Wajibu wa Mwalimu na Mwanafunzi

Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na Mshirika wake, Mjzu na Mwenye Hekima, na ninashuhudia kwamba Bwana wetu Muhammad S.A.W, ni Mja wake na ni Mjumbe wake. Ewe Mola wetu tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu, yeye na Jamaa zake, na Maswahaba wake, wenye kung’aa mapaji ya nyuso zao na waliobarikiwa, na kila mwenye kuwafuata mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu:

Sisi tunakaribia kuuanza mwaka mpya wa masomo, na tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwaka huu uwe ni wa bidii na jitihada, na kufaulu kwa watoto wetu wote. Jambo lisilokuwa na Shaka ni kwamba Uislamu umeipa Elimu kipaumbele cha hali ya juu, na ukaipa nafasi maalumu kwani elimu ndio uhai wan yoyo za watu, na ni taa ya macho; kwani Elimu kwa mwenye nayo, humfikisha katika nafasi za walio juu kwa daraja, hapa Duniani na kesho Akhera. Na kwa Elimu, mja ana uwezo wa kuunganisha undugu na kujua Halali na Haramu, na Mwenyezi Mungu huyanyanyua mataifa kwa Elimu na kuyafanya yakawa na viongozi na wanachuoni walio bora, ambao tunatakiwa kuzifuata nyayo zao na kuiga vitendo vyao. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

‏‏}قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لاَ يَعْلَمُونَ{

Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua?

     Uislamu ulionesha jinsi unavyoijali Elimu na kuisisitizia kwa watu, tangu mwanzoni mwa kuteremka kwa Qurani Tukufu: anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ * الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ * عَلَّمَ الإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ}

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. Kisha inakuja ishara ya kalamu baada ya hapo, kalamu ambayo ni njia ya kuandikia kuihamishia Elimu; na katika aya hizi kuna mzinduo kwa watu wote juu ya uwazi wa fadhila za Elimu na kuwatia utashi watu katika kuitafuta Elimu na kuihimiza.

Elimu ina nafasi ya juu, na wenye elimu wana hadhi zao za juu mno, na kama si elimu na wanachuoni, basi watu wangepotea. Kwa hivyo, Elimu ni nuru ambayo mtu aliyenayo huuona uhalisia na ukweli wa mambo mbali mbali, na wanachuoni kwa watu ni nyota mbinguni zinazowaongoza. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {أَفَمَن يَعْلَمُ أَنَّمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَى إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الأَلْبَابِ}

Je! Anaye jua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Wenye akili ndio wanao zingatia.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amewagawa watu katika aya hii kwa migawanyiko miwili: Mjuzi na Kipofu; na akakifanya kinyume cha elimu kuwa ni Upofu. Kwahiyo Macho hapa ni Elimu na Maarifa, na wala sio Macho ya kuonea vitu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {فَإِنَّهَا لاَ تَعْمَى الأَبْصَارُ وَلَكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ}

Kwani hakika si macho yanayo pofuka, lakini zinazo pofuka ni nyoyo ziliomo vifuani.

Na kwa hivyo, Qurani Tukufu imeinyanyua Elimu na kuiweka juu, na kuipa jina la Uthibitisho. anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ كَبُرَ مَقْتًا عِنْدَ اللَّهِ وَعِنْدَ الَّذِينَ آمَنُوا}

Hakika hao wanao bishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya uthibitisho wowote uliyo wajia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenezi Mungu na mbele ya walioamini.

Na Mtume S.A.W, amebainisha nafasi ya Elimu na fadhila zake, akasema: Mtu yoyote atakayesafiri kwa ajili ya kutafuta Elimu, Mwenyezi Mungu atampeleka katika njia ya Pepo. Na kwamba Malaika wanaweza Mbawa zao kwa kumridhia Mtafuta Elimu, na kwamba vilivyomo Mbinguni na Ardhini, Nyangumi katika vina vya Baharini, vinamwombea Msamaha mwenye Elimu kwa Mwenyezi Mungu. Na tofauti ya Fadhila baina ya Mwenye Elimu na Mfanya ibada ni kama ni kama fadhila baina ya Mbala mwezi Usiku wa kuangaza kwake, na sayari zingine, na wanachuoni ni warithi wa Mitume, na Mitume hawakurithisha fedha bali walirithisha Elimu s, na yoyote atakayeichukua elimu basi atakuwa amechukua kitu bora cha kumtosha. Kutoka kwa Abu Dhari R.A: amesema: Anasema Mtume S.A.W: Ewe Abu Dhari, ukienda kufundisha aya moja ya Qurani ni boza zaidi kwako kuliko kuswali rakaa elfu moja.

