Sura angavu za Maisha ya Maswahaba R.A

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

 {وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ}

Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba umswalie, umrehemu na umbariki Mtume wetu na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata hadi siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewachagua Manabii na Mitume wake, A.S, miongoni mwa viumbe vyake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اللَّهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ}

Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawachagulia Mitume wasaidizi wao katika kuzifikisha risala za Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Msema Ukweli, amemchagulia Mtume Muhammed, watu walio wasafi, na Maswahaba wateule, waliomwamini yeye na wakawa wanamuheshimu na kumnusuru na wakaifuata nuru aliyoteremka nayo. Anasema Abdallah bin Masoud R.A: amesema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameziangalia nyoyo za waja wake na akamchagua Muhammad S.A.W, na kumpa ujumbe wake na alimchagua kwa Kujua kwake kisha akaziangalia nyoyo za watu baada ya Muhammad na akamchagulia Maswahaba na akawajaalia wakawa ni wenye kuinusuru Dini yake na wakawa Mawaziri wa Mtume wake S.A.W. kwa hiyo wanachokiona Waumini kuwacni kizuri basi hata mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kizuri pia, kile ambacho Waumini wanakiona kuwa ji kibaya basi hata mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kibaya.

Walikuwa R.A, ni wakweli wa Imani katika watu, ba wenye ujuzi zaidi kielimu katika Watu, na wenye fahamu ya ndani zaidi, na wenye kazi bora katika Watu, waliibeba bendera ya Dini na kupeperusha katika maeneo mbalimbali Ulimwenguni, kwa hekima na Mawaidha Mazuri, na wakaifikisha risala ya Mola wai Mlezi kwa ufikishaji  ulio bora zaidi, wakastahiki wawe ni chaguo la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume S.A.W. Kutoka kwa Ibnu Abas R.A, amesema katika Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {قُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلامٌ عَلَى عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَى}:

Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa.

Kwamba Maswahaba wa Mtume S.A.W, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemteulia Mtume wake S.A.W, kwani wao ndio waliofuata Mfumo wa Uislamu kutoka katika chanzo chake cha asili na kisafi na hawakutoka katika njia yake iliyonyooka.

Hakika Maisha ya Maswahaba yalijaa sura nyingi angavu ambazo ziliunda utekelezaji wa kivitendo wa Uislamu Sahihi, na miongoni mwazo ni: Rehma. Mtume S.A.W, alipandikiza kwa Maswahaba wake Maadili ya rehma, na kwa hivyo, Ayina bin Husnu alipomwona Omar R.A, siku moja akimbusu mmoja wa watoto wake, na akiwa amempakatia, Ayina akasema: Unabusu Wakati wewe ni Amiri wa Waumini? Kama mimi ningelikuwa Amiri wa Waumini nisingelimbusu mtoto. Omar R.A, akamwambia: Mimi nifanye nini ikiwa Mola wako Mlezi amekuondoshea rehma na upole moyoni mwako? Hakika mambo yalivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu huwarehemu waja wake walio wapole wenye kuwahurumia wengine. Na katika tukio hili, Bwana wetu Omar amejifunza kutokana na tukio lililomtokea Mtume Muhammad S.A.W, alipokuwa na Aqrau bin Haabis; ambapo Mtume S.A.W, alimbusu Bwana wetu Husein bin Ali R.A, mbele ya Aqrau, na Aqrau akasema: Hakika mimi nina watoto kumi na sijawahi kumbusu yoyote kati yao. Mtume S.A.W akamwangalia kisha akasema: asiyehurumia watu na yeye hahurumiwi.

