Fiqhi (Elimu) ya Ujenzi wa Mataifa

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa Viumbe vyote, asemaye katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَتَعَاوَنُوا عَلَى البِرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُوا عَلَى الإِثْمِ والعُدْوَانِ}

Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakuna shaka yoyote kwamba Mataifa yote na wakazi wake yanataka kujijenga yawe na nguvu na utulivu, kwa kila aina ya nguvu na nyenzo zilizopo, ili kuyafikia malengo yake, na kuzijenga nchi ni elimu inayohitaji uzoefu na utambuzi na kuyajua mazingira na changamoto zake ipasavyo. Na kuna toauti kubwa baina ya Fiqhi ya Watu na Makundi na Fiqhi ya Ujenzi wa Mataifa na utashi wake katika ulimwengu wenye kasi ya Mabadiliko na Mageuzi ambao haujui isipokuwa lugha ya Mikusanyiko na Jumuiya Mbali mbali za kisiasa, kiuchumi na kitamaduni, na Mikusanyiko hiyo na Jumuiya hizo zinaendeshwa kwa misingi, sheria na mikataba ya kimataifa ambayo mwenye akili ukiongezea na nchi yoyote haiwezi kuipuuza au kutoitekeleza au kwenda sambamba na uhalisia wa hali ilivyo.

Kwa hivyo, nchi nil indo, nchi ni usalama, nchi ni kujiamini, nchi ni utulivu, nchi ni mfumo wa uendeshaji, nchi ni taasisi mbali mbali, nchi ni ujenzi wa kifikra, kisiasa, kiuchumi, kimfumo na kisheria, na bila ya nchi hakuna kinachokuwepo isipokuwa machafuko.

Na miongoni mwa njia za ujenzi wan chi: ni kuziimarisha taasisi zake, na kutanguliza sheria, nchi ya yenye Katiba, nchi yenye uadilifu. Na hili linamtaka kila mmoja aheshimu sheria za nchi na mifumo yake, na kufuata sheria za barabarani na masharti yake, na kutozikwepa na kwenda kinyume cha barabara, au kuongeza kasi, au mambo mengine mengi ambayo yanazingatiwa kuwa ni ukiukaji wa haki za barabarani, na haki za watu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

{وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ وَأَحْسِنُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ}

wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Hakuna kujidhuru au kumdhuru mtu mwingine.

Kuulinda mfumo wan chi na kuuheshimu kunachangia ujenzi wan chi yenye nguvu na iliyo tulivu; kwani hapana budi kwa kila jamii iwe na misingi na sheria zake zinazoongoza mwenendo wa kila mtu, na kumlindia haki zake, na kumuwajibisha ndani ya jamii hiyo kila mtu atekeleze wajibu wake. Na bila ya kuuheshimu Mfumo wa nchi na kuufuata, na kutanguliza Sheria, nchi haziwezi kutulia au kuwa na uadilifu.

Hakika kuheshimu Sheria na kuzifuata kunazingatiwa ni katika njia muhimu mno za kujwnga nchi. Sheria ni ulinzi wa kila mwananchi, kwani haiingii akilini jamii kuendelea kuwa na utulivu bila ya kuheshimu sheria za nchi. Hapana budi kila mmja abebe jukumu lake ili kuyafikia masilahi ya taifa ambayo Jamii nzima itayavuna matunda yake. Anasema Mtume S.A.W: Nyinyi nyote ni wachunga na nyonte mtaulizwa kuhusu mnaowachunga. Imamu ni mchunga na ataulizwa kuhusu wale anaowachunga. Na mwanaume ni mchunga wa watu wake naye ni mwenye kuulizwa kuhusu anaowachunga. Na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mume wake na ataulizwa kuhusu anaowachunga. Na mtumishi ni mchunga wa mali ya mkuu wake na ataulizwa kuhusu anachokichunga…

Kwa hiyo, Jamii yenye kuyabeba majukumu yake ni jamii yenye mshikamano, na kila mmoja anazitambua haki za mwingine, na anamuheshimu mwingine. Tunahitaji kwa kiwango kikubwa kuheshimu Mfumo wan chi na kuzifuata Sheria zake, na kuchunga haki za wengine, ili uadilifu utawale na jamii ineemeke kwa usalama, amani na utulivu. Na tunaiona nchi yetu ikiwa katika nafasi isiyostahiki kati ya nchi zote Duniani.