Na anasema Imamu Ali R.A: Elimu ni bora kuliko Mali; Elimu inakulinda na wewe unailinda Mali, Elimu inaongoza na Mali inaongozwa, na Mali hupungua kwa kuitoa wakati ambapo Elimu huongezeka kwa kuitoa.

Na Elimu ina Maadili Makubwa mno na adamu nzuri ambazo Mwanafunzi na Mwalimu wanapaswa kuwa nazo na wote wanalingana katika hayo. Miongoni mwa muhimu katika hizo ni: Kuwa na nia njema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni wajibu kwa Mwalimu na Mwanafunzi waitafute Elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu tu, na wajiepushe n aria na kutaka umaarufu. Kwani hakika ya Elimu ina matamanio yaliyojificha na yanapofanikiwa kuingia moyoni, hudhibitiwa na kupenda kujionesha, kutaka kujulikana, na kuwa na utashi wa kuwa kimbele mbele, na huwenda hali hii ikaathiri mwenendo mzima wa mtu huyu mpaka anajikweza mbele za watu. Na Mtume S.A.W ametutahadharisha na yote hayo, akasema: Mtu yoyote atakayeitafuta Elimu kwa lengo la kujionesha kwa wajinga, au kujigamba kwa wanachuoni, au ili watu wamtazame yeye, basi ataingia Motoni.

Na miongoni mwayo ni: Unyenyekevu. Na Maliki alimwandikia Radhiid akasema: Unapoijua elimu yoyote, basi uonekane una elimu hiyo, una utulivu wake, una alama zake, una unyenyekevu wake na upole wake; na kwa ajili hiyo, anasema Omar R.A: Jifunzeni Elimu, na mjifunze utulivu na unyenyekevu kwa elimu hiyo. Kwani Elimu na Kiburi havitulizani pamoja, na wala Elimu haipatikani kwa Maasi, bali hupatikana kwa kutafutwa kwake na uchamungu huongezeka, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 }وَاتَّقُوا اللَّهَ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّهُ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ{

Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakufundisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Na wanasema wenye busara: Mwenye kuyafanyia kazi aliyojifunza, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu: humfundisha Elimu ambayo alikuwa haijui. Kwa hiyo, kuitumia Elimu ni sharti la kuifikia Elimu ya kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Mja Mwema katika Surat Alkahf:

 }فَوَجَدَا عَبْدًا مِنْ عِبَادِنَا آَتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِنْ عِنْدِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِنْ لَدُنَّا عِلْمًا{ ، وَيَقُولُ سُبْحَانَهُ:

Basi wakamkuta mja katika waja wangu tuliye mpa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyo toka kwetu.

Anasema Mweyezi Mungu Mtukufu kuhusu Mtume Suleiman A.S:

 }فَفَهَّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ وَكُلاًّ آتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا{

Na tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na elimu.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Bwana wetu Yahaya A.S:

 }يَا يَحْيَى خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ وَآَتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً وَكَانَ تَقِيًّا{Ewe Yahaya! Kishike kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hekima angali mtoto. Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mchamungu.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kauli ya Malaika:

 }سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَا{.

Umetakasika Wewe, Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyotufunza wewe.

(إِنَّ الْهَدْيَ الصَّالِحَ ، وَالسَّمْتَ الصَّالِحَ ، وَالاقْتِصَادَ ، جُزْءٌ مِنْ خَمْسَةٍ وَعِشْرِينَ جُزْءًا مِنَ النُّبُوَّةِ).