Maswahaba R.A, walikuwa pia ni mifano mizuri ya kuigwa katika kusamehe na Usamehevu. Na katika sura zenye ubora wa hali ya juu ni ile ya Bwana wetu Abu Bakar Swiddiq katika Usamehevu wake kwa Musatwah bin Athaathah. Abu Bakar alikuwa akimpa pesa za matumizi kwake kutokana na ukatibu wake na ufakiri wake. Na Musatwah alikuwa miongoni mwa watu waliomzungumzia vibaya Bi Aisha R.A. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha aya za kuonesha kuwa Bi Aisha hana yoyote.hatia yoyote, Abu Bakar akataka kumnyima Musatwah pesa za matumizi, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha Kauli yake:

{وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَالسَّعَةِ أَنْ يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَى وَالْمَسَاكِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا أَلَا تُحِبُّونَ أَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ}

Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

Akasema Abu Bakar Swiddiq R.A: Ndivyo hivyo. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, miki ninapenda Mwenyezi Mungu anisamehe. Na akarejesha tena kumpa nduguye Musatwah pesa za Matumizi, huku akisema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kamwe mimi Sitazisitisha pesa za matumizi kwa Musatwah.

Na miongoni mwazo ni: Ari ya hali ya juu na ushindani katika kutenda mambo ya Kheri. Hakika Maswahaba R.A,  walijifunza kutoka kwa Mtume S.A.W, jinsi ya kuwa na ari ya haoi ya juu pamoja na ushindani katika kutenda mema na kuyatafuta mambo yaliyo juu ambapo anasema Mtume S.A.W: Mbapo mwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mwombeni Pepo ya Firdaus. Kwani pepo hiyo ndio ya kati katika Pepo na ni ya Daraja la juu – ninaona – juu yake kuna Arshi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutokea hapo Mito ya Peponi huwa inaanzia, na jambo hili ndilo lililowafanya Maswahaba watukufu watazamie Mambo ya juu katika kila jambo. Anasema Bwana wetu Omar R.A: Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu alituamrisha tutoe sadaka, na jambo hilo likaenda sambamba na mimi kuwa na fedha, na nikasema: Leo  nitamshinda Abou Bakar ikiwa kuna uwezekano wa kumtangulia leo. Nikaja na nusu ya Mali yangu kwa Mtume S.A.W, na Mtume akasema: Umewaachia kitu gani watu wako wa nyumbani? Nikasema: Nimewaachia mfano wa mali hii. Akasema: Na Abu Bakar R.A, alikuja hapa na mali yake yote aliyonayo, na Mtume S.A.W, akamwambia: Umeiachia kitu gani familia yako? Akasema: nimeiachia Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake. Nikasema: Kamwe siwezi kushindana na wewe katika kitu chochote.

Na tumtazame Swahaba huyu hapa, Kaab bin Aslamiy R.A, amesema: Nilikuwa ninalala na Mtume S.A.W, nikamletea baadhi ya vitu vyake akaniambia S.A.W: Omba utakacho. Akasema: ninaomba niwe nawe Peponi, akasema au kuna ombi jingine?. Nikasema: ni hicho hicho. Basi Mtume S.A.W, akasema: basi nisaidie mimi kwa kusujudu kwako kwa wingi.

Na miongoni mwayo: Ni kujinyima na kutokuwa na tamaa. Maswahaba wa Madina walikuwa ni mifano bora zaidi katika hili la kujinyima. Kutoka kwa Abu Huraira R.A, amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu S.A.W, Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika mimi nimekumbwa na njaa. Mtume akampeleka kwa wakeze na hakukuta chakula chochote. Akasema S.A.W: Ajitokeze mtu wa kuwa mwenyeji wa huyu kwa usiku huu, Mwenyezi Mungu atamrehemu? Mtu mmoja katika Watu wa Madina akasimama na akasema: Mimi hapa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akaenda kwa watu wake nyumbani na akamwambia mkewe: Tuna mgeni wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, usiache kumpa kitu chochote tulichonacho. Akasema yule mke wake: Ninaapa ya kwamba mimi sina chochote isipokuwa chakula cha watoto. Akasema Mume: watoto watakapo chakula cha usiku uwalaze na uje, kisha uzime taa, na yuyapumzishe matumbo yetu usiku wa leo. Mke wake akafanya hivyo. Kisha Mume akaenda kwa Mtume S.A.W, na Mtume akasema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amestaajabishwa au – amefurahishwa – na fulani pamoja na fulani. Na hapo ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha Kauli yake:

{وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ}

bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.