Na miongoni mwa njia za ujenzi wa Mataifa: Ni Ujenzi wa Uchumi. Hii ni katika nguzo muhimu sana za Msingi ambazo nchi haiwezi kujengwa au kusimama isipokuwa kwazo. Uchumi wenye nguvu huziwezesha nchi kutekeleza majukumu yake ya ndani na ya nje, na kuwaandalia maisha mazuri wananchi wake. Na uchumi wa nchi unapodhoofika basi umasikini huenea pamoja na magonjwa mbali mbali, na maisha yakakosa utulivu, maadili yakavurugika na kuongezeka kwa uhalifu, na ikawa ni fursa pana kwa maadui wanaozinyemelea nchi zilizo katika hali hiyo, ambao lengo lao ni kuziangusha na kuingiza ndani yake machafuko yasiyokwisha. Kwa hiyo, Mataifa yasiyozalisha nyenzo zake za kimsingi huwa mzigo kwa mengine, na hukosa kauli na uhuru wa maamuzi.

Hakika uchumi wenye nguvu katika nchi huziwezesha nchi hizo kuheshimiwa na nchi zingine; kwa hiyo, Uislamu unajali mali kwa kuwa mali ni uti wa mgongo wa Maisha, na maisha hayawezi kuendelea isipokuwa kwa mali. Na ujenzi wa Nchi kiuchumi unahitaji utendaji bora na uzalisha mwingi. Hakuna taifa lolote linaloinukia, au taasisi yoyote, au familia yoyote isipokuwa kwa kufanya kazi ipasavyo. Kinachohitajika sio kazi tu, bali utekelezaji kamilifu na kuongeza uzalishaji ambao unakuwa na mrejesho mzuri wa kiuchumi kwa wananchi wote. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuasa juu ya kufanya kazi Duniani, akasema:

{فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانْتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِنْ فَضْلِ اللَّهِ وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيرًا لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}

Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِنْ رِزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ }

Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.

Na Mtume S.A.W, anakizingatia chakula kizuri anachokila mtu ni kile anachokichuma kwa mikono yake na kwa bidii yake, ambapo anasema S.A.W: Mtu hajawahi kula chakula chenye kheri kamwe kuliko kile kinachotokana na kazi ya mikono yake. Na kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Daudi A.S, alikuwa anakula kutokana na kazi ya mikono yake.

Na anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakaeshinda mchana kutwa akiwa ni mwenyekuitegemea kazi ya mikono yake miwili atakuwa ameshinda muda wote huo hali ya kuwa amesamehewa madhambi yake.

Na katika wito wa uzalishaji, anasema Mtume S.A.W: iwapo Kiama kitasimama na katika mkono wa mmoja wenu kuna mche, na ikiwa ataweza kuupanda mche huo kabla hajasimama mpaka aupande basin a aupande.

Na anasema Mtume S.A.W: Hakuna Muislamu yoyote anaepanda mbegu yoyote au akalima zao lolote, kisha ndege au mwanadamu au mnyama yoyote akala kutokana na kazi hiyo, ispokuwa Muislamu huyo huandikiwa kwa kitendo hicho ametoa sadaka.

Kwa hiyo, kwa kazi na uzalishaji, ardhi huhuishwa na Mataifa hujengwa, na Mtu huilinda heshima na hadhi yake.

Na miongoni mwa njia za ujenzi wa Mataifa ni: Mzinduko wa Kitamaduni, Kidini, Kifira na Kielimu. Hakika kukosekana kwa Mzinduko au kudhoofika kwake, hakuwezi kuchangia ujenzi wan chi yenye nguvu na utulivu, na kwa hivyo hapana budi kuinua kiwango cha mzinduko kwa watu wote ili kila mmoja wao aujue wajibu wake na azijue haki zake.

