidia maadui wa nchi yake dhidi ya watu wake, majirani zake na ndugu zake.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَنْ تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَنْ يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِنْ عِنْدِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنْفُسِهِمْ نَادِمِينَ}،

{Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenyekujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao}.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَإِنَّ مِنْكُمْ لَمَنْ لَيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَابَتْكُمْ مُصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيَّ إِذْ لَمْ أَكُنْ مَعَهُمْ شَهِيدًا * وَلَئِنْ أَصَابَكُمْ فَضْلٌ مِنَ اللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَنْ لَمْ تَكُنْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُ مَوَدَّةٌ يَا لَيْتَنِي كُنْتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا}

{Na yupo kati yenu anaye bakia nyuma; na ukikusibuni msiba husema: Mwenyezi Mungu kanifanyia kheri sikuwa nao. Na ikikufikieni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu husema – kama kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu naye: Laiti ningeli kuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makubwa}.

Mnafiki hufurahi pale shari inapolifikia taifa na wananchi wake, au fitna ikaenea baina yao, au ubonjwa ukasambaa kwao, au wakavunjika nguvu yao.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنْ تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِنْ تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا وَإِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئاً إِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ}.

{Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo}.

Na Wanafiki wapya, pamoja na kuwa na sifa ya Uongo, Hiana na Kuvunja ahadi, kuvunja mikataba na makubaliano, na kuvuruga Rai ya Umma, na kuifanyia Dini hiana, wao wamejumuisha pia aina mpya ya Udanganyifu, ambapo iliyo wazi zaidi kati ya hizo ni Kuiuza Dini, na kuitumia Dini kwa maslahi ya makundi ambayo yanataka kuifanya Dini kama ngazi ya kupandia katika Uwanja wa Siasa, wakijipamba kwa aina mbali mbali za ufuasi wa juu juu wa Dini, na Udini wa Kisiasa, na kuinasibisha Imani kwao wao na kuikanusha kwa wengine wasio kuwa wao, wakihangaikia kujipatia pazia la kisheria la kazi zao, ukiongezea na kuwa wanafiki hao wapya wana sifa ya Uhaini wa Nchi na chuki dhidi ya nchi na pia kuiuza kwa thamani ya chini. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiahidi aina hii ya watu kwamba wao watazungukwa, na kwamba ghadhabu za Mwenyezi Mungu Mtukufu zitawakumba hapa Duniani na kesho Akhera, na wale wanaopanga njama za kuwatumbukiza Waislamu katika Misukosuko na Matatizo basi vyote hivyo vitawarejea wao wenyewe.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ}

{Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya}.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu na amewaadhibu Wafuasi wa Unafiki Mkubwa kwa kuyumbayumba na kutokuwa na Utulivu, na kupatwa na kihoro na fedheha katika kila jambo lao.

 Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{مُذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَلِكَ لَا إِلَى هَؤُلَاءِ وَلَا إِلَى هَؤُلَاءِ وَمَنْ يُضْلِلِ اللَّهُ فَلَنْ تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا}

{Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako na huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, kabisa hutompatia njia}.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ}

{Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki? }

Na Mwenyezi Mungu ameziepusha nyoyo zao na Ufahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W, na kwa hivyo uongofu haufiki katika nyoyo zao, na wala heri yoyote haiwi safi kwao.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{ذلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلى قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لا يَفْقَهُونَ}

{Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote}.

Na kwa upande wa adhabu yao katika Siku ya Mwisho, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمِمَّنْ حَوْلَكُمْ مِنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ سَنُعَذِّبُهُمْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَى عَذَابٍ عَظِيم}

{Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa}.

Kwa hivyo, Adhabu ya kwanza wanaipata hapa Duniani, na Adhabu ya pili wanaipata Kaburini. Adhabu kubwa itakuwa Siku ya Mwisho, ambapo Mwenyezi Mungu atawakusanya Motoni, Wanafiki wote pamoja na wale waliokuwa nao katika mambo ya Shari.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ اللّهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا}

{Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanaafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannamu}.

 Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَنْ تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا * إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّهِ فَأُولَئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا}.

{Hakika wanaafiki watakuwa katika t’abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru. Isipo kuwa wale walio tubu, na wakatengeneza na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakamtakasia Dini yao Mwenyezi Mungu. Basi hao ni pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atakuja wapa Waumini ujira mkubwa}.

Na kwa ajili ya kuilinda nchi na kuvilinda vilivyomo, mshikamano na amani yake, hapana budi kwa kila mwananchi mwenye moyo msafi na mkunjufu, kuwa macho kama mlinzi, mtu mmoja mmoja au taasisi, na hapana budi kukusanya nguvu na juhudi kwa kila mwenye heshima, ili kukata mizizi ya Wahaini na Watumikao na wapelelezi wanaoshirikiana na Maadui miongoni mwa wahalifu, na kuwafedhehesha mbele ya watu wenye kushuhudia, na kuwafanya wakawa zingatio kwa kila mwenyekufikiria kupita njia ya wahaini na watumiwa, , kwa ajili ya kuilinda Dini yetu, nchi yetu na watu wake wote,na kabla ya yote hayo, kumridhisha Mola wetu Mtukufu, na kuzilinda nchi zetu, ili zisije zikapatwa na yale yaliyotokea katika nchi nyingine ambazo zilizembea na kupuuzia katika kupambana na Wahaini na Watumiwa na kudhani kuwa jambo lango ni dogo tu. Na Jambo hili halijawahi kuwa dogo katika historia ya Mataifa mbali mbali.

Ewe Mola wetu zitakase nyoyo zetu na unafiki, na uyatakase macho yetu na Hiana, na uzilinde ndimi zetu na Uongo, na uilinde nchi yetu na watu wake.

اللهم طهر قلوبنا من النفاق ، وأعيننا من الخيانة

وألسنتنا من الكذب، واحفظ بلادنا وأهلنا

Adabu na Haki za Misingi za Jamii na athari zake katika upevukaji wa Jamii na Ujenzi wa Ustaarabu

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote. Ambaye anasema katika kitabu chake Kitukufu:

     {قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ}

Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Yeye Pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Anasema Mtume wetu Muhammad S.A.W: Mwenyezi Mungu Mtukufu amenifunza adabu na akanifundisha vizuri.

Ewe Mola wetu, mswalie, mrehemu na umbariki Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata kwa Wema mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika Uislamu umekuja kwa mfumo uliokamilika, unaopandilia uhusiano wa mwanadamu na Mola wake, na uhusiano wa watu, na uhusiano wa Ulimwengu mzima. Na Sheria ya Kiislamu imejaa taratibu na Adabu Kuu ambazo zinachangia katika kukuza Jamii na kuifanya isonge mbele kimaendelea na kuiletea maisha bora. Na miongoni mwa Adabu hizo ni: Adabu ya kuomba idhini, ambapo Uislamu umeiweka adabu hii ya kuomba idhini, na kuifanya kuwa ni katika adabu za Uislamu ambazo zinawapa watu mazingira ya kujitenganisha na wengine, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتاً غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّى تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَى أَهْلِهَا ذلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ}

Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka.