Na katika tukio zuru linalokusanya baina ya hali ya upendeleo kwa mwingine waliokuwa nayo Maswahaba wa Madina R.A, na hali waliyokuwa nayo Maswahaba wa Makkah ya kujizuia na tamaa, Bwana wetu Saad bin Rabiigh anapendekeza kwa Bwana wetu Abdulrahmaani bin Aufi R.A, ampe nusu ya mali zake, akakutana na Bwana wetu Abdulrahmaani R.A, akiwa na kila aina ya kujizuia na tamaa, alichokifanya ni kumwomba amjulishe sehemu lilipo soko, na akafanya biashara na akajitahidi mpaka akawa ni miongoni mwa matajiri wakubwa wa Madina.

Na miongoni mwayo ni: Kurejea katika Haki. Maswahaba R.A, walikuwa na hima kubwa katika Haki, hawawi na kiburi katika kurejea kwenye haki. Kutoka kwa Abu Masoud Answaariy R.A, alisema: nilikuwa nikimpiga kijakazi wangu, nikaisikia sauti ikitokea nyuma yangu: Tambua ewe Abu Masoud kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye uwezo zaidi juu yako kuliko uwezo wako juu ya kijakazi huyu. Nikageuka na kuangalia nikamwona Mtume S.A.W, nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu kijana ni huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akasema: Kama usingelifanya hivyo basi Moto ungekutafuna. Au Moto ungekukamata.

Na miongoni mwayo ni: Kutekeleza ahadi. Mtume S.A.W, alipandikiza thamani ya kutekeleza ahadi katika nyoyo za Maswahaba wake na akawahikiza kuwajibika na Jambo hili. Tunamwona Bwana wetu Muawiya bin Abu Sufiyani R.A, ambapo baina yake na Warumi palikuwa na Ahadi na Muawiya R.A, akafikiria kutoka na kuelekea karibu na Mipaka ya Urumi, ili muda wa ahadi ukimalizika awavamie. Akajiwa na mtu katika Maswahaba wa Mtume S.A.W, huku akisema Mtu huyo, Allahu Akbar, Allahu Akbar, ni utekelezaji wa Ahadi na sio kinyume chake. Watu wakamwangalia alikuwa ni Amru bin Absa R.A, Muawiya akamtumia mtu na akamuuliza: akasema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu S.A.W, anasema: Mtu yoyote mwenye ahadi baina yake na wengine basi asiuongeze ugumu wake, wala asiifungue ahadi mpaka itakapoumaliza muda wake au akakata nao ahadi kwa mujibu wa vitendo vyao. Muawiya akarejea nyuma na hakuchukua hatua aliyotaka kuichukua.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Hana mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu Muhammad ni Mja na Mtume wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, mswalie, mrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake Wote, na yoyote atakaewafuata mpaka Siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika Maswahaba wa Mtume S.A.W, walikuwa ruwaza njema katika ujenzi wa Dunia kwa Dini, kwani kila mmoja wao alikuwa na kazi anayoifanya, na anaijua vizuri na kuitekeleza ipasavyo. Miongoni mwao alikuwamo Mfanyabiashara, Kiongozi, Mbeba Elimu, na wengine wengi. Anasema Mtume S.A.W: aliye mpole zaidi wa Uma wangu katika umma wangu huu ni Abu Bakar, na aliye Mkali zaidi katika Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ji Omar, na mwenye haya zaidi ni Othman, na Mjuzi zaidi wa Halali na Haramu ni Muadh bin Jabal, na msomaji zaidi wa Kitabu chake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Ubayu. Na Mjuzi zaidi wa Elimu ya Mirathi ni Zaidu bin Thabit. Na kila Umma una mwaminifu wake zaidi, na Mwaminifu zaidi wa Umma huu ni Abu Ubaidah bin Jarraah.

