Hatari ya Vumi na kujenga Mzinduko wa Bandia

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا * يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا}

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa. Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo. Na baada ya utangulizi huu:

Hakika mapambano baina ya haki na batili ni ya tangu zamani, tangu kuwepo kwa mwanadamu, na yanaendelea mpaka siku Mwenyezi Mungu atakapoamua kuichukua Dunia na vilivyomo ndani yake, na kwamba miongoni mwa njia za wazi za watu wa batili katika mapambano yao na watu wa haki: ni utengenezaji wa Vumi na kuzieneza baina ya watu.

Na katika mambo yasiyokuwa na shaka ndani yake ni kwamba Neno ni amana na ni jukumu kubwa, liwe nia kusomwa, la kusikilizwa au la kuonekana. Na Vumi si lolote isipokuwa ni neon linaloenea baina ya watu, na hutolewa na watu wenye maradhi ya moyo, au mamlaka, au hata shirika, ambayo yote yanako chini ya nguvu za shari ambazo zinafanya kazi zake kwa siri, na husambazwa Vumi hizo kwa midomo bila ya kuwa na uthibitisho wowote, au kubaini ukweli wake, na huziathiri vibaya akili na nafsi za watu, na hueneza fikra zake za kubomoa na itikadi zake chafu, na jamii ikabadilika na kuwa katika hali ya wasi wasi na shaka, bali na usalama ukatoweka, na kujiamini baina ya watu kukadhoofika,. Kisha unauona Uma ulio mmoja unashukiana wenyewe kwa wenyewe, na kila mmoja anamfanyia hiayana mwenzake; na kwa hivyo amesema Mtume wetu S.A.W: Inamtosha mtu kuwa mwongo kwa kuzungumzia kila analolisikia. Kwa hivyo ikiwa kulizungumzia kila analolisikia mtu ni aina miongoni mwa aina za uongo na mtu huadhibiwa kwa kufanya hivyo, tena adhabu kali kweli kweli, itakuwaje basi kwa mtu anayeyazungumzia yale ambayo hajayaona au kuyasikia?

Uislamu umechukua msimamo mkali juu ya Vumi na wanaozieneza, na ukauzingatia mwenendo huu kuwa unaenda kinyume na Tabia Nzuri, na Maadili Mema yaliyoletwa na Sheria ya uislamu, na hiyo ni pale ulipowaamrisha wafuasi wake kuulinda Ulimi kutokana na kuyaingilia mambo yanayoeneza fitina na kuibua migongano katika Jamii, na ukawaamrisha wawe wakweli katika wanayoyasema, na kuzilinda ndimi zao na kuthibitisha kila kinachoyafikia masikio yao mpaka wasiwe wao ni sababu ya kueneza fitina, na kuiharibu Jamii, na kuzivuruga heshima zao. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ}

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ}

Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا}

Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo – hivyo vyote vitaulizwa.

Na katika Hadithi ya Muadh bin Jabal R.A, baada ya Mtume S.A.W, kumbainishia Mambo ya Farahdhi ya Uislamu, na milango ya Heri, alimwambia: na ukitaka nitakujulisha kichwa na Jambo na Nguzo yake na Kilele chake, akasema Muadha: Ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema S.A.W: Ama kichwa na Jambo lenu ni Uislamu, na Nguzo ya Jambo lenu ni Swala, na Kilele chake ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukitaka nitakueleza jambo zito kuliko yote hayo. Akasema Muadhi: ni kipi hicho ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: akaelekeza kidole chake kwenye Mdomo wake, kisha akasema: kisha nikamwambia: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Je hakika sisi tunazingatiwa kwa yale tuyasemayo kwa midomo yetu? Akasema: Ndio. Na siku ya Kiama watu watavutwa kwa pua zao na kutupiwa katika moto wa Jahanamu kwa sababu ya machumo ya midomo yao!