Na haya yanapatikana kwa kuunda Mzinduko na Silika pamoja na Mwenendo wa watu wote kupitia Malezi ya Tabia, Utamaduni wenye manufaa, na kupambana na Ujinga. Kwa hiyo, ni wajibu wa taasisi zote za Dola kuwa bega kwa bega kwa ajili ya ujenzi wa Mzinduko wa Kitamaduni, Kidini, Kifikra na Kielimu ambao utawawezesha watu wote kutambua kiwango cha changamoto zinazoielekea Dola yao na jinsi ya kupambana nazo pamoja na kupambana na vumi na kuzitokomeza kabla hazijaathiri, na kutofuata maneno ya uzushi na ya uongo pamoja na vumi zinazolenga kupotosha ambazo zinajaribu kuiathiri nchi yetu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ}

Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.

Vile vile tunatakiwa tuwe macho na wenyekuzinduka, na tuwaidhike kwa wengine, na tunufaike kutokana na majaribio ya Maisha na kila aina ya uzoefu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ}

Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu!

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Muumini hagongwi na nyoka kwenye shimo moja mara mbili.

Na tunapaswa tutambue ya kwamba ujenzi wa nchi na Kuilinda ni amana juu yetu sote, kila mmoja katika Nyanja zake, pamoja na kuthibitisha kwetu kwamba Ujenzi hautimii kwa mikono wa Wabomoaji. Kama asemavyo Mshairi:

   Ni lini ujenzi wa nyumba utakamilika

                             Ikiwa unaijenga na mwingine anaibomoa.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Mnusuru nduguyo aliyedhulumu au aliyedhulumiwa. Mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Ninamnusuru anapokuwa ni mwenyekudhulumiwa, je waonaje ikiwa ni mwenyekudhulumu? Nitamnuduru vipi? Akasema: Unamzuia kufanya dhuluma, kwani kufanya hivyo ndio kumnusuru.

Kwa hivyo kila mmoja wetu kwa mujibu wa majukumu yake, anatakiwa amzuie kila mwenye kutoka nje ya umoja wa kitaifa au kuyadhuru masilahi ya Taifa, Mzazi amzuie mwanae, Na kaka amzuie nduguye, na Rafiki amzuie rafiki yake, na tusiwe sisi sote na fikra hasi tusiojua yanayotokea katika mazingira yetu. Anasema Mtume S.A.W:  Msiwe wafuasi, wanaosema: Ikiwa watu watafanya wema na sisi tutafanya wema, na ikiwa watu watadhulumu na sisi tutafanya dhuluma, lakini zitulizeni nafsi zenu, ikiwa watu watu watafanya vizuri na nyinyi mfanye vizuri, na ikiwa watu watadhulumu basi nyinyi msidhulumu.

Anasema Mtume S.A.W:

Mfano wa Mwenye kusimama katika Mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na yule mwenyekuivuka ni kama mfano wa watu waaliopiga kura ya kuingia katika jahazi, baadhi yao wakapata nafasi za juu na wengine wakabata nafazi za chini ya jahazi hilo. Waliokuwa chini ya Jahazi hilo, wakawa pindi wanapotaka kutafuta maji ya kunywa huwaendea walio juu na kuwaambia: mnaonaje kama sisi tukiitoboa sehemu yetu ya chini kwa kuitoboa na bila ya kuawaudhi walio juu yetu itakuwaje? Ikiwa walio juu watawaacha walio chini walitoboe Jahazi basi wote wataangamia, na ikiwa watawazuia basi wote wataokoka.

Haitoshi Mtu kuwa mwema yeye mwenyewe, bali uhakika wa mambo ni kwamba Fiqhi ya Kipindi maalumu inahitaji  kuvuka kipindi cha wema na kuelekea katika kipindi cha Marekebisho,

             ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {لَا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِنْ نَجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا}

Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَى بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ}

Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema.

Marekebisho ndio njia ya Mitume na Manabii, na kwayo hujengwa Mataifa, Na kuulinda Umoja, Nguvu na Mshikamano pamoja na Mfungamano wake, ili Watu waishi kwa amani na nia safi, hakuna migogoro wala mgawanyiko, machafuko, ugaidi wala ufisadi ardhini kwa kuua au kusababisha uharibifu wowote.

Ninaisema kauli yangu hii, Ninamwomba Mwenyezi Mungu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

*      *      *

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ninashuhudia kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata wao mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu.