Na miongoni mwazo: kujipamba kwa unyenyekevu, ambapo Elimu ina utulivu wake, heba yake, na utukufu wake, na miongoni mwa alama za shime hiyo, ni kuujali mwonekano mzuri, usafi, manukato na kujiepusha na vikao vya mambo ya kipuuzi. Anasema Mtume S.A.W: (……………………………………na uchumi ni sehemu moja ya sehemu ishirini na tano za Utume)

Na mwanachuoni kwa muulizaji ni kama daktari kwa mgonjwa analazimika kuwa mpole kwake na amshike mkono na kumuongoza njia sahihi. Kutoka kwa Muawiya bin Hakiim R.A amesema: Nilipokuwa ninaswali na Mtume S.A.W, mtu mmoja miongoni mwetu akapiga chafya: na mimi nikasema: Mwenyezi Mungu akurehemu, watu wote wakanitupia macho yao, nikasema: Mama yangu wee! Mna nini nyinyi mbona mnaniangalia hivyo? Wakawa wanapiga mikono yao kwenye mapaja yao na nilipowaona wananinyamazisha nikanyamaza. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu S.A.W, alipomaliza kuswali, hakika yeye ni mfano wa mzazi wangu, sijawahi kumuona mwalimu yoyote kabla yake au naada yake mbora wa kufundisha kama yeye S.A.W, Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajawahi kunitenza nguvu wala kunipiga au hata kunitukana.

Vile vile kuna mambo kadhaa ambayo Mwanafunzi anapaswa ajipambe nayo, na muhimu katika hayo ni:

* Kupupia katika kuitafuta Elimu, na kuendelea kuitafuta bila ya kuhisi uvivu au uzembe. Mwanafunzi hatakiwi kuupoteza muda wake kwa mambo yasiyokuwa na faida. Inasemwa kwamba: huwezi kuipata Elimu kamili kwa kuitumikia kidogo. Na Imamu Shafi Mo;a amrehemu, alipoulizwa: utashi wako wa Elimu ukoje? Akasema: Ninasikia katika kila neon kwa yale ambayo sijawahi kuyasikia, na viungo vyangu vinatamani viwe na masikio ili vineemeke na Elimu hiyo kama yanavyoneemeka masikio yangu. Akaambiwa: unaipupia vipi Elimu? Akasema: kama pupa ya makundi yaliyozuiliwa kukifikia kilele cha ladha ya mali zao. Akaambiwa: Na vipi unaitafuta Elimu? Akasema: kama mama mzazi anavyomtafuta mtoto wake pekee aliyepotea, na hana mtoto mwingine.

* Kumheshimu Mwalimu. Na mwanafunzi asithubutu kujikweza kwa maneno, au kitendo chochote mbele ya Mwalimu wake. Anasema Imamu Shafi Mola amrehemu: nilikuwa ninaufungua kila ukurasa wa Kitabu mbele ya Imamu Maliki Mola amrehemu, kwa utulivu na kwa kumuheshimu yeye; ili asisikie mteremko wa karatasi. Naye Rabiiu Mola amrehemu anasema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, kwa kumuheshimu, sijawahi kupatwa na kiu nikayanywa maji huku Imamu Shafi ananiangalia.

Anasema Shaukiy:

Simama kwa Mwalimu na umtukuze

                           Mwalimu anakaribia kuwa Mtume

Hapana shaka kuwa sisi tuna haja zaidi ya kuzipata elimu ambazo zitatusaidia kuijenga Dini yetu kwa kiasi cha mahitaji yetu ya elimu hizo ambazo kwazo Dini yetu itasimama imara. Hatuna muda wa kuupoteza kwa starehe, ambapo mchakato wa utafiti wa kisayansi, Ubunifu na Uvumbuzi, vimekuwa ni wajibu kwa wakati tulio nao, huwenda tukaliwahi Jahazi la Maendeleo, au hata tukafanikiwa kkuwahi kilichotupita katika njia ya kuyaelekea maendeleo. Kwa hiyo ni wajibu kwa kila mmoja wetu kuwa na moyo wa ubunifu, kutangulia, kiu cha maendeleo, au kwa uchache wa makadirio, tuwe angalau na utashi wa Umma wetu kurejea katika zama za Wakubwa zetu miongoni mwetu pamoja na Mababu zetu, ambao walisafiri kwa ajili ya kutafuta Elimu na wakajitahidi katika kuisaka mpaka wakachukua nafasi ya uongozi Duniani kielimu na wakawa wajuzi wa kila fani na sayansi ambazo walibobea ndani yake, na zikawa chimbuko safi la Elimu hizo, na nuru iangazayo mataifa yote ulimwenguni pamoja na staarabu mbali mbali baada yake, na ikawa ni alama yetu.