Hakika ya usambazaji wa Vumi na utangazaji wake ni mwenendo wa Wanafiki katika kuyafikia malengo yao ya kuutikisa usalama, na kuulenga Umoja wa Uma, na kuudhoofisha ukuaji wa Uchumi wake, na kuuvuruga utulivu na amani yake, na pia kueneza hali ya kuvunjika moyo na kukata tama na kuwa na fikra hasi ndani ya nyoyo za wananchi kwa ujumla, na vijana kwa sifa maalumu. Na Qurani Tukufu imewaita watu wa aina hii kuwa ni waenezao fitna; kwani jina hili linakusudiwa kwalo kujiingiza katika habari mbaya na fitina ambazo lengo lake ni kuzua migongano mikali katika Jamii. Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا}

Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.

Kwa hivyo, Vumi ni moja ya njia za Vita ambayo hata Mtume S.A.W hakusalimika nazo. Na hakika Mtume S.A.W, alipambana na Washirikina kwa sababu ya wao kueneza Vumi ambazo lengo lake ni kuvuruga ulinganiaji wake na kuiharibu sura ya ulinganiaji huo, na wakaeneza uongo baina ya watu kwamba Mtume S.A.W, ni mchawi! Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَقَالَ الْكَافِرُونَ هَذَا سَاحِرٌ كَذَّابٌ}

 na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.

Na kwa upotovu wakadai kuwa Mtume alikuwa Mshairi na Mwendawazimu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَجْنُونٍ}

Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?

Na wakati mwingine walieneza vumi kwamba Mtume S.A.W, ni kuhani, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawajibu kwa kusema:

{إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ * وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ قَلِيلًا مَا تُؤْمِنُونَ * وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ * تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ}.

Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe mwenye heshima. Ni machache sana mnayoyaamini. Wala sio kauli ya mtunga mashairi. Wala sio kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbuka. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Na katika siku ya Uhudi, Washirikina walieneza uvumi kuwa Mtume S.A.W ameuawa, wakiwa na utashi wa kutaka kuwasambaratisha Waislamu waliomzunguka Mtume, na kudhoofisha nguvu yao, na hivyo safu za waislamu zikatetereka kwa kiwango kikubwa na wakavunjika moyo na baadhi yao kukimbia, huku wengine wakiweka silaha chini na wengine wakaendelea kuwa na Mtume S.A.W.

Na katika siku ya Hamraail Asadi, Washirikina walieneza uvumi kwamba Makureshi wameandaa jeshi kubwa kwa ajili ya kuuvamia Mji wa Madina, na kupambana na Mtume S,A.W, na kuufyeka Uislamu, lakini Waislamu waliendelea kuwa na Mtume S.A.W katika Dini yao wala vumi hizo hazikuwababaisha hata kidogo. Na Mwenyezi Mungu akawasifu kwa kauliyake aliposema:

 {الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ * فَانْقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّهِ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ}.

Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa. Basi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.

Na hakika, Maadui wa Uislamu walikusudia hasa kuzua Vumi baada ya Mtume kugeuza Kibla kutoka Baitul Maqdis na kuelekea Baitul Haraam, na Mayahudi wakawa na kiburi cha kushuku usahihi wa kuelekea Baitul Haraam, na wakasema: kama Kibla cha kwanza ndio cha kweli basi kwa hakika nyinyi waislamu mmeitelekeza Haki, na kama Kibla cha kwanza ni batili, basi ibada zenu mlizokwishazifanya zimebatilika. Na kama Muhammad S.A.W, angelikuwa kweli ni Mtume, asingekiacha Kibla cha Mitume waliomtangulia kabla yake, na kukibadilisha kwa kingine, na anachokifanya leo kesho huenda kinyume nacho.