Na Mtume S.A.W ametufundisha sisi jinsi ya kuomba idhini, na kwa ajili hiyo mtu anapaswa kuanza kutoa salamu, kisha kutaja jina lake. Mtu mmoja aliomba idhini kwa Mtume S.A.W akiwa nyumbani kwake, akasema: Je ninaweza kuingia? Mtume S,A.W akamwambia mtumishi wake: Mtokee mtu huyu, na umfundishe jinsi ya kuomba idhini ya kuingia, na umwambie: Sema: Asalaamu alaikum, je niingie? Yule Mtu akamsikia na akasema: Assalaamu Alaikum. Je niingie? Na Mtume S.A.W akamwidhinisha aingie, na akaingia. Na kutoka kwa Jabir R.A, Anasema: Nilienda kwa Mtume S.A.W, na nikaugonga mlango wake, akasema: Ni nani huyu? Nikasema: Ni mimi. Akasema: Mimi mimi! Kama vile aliyachukia maneno haya.

Na miongoni mwa adabu za kuomba idhini ni kuinamisha macho, na kutouelekea mlango. Anasema Mtume S.A.W: Hakika mambo yalivyo, kuomba idhini kumewekwa kwa sababu ya macho. Na kutoka kwa Saadu bin Ubaadah R.A, anasema: Kwamba yeye aliomba idhini ya kuingi huku akiwa ameuelekea mlango, na Mtume S.A.W akamwambia: Usiombe idhini ya kuingia na wewe ukiwa umeuelekea mlango. Na imepokelewa kwamba Mtume S.A.W alikuwa pindi anapoiendea nyumba yoyote na akafika mlangoni akitaka kuomba idhini ya kuingia hakuuelekea mlango, alikuwa anaujia mlango upande wa kulia au kushoto, na anapopewa idhini ya kuingia huingia, na kama hakupewa idhini basi huondoka.

Na miongo mwa adabu kuu ambazo Uislamu umezilingania: ni adabu ya jinsi ya kuwa njiani na katika maeneo ya umma. Uislamu umeipa haki barabara ambayo lazima itekelezwe. Anasema Mtume S.A.W: Tahadharini na kukaa njiani. Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tunalazimika kuwa katika vikao vyetu vya njiani. Tunazungumza ndani yake. Mtume S.A.W akasema: Mtakapokuja katika vikao vyenu vya njiani, basi ipeni njia haki yake. Wakasema: Ni ipi hiyo haki ya njia? Akasema Mtume S.A.W: kuinamisha macho, na kuondosha kila kinacholeta maudhi, kuitikia salamu, na kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Na anasema Mtume S.A.W:  Imani ina sehemu sabini na kitu – au sitini na kitu – na sehemu iliyo bora kuliko zote ni kusema Hapana Mola mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nay a chini yake ni kuondosha maudhi njiani. Na haya ni sehemu ya Imani.

Kwa hiyo mtu anayeitumia njia au sehemu yoyote ya umma, anapaswa kutonyanyua sauti yake, au kuzungumza kwa sauti ya juu yenye kusumbua, na kutocheka kwa sauti yenye kukiuka maadili, na kutotupa uchafu hovyo njiani bali kuuweka uchafu huo katika sehemu husika, bali ni wajibu kuuondosha uchafu njiani, kama ambavyo ni lazima kutozorotesha njia, na kuwaudhi wapitao kwa kuwakodolea macho au kuwanyanyasa kwa maneno au hata kwa vitendo.

Na miongoni mwa adabu, ni adamu ya Usafi. Uislamu unauzingatia usafi kamili wa mwili, nguo na eneo kama ni kitu kisichotenganishwa na shria, kwa namna inayoendana na umuhimu wake kama mwenendo wa kibinadamu, na thamani ya kistaarabu; na kwa hivyo, Uislamu umetuasa tufuate na kutekeleza mjumuiko wa adabu mbali mbali zinazomfanya mwanadamu awe na mwonekano mzuri, watu hawachukizwi naye. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu waumini wenye kupupia usafi wa miili yao, na kujisafisha kwa nje na ndani yao, akasema:

 {إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}

Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojisafisha.

Na Mtume S.A.W anasema: Hakika Mwenyezi Mungu anaupenda uzuri, naye ni msafi anaupenda usafi…

Na anasema Mtume S.A.W: Usafi ni sehemu ya Imani… Na mtume S.A.W alimwona mtu mmoja akiwa amejawa na vumbi – nywele zake zimetawanyika – akasema Mtume S.A.W: Je Mtu huyu hakupata kitu cha kuziweka sawa nywele zake? Na amlimwona mtu mwingine aliyevaa nguo chafu, akasema S.A.W: je mtu huyu hajapata kitu cha kusafishia nguo zake?

Mtume S.A.W ametuasa pia juu ya usafi wa meno, na amefanya hivyo kwa sababu ya kupupia usafi na uzuri wa harufu yam domo, na kutowaudhi watu kwa harufu mbaya yenye kukera ambayo inaweza kuwafanya watu wamkimbie. Anasema Mtume S.A.W: Kama nisingeuhofia Umma wangu – au watu wote – basi ningewaamrisha kupiga mswaki katika kila swala.

Na miongoni mwa adabu za Uislamu, ni adabu ya Mazungumzo. Mazungumzo ni katika njia za kutambuana na kurekebisha makosa. Na Uislamu umeufungua mlango wa mazungumzo baina ya watu wote; mpaka kufikia uongofu wa ukweli, bila ya uzito wowote au vikwazo. Lakini mazungumzo yanapaswa yawe mbali na kuwasema vibaya watu wengine, au kuwadharau au hata kuwadhalilisha. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ}

Na ujadiliane nao kwa njia iliyo bora.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَقُلْ لِعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ..}

Na Waambie waja wangu waseme maneno mazuri…

Na anasema Mtume S.A.W: Muislamu sio wa kuwasema wengine vibaya, au kuwalaani au kutoa kauli chafu au maneno ya kukera.

Kwa hivyo, mazungumzo yanatakiwa yawe mazuri yenye kufuata misingi ya elimu na kutotoka nje ya lengo kuu pamoja na kuchunga mazingira. Na katika misingi hiyo ya kielimu ni kuwa na uhakika na maelezo yanayotolewa pamoja na kutoharakisha katika kunukulu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ}

Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenyekujuta kwa mliyoyatenda.

Na anasema Mtume S.A.W: kufanya mambo kwa utulivu kunatokana na Mwenyezi Mungu, na kufanya mambo kwa haraka haraka kunatokana na Shetani.

Na anasema Mtume S.A.W:  Kufanya mambo kwa utulivu kunatakiwa katika kila jambo isipokuwa kazi ya Akhera tu.

Na anasema Mtume S.A.W: Inamtosha Mtu kuwa mwongo kwa kukizungumzia kila anachokisikia. Na miongoni mwa adabu za mazungumzo:  ni kutokariri mara kwa mara vumi au kuzizungumzia kwa kina; kwani mwenye kufanya hivyo anachangia kuzitangaza na kuzisambaza. Vumi huvuma na kuenea zaidi zinapopata ndimi za kuzikariri na msikio ya kuzisikiliza na nafsi zinazozikubali na kuzipitisha.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُمْ مَا لَيْسَ لَكُمْ بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِنْدَ اللَّهِ عَظِيمٌ}

Mlipo yapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.

