Huu ndio Uislamu

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu.

{وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَاتَّخَذَ اللَّهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا}

Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo. Na baada ya utangulizi huu:

Na baada ya autanguli huu,

Hakika Uislamu wa kweli ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtii, na kumfuata yeye Mtukufu, na upendo, kufuata, na kumuiga Mtume wetu S.A.W, na kuwa na tabia njema, na kuwa mnyenyekevu,  na nafsi iliyo safi, na kuwa na uso mkunjufu katika kuonana na watu wote, na ulaini na upole, na uzuri pamoja na Ulimwengu wote, na kujenga na kuinua ujenzi miji, na ustaarabu na maendeleo miji, Uislamu ni mfumo wa maisha wanayoishi wafuasi wake katika harakati zao na utulivu wao na vitendo vyao vyote.

Hakika ya Uislamu, ni dini inayolingania Marekebisho na Utengemavu, na ujenzi wa Dunia kwa Dini, na wala sio kuibomoa Dunia kwa jina la Dini, na Dini ya Kiislamu inalingania Huruma, Usalama na Amani kwa Ulimwengu wote, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ}

Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.

Hakika ya mwenye kuzingatia Nguzo za Uislamu zilizotajwa katika Hadithi ya Jiburilu A.S, alipomuuliza Mtume S.A.W, akisema: Ewe Muhammad, niambie kuhusu Uislamu, Mtume S.A.W, akasema: (Uislamu ni kukiri kwa Moyo na kushuhudia kwa ulimi kwamba hakuna mungu mwingine apasae kuambudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ukasimamisha Sala tano, na ukatoa Zaka, na ukafunga Mwezi wa Ramadhani, na ukahiji Makkah kama utaweza kufanya hivyo…), atatambua kwamba huchangia kuujenga utu wa mtu uwe sawa. Mtu anapoamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na hana mshirika wake, na kwamba Bwana wetu Muhammad S.A.W, ni Mja wake na ni Mtume wake, atahangaikia kuifanyia kazi shahada hii kwa kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumnyenyekea, Mola wa viumbe vyote, akawa anafuata Maamrisho yake, na akajiepusha na Makatazo yake, na akasimama katika mipaka yake, na wala hayapuuzii yale aliyokalifishwa, na wala hahitaji kisichokuwa chake, vile vile anajitahidi katika kumfuata Mtume S.A.W, na kutangamana na watu kama vile Mtume alivyotangamana nao; kwa upole, huruma, unyenyekevu na ulaini.

Hakika Sala ndio Nguzo Kuu miongoni mwa Nguzo za Uislamu, na matunda yake humrejea mja huyu, kwa kumzuia na maovu na yaliyokatazwa, kuwa na msimamo katika njia ya Mwenyezi Mungu, na anaishi Mwislamu kwa amani na salama yeye na nafsi yake pamoja na Jamii yote kwa ujumla. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ}

SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.

Na utoaji Zaka kuna pande za kiimani na za kiutu; kwani zaka huinyoosha nafsi isiambatane zaidi na mali, mpaka mtu atambue kwamba Mali ni njia na wala sio lengo kuu la binadamu, na zaka pia ni mlango wa ushirikiano baina ya watu, kuhurumiana, kutoa, kujitoa, kuitoa nafsi, kuwapendelea wengine na wala sio kujipendelea, au kuwa bahili na mgumu wa kutoa. Kwani Muumini ni msamehevu, mtoaji na mkarimu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwasifu Maanswaar (Maswahaba wa Madina) R.A:

{وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِنْ قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ}.

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

Na vile vile Saumu, hii udhibiti maadili ya Mwislamu na kumfanya adumu katika katika kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na humzoesha mvumilivu na subira na kuiimarisha Nafsi yake na kuiweka zaidi kwa kuiepusha na kila kinachomkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mtume wetu Muhammad S.A.W, anasema: Saumu ni Kinga, na inapokuwa siku ya kufunga ya mmoja wenu, basi asitoe maneno machafu, wala asifoke foke, na iwapo mtu atamtukana au akamfanyia ugomvi, basi na aseme: Hakika mimi ni mtu niliyefunga.

 Na anasema Mtume S.A.W: Asiyeacha Uongo na kuutumia, basi hana yeye kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu haja yoyote ile ya kuacha chakula chake na kinywaji chake.

Vile vile Hija ni uwajibikaji wa kimwenendo na kimaadili kabla ya Hija, wakati wa Hija na baada ya kumaliza Idada zote za Hija. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّهُ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ}

Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!

Kutoka kwa Abu Huraira R.A, amesema: Nimemsikia Mtume S.A.W, anasema: Mtu yoyote atakayehiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajatoa maneno machafu, na wala hajafanya uovu wowte, basi atarejea kama siku alivyozaliwa na mama yake (kwa kutokuwa na kosa hata moja).