Na wakasema Wanafiki:  Waislamu wana nini hawa, walikuwa na Kibla kisha wakakiacha? na wakasema Washirikina: Hakika Muhammad S.A.W amekumbwa na mzubao katika Dini yake anakaribia kurejea katika Dini yetu na katika Kibla chetu. Lakini Qurani Tukufu imewavurugia mpango wao, na kuharibu vitimbi vyao, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwambia Mtume wake S.A.W kwa yale wayasemayo Wajinga hawa wote kabla ya kuwatenga na akamwandalia mazingira ya kukigeuza Kibla kwa namna ambayo itazituliza nyoyo za Waumini kuitia nguvu Imani katika nyoyo zao ili walipokee jambo hili tukufu. Na vile vile  katika siku ya Hunainiulienea Uvumi ya kwamba Mtume S.A.W ameuawa, na Mtume S.A.W akasimama  na akasema: Mimi ni Mtume na wala sio uongo, mimi ni mtoto wa Abdil Mutwalib.

Hakika katika kueneza Vumi na kuzitangaza kuna hatari isiyofichika kwa wenye akili, na kupelekea umwagaji wa damu, kufujwa kwa mali ya uma, kuvunjwa kwa heshima za watu, na maisha kuwa na mgongano, na sisi tuna dalili nzuri katika hili kutokana na Mauaji ya Khalifa wa tatu Othman bin Afaan R.A, wahalifu walimzingira kwa sababu ya Vumi tu na habari za uongo zilizovumishwa na  Myahudi, Abdullahi bin Sabai, bali walimzuia kunywa maji na yeye ndiye aliyekinunua kisima cha Ruma kwa mali yake ya halali. Kutoka kwa Naila, mke wa Othman bin Afaan, R.A, amesema: ilipowadia siku aliyouawa Othman, siku ya kabla ya kuuawa kwake alishinda akiwa amefunga, na ulipowadia wakati wa kufungua kinywa, aliwaomba maji ya kunywa na hawakumpa, kisha akalala bila ya kufungua kinywa, na ulipowadia wakati wa kula daku niliwafuata majirani zangu na nikawaomba maji ya kunywa wakanipa kiasi cha maji, nikaja nayo na nikamgusagusa na akaamka, na nikamwambia: Haya hapa maji ya kunywa, akanyanyua kichwa chake na akauangalia wakati wa kuchomoza Alfajiri, kisha akasema: Mimi nimeamka hali ya kuwa nimefunga na kwamba Mtume S.A.W, amenitokea katika sakafu hii akiwa na maji ya kunywa akaniambia: kunywa maji ewe Othman, nikayanywa mpaka kiu kikaniishia, kisha akasema: ongeza tena, nikayanywa mpaka nikashiba, kisha akasema: Hakika watu watakujia kwa wingi dhidi yako, na ikiwa utapambana nao utakuwa umepata ushindi, na ikiwa utawaacha basi utafuturu pamoja nasi. kisha wakamvamia siku hiyo na wakamuua.

