Nafasi ya Mashahidi, na kujitolea kwa ajili ya Nchi

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{ولا تقولوا لمن يقتل في سبيل الله أموات بل أحياء ولكن لا تشعرون}

Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika wanachi wa Misri katika siku hizi, wanasherehekea moja kati ya kumbukumbu zao muhimu sana za kudumu katika historia ya nchi yao na ni siki miongoni mwa masiku ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo yeye Mwenyezi Mungu amewapa Wamisri Ushindi na urejeshaji wa Ardhi yao pamoja na heshima, hakika huu ni uadhimishaji wa ushindi wa tarehe sita mwezi wa Oktoba mwaka wa 1973 – sawa na tarehe 10 mwezi wa Ramadhani mwaka wa 1393 – na tukio hili kubwa ambalo mwanajeshi wa Misri ameandika kutokana na tukio hili maana ya juu za Ushindi, Kujitolea, Uhanga, na tukio hili limedhihirisha jinsi mwanajeshi wa Kimisri alivyo kimaumbile kwa Imani yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na imani yake ya kupata ushindi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukweli wake na nafsi yake, na nguvu za kuazimia kwake na utashi alionao katika kulifikia lengo lake na muradi wake.

Wakati malengo yanapokuwa na hadhi ya juu, na Makusudio Matukufu, na Peo nzuri; hakika kujitoa Muhanga hapana budi kuwa na thamani ya hali ya juu, na wala hakuna kilicho ghali zaidi, au chenye thamani ya juu zaidi kuliko kuitoa nafsi muhanga kwa kutaka kufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtu huitoa roho yake kwa ajili kwa ajili ya kuilinda Dini yake, ardhi yake, heshima yake, na kuilinda heshima ya nchi yake na matukufu yake. Ili ajipatie nafasi ya juu ambayo ni nafasi ya kufa Shahidi.

Hakika nafasi ya Kifo cha Shahidi ni tunu na tuzo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, anampa tunu hiyo ampendaye baada ya Manabii, na Wasema Kweli. Anasema Mwenyezi Mungu:

{وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا}

Na wenye kumt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!

Chaguo la Mwenyezi Mungu Mtukufu kumteua Mtu ili awe Shahidi ni katika Dalili za juu za ridhaa yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtu huyo. Je? Kuna daraja la juu kabisa zaidi hili! Na Qurani imelidokeza jambo hili kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَيَتَّخِذَ مِنْكُمْ شُهَدَاءَ}

na awateuwe miongoni mwenu mashahidi.

Kwani Shahidi ameitoa nafsi yake kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kumridhisha Mola wale Mlezi na kwa ajili ya kuilinda nchi yake, na akaipendelea Akhera kuliko Dunia na akawa juu zaidi na akayashinda matamanio yake na matashi yake pia, na akaingia katika mapambano makali kwa kujitoa yeye mwenyewe kwa ajili ya Dini yake na Nchi yake. Pongezi kwa Shahidi kupata nafasi hii iliyobarikiwa, na faida ya mauzo yake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ  فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآنِ }

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo wanapigana kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, wanaua na wanauawa hii ni ahadi ya MWenyezi Mungu amejilazimisha kwa haki katika Taurati na Injili na Qurani.

Uzuri ulioje wa sifa nzuri kama hii ya malipo ya Pepo! Katika Hadithi ya Mtume S.A.W, kwamba Umu Rabiiu binti Baraau nae ni Mama Harith bin Suraaqah, alimjia Mtume S.A.W, na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hebu nihadithia kuhusu Haaritha? – Na Harithah alikuwa ameuawa siku ya Badri, alipigwa mkuki bila kujulikana aliyempiga mkuki huo vitani – Ikiwa yuko peponi nitavumilia, na ikiwa kinyume na hivyo nitajitahidi juu yake kwa kumlilia. Mtume S.A.W. akasema:  Ewe Mama Haarithah, Hakika yeye yuko katika Pepo za Peponi, na kwamba mwanao amejipatia Pepo ya Firdausi ya juu mno.