Na anasema Mtume S.A.W: Mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, asimuudhi jirani yake, na mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake amkirimu Mgeni wake, na mtu Mwenyekumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na aseme maneno mazuri au anyamaze.

Na katika adabu kuu zilizokuja katika Uislamu: ni kupunguza sauti; na maana yake ni mtu kutoinyanyua sauti yake kuliko kiwango kilichozoeleka na hasa katika uwepo wa aliye juu yake kihadhi. Na Katika Qurani Tukufu kuna wasia wa Luqman kwa mwanae ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ إِنَّ أَنْكَرَ الْأَصْواتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ﴾ [لقمان: 19].

Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.

Na Mwenyezi Mungu amewasifu wale wanaopunguza sauti zao na hasa katika uwepo wa Mtume S.A.W.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ أُولَئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَى لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ﴾ [الحجرات: 3].

Kwa hakika wanao teremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.

Na miongoni mwa adabu: ni kumwongoza aliyepotea na kumrejesha katika njia iliyo sawa, kwa kumwelekeza.

Anasema Mtume S.A.W:  Tahadharini na ukaaji wa njiani. Wakasema Maswahaba; sisi hatuna budi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa katika vikao vyetu tunazungumza kwenye vikao hivyo. Akasema: Na mtakapovijia vikao vyenu basi ipeni njia haki yake. Wakasema: Ni ipi haki hiyo ya njia? Akasema: ni kuinamisha macho, kuondosha maudhi, kujibu salamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya, na kumwongoza aliyepotea.

Ninasema kauli yangu hii na ninamwomba Msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili yangu na kwa ajili yenu

*        *        *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye peke yake na hana mshirika wake, na ninshuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja wake na ni Mjumbe wake. Ewe Mola wangu swalie, mpe rehma na umbariki yeye, na jamaa zake na maswahaba wake wote.

Ndugu zangu waislamu: kuna adabu kuu zingine zenye umuhimu mkubwa ambazo hapana budi tujipambe nazo kama waislamu. Miongoni mwazo ni: Kumsaidia mwenye matatizo: Uislamu umeijaalia adabu hii kama ni moja ya matendo mema mno yanayomkurubisha mja kwa Mola wake. Kutoka kwa Abu Dhari R.A: kwamba Mtume S.A.W anasema: Haina nafsi ya mwanadamu isipokuwa wajibu wa kutoa sadaka kila siku inayochomozewa na jua. Ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tutapata wapi sadaka hiyo tutakayoitoa? Akasema: Hakika milango ya kheri ni mingi: Kumsabihi Mwenyezi Mungu, na kutoa takbiira na kusema laailaaha illa laahu, na kuamrisha mema na kukataza mabaya, na kuondosha maudhi njiani, na kumsikilizia kiziwi, na kumwongoza kipofu na kumwelekeza mwenye kutaka kuelekezwa haja yake na kuhangaika kwa nguvu zote iwezekanavyo kwa kuichosha mikono yako kwa ajili ya kumsaidia mnyonge, yote haya ni sadaka kutoka katika nafsi yako na kwa ajili ya nafsi yako. Sahiihu bnu Habbaan.

Na miongoni mwa sadaka nyingine:  ni kuwasaidia wanyonge na wenye mahitaji maalumu kwa ajili ya kuleta mlingano katika maisha yetu, kwa ushahidi wa kauli ya Imamu Ali R.A: “Mwenyezi Mungu amefaradhisha katika mali za matajiri vyakula vya mafukara isipokuwa panapokuwapo uchoyo wa tajiri na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawauliza Matajiri kwa hili”. Na malezi haya yanahesabika kama nyongeza kubwa ya pato la kitaifa kwamba kuwalea watu ni haki na wajibu wa jamii. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu yukaribu na mwenyekuvunjika moyo wake, ni Mpole anayewahurumia waja wake. Hadharau chochote katika wema hata kama ni neno zuri; anasema Mtume S.A.W: Usidharau chochote katika wema, hata kama unakutana na nduguyo na uso mkunjufu.

Na anasema Mtume S.A.W: na hakika nyinyi mna nusuriwa na kupewa riziki kwa ajili ya walio wanyonge katika nyinyi! Na Mwenyezi Mungu humsaidia Mja anayeendelea kumsaidia nduguye.

Na katika adabu: ni kumuheshimu mkubwa na kumnyenyekea pamoja na kuwa mpole kwake na kutomnyanyulia maneno, na kwa hiyo uchungwe utu uzima wake na utangu wake katika Uislamu, na hadhi yake itambulike pamoja na nafasi yake. Na mkubwa pia anaamrishwa kuwaonea huruma wadogo na kuwa mpole na laini kwao. Anasema Mtume S.A.W: Hakuna Mwislamu yoyote anayemkirimu mwenye mvi isipokuwa Mwenyezi Mungu atamlipa yeye kwa kumpa mtu atakayemkirimu katika umri wake wa uzeeni.

Na huu ni katika mwonekano wa utukufu wa Uislamu, rehma na usamehevu wake, uadilifu na utoaji wa haki pamoja na ari ya kumkirimu mwanadamu. Na Mtume S.A.W ametufundisha tuwe na adabu kwa Mwenye mvi, mwenyekuhifadhi Qurani Tukufu, Kiongozi Mwadilifu, kama ni sura miongoni mwa sura za kumtukuza Mwenyezi Mungu aliyetukuka, ambapo anasema S.A.W: Hakika katika kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumkirimu mwenye mvi aliye mwislamu, na Mwenyekuihifadhi Qurani Tukufu asiyejikweza au kutoijali, na kumheshimu kiongozi mwadilifu. Anasema Mtume S.A.W: Sio katika sisi mtu asiyemhurumia mdogo kati yetu, na anayemdharau mkubwa kati yetu. Na akaamrisha mema na akakataza mabaya.

Hakika uelewa mzuri wa Usamehevu wa Uislamu haushurutishi mwenye mvi awe mwislamu. Imepokelewa kuwa Mtume S.A.W alitoa sadaka yake kwa watu wa nyumba ya myahudu, kwani jambo hili linafanyika kwao. Na huyu hapa Bwana wetu Omar bin Abdul Aziiz R.A: anamwandikia mfanya kazi wake huko Basra akisema: angalia katika watu wa Dhima yule aliyezeeka, nguvu zimemwishia, na hawezi tena kuzalisha mali, basi mtolee kutoka katika Nyumba ya Mali ya Waislamu kiasi kinachomsaidia.