Na katika zama zetu hizi, mambo mengi yamebadilika, na uwanda huu mwovu umechukua maumbile  mbali mbali na sura nyingi; kwa kuangalia maendeleo makubwa na  ya kasi yanayoshuhudiwa na ulimwengu, katika njia za mawasiliano na teknolojia, ambapo Uvumi umekuwa ukienea kwa kasi ya ajbu, na kuwasili pia kwa kasi kubwa, Uvumi umekuwa ukiathiri sana, bali umekuwa ni njia miongoni mwa njia zinazotumika katika vita na mitindo yake, Hivi sasa vita sio tena ya upande mmoja wa upeo kwa maana sio upande mmoja wa kijeshi tu, au wa kiusalama tu, au hata wa kiukachero tu kwa mweleweko wa kawaida uliozoeleka wa mifumo ya kizamani ya kiupelelezi, bali mbinu zake zimepevuka kwa upande wa mfumo wake wa kutumia silaha ya Vumi na kugushi Mzinduko ambapo sasa limekuwa ni jambo linalotafitiwa na mafunzo yanatolewa na pande zinazohusika na amabazo zinashukiwa, na huajiriwa kwa ajili hiyo vikosi vya kielektronia pamoja na kutumika kiwango cha juu cha njia za kudhibiti na kushinikiza kisiasa, kiuchumi na kinafsi, na majaribio hatarishi katika kuwachochea wananchi na kuwafanya wawe dhidi ya viongozi wao, na kuchafua nembo za Taifa na Mafanikio yake, na kushuku kila mafanikio na kuyadharau pia, na kuungana kwa Makundi na Nguvu za Kigaidi, na Majaribio ya kutaka kupenya katika Taasisi, na kuibua chokochoko zinazoweza kupelekea mtengano ulioandaliwa na ambao haujawahi kutokea, pamoja na kuyatumia kitaalamu Maelezo na Habari, na kutoa mafunzo kwa baadhi ya njia za kisasa za mawasiliano ya kijamii, bali nyingi katika njia hizo, na kuyatumia matatizo na shida ambazo baadhi ya watu hawawezi kuzivumilia, na kujaribu kuvunja Utashi wa wananchi, na kufanya kazi ya kuvunja heba ya viongozi, na kuwashuku wanachuoni wa kitaifa na nyanja mbali mbali, na kuwaunga mkono wapinzani wao, na kuelekeza risala za vitisho visivyo wazi baadhi ya nyakati, na vilivyo wazi katika nyakati zingine kwa wale wenye kuendelea kushikamana na Misingi yao ya Nia njema kwa nchi zao, kwa kuonesha matokeo ya wale ambao hawakuufuata mkumbo wao na wakajiunga nao katika njama zao ovu, na wakanyanyua bendera ya kusalimu amri na wakanyenyekea kisha kuwanyenyekeza walio nyuma yake.

Jambo lisilokuwa na shaka yoyote ni kwamba, kuendela kuwa na nguvu za kupambana na Mawimbi yote haya Makali ni jambo linalohitaji Akida ya Imani na Uzalendo imara, na kuwa na imani na Mwenyezi Mungu isiyo na mipaka, hayo ni kwa kuwa watu wengi sana huwenda wakawa wanapuuzia yale wayafanyao kwa kushiriki katika baadhi ya habari, au takwimu, au visa bila ya kuthibitisha, au kutafuta ukweli wa vyanzo vyake, na akawa miongoni mwa walioshiriki kuieneza na kuisambaza fitina pamoja na kuichochea. Na ni mara chache sananeno la uongo neno la uongo lisilokuwa na msingi wowote wa ukweli kusemwa na Mja au akaliandika au akashiriki katika neno hilo na kulifikisha mbali ikawa ni sababu ya yeye kuadhibiwa siku ya Kiama. Anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Mja atasema neno katika ridhaa ya Mwenyezi Mungu, bila ya yeye kulizingatia, Mwenyezi Mungu akamnyanyua kwa neno hilo cheo cha juu, na kwamba Mja anaweza akazungumza maneno yanayomchukiza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala yeye hayazingatii maneno hayo, na Mwenyezi Mungu akamtumbukiza katika Moto wa Jahanamu. Hadithi hii iko katika Swahiihul Bukhari.

Ninayasema maneno yangu haya na ninamwomba Mwenyezi Mungu anisamehe mimi na akusameheni na nyinyi.

*       *       *

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ninashuhudia kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata wao mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu.

Uislamu umeweka mfumo uliopangika kwa ajili ya kuilinda jamii kutokana na vumi mbali mbali, na miongoni mwa alama za Mfumo huo:

NI uwajibu wa kuthibitisha habari na kuwa na kutulizana kabla ya kueneza katika jamii. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ}

Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.

Na anasema Mtume S.A.W: kufanya mambo kwa utulivu kunatokana na Mwenyezi Mungu, na kufanya mambo kwa haraka hutokana na Shetani. Na anasema Mtume S.A.W: Kufanya Mambo kwa utulivu katika kunatakiwa katika kila jambo isipokuwa katika Kazi ya Akhera.