Hakika Shahidi wa kweli ni yule aliyejitolea kwa nia njema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akajitoa kwa ajili ya njia yake, na akaitoa nafsi yake na akawa mkweli kwa hilo ili neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu liwe juu. Na kwa ajili ya kuilinda ardhi ya nchi yake na kuinyanyua bendera ya nchi hiyo. Kutoka kwa Abuu Musa R.A, amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume S.A.W, na akasema: Mtu anapigana vita kwa ajili ya ngawira, na mtu anapigana vita kwa ajili ya kukumbukwa, na mtu anapigana ili nafasi yake ionekane, ni nani yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakaepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi mtu huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Shahidi wa kweli vile vile: ni mtu ambaye haukubali udhalili kwa hali zake zote, na anapinga kudhalilishwa na kupuuzwa, na anapambana na kila anaejaribu kushambulia mali zake au chochote anachokimili. Kutoka kwa Abu Hurairah R.A: alisema: Mtu mmoja alimjia Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Je unaonaje kama atakuja Mtu anataka kuchukua mali yangu? Akasema Mtume S.A.W: Usimpe mali yako. Je unaonaje ikiwa atapigana na mimi? Akasema Mtume S.A.W: pigana nae. Akasema yule Mtu: Je unaonaje ikiwa Mtu huyo ataniua? Akasema Mtume S.A.W: wewe ni Shahidi. Akasema yule Mtu: Je unaonaje ikiwa mimi nitamuua? Akasema Mtume S.A.W: Yeye ni wa Motoni.

Na shahidi wa kweli: ni yule anaeitetea ardhi yake, heshima yake au nchi yake. Kwa hivyo, kuitetea nchi yako, au heshima yako kwa Mwislamu ni haki kama vile ilivyo Haki ya kuitetea Nafsi, Dini au Mali; kwa kuwa Dini lazima iwe na Nchi inayoibeba na kuilinda. Kutoka kwa Saad bin Zaid R.A, anasema: Mtume S.A.W, anasema: Mtu yoyote atakayeuawa kwa ajili ya Mali yake basi yeye ni Shahidi, na Mtu yoyote atakayeuawa kwa jili ya watu wake basi mtu huyo ni Shahidi, na Mtu yoyote atakayeuawa kwa ajili ya Dini yake basi huyo ni Shahidi. Na mtu atakayeilinganisha maana ya Shahada kwa mtu kuitoa muhanga nafsi yake katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kila hali inayohitaji ndani yake utetezi wa Dini kwa ajili ya kulinyanyua juu neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa ajili ya Ardhi ili ailinde na kujibu mshambulizi dhidi yake atakuwa anapigana jihadi; kwani kuipenda nchi ni sehemu ya imani. Kongole kwa wale wote waliokufa mashahidi katika vita vya kupita na kuelekea katika njia ya Milele, haowee ndio ambao Damu yao tukufu imemwagika kwa ajili ya Nchi tukufu iliyo safi, na roho zao zikapanda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakafuzu radhi zake, na Neema ambayo amewaahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwayo, na tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie sisi tuwe miongoni mwa Mashahidi. Na Mashahidi wanaoipigania njia ya Mwenyezi Mungu wana wao matunda matukufu. Na miongoni mwayo ni aliyoyasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qurani Tukufu kwamba Mashahidi wako hai kwa Mola wao wanaruzukiwa, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ * فَرِحِينَ بِمَا آَتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِمْ مِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ * يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ}

Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.