     Na miongoni mwa haki za Jamii kwa watoto wake kuchunga masilahi makuu ya nchi, hata kama tutachukua mfano wa suala la ongezeko la wakazi, hakika sisi tunathibitisha kuwa kuna mambo mawili. La kwanza: Kwamba baadhi ya watu wanajiangalia wao wenyewe ikiwa wanao uwezo na ni matajiri, na uwezo sio tu uwezo wa kifedha, bali ni uwezo wa kifedha nakimalezi, na kila kinachojumuisha kila upande wa matunzo na malezi, na wala sio uwezo wa mtu tu, isipokuwa ni jambo linalopindukia nyenzo za mtu mmoja mmoja na kuelekea katika nyenzo za mataifa katika kutoka huduma bora ambazo mtu peke yake hawezi kuzitoa huduma hizo, na kuanzia hapo, hali na nyenzo za mataifa ni moja ya sababu muhimu ambazo lazima ziwekwe katika zingatio kwenye kila upande wa mchakato wa idadi ya wakazi

Mtu anaeishi kwa ajili ya ke binafsi hakustahili kuzaliwa. Kwa hiyo ongezeko la wakazi lisilodhibitika halioneshi athari yake kwa mtu mmoja mmoja au kwa familia tu, bali bali linajenga madhara makubwa mno kwa nchi zisizofuata njia za kielimu katika kutibu masuala ya wakazi na kwamba upana na ufinyu katika Suala hili havipimwi kwa vipimo vya mtu mmoja mmoja katika kujitenga na hali za Mataifa na nyenzo zake kuu.

Pili: Kwamba uchache wenye nguvu ni bora kuliko wingi ulio mnyonge na dhalili ambao ameuzungumzia Mtume S.A.W kwamba ni wingi unaofafa na wa sungusungu, kwani hali za aina yake ambazo baadhi ya Mataifa yanazipitia katika mazingira yasiyoziwezesha kujipatia nyenzo za kimsingi katika afya, elimu na miundo mbinu katika hali ya uwingi unaodhibitika, na kwa namna inayopelekea kuwa wingi huo ni sawa na uwingi wa sungusungu. Hakika mtu yoyote mwenye akili anatambua kwamba panapotokea ukinzani baina ya Ubora na uwingi basi hakika zingatio la kweli huwa katika ubora na wala sio uwingi na hapo ndipo uchache wenye nguvu unapokuwa bora mara elfu moja kuliko uwingi wenye unyonge na Udhaifu.

Na hii ni kwa kuwa wingi unarithisha unyonge, au ujinga au ukengeukaji wa gurudumu la ustaarabu, na ambako huwa ni upuuzi mzito ambao hauhimiliki au hauyafikii matakwa ya vyanzo vya dola na nyenzo zake, huo ni wingi aliousifu Mtume wetu S.A.W, kama wingi unaofanana na wingi wa sungusungu ambao hauna faida yoyote bali ni uwingi unaodhuru na wala haunufaishi.

Ewe Mola wetu tuongoe tuwe na tabia njema zaidi, kwani hakuna wa kutuongoza katika tabia njema zaidi isipokuwa Wewe, na utuondoshee kila baya, kwani hakuna wa kuondosha mabaya isipokuwa Wewe, na utujaalie tuwe katika waja wako wenye nia safi.

 

Moyo wa Kushirikiana Kikazi na Masharti yake

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mlezi wa viumbe vyote, asemaye katika Kitabu chake Kitukufu:

 {وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ}

Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye kujua siri na dhahiri; naye atakuambieni mliyokuwa mkuyatenda.

Na ninashudua kwamba hakuna mungu mwingine apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ninashuhudia kuwa hakika Bwana wetu Muhammad ni Mtume wetu, na ni Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake. Ewe Mola wangu mswalie, mpe salamu na umbariki Mtume wetu, na Ali zake, na Maswahaba wake, na atakayewafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu;

Hakika ya Mataifa hayajengwi kwa maneno au maberamu, bali hujengwa kwa elimu, kutoa, na kujitolea. Na miongoni mwa njia za ujenzi wa Mataifa na maendeleo yake, ni kufanya kazi kwa bidii kamili, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu na Msema kweli:

{وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ}

Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye kujua siri na dhahiri; naye atakuambieni mliyokuwa mkuyatenda.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda pindi mtu anapofanya kazi yake basi aitekeleze ipasavyo. Kwa hiyo, Dini na Taifa kwa pamoja vinatuhijaji juhudi, jasho,  kufanya kazi kwa Bidii na kuzalisha, na hasa kwa kuwa Dini yetu ya Uislamu ni Dini ya Kazi na kuifanya iasavyo. Na kwa kuwa mtu ni elementi muhimu nay a msingi katika ujenzi wa jamii, kwahiyo mchango wake halisi katika ujenzi huu, haukamiliki na wala hautimii isipokuwa kupitia kazi ya kila mmoja katika jamii husika, ambapo mtu yeye peke yake anaweza kufanikisha baadhi ya kazi lakini inapoongezwa fikra katika fikra ya mwingine, na juhudi yake kuongezwa katika juhudi ya mwingine, hapana shaka kwamba mafanikio yatakayopatikana yatakuwa makubwa zaidi na yenye manufaa mapana; na kwa hivyo, Uislamu unaipa hadhi ya juu kazi ya pamoja na kuifanya kuwa ni katika sababu muhimu sana na ni misingi ya ujenzi wa nchi mbali mbali na Staarabu, kwa kuwa ndani yake kuna utumiaji mzuri wa nishati, na uunganishaji wa ari, na ushirikiano kwa ajili ya kuyafikia malengo ya pamoja ambayo yanabeba heri kwa ajili ya watu wote. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ}.

Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mkali wa kuadhibu.

Na mzingatiaji wa jinsi Qurani inavyo zungumza, ataona kuwa aya zake ambazo zinahimiza uenezaji wa Moyo wa utendaji na kufanya kazi kwa pamoja, pamoja na kuwa na ari kama kitu kimoja, ni nyingi na za kila aina, na kwa ajili hiyo kuna kauli ya Mwenyezi Mungu katika jambo hili kwa waja wake, anasema:

 {يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}

Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni nyinyi na wake wa kabla yenu, ili mpate kukoka.

Na kuhusu Swala ambayo ni alama kuu miongoni mwa alama za Dini ya Kiislamu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ}

Na simamisheni Swala.

Na kwa matamshi ya ujumla, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}

Enyi mlioamini, rukuuni na msujudu na muabuduni Mola wenu Mlezi na tendeni mema ili mfanikiwe.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimsemesha Mtume wake S.A.W:

 {وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَنْ ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا}

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la dunia. Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka.

Na amasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا}

Na shikamaneno kwa kamba ya Mnweyezi Mungu wala msifarikiane.

Na Mweenyezi Mungu Mtukufu akatuonya na migawanyiko na makundi kwa kusema:

 {وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ وَاصْبِرُوا إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِين}

Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri. 

Na jambo lisilokuwa na shaka ndani yake ni kwamba, kufanya kazi na kutekeleza majukumu kwa moyo huu wa ushirikiano huongeza mapenzi  na upendo baina ya watu na mjongeleano pia baina ya watu wa jamii moja na hupelekea wasifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kupatikana, aliposema:  

{وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً}

Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja.