Kutozikariri Vumi kupitia njia yoyote miongoni mwa njia zinazosomwa, zinazosikilizwa au zinazoonekana; kwani kufanya hivyo ni kuchangia katika kuzitangaza na kuzieneza. Vumi hueneza kwa kasi pale zinapopata ndimi za kuzitajataja, na masikio ya kuzisikiliza, na nafsi zinazozikubali na kuziamini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُمْ مَا لَيْسَ لَكُمْ بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِنْدَ اللَّهِ عَظِيمٌ}.

Mlipo yapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.

Anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote anaemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi aimuudhi jirani yake, na Mtu yoyote anaemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi amkirimu mgeni wake, na Mtu yoyote anaemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basin a aseme maneno ya heri au anyamaze. 

Na kuwa na Dhana Njema kwa watu na kutoharakisha katika uwatuhumu. nasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {لَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنْفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَذَا إِفْكٌ مُبِينٌ}

Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?

Kwa hiyo Muislamu anaamrishwa awe na dhana nzuri kwa watu na ayachukulie yatokayo kwa watu kama ni mazuri; kwani dhana mbaya ni maradhi yaangamizayo na hupelekea mgongano wa maisha, na kueneza Ugomvi baina ya watu. Na Mtume S.A.W, ametukanya juu ya hayo kwa kauli yake aliposema: Jiepusheni na dhana kwa hakika ya dhana ni Mazungumzo ya urongo, na wala msifuaatiliane, na wala msichunguzane, wala msihusudiane, wala msiwekeane majungu, wala msibughudhiane, na muwe Waja wa Mwenyezi Mungu mlio ndugu.

Kuomba msaada kwa wenye uzoefu na wabobezi katika kuyabainisha mambo ya kweli, na kutoharakisha katika kutoa Maamuzi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akitoa wasifu wa Wanafiki:

{وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَى أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنْبِطُونَهُ مِنْهُمْ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا}

Na linapo wafikia jambo lolote linaloihusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet’ani ila wachache wenu tu.

Kwa maana ya kwamba walikuwa wakiuvizia usalama na utulivu wa Jamii ya Kiraia, na wanaposikia kitu katika habari zinazohusiana na Usalama wa Waislamu na hofu yao waliyoitangaza, au wakaonesha yanayokusudiwa kusambaza mfadhaiko, wasiwasi na mgongano.

Anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakaekemea uvunjwaji wa heshima ya ndugu yake, Mwenyezi Mungu atauepusha uso wake na Moto Siku ya Kiama.

Na tutambue ya kwamba Neno ni amana na tutaulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Siku ya Kiama.

Sisi sote tutambue ya kwamba maadui zetu wote wanazitumia vita za kizazi cha nne na kizazi cha tano, na vumi pamoja na kupotosha mafanikio yaliyoikiwa, na alama kuu za taifa, na majaribio ya kutaka kuharibu kila kitu cha uma, kama ni njia za kuiangusha nchi yetu na kuidondosha au kuisambaratisha kabisa; kwa ajili ya kuyafikia malengo na makusudio yao. Tunalazimika kutambua ya kwamba mbele yetu kuna vita kali inayoandaliwa dhidi yetu, na vumi ndizo mafuta ya kuwashia moto wake. Kwa hivyo tunalazimika kuhakiki na kuthibitisha ukweli ili tusije tukaangukia katika vitimbi vya maadui zetu. Na tunalazimika kujiamini sisi wenyewe, na katika majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Na wala tusiwasikilize maadui wa nchi yetu pamoja na wale wanaofanya kazi ya kutuangusha, au kupunguza mori tulio nao, au hata wale wanaofikiria kutuvunja moyo na kueneza hali ya kukata tamaa baina yetu, na haya yote yanatuhitaji sisi tuwalinde vijana wetu kwa Mzinduko na kwa Uhalisia, pamoja na kutambua ukubwa wa changamoto zinazotuelekea, pamoja na kujaribu kuzitatua.

Ewe Mola wetu tunakuomba uzifanye tabia zetu ziwe nzuri, na uilinde Nchi yetu, na utuwafikishe kwa yale unayoyapenda na kuyaridhia.

Amin.

 *      *       *