Ulinzi wa Nchi kwa ujumla na Masilahi yake Makuu

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

 {وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ}

Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika wake. Na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu mjaalie rehma na amani na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Uislamu umeijenga Nchi ya Kweli kwa kuiwekea Misingi na kuijengea Nyenzo zake. Uislamu umehimiza Ulinzi wa Nchi.    na ukaweka jukumu la Ulinzi wa Nchi na Shime kuwa ni jukumu la pamoja baina ya Wananchi wake wote. Na kila Mzinduko ulipoongezeka kwa wananchi wa Jamii ya Kiislamu juu ya Thamani ya Nchi, na hatari yake, ndipo ushirikiano ulipoongezeka zaidi, na kuwa bega kwa bega, na kufungamana kwa ajili ya kuilinda Nchi. Na hapo ndipo nguvu ya Jamii inapopatikana na wote wakawa kitu kimoja a kujihisi kama wamoja, ambapo Mtume wetu S.A.W, ametuhimiza juu ya Jambo hili akasema Mtume wetu S.A.W: Muumini na Muumini mwenzake ni kama Jengo linalosimama pamoja, na akavishikanisha vidole vyake. Na akasema S.A.W: Mfano wa Waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na na kuoneana huruma kwao ni mfano wa Mwili mmoja; kiungo kimoja kinapougulia mwili mzima pia huugulia kwa kukesha na homa.

Jambo lisilokuwa na shaka yoyote ndani yake ni kwamba moja ya nguzo muhimu za ulinzi wa Nchi ni: Kuyatanguliza Masilahi Mapana ya Uma yanayowanufaisha Watu wote, juu ya Masilahi Binafsi na Finyu ambayo yanawanufaisha wahusika tu. Kwa ajili ya kuitakasa nafsi ya Binadamu kutokana na shari za umimi, na hivyo ni kwa kuwa Masilahi ya Uma yanakusanya kila kinachoyasimamisha Maisha ya Jamii kwa ujumla kwa hali na mali, na kuleta kheri na manufaa kwa watu wote, na kuwaondoshea shari na maovu, na kuwaletea ulinzi wan chi, na utulivu wake na amani ya ardhi yake. Na hapana shaka kwamba kuutengeneza Uma na Jamii kwa ujumla ndilo jambo linalofanywa na Fiqhi ya jinsi ya kuweka Vipaumbele.

Qurani Tukufu imetuthibishia kwamba kuyalinda masilahi ya taifa a kuyatanguliza juu ya masilahi binafsi ndio Mfumo wa Mitume ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Manabii wake wote. Kwani Mwenyezi Mungu hakuwaleta Mitume na Manabii isipokuwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu wake, na kuwaletea kila kheri bila ya malipo yoyote ya mali, au manufaa yoyote ya Dunia. Anasema Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Mtume wake Nuhu A.S:

{وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّهِ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّهُمْ مُلَاقُو رَبِّهِمْ وَلَكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ}

Na enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali kwa ajili ya haa. Mimi sina ujira isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na mimi sitawafukuza walioamini. Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi, lakini mimi ninakuoneni mnafanya ujinga.

Na anasema Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Mtume wake Hud A.S:

{يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي أَفَلَا تَعْقِلُونَ}

Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Haukuwa ujira wangu isipokuwa kutoka kwa Yule aliyeniumba, basi hamtumiii akili?

Na anasema Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Mtume wake Shuaibu A.S:

{إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّهِ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ}

Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye ninaelekea.

Na Sheria Tukufu imekuja na ikawa sambamba na akili ya Mwanadamu, na inanasibiana nae, na ikayataka mambo ambayo lengo lake yalete masilahi kwa wananchi wote. Miongoni mwayo ni: kuyafikia mahitaji Muhimu ya Jamii, na kuchunga Fiqhi ya Uhalisia, na ikiwa haja ya Jamii ni ujenzi wa Hospitali na kuziwekea vifaa mbali mbali vya kuwatibu mafukara na kuwauguza basi hapo kuna kipaumbele, na ikiwa haja ya Jamii ni ujenzi wa Shule na vyuo mbali mbali na kuvifanyia ukarabati na kuviandalia vifaa mbali mbali pamoja na kuwagharamia wanafunzi wake na kuwalea, basi hicho ndicho kipaumbele. Na ikiwa haja ya jamii ni kuwepesisha ndoa kwa wenye ugumu wa kuoa na kuwalipia madeni wenye kudaiwa na kuwaondoshea uzito watu wenye matatizo ya kushindwa kulipa madeni basi hicho ndicho kipaumbele. Kwa hiyo kukidhi haja za watu na kuwasimamia matakwa yao ni katika mambo ya wajibu kisheria na kitaifa. Anasema Mtume S.A.W: Hawi mwislamu ni mwenyekuniamini mimi anapolala akiwa ameshiba na jirani yake ana najaa pembezoni mwake, na yeye anajua hivyo.