Tunajenga kama walivyokuwa waliotutangulia

                   Unajenga na unafanya kama walivyofanya wao

Kwa hivyo hapana budi kwa Mwanafunzi na Mwalimu wapambike kwa tabia njema, na matendo yao wote lazima yaendane na maneno yao mpaka jamii iathiriwe na hali hiyo. Umma wetu ulipofungamanisha baina ya Elimu na Maadili mema, uliishi katika hadhi ya juu baina ya Mataifa mbalimbali Duniani. Na ambapo Elimu na Maadili mema vilishamiri kwa kiwango cha juu mno pamoja na Maendeleo ya kiuchumi.

Ninaisema kauli yangu hii, na ninamwomba Mwenyezi Mungu anisamehe mimi pamoja nanyi.

****

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Viumbe vyote, na rehma na amani ziwe juu ya Mwisho wa Mitume na Manabii, Bwana wetu Muhammad S.A.W, na Jamaa zake, na Maswahaba wake ni kila mwenye kuwafuata mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika Uislamu umeinyanyua juu hadhi ya Elimu na Wanazuoni bila kujali ubobezi wao. Elimu yenye manufaa inakusanya kila elimu ambayo inawanufaisha watu katika mambo ya Dini yao na Mambo ya Dunia yao, na kwa hivyo tunaona kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Hakika wamchao Mwenyezi Mungu katika waja wake ni wanazuoni. Imekuja kauli hii ya Mwenyezi Mungu katika kuonesha gumzo la elimu za kimazingira ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

 }أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ * وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَلِكَ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ{

 Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameyateremsha maji kutoka mawinguni na tumeyaotesha matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupena myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana. Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe. .

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 }إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَاخْتِلاَفِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لآَيَاتٍ لأُولِي الأَلْبَابِ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَاماً وَقُعُوداً وَعَلَى جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ{

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kuhitalifiana usiku na mchana ziko ishara kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala. Na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi…

Vile vile maana ya Elimu yenye manufaa ni kila kinachowanufaisha watu katika maisha yao ya Duniani na Akhera, katika Elimu za Dini au za Kilugha au za Tiba, Madawa, Fizikia, Kikemia, Anga, Uhandisi, Nishati, na aina zingine mbali mbali za elimu na maarifa yenye manufaa kwa watu. Elimu ni msingi wa Mwananchi Mbunifu na Mvumbuzi mwenye Uzalendo, na dalili ya hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

}فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ{

Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.

Neno kukumbuka lina maana pana zaidi kuliko kuishia katika elimu yenyewe, kwani suala hapa ni lenye kuihusu kila aina ya elimu yenye manufaa. Jambo ambalo halina shaka yoyote ndani yake ni kwamba sisi tunazihitaji mno elimu zote ambazo zinaijenga Duniani yetu kama tunavyohitaji elimu zote ambazo zitaifanya Dini yetu isimame imara.

Na huwenda wajibu wa wakati huu na faradhi yake kwa Wanazuoni wa zama hizi ni kusahihisha Mieleweko na Maana mbali mbali zilizopotoshwa, pamoja na kurekebisha na kusahihisha sura ya Uislamu na Waislamu iliyopo akilini na iliyovurugwa mno, na kufanya kazi ya kueneza Fikra Sahihi ya Uislamu Ulio Sahihi. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie tuwe waaadilifu kwa watu hawa, na atufundishe tusio yajua, na atukumbushe tunayoyasahau, na atujaalie uongofu katika Dini yetu.