Na kauli ya Mtume S.A.W inauthibitisha ukweli huo anaposema: Mfano wa Waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao, na kuhisiana, ni mfano wa mwili mmoja pindi kiungo kinapougulia maumivu basi mwili mzima huwa unaugulia maumivu hayo kwa kukesha na kwa kuumwa.

Na Shekhe mmoja alipotaka kuwafundisha watoto wake umuhimu wa ummoja na kwamba umoja ni sababu ya nguvu, na hatari ya mgawanyiko na kwamba mgawanyiko huo ni sababu ya kutawanyika na kupotea, alikuja akiwa na mzigo wa kuni na akasema: ni nani anayeweza kuuvunja mzigo huu wa kuni kwa kipigo kimoja? Au hata kwa mapigo mawili? Kila mmoja wao akajaribu bila mafanikio, kisha yule mzee akaufungua ule mzigo wa kuni na kuwagawiya watoto wake, kila mmoja akapewa kuni moja na akaweza kuivunja kwa kipigo kimoja tu, kisha yule mzee akasema:

mishale inapokusanyika pamoja inakataa kuvunjika,   na inapotawanyika huvunjika mmoja mmoja.

Na Qurani imetutolea mifano mingi sana mizuri ambayo inavutia kazi ya pamoja na kuipupia, na imeweka wazi jinsi athari zake zilivyo katika kuyafikia malengo makuu. Tunamwona Mtume wetu Ibrahim A.S, alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu ajenge Kaaba Tukufu; alienda kwa Mwanae Ismaili A.S, na akamwambia:

Hakika Mwenyezi Mungu ameniamrisha jambo. Akasema: fanya kama ulivyoamrishwa na Mola wako. Akasema: je utanisaidia? Akasema: nitakusaidia. Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameniamrisha mimi niijenge nyumba yake Tukufu ya Kaaba hapa nilipo. Na kuanzia hapo, akaunyanyua msingi wa Nyumba hiyo Tukufu, na Ismaili A.S akawa analeta mawei, na Ibrahim A.S anajenga, na wawili hawa wakafanikiwa kuijenga nyumba ya kwanza ya Mwenyezi Mungu Mtukufu waliojengewa watu. Na Qurani tukufu imeuhifadhi milele ukumbusho huu mkubwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu aliposema:

  { وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنْتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ}

Na akumbukeni Ibrahim na Ismaili walipoinyanyua misingi ya ile nyumba wakaomba: Ewe Mola wetu Mlezi, tukubalie hakika Wewe ndiye Msikivu Mjuzi.

Na katika Surat Alkahf, Mwenyezi Mungu Mtukufu anatusimulia mfano mzuri wa ushirikiano na umoja kamili pamoja na kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano wa pamoja, katika Kisa cha Dhulqarnaini, pindi alipowasili mfalme huyu mwadilifu kwa watu wasiomjua wala yeye hawajui, na wakamwomba msaada, nay eye akawasaidia kile walichokiomba, lakini akawataka washirikiane naye, na akawashirikisha katika Kazi na kuitumia nguvu yao, wakawa wote ni mkono mmoja mpaka wakafanikiwa kulijenga jingo kubwa ambalo lilikuwa sababu ya kuwalinda wao kutokana na mateso ya Yajuuja na Maajuuja. Na katika jambo hili, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{حَتَّى إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِنْ دُونِهِمَا قَوْمًا لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا * قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَى أَنْ تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا * قالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا * آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ حَتَّى إِذَا سَاوَى بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انْفُخُوا حَتَّى إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا * فَمَا اسْطَاعُوا أَنْ يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا}

Hata alipo fika baina ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao takriban hawakuwa wanafahamu lolote. Wakasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Hakika Yaajuja na Maajuja wanafanya uharibifu katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu na wao ngome? Akasema: Yale Mola wangu aliyoniwezesha ni bora zaidi. Lakini nyinyi nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitakujengeeni kizuizi baina yenu na wao. Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipo ijaza nafasi iliyo kati ya milima miwili, akasema: Vukuteni. Mpaka alipokifanya (chuma) kikawa kama moto akasema: Nileteeni shaba iliyo yayuka niimwagie. Basi hawakuweza kuukwela wala hawakuweza kuutoboa.

Na hivi ndivyo Mtume Musa A.S, aliyezungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu, anamuomba Mwenyezi Mungu amtie nguvu kwa kusaidiwa na ndugu yake Haruna A.S, ili awe Msaidizi wake anaemtegemea katika Jukumu lake alilopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na katika hili, anasema Msema kweli, Mwenyezi Mungu aliyetukuka, kupitia ulimi wa Bwana wetu Musa A.S:

{قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي * وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي * وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِنْ لِسَانِي * يَفْقَهُوا قَوْلِي * وَاجْعَلْ لِي وَزِيرًا مِنْ أَهْلِي * هَارُونَ أَخِي * اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي * وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي * كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا * وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا*إِنَّكَ كُنْتَ بِنَا بَصِيرًا}

Musa akasema: Ewe Mola wangu Mlezi, nikunjulie kifua change, na unifanyie nyepesi kazi yangu, na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, wapate kufahamu maneno yangu. Na nipe waziri katika watu wangu, Haruna ndugu yangu. Kwake yeye niongeze nguvu zangu. Na umshirikishe katika kazi yangu. Ili tukutakase sana. Na tukukumbuke sana. Hakika wewe unatuona.

Vile vile mzingativu wa Sira ya Mtume S.A.W iliybarikiwa, ataona ndani yake kuna kurasa zenye kuangazia ushirikiano na ushirika na kazi ya pamoja katika maisha ya Mtume S,A,W pamoja na Maswahaba wake R.A. anasema Bwana wetu Uthmani bin Afaan R.A: Ninaapa, hakika sisi tulisahibiana na Mtume S.A.W safarini na nyumbani, na alikuwa akitusaidia kwa kazi ndogo ndogo na kubwa kubwa.

Vile vile Mtume S.A.W alikuwa akishirikiana nao katika kazi na ujenzi yeye mwenyewe, na anawahimiza kuwa pamoja na kutotengana. Na katika siku ya Vita vya Khandaki, anasema Buraau bin Aazib R.A: nimemuona Mtume  wa Mwenyezi Mungu S.A.W, siku ya Ahzaab akibeba mchanga, na mchanga uliufunika weupe wa tumbo lake, huku akisema: Ewe Mola wetu kama sio wewe tusingeongoka, wala tusingetusingetoa sadaka wala tusingeswali, tunakuomba utushushie utulivu juu yetu, na uikitishe miguu yetu pindi tutakutana na makafiri vitani, hakika watu wa Makkah na makundi mbali mbali yametugeukia, na wanapotaka fitna sisi tunaikataa.