 Na hivi ndivyo ilivyo. Nguzo zote za Uislamu zina athari zinazoleta na kheri, Usalama na Amani zake kwa Jamii yote.

Hakika mtu anaeuangalia undani wa Dini yetu tukuzwa, atatambua ya kwamba hii ni Dini ya Tabia njema, na ni ujumbe uliokuja kutimiza Tabia hizi njema, ambapo anasema Mtume S.A.W: (Hakika mimi nimetumwa ili nije kukamilisha Tabia njema), ambapo Ukweli, Utekelezaji wa ahadi, Uaminifu, Wema, na kuunga undugu

Utoaji, ukarimu, Uokozi, Utu, Utambuzi, kujipamba na wema, na kuzuia maudhi kwa wengine, na kumnusuru mwenye matatizo, na kumwokoa mwenye kuomba uokovu, na kuwafariji wenye kukumbwa na matatizo, na kuwa mpole kwa wanyama, basi huo utakuwa Uislamu ulio sahihi na ndilo lengo lake kuu.

Katika jambo lisilo na shaka ni kwamba Kuujua Uislamu wenyewe, na kuzijua siri za ujumbe wake wa Usamehevu, na kusimama kidete katika Makusudio yake Makuu na Malengo yake Makuu, na kuyatekeleza yote kwa kuangazia mapya ya zama hizi, yanazingatiwa kuwa ni katika mambo ya lazima kwa ajili ya kupambana na changamoto za kisasa, na kuyazuia Makundi ya Kigaidi na ya Misimamo mikali, na kuizingira fikra iliyokengeuka na kuvunja mzunguko wake dumavu na uliojifunga, na Ufahamu mbaya, na Ufinyu wa peo, na kutoka katika Ufinyu huu kuelekea katika Ulimwengu unaokukribisha zaidi, mpana na ulio mwepesi, komavu na wenye mzinduko zaidi, na kuona na kuujua undani wa kitu, kwa ajili ya kuyafikia masilahi mapana ya nchi na Waja, na kusambaza Maadili ya Kibinadamu ambayo yanaleta usalama na amani, usalama, utulivu na furaha kwa binadamu wote.

Hakika miongoni mwa mambo ya wajibu mno na yaliyo muhimu zaidiambayo kila Mwislamu anapaswa kuyafanya ni kuwadhihirishia watu wote Utukufu wa Dini ya Uislamu ili ulimwengu mzima utambue kuwa Uislamu ni Dini ya Amani na inalingani Amani na inaiheshimu amani. Amani ni jina miongoni mwa Majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{هُوَ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ}

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama.

Na salamu ya Kiislamu ni Amani, na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَى إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا}

Wala msimwambie anayekutoleeni salamu; wewe sio Muumini

Na Maamkizi ya watu wa Peponi ni Salamu kwa maana ya amani, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ سَلَامٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ  فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ}

Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.

Na ilikuwa moja kati ya Dua zake Mtume S.A.W, baada ya kila Sala:

 (اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلاَمُ ، وَمِنْكَ السَّلاَمُ ، تَبَارَكْتَ يا ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ).

Ewe Mola wangu, wewe ni Amani, na amani inatoka kwako, umetukuka ewe Mwenye Utukuzo na Ukarimu.

Hakika Uislamu ni Dini inayoilinda heshima ya binadamu, inazuia kuteta na kusengenya uhasidi na kubaguana, kudharauliana na maudhi ya aina yoyote iwayo; iwe kwa kauli, kwa kitendo au hata kwa ishara, au hata kwa kudokezea, ambapo anasema Msema Kweli, Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَى أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَى أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَئكَ هُمُ الظَّالِمُون}

Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane heshima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kuamini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Mtu yoyote atakaemnyooshea nduguye chuma, hakika Malaika humlaani mpaka anapoacha kufanya hivyo, hata kama mtu huyo atakuwa ni nduguye wa mama mmoja na baba mmoja.

Na Mtume S.A.W, ametukataza Kupiga na kuchora usoni, na alipomwona mnyama amepigwa chapa usoni, akasema S.A.W: Mwenyezi Mungu amlaani aliyempiga chapa mnyama huyo usoni.

Na Mtume S.A.W, alipoulizwa kuhusu mwanamke anaefunga na kusali lakini anamuudhi jirani yake, akasema S.A.W: Huyo ni wa Motoni. Na anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote anayemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Siku ya Mwisho, basi asimuudhi Jirani yake, na mtu yoyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi amkirimu Mgeni wake, na yoyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi aseme maneno mazuri au anyamaze.