Na miongoni mwa njia za kuijenga nchi na kuilinda ni: Ujenzi wa Kijamii. Uislamu unahimiza sana nguvu za mifungamano na mahusiano ya kijamii baina ya watu wote katika jamii, na kuwa bega kwa bega pamoja na kuhurumiana kwa watu wa jamii moja, na kutowasababishia watu wengine madhara, kutokana na kauli ya Mtume S.A.W aliposema:

Hawi muumini wa kweli yoyote kati yenu mpaka ampendelee ndugu yake kile anachokipenda yeye.

Na anasema Mtume S.A.W: Ninaapa hawi muumini wa kweli, Ninaapa hawi muumini wa kweli, ninaapa hawi muumini wa kweli: Pakasemwa: Ni nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema: ni yule ambaye jirani yake hasalimiki kwa mabaya yake.

Na anasema Mtume S.A.W: Hawi ni mwenyekuniamini mimi yule atakayelala akiwa ameshiba na hali ya kuwa anajua kwamba jirani yake wa karibu ana njaa.

Na miongoni kwa alama za Ujenzi wa Kijamii ni: Mshikamano wa Kifamilia unaoilinda familia yote. Familia ndio jingo la kwanza ambalo ndani yake hujengekeka ngome ya Jamii. Familia ndiyo inayobeba jukumu la kuwalinda chipukizi na kuwalea pamoja na kuwakuza kimwili na kiakili. Na chini ya kivuli cha familia, hupatikana hisia za Upendo na huruma pamoja na kuleana. Na katika familia yenye mshikamano, huzalika upendo mzuri na mambo mema, na huenea hali ya kupendana lakini hata hivyo haiishii hapo tu, kwani familia ina majukumu yake kwa watoto wake. Anasema Mtume S.A.W: Inamtosha mtu kupata madhambi kwa kuwatelekeza anaowalea.

Na je? Kuna upotevu wowote mkubwa kuliko kuwaacha wanao wa kuwazaa wawe katika mazingira hatarishi ya fikra potoshi au makundi yaliyopotoka bila ya kutekeleza wajibu wako kwao katika kuwakuzia mzinduko wa kifikra na changamoto zinazotuzunguka, pia tuwakumbushe daima wajibu wao kwa nchi yao, kwani kuipenda nchi kunarithisha upendo kwa wote.

يقول شوقي :

نقــوم على الحماية ما حيينــا *** ونعهــد بالتمـام إلى بنينــا

وفيك نموت مصر كما حيينــا *** ويبقى وجهك المفدى حيًّـا

Na miongoni mwa njia za ujenzi wa nchi ni: kuinua viwango vya Maadili mema ya kitabia na kimwenendo. Mataifa na staarabu ambazo hazijengwi kwa Maadili ya Kitabia yanakuwa legelege, na staarabu zake zinakuwa legelege zaidi bali huwa zinabeba sababu za kuanguka kwake katika msingi wa ujenzi wake na sababu za kusimama kwake. Kwani Tabia njema humuinulia muislamu daraja za imani na huongeza uzito wa mizani yake wakati wa kupimwa. Anasema Mtume S.A.W: Hakuna kitu kilicho kizito zaidi katika mizani ya mja muumini siku ya Kiama kuliko Tabia njema, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia Mwovu aliyepindukia katika uovu wake.

Mtume S.A.W alipoulizwa kuhuku kinachowaingiza watu Peponi kwa wingi ni kitu gani? Akasema: Ni kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Tabia njema. Na Mtume S.A.W ameihesabia Tabia njema kama ni kigezo cha ukamilifu wa Imani au upungufu wake, akasema: Waumini wenye Imani iliyokamilika ni wabora wao kitabia.

Hakika mwenyekujipamba na Tabia njema hukingwa na na Machafu pamoja na Maneno mabaya yaangamizayo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِنْ فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِنْ قَرَارٍ}

Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, ulio ng’olewa juu ya ardhi. Hauna uimara.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atuongoze tuelekee katika Tabia zilizo bora zaidi, na Maneno Mazuri, na atudumishie sisi neema ya Usalama, Amani na Utulivu, na ailinde nchi yetu na watu wake, na nchi zote Ulimwenguni kutokana na uovu na jambo lolote baya.