 Na Bwana wetu Salmaan Farisiy R.A, alipotaka kulima na kupanda mitende mia tatu, ili ajikomboa kwayo kutoka katika utumwa, Mtume S.A.W akawaambia Maswahaba wake: Msaidieni ndugu yenu. Anasema Salmaan R.A: Wakanisaidia kwa mitende: Mtu mmoja akaleta miche thelathini ya mitende, na mwingine akaleta miche ishirini. Na mwingine analeta miche kumi na tano, na mwingine analeta kiasi alichonacho, mpaka nikawa nimekusanya miche mia tatu. Na Mtume S.A.W akaniamrisha niichimbie mashimo akasema: na utakapomaliza unijie, mimi niwe mwenye kuipanda kwa mkono wangu. Akasema: nikaichimbia vishimo vya kupandia, na wenzangu wakanisaidia, mpaka nikamaliza kazi hiyo na nikamwambia Mtume S.A.W, naye akatoka S.A.W, akiwa pamoja na mimi, mpaka kwenye shamba, tukawa tunamsogezea mche mmoja mmoja na anaupandikiza S.A.W kwa mkono wake.

Mtume S.A.W amewasifu mno watu wa ukoo wa Ash-ari, kwa sifa za juu mno, pale walipokuwa na moyo wa kufanya kazi pamoja, moyo huu iliwatangulia kila wakati katika miamala yao wakiwa katika nyakati ngumu kabisa. Anasema Mtume S.A.W: Hakika Watu wa Ash-ariy wanapofiwa na walezi wa familia zao vitani, au wanapopungukiwa na chakula cha kuzilisha familia zao Madina, hukusanya walicho kuwa nacho katika kitambaa kimoja, kisha hugawana baina yao katika chombo kimoja kwa usawa, watu hawa ni wangu mimi na mimi ni wa.

     Ninaisema kauli yangu hii na nimamwomba msamaha Mwenyezi Mungu mimi pamoja na kukuombeeni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mlezi wa viumbe vyote. Peke yake na wala hana mshirika wake. Na ninashudua kwamba hakuna mungu mwingine apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ninashuhudia kuwa hakika Bwana wetu Muhammad ni Mtume wetu, na ni Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake. Ewe Mola wangu mswalie, mpe salamu na umbariki Mtume wetu, na Ali zake, na Maswahaba wake, na atakayewafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.

                                  Ndugu zangu Waislamu:

Hakika ya kazi ya pamoja tunayoilingania ni kazi ambayo hujenga na wala haibomoi, na huwakusanya watu na wala haiwagawi. Nayo ni ile inayofanywa kwa misingi ya kisheria ya kuleana baina ya watu wa jamii moja kwa namna ambayo haonekani ndani yao mwenye njaa au anaehitajia kitu, au kwa misingi ya  kimalezi na kielimu kama ushirikiano wa wanachuoni katika tafiti zao za kisayansi, na wanafunzi katika kazi zao za kielimu wanazopewa shuleni, au kwa misingi ya kitaifa kwa ajili ya kazi ya kuliendeleza Taifa na kulikuza kimaendeleo katika Nyanja zote muhimu.

Na wala sio kazi inayojengeka kwa miito angamizi ambayo watu hukusanyika kwa ajili ya kuua au kuharibu mali au kumwaga damu za watu, na kuharibu mataifa, na kufanya majaribio ya kutaka kuyadhooofisha au kuyaangusha mataifa hayo. Miito hiyo inajengeka kwa uongo na uzushi, na kuvuruga ukweli wa mambo, bila kujali Dini, Taifa au hata Dhamira ya mtu.

Hakika ya kazi ya pamoja inayolinganiwa ni kazi ya ujenzi kwa ajili ya masilahi ya Dini, Taifa na Utu, navyo vyote hivyo vinaambatana na hakuna hata kimoja kinachojitenga na kingine katika hivyo. Kuna haja ya kuweka misingi imara ya watu kuwa na moyo huu wa kufanya kazi pamoja katika nafsi za watoto wetu, na kubadilisha ukawa ni mfumo wanaouishi katika maisha yao. Upendo ukatawala na mjongeleano ukaongoza baina ya watoto wa jamii moja. Na sisi sote tukapanda zaidi na tukawa katika nafasi inayolingana na nafasi yetu katika kila Nyanja. Sisi tunasisitiza kuwa wanachi, pindi watoto wao wanapoongozwa na moyo wa kufanya kazi kwa pamoja basi njia hii itazifanikisha kazi ambazo zitaonekana kwa wengine kuwa haziwezekani kufikiwa. Na kuona na kujaribu na uhalisia wake, sasa na tangu zamani, ni dalili tosha ya haya yamsemwayo.

Tunakuomba ewe Mola wetu utupe usalama katika nchi zetu, na uwawafikishe wanachuoni wetu na viongozi wetu katika mambo yetu, na uilinde nchi yetu kutokana na vitimbi vya wenye navyo na kila aina ya uovu wa waovu. Amin.

Mweleweko wa Ahadi ya Usalama katika zama zetu.

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa Viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْؤُولاً}

Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi ni yenyeuulizwa.

Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad, ni Mja wake na Mjumbe wake, anaesema katika Hadithi yake Tukufu: Hakika waja wa Mwenyezi Mungu mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale wanaotekeleza ahadi zao na wanaofanya mazuri. Ewe Mola wetu, Mswalie na umpe rehma na amani na umbariki Mtume wetu S.A.W, na Ali zaki na Maswahaba wake, na kila mwenye kuwafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu;

Hakika Uislamu ni Dini Usalama, amani, utendaji wa mazuri na wema; na hakuna shaka yoyote kwamba utekelezaji wa Ahadi una thamani kubwa ya kimaadili na kibinadamu inayounga mkono kujiamini na kuleta usalama na amani baina ya mataifa yenyewe kwa yenyewe, na kukuza mahusiano mazuri na upendo pamoja na kujenga na kusonga mbele kinaendeleo kwa wananchi wa taifa moja, na kwa hivyo, utekelezaji wa ahadi ni sehemu ya imani na ni dalili miongoni mwa dalili za ukweli na Wema, na ni Adabu ya kidini iliyo bora, na tabia njema pamoja na mienendo ya kiislamu iliyonyooka.

Hakika Uislamu umewaamrisha wafuasi wake umuhimu wa kuwa na tabia za kutekeleza ahadi zao na mikataba pamoja na makubaliano, na ukasisitizia hayo kwa nguvu zote pale aliposema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَأَوْفُواْ بِالْعَهْدِ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْؤُولاً}

Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi ni yenye kuulizwa.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَأَوْفُواْ بِعَهْدِ اللّهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلاَ تَنقُضُواْ الأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلاً إِنَّ اللّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ}

Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo.

Kwa maana ya kuwajibika na utekelezaji wa ahadi zote mlizojiwajibisha nyinyi wenyewe, iwe baina yenu au baina yenu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, au baina yenu na watu wengine, na wala msitokwe na imani baada ya kuwa mmekwishajihakikishia ndani ya nyoyo zenu. Na mkamfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa ndiye mlezi wenu na mdhamini wenu pale mlipoahidi. Na yoyote atakayepitisha makubaliano basi anawajibika kuyaheshimu, na atakayetoa ahadi anawajibika kuitekeleza. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba watekelezaji wa Ahadi zao na mikataba yao wao ndio watu wa upendo na wao ndio watu wa ukweli na uchamungu kwa Muumba wao. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{بَلَى مَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ وَاتَّقَى فَإِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ}

Sivyo hivyo, bali anaye timiza ahadi yake na akamchamngu basi Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُواْ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاء والضَّرَّاء وَحِينَ الْبَأْسِ أُولَـئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَأُولَـئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ}

Na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha kwamba watu hao ndio wenye malipo makubwa, na ni warithi wa pepo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَنْ أَوْفَى بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا}

Na anaye tekeleza aliyo muahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.

Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha malipo haya makubwa katika sehemu nyingine ya Qurani Tukufu aliposema:

 {وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ * وَالَّذِينَ هُمْ بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ * وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ * أُولَئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُكْرَمُونَ}

Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, Na ambao wanazihifadhi Sala zao. Hao ndio watakao heshimiwa Peponi.

Na Mtume S.A.W amenyanyua thamani ya kutekeleza ahadi na akaonya kwa mwenye kuivunja, au kutoitekeleza ipasavyo; ambapo katika kufanya uhaini wa kutoitekeleza ahadi kuna ufisadi katika jamii mbali mbali. Na kwa mujibu wa Imani baina ya watu, na upotezaji wa amana za watu, Mtume S.A.W anasema:

Alama za Mtu Mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huenda kinyume na ahadi yake, na anapoamini hufanya hiana. Na anasema Mtume S.A.W: Waislamu hufuata Masharti yao waliojiwekea, isipokuwa sharti linaloharamisha kilichohalalishwa au kuhalalisha kilichoharamishwa. Na Mtume S.A.W ameonya kuhusu adhabu ya Mtu aliyevunja ahadi yake akasema: Mwenyezi Mungu atakapowakusanya Wa Mwanzo na wa Mwisho siku ya Kiama, patanyanyuliwa alama kwa kila Mvunja ahadi na patasemwa: Alama hii ni alama ya uvunjaji wa Ahadi wa Fulani bin Fulani. Anasema Ibnu Kathiir R.A: Na hekima iliyopo katika jambo hili ni kwamba kwa kuwa kwenda kinyume na ahadi hutokea kwa kificho, watu hawawezi kuona kinachoendelea, itakapofika siku ya Kiama, jambo hili litawekwa wazi kwa kuwekewa wazi muhusika kile alichokifanya, na hivyo ndivyo yatakapowadhihirikia watu yale yaliyokuwa yakifanywa kwa siri na wahusika, miongoni mwa vitimbi na uhaini, na Mwenyezi Mungu atawafedhehesha wahusika mbele ya viumbe vyote. Na kwamba katika jumla ya ahadi zilizoamrishwa na Sheria ya Uislamu iliyo tukufu zitekelezwe, na kuthibitisha utekelezaji wake, na kutozivunja, ni ahadi ya Usalama; nao ni kwa mujibu wa mweleweko wa zama hizi: Ni kile kinachotolewa na nchi, kama kibali au visa vya kuingilia nchi nyingine, au idhini ya kuingia nchini mwake kwa wananchi wa nchi nyingine, iwe ni kwa sababu za kitalii au matembezi  au kuishi, kwa mujibu wa taratibu na mikataba na makubaliano ya kimataifa ya kuamiliana na wanadiplomasia, na wanaokuwa katika hukumu ya wanadiplomasia, au kwa mujibu wa mikataba na makubaliano ya nchi mbili kwa njia yoyote miongoni mwa njia zilizopitishwa na zinazokubalika kisheria, na kutambuliwa na nchi yenye kupokea wageni kwa mujibu wa sheria zilizopo na baada ya mtu kupata kibali tu cha kuishi, au kibali cha kuingia nchi hiyo au idhini ya kuingia, basi mtu huyo atakuwa tayari ana haki na heshima katika nchi hiyo na anakuwa katika mkataba ambao umetolewa na nchi kwa ajili ya kila mwananchi na yoyote anayeishi ndani ya nchi hiyo kuwajibika na kuufuata ipasavyo, na haijuzu kuuvunja au kwenda nao kinyume, au hata kuuvuruga, haifai kisheria wala kikanuni. Na yoyote atakayeona katika watu jambo linalokiuka sheria na kuugusa usalama wa nchi yake au kinyume na mfumo wa serikali yake, hana budi isipokuwa kutoa taarifa kwa wahusika ili waweze kulishughulikia na kuchukua hatua zinazofaa, mpaka vyombo vya dola viweze kumchukulia hatua mtu huyo kwa yale aliyoyafanya, kwa mujibu wa sheria na taratibu zake, kwani hakuna mtu yoyote anayeweza kumchukulia hatua mtu huyo kwa yale aliyoyafanya au yaliyomkuta kwa kukiukwa haki yake na kama hatua haitachukuliwa basi jambo hili linaweza kupelekea machafuko na kutodhibitika tena.

Na miongoni mwa mambo yasiyo na shaka ndani yake ni kwamba, utekelezaji wa ahadi hii ni katika mambo ya wajibu na yenye kutekelezwa kisheria, kikanuni, kitaifa, na hata kibinadamu. Kama Dini yetu tukufu imenyanyua cheo cha Ahadi ya Usalama, kama ni jukumu la waislamu wote kwa pamoja, maana yake ni kwamba ahadi anayoiahidi mwislamu yeye mwenyewe inakuwa wajibu kwa wote waliopamoja naye, inakuwaje ikiwa ahadi hiyo ni mkataba unadhibitiwa na kupangiliwa na sheria pamoja na kanuni, kwa kushirikiana, kila mmoja kumtia nguvu mwingine na kumuunga mkono na kuwajibisha? Basi hapana shaka kwamba hiyo hupelekea katika utekelezaji wa  majukumu na mikataba ya ahadi, na wala sio kuivunja au kuipoteza, na hata kuigusa tu.

Hakika uislamu ni Dini inayolinda Ahadi za aina mbali mbali na mikataba, Dini isiyotambua udanganyifu, wala haitambui hadaa, au hiyana, na haikuthibiti wakati wa Mtume S.A.W,  – tangu mwanzo wa Ulinganiaji wake – wala kutoka kwa Swahaba wake yoyote kati ya maswahaba wake R,A, kwamba waliwahi kumnyima Usalama mtu yoyote, au waliwahi kuvunja ahadi walioitoa kwa mtu yoyote, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimsemesha Mtume wake S.A.W:

{وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَانبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَى سَوَاء إِنَّ اللّهَ لاَ يُحِبُّ الخَائِنِينَ}

Na ukichelea khiana kwa watu Fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hawapendi makhaini.