Ninaisema kauli yangu hii, na ninamwomba Mwenyezi Mungu anisamehe mimi na akusameheni na nyinyi. 

* * *

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ninashuhudia kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakaewafuata wao mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu.

Mtume S.A.W, aliijenga misingi imara ya Mafunzo ya Uislamu wenye Usamehevu, na Tabia zake Njema, na Maadili Mema na Mazuri katika nyoyo za Maswahaba wake mpaka ukawa huo ndio Mfumo wa Maisha yao wanayoyaishi na kutangamana kwayo na watu wengine wote. Tunamwona Swahaba huyu, Jafar bin Abu Twaalib R.A, anasimama mbele ya Mfalme Najashi – Mfalme wa Uhabeshi, ambayo ni Ethiopia kwa sasa – akiweka wazi moja katika Maadili haya mema ya Uislamu, na hizo Tabia zake Njema kwa uweledi wa hali ya juu, na maneno ya kuaminika, anasema: Ewe Mfalme, sisi tulikuwa taifa la watu wa zama za Ujinga, tunayaabudu Masanamu, tunakula Mizoga, tunafanya Uzinzi, tunauvunja undugu, tunamtendea uovu ujirani, na Mwenye Nguvu anmmaliza Mnyonge miongoni mwetu, na tulikuwa hivyo hivyo mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, akatuletea Mtume miongoni mwetu, tunaijua nasaba yake, ukweli wake, uaminifu wake, Tabia yake njema, akatulingania tuelekee kkwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili tumpwekeshe, tumuabudu, na tujivule nay ale yote tuliokuwa tukiyaabudu sisi na baba zetu kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile Mawe na Masanamu, na akatuamrisha tuseme ukweli, tufikishe amana, tuunge undugu, tuwe na ujirani mwema, tuyaache yaliyoharamishwa na tusiuane, na akatuzuia uzinzi na Maneno ya uongo, na kula mali ya yatima, na kuwatuhumu uzinzi wanawake walioolewa, na akatuamrisha tumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu aliye peke yake, na wala tusimshirikishe na kitu chochote, na akatuamrisha kusali, kutoa Zaka, kufunga…

Kwa hivyo, Mwislamu wa kweli hadanganyi, hagushi, hafanyi uhaini, Mwislamu wa kweli ni yule ambaye Waislamu wenzake wamesalimika na Ulimi wake na mkono wake. Na Muumini wa kweli ni yule ambaye watu wote wamesalimika damu zao, heshima zao, Mali zao, na nafsi zao, Mwislamu wa kweli ni yule ambaye Tabia njema za Kiislamu huonekana wazi kwake, haiwafikii watu kutoka kwake isipokuwa kheri na wema, na kama tungelitaka kuweka maana halisi na ya kweli ya Mwislamu wa kweli na tusingeipata maana nzuri kuliko au ile jumuishi zaidi aliyoitoa Mtume S.A.W, kwamba: Mwislamu ni yule ambaye Watu wote wamesalimika kwa Ulimi wake na Mkono wake, ambapo anasema S.A.W: Je niwaambieni ni nani Muumini wa kweli? Ni yule ambaye watu wote wamemwamini kwa Mali zao na Nafsi zao, na Mwislamu ni yule ambaye watu wote wamesalimika kwa Ulimi wake na Mkono wake, na Mpiganaji wa Jihadi ni yule mwenyekupambana na nafsi yake katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mhamaji (Muhaajir) ni yule aliyoyahama Makosa na Madhambi yake.

Hakika risala ya Uislamu ni risala ya Ubinadamu, Hekima, Usamehevu, Huruma, Moyo mpana, Na ukubalifu, ni risala inayowakusanya watu na sio kuwatenganisha na kuwasambaratisha, Uislamu ni Uadilifu kamili, huruma kamili, usamehevu kamili, uwepesishaji kamili, utu kamili, na kila kila kinachozifikia maana hizi zenye hadhi ya juu nazo zimo ndani ya Uislamu, na mtu yoyote anayegongana au kujigonganisha na maana hizi zote; hakika mtu huyo atakuwa anajigonganisha na Uislamu, Malengo na Makusudio yake Makuu.

Ewe Mola wetu tuongoze katika Tabia zilizo bora zaidi, kwani hakuna wa kutuongoza katika Tabia bora zaidi isipokuwa wewe, na tunakuomba utuepushe na utukinge na tabia mbaya kwani hakuna wa kutuepusha na tabia mbaya isipokuwa wewe, na tunakuomba uzilinde nchi zetu na wananchi wake na majeshi yake ya ulinzi na ya usalama, na uyakinge na jambo baya, ewe Mpole wa wapole.