Na kazi za Maswahaba R.A, zilikuwa na matunda yake mazuri. Na Mtume S.A.W, alikuwa akiwahimiza na kumkumbusha kila mmoja wao kile anachoweza kukifanya vizuri zaidi kwa ajili ya kuonesha kumjali Swahaba huyo na kazi yake anayoifanya. Na katika hayo ni yale yaliyokuwapo kwa Bwana wetu Othman bin Afaan siku ya Vita vya Tabuk, ambapo aliingia alipo Mtume S.A.W, akiwa na Dinari elfu moja na akamkabidhi Mtume S.A.W. Na Mtume S.A.W, akasema: Baada ya kitendo chake hichi, kamwe hakuna Kitu chochote atakachokifanya Othman kikamdhuru.

Na miongoni mwayo ni kuichunga halali, na kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kila Jambo. Na katika hili ndivyo alivyokuwa Bwana wetu Jurair bin Abdillah R.A, ambapo Mtumishi wake alimwamuru amnunulie farasi na akamnunulia farasi kwa dihamu mia tatu. Na akaja na farasi pamoja na mwenye farasi ili amlipe na Jurair akamwambia mwenye farasi: farasi wako ni bora kuliko dirhamu mia tatu, je unaweza kumuuza kwa dirhamu mia nne? Akasema: hiyo ni juu yako wewe. Akasema: Farasi wako ni bora zaidi ya hiyo. Je unaweza kumuuza kwa dirhamu mia tano? Kisha akaendelea kuongeza mia mia mpaka akafikia dirhamu mia nane, na akamnunuackwa bei hiyo. Na akasemwa katika hilo akasema: Hakika mimi nimempa Mtume S.A.W ahadi ya utiifu juu ya kumnasihi kila mwislamu.

Kila mmoja wao akawa anatambua wajibu wake na anautekeleza ipasavyo na wala hapundukii katika majukumu yake. Na Bwana wetu Abu Bakar R.A, alimpa Bwana wetu Omar R.A, Majukumu ya Ukadhi, na Bwana wetu Omar akakaa kiasi cha mwaka, hakuna mtu yeyote anayemwendea, na hapo ndipo alipomtaka Bwana wetu Abu Bakar amtoe katika Ukadhi huo, akasema: Je unataka uondoshwe kwenye Ukadhi kutokana na ugumu wa kazi ewe Omar? Omar R.A, akasema: Hapana ewe Khalifa wa Mtume S.A.W; baoi ni kwa sababu ya kutohitajika kwangu kwa Waumini, kila mmoja wao anaijua haki yake, na wala hahitaji zaidi ya hivyo, na anaujua wajibu wake na wala hazembei katika utekelezaji wake, kila mmoja wao anampendelea ndugu yake kile anachokipenda yeye mwenyewe, na pindi mmoja wao anapokuwa haonekani wao humtafuta, na anapoumwa wao humtembelea, na anapoishiwa wao humsaidia, na anapohitaji wao hukidhi mahitaji yake, na anapokuwa na msiba wao humhani na kumliwaza, Dini yao ni Kunasihiana, na Tabia zao ni kuamrishana Mema na kukatazana Mabaya. Watu wa aina hii ni kipi watakachokigombania?

Tutambue kwamba sisi tunahitaji zaidi kurejea katika Maadili ya Mifano hii mema ya Maswahaba wa Mtume S.A.W, na kujipamba kwa Tabia zao pamoja na kuionesha sura sahihi ya Dini yetu ya Uislamu, Dini ya Rehma, Usamehevu, Utu, na Amani kwa Watu wote.

Ewe Mola wetu tulindie nchi yetu, wananchi wake, na Majeshi yake ya Ulinzi na Usalama, na Uijaalie Maendeleo, na Maisha Mazuri, pamoja na Nchi zote Duniani.