Mashahidi wako hai na wala hawajafa. Wao wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. Na riziki yao inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Wao wanafuraha kwa yale aliyowapa Mola wao Mlezi; ambapo amewapa Pepo ya Milele ambayo ndani yake hakuna kilichowahi kuonwa na macho ya mwanadamu au kusikika kwa masikio ya mwanadamu au hata kuwahi kufikirika katika akili ya mwanadamu, na wao wanapeana habari njema kwa ndugu zao wajao kwao, ambapo hakuna kuhuzunika wala hakuna habari yoyote mbaya au ya kuhuzunisha isipokuwa habari njema tu, na fadhila pamoja na neema za kila aina. Kutoka kwa Jaabir bin Abdillahi R.A, amesema: Mtume S.A.W alikutana name, akaniambia: Ewe Jabir mbona mimi ninakuona wewe una huzuni? Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Baba yangu amekufa shahidi, na ameacha watoto na deni. Akasema Mtume S.A.W: Je nikupe habari njema za yaliyomkuta baba yako? Akasema: Ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: akasema Mtume S.A.W: Mwenyezi Mungu hakuwa kuzungumza na yoyote isipokuwa nyuma ya pazia, na alimpa uhai baba yako na akazungumza nae bila ya pazia baina yao au yoyote kuwa kati yao. Akasema: Ewe Mja wangu, Tamani chochote kwangu na mimi nitakupatia. Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi ninakuomba unifufue mimi ili nipigane vita kwa ajili yako kwa mara nyingine tena, Mwenyezi Mungu akamwambia: Hakika Mambo yalivyo neno langu limeshatangulia ya kwamba wao waliokwenda huko hawarejei. Akasema: Ikateremshwa aya hii:

{وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا}.

Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti.

Na katika nafasi za Mashahidi: ni kwamba wao kwa mola wao wana mambo sita yamekuja yakiwa yamefafanuliwa ndani ya Hadithi ya Mtume S.A.W, iliyopokelewa na Miqdam  bin Ma-adi Yakrib, R.A, amesema:  anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W: Shahidi ana mambo sita kwa Mola wake Mlezi, atasamehewa katika kundi la mwanzo, na takiona kiti chake Peponi, na ataepushwa na Moto wa Jahanamu, na ataepushwa na mfadhaiko mkubwa, na tavikwa Taji la Unyenyekevu kichwani mwake, yakuti ya huko ni bora kuliko Dunia na vilivyomo ndani yake, na ataozeshwa Mahurul-aini sabini na mbili, na ataombewa ndugu zake sabini – na katika mapokezi mengine – jamaa zake wote.

Na miongoni mwa aina za makarama ya Mashahidi: -ni mwamba Malaika wanawafunika kivuli kwa mbawa zao. Kutoka kwa Jabir bin Abdillahi R.A, amesema: Baba yangu alipelekwa kwa Mtume S.A.W – kwa maana akiwa Shahidi wa Vita vya Uhudi – na kuwekwa mbele yake, akaiwekwa mikononi mwa Mtume S.A.W, na mimi nikaenda nikamfunua uso wake, na watu wangu wakazinuzia, na Mtume S.A.W akasikia sauti ya kelele, akasema: unalia nini? Usilie, Malaika bado wanaendelea kumwekea kivuli kwa mbawa zao. Na miongoni mwazo: ni kwamba Shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa katika kundi la mwanzo linaloingia peponi bila ya hesabu wala adhabu yoyote. Kutoka kwa Abdillahi bin Amru bin Alaaswiy R.A, amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu akisema: Hakika Mwenyezi Mungu ataiita Pepo siku ya Kiama, na itakuja ikiwa na mapambo yake na ataiambia: Wako wapi waja wangu waliopigana kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakauawa katika njia yangu, na wakanyanyaswa katika njia yangu, na wakapigana jihadi katika njia yangu? Ingieni Peponi bila ya hesabu wala adhabu. Kisha wanakuja Malaika, na wanasema: Ewe Mola wetu Mlezi hakika sisi tunakusabihi wewe usiku na mchana, na tunakutakasia wewe, ni akina nani hao ambao umewapendelea zaidi kuliko sisi? Atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: hao ni wale waliopigana kwa ajili ya njia yangu, na wakanyanyaswa katika njia yangu, basi Malaika wataingia kwao kupitia milango yote na kusema: Amani iwe juu yenu kwa mliyoyavumilia, ni neema iliyoje ya Nyumba mliyoiendea.na miongoni mwazo ni: Kwamba Mashahidi katika Pepo wana makazi bora kabisa kuliko yote. Kutoka kwa Smurata bin Jundabi, R.A, amesema: Anasema Mtume S.A.W: Usiku niliwaona wanaume wawili walinijia na wakanipandisha juu ya Mti, na wakaniingiza ndani ya Nyumba ambayo ni bora kuliko zote, nilizowahi kuziona, wakaniambia: Hakika hii ni nyumba ya Mashahidi. Na kwa haya yote, Mashahidi peke yao ndio wanaopenda kurejea Duniani na akauawa katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mara nyingine, kama ilivyo katika Hadithi ya Anasi R,A, kwamba amesema: Kwamba Mtume S.A.W amesema: Hakuna mtu yoyote anayeingia Peponi kisha akapenda kurejeshwa Duniani, na kwamba yeye kila alichonacho ardhini isipokuwa huutaka Ushahidi, kwani hakika yeye anatamani arejee ardhini, na auawe mara kumi; kwa yale anayoyaona mioni miongoni mwa makarama ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na katika mapokezi mengine: Kwa jinsi anavyoziona fadhila za kufa Shahidi.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na nyinyi.