Na siku Bwana wetu Muawiya alipokuwa na Mkataba wa Ahadi baina yake na Taifa la Warumi, na Muawiya akataka kutoka karibu na mipaka ya Warumi, pindi mkataba utakapokwisha atawashambulia, Mtu mmoja miongoni mwa Maswahaba wa Mtume S.A.W akamuwahi huku akisema: Mwenyezi Mungu Mkubwa, Mwenyezi Mungu Mkubwa, Tunapaswa kutekeleza ahadi na wala sio kuivunja. Maswahaba wote wakamwangalia, alikuwa ni Amru bin Absah, R,A, Muawiya R.A, akamtumia mtu, akamuuliza, akasema: Nimemsikia Mtume S.A.W akisema: Mtu yoyote anaewekeana ahadi na watu, basi asiikaze ahadi yake au kuilegeza, mpaka atakapoitimiza jinsi ilivyopangwa, au akawatupia mkataba wao ni sawa na kuuvunja, Muawiya akarejea, bali utukufu wa Uislamu ukaonekana na kudhihiri wazi wazi katika sura zake za hali ya juu, katika amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake S.A.W. kusaidia mtu anayeomba msaada wa kuokolewa hata kama mtu huyo ni mshirikina, bali hata kama mtu huyo atakuwa ni adui wa Waislamu, ambapo

anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{و َإِنْ أَحَدٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ اللهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا يَعْلَمُونَ}

Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu.

Mtume S.A.W amejenga misingi imara ya Maadili haya yanayoleta Usalama na amani kwa binadamu, kama asemavyo Mtume wetu S.A.W: Hana Imani Mtu asiyekuwa Mwaminifu, na wala hana Dini Mtu asiyekuwa Ahadi (kwa maana asiyetekeleza ahadi).

Na anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakayemuua Mtu aliyewekeana naye Ahadi, basi hata inusa harufu ya Pepo, na kwamba Harufu ya pepo inapatikana umbali wa mwendo wa miaka arubaini.

Na anasema Mtume S.A.W: Mwislamu ni Yule ambaye Watu wote wamesalimika na Ulimi wake na Mkono wake, na Muumini ni Yule ambaye maisha yao pamoja na mali zao vimesalimika naye. Na huyu hapa Mtume S.A.W anatujengea sisi kiutendaji mifano mizuri ya utekelezaji wa ahadi mpaka ile ahadi yake na maadui zake; Kutoka katika Siku ya Badri, anasema Hudhaifa bin Yamaan R.A: Hakikunizuia mimi kuishuhudia Badri isipokuwa mimi nilitoka nikiwa mimi na Baba yangu, tukawachukua makafiri wa Kikureshi, wakasema:  Hakika nyinyi mnamtaka Muhammad, tukasema: Hatumtaki yeye. Hatutaki isipokuwa Madina, Wakachukua kutoka kwetu ahadi ya Mwenyezi Mungu na miadi yake, kwamba: tutaelekea Madina, na wala hatutapigana tukiwa pamoja naye, tukaja mpaka kwa Mtume S.A.W, na tukamweleza habari hii, akasema S.A.W: Nendeni tunawatekelezea ahadi yao, na tunamwomba msaada Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yao.

Na kwa kauli hiyo ya Mtume S.A.W, hakika sisi sote, tunawajibika kuzilinda ahadi tunazozitoa na kuwekeana na watu, pamoja na mikataba ambayo nchi inatuwajibisha tuitekeleze kwa kila mtu ndani ya nchi yetu na tuwe ni wenye kushirikiana katika kuyalinda maisha yake, heshima yake, na maisha yake binafsi, ambapo tuna wajibu pia wa kumkaribisha vizuri, na kumkirimu; ili aone katika sisi yale tuyapendayo ayaone katika macho yake na akili yake kuhusu utukufu wa Dini yetu, na undani wa Ustaarabu wetu, na utukufu wa utu wetu; kwa namna inayochangia katika kujenga picha ya kiakili tuitakayo sisi, na kwa Taifa letu, na Jamii yetu, nah ii ndio hali ya kila Umma na Mataifa yaliyo juu kiustaaranu.

Ninaisema kauli yangu hii, na nimamwomba Mwenyezi Mungu pamoja na kukuombeeni nyinyi msamaha.

*   *   *

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mola wa viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad nMja wake na ni Mjumbe wake. Ewe Mola wetu tunakuomba umswalie Mtume na umpe rehma na amani na umbariki, yeye na Aali zake na Maswahaba wake wote, na kila atakayemfuata kwa wema mpaka siku ya Mwisho, siku ya Malipo.

 Ndugu zangu Waislamu.

Hakika Uislamu ni Dini ya Uadilifu, Usamehevu na kuishi kwa amani. Na Mwislamu daima anatakiwa kuishi katika amani na usalama, amani katika kila sehemu anayokuwapo, ndani ya nchi yake au nje ya nchi yake; na anapohama Mwislamu huyu na kwenda katika nchi nyingine, iwe nchi hiyo ni ya kiislamu au sio ya kiislamu, hakika ruhusa ya kuingina inayotolewa na nchi hiyo inakuwa ni kama mkataba wa usalama, ambapo atakuwa na amani na usalama huko aendako, na ruhusa hiyo ni kama mkataba wa Usalama wake kwa wenye nchi hiyo; wanampa usalama kamili, na wanasalimika naye kwa mali na nafsi zao, na unamuwajibisha mkataba huo kufuata sheria zote za nchi hiyo na kuwajibika kikamilifu na anatakiwa atekeleze wajibu wake wa usalama na ukweli. Anazuiwa kuchukua kitu chochote katika mali za watu kinyume na sheria, au kuishambulia heshima ya mtu yoyote, au kuvunja ahadi anayotakiwa kuitekeleza kwa njia yoyote miongoni mwa njia za kuvunja ahadi, mpaka awe balozi mzuri wan chi yake, Dini yake na Ustaarabu wake. Pindi anapoingia tu katika nchi hiyo, anakuwa tayari anawajibika na anakuwa ameshaweka ahadi na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atatekeleza, mpaka asije akajikuta katika hali aliyoisema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالَّذِينَ يَنْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ أُولَئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ}

Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.

Anasema Imamu Shafi Mwenyezi Mungu amrehemu, katika kitabu chake cha Ummu: Mwislamu anapoingia katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu kwa kuwa na amani nao, basi hairuhusiwi kwake kuchukua chochote katika mali zao – ziwe nyingi au kidogo – hata kama wao walikuwa katika hali ya vita na waislamu; kwani yeye akiwa nao anakuwa katika usalama wao, na wao wanapokuwa naye pia wanakuwa nae katika usalama kama ilivyo yeye na wao. Na kwa kuwa haijuzu  kwake katika usalama wao isipokuwa vinavyokuwa halali katika mali za waislamu.

Nimetosheka na kuyataja maneno ya Imamu Shafi na kuyanasibisha na kitabu chake cha Ummu; kwa kuchelea kuingia katika upembuzi wa kifiqhi unaoweza kuwa na baadhi ya mambo yasiyokubaliwa na baadhi ya watu. Na ninaliacha jambo hili kwenu.

Anasema Mshairi:

Utekelezaji wa Ahadi ni katika Sifa za watu wema

Na uvunjaji wa ahadi ni katika sifa za waovu

Na kwangu mimi hakizingatiwi kitu kuwa katika mazuri

Isipokuwa kulinda upendo na kuzuia uchonganishi

Ewe Mola wetu tuongoze katika Tabia njema zaidi, hakuna wakutuongoza tukelekea kwenye bora zaidi isipokuwa wewe. Na tunakuomba utuepushe na ubaya wake, na hakuna wa kutuepusha nao isipokuwa wewe.