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ninashuhudia kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata wao mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu.

Hakika kuyafikia malengo makubwa na kuzipata peo kuu katika maisha haya ya Duniani kunahitaji kujitolea kwa kiwango cha juu kinachoendana na Dunia, na kwamba hapana shaka yoyote kwamba Malengo yanapokuwa Makubwa na Makusudio yakawa na hadhi ya juu na pia kuyafikia Malengo Makuu, kunahitaji kujitolea kwa kiwango cha juu na utukufu wake, na hadhi ya juu ya nafasi zake, na hali hii ni ya kila aliyejitoa Muhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu, na katika Dini yake na Nchi yake.

 Na Wajibu wetu sisi kuielekea nchi yetu tukufu na Dini yetu ni kunatuhitaji tuwe ni wenyekujitahidi, kushirikiana na kuwa bega kwa bega sisi sote, ili tuilinde amani yake na kuitetea pia, na kuilinda na kila aina ya maadui wanaoinyemelea, au hatari yoyote inayoitishia, na tuwe sisi macho yayayokesha kwa ajili ya kuulinda uma wetu, na tuwe bega kwa bega sisi sote bila kumbagua yoyote tuwe ngome ya kumzuia yoyote anayejaribu kuwa na nia ya kuichezea nchi yetu, kila mmoja kwa mujibu wa uwezo wake, na kwa mujibu wa kazi ya kila mmoja wetu na majukumu yake.

Pongezi ziwe kwetu sote kwa kuwa na wanajeshi wetu ambao waliungana katika kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakayasadikisha yale waliomuahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakaweza kwa ari yao yenye nguvu, na yakini iliyothibiti na yenye mizizi imara, waipitishe nchi yetu hii pendwa kuelekea katika ujenzi na uimarishaji wake, na kongole kwa Wanajeshi wetu Mashujaa siku walipojipatia Ushindi Mtukufu. Na hakika sisi tuna mchango mwingine ambao ni kuondoka na kuvuka tukielekea eneo  la Maendeleo na Maisha bora, na kufanya kazi  na kuzalisha, ili tuuthibitishie Ulimwengu wote kuwa waliouvuka mpaka wa Ngome na kuivuka na kisha kuvamia ngome nyingine za mashambulizi katika siku tukufu, watoto wao na wajukuu wao wana uwezo wa kuvamia kila lililo gumu katika njia ya kuifikia amani na usalama pamoja na maendeleo na maisha bora kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba tuwe safu moja nyuma ya viongozi wetu wa kisiasa Majeshi yetu shupavu na askari polisi wetu wazalendo na taasisi zote za nchi za kitaifa.

Ewe Mola wetu, tunakuomba uilinde Nchi yetu, na uwalinde Watu wake, uidumishe neema ya Amani na Usalama na uiruzuku Utajiri, Maendeleo na Riziki iliyo pana.