Na miongoni mwayo ni: Kulinda Mali ya Uma. Na hili ni jambo ambalo wananchi wote wanashirikiana. Na uharamu wa Mali ya uma ni mkubwa zaidi kuliko ule wa mali binafsi; kutokana na wingi wa haki zinazoambatana na Mali hiyo ya Uma, na wingi wa dhimaya anaezimiliki, na kwa hivyo Uislamu umetahadharisha ubadhirifu wa mali hiyo au kuiiba au kusababisha madhara yoyote. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَنْ يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ثُمَّ تُوَفي كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لاَ يُظْلَمُونَ}

Na atakayefanya khiyana atayaleta siku ya Kiama aliyoyafanyia khiyana, kasha kila mtu atalipwa kwa aliyoyachuma, kwa ukamilifu wala hawatadhulmiwa.

Kwa hivyo Mali ya Uma ni miliki ya Watu wote, na wala sio miliki ya kundi maalumu miongoni mwao, na wafanya kazi wa sekta hiyo wao ni walinzi walioaminiwa kuilinda Mali hiyo na kuikusanya na kuitumia kwa wahusika. Si halali kwa mtu yoyote kuishambulia au kuchukua sehemu ya mali hiyo asiyoistahiki, kwani kufanya hivyo ni uhaini na dhuluma; na kula mali za watu kwa njia Haramu.

 Uislamu umeamrisha kuzilinda taasisi zote za Serikali kama vile Majumba ya Ibada, Shule na Vyuo, Hospitali, Bustani na Maeneo ya Uma, na kadhalika. Vyote hivyo ni miliki ya wananchi wote. Na manufaa yake ni kwa ajili a watu wote. Na Uilsmu umetutahadharisha kwa ukali dhidi ya kuzishambulia taasisi za Serikali au kuzipoteza au kuziharibu kwa namna yoyote iwayo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا}

Na wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa…

Mpaka watu wasije wakadhani kwamba inajuzu kutumia mali ya uma kwa njia amayoitaka yeye na jinsi atakavyo, kwa madai kuwa ni haki yake kama ilivyo kwa wengine, na kufahamu hivyo ni kosa. Kwani wajibu wetu ni kuzilinda taasisi za Uma a kulihifadhi pamoja na kuziendeleza na kuziboresha; kwani tasisi hizi si za mtu kinyume na mwingine au kundi la zama Fulani; bali ni letu sote na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Miongoni mwayo ni: ulinzi wa barabara na njia, na kuzichunga haki zake. Anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W: Ole wenu na kukaa barabarani. Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tunalazimika kukaa katika vikao vyetu, tunazungumza katika vikao hivyo. Akasema Mtume S.A.W: Mnapoviendea vikao vyenu basi  muipe barabara haki yake. Wakasema: Ni ipi hiyo haki ya barabara? Akasema: Ni kuinamisha macho, na kuondosha adha kwa watu, kujibu salamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Na anasema Mtume S.A.W: Imani ni imegawanyika mara Sabini na kitu – au sitini na kitu – na bora yake ni kusema Hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ya chini yake ni kuondosha madhara jiani, na Haya ni sehemu ya Imani.

Na miongoni mwayo ni: kushiriki huduma ya kitaifa ambayo inazinatiwa kuwa ni moja ya mambo muhimu ya wajibu ambayo yanafanywa na mtu kwa ajili ya Dini na Nchi yake, na ni dalili ya  uzalendo wake kwa nchi yake, na ukweli wa uzalendo wake, na mapenzi yake kwa nchi yake. Kwani nchi na heshima yake havina hatari ndogo kuliko nafsi yake, Dini yake Mali yake, au Vitu vyake. Vile vile hii hujenga kwa wananchi maana za ushujaa, utu na mwonekano mwema wa mtu, na Maadili Mema yaliyoletwa na Dini yetu tukufu. Anasema Mtume S.A.W: Macho ya aina mbili hayataguswa na Moto. Jicho lililolia kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha kwa ajili ya kulinda katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Na katika Msilahi ya Uma ambayo lazima yachungwe – ni ulinzi wa Serikali – unaokuwa baina ya nchi nan chi zingine, au shirika, au taasisi za kigeni miongoni mwa mikataba: kwa hakika hatua yoyote ya Kifiqhi au ya Fatwa, au ya ulinganiaji, lazima iwe hatua ya kitaasisi, inayotokana na kiongozi Muhusika au anaemwakilisha kiongozi huyo. Na ni juu ya anyeyazungumzia mambo haya aweke zingatio katika kila kinachobabaisha kijamii, kitaifa na kimataifa na kuungana na jambo analolizungumzia, ili zisitoke baadhi ya rain a fatwa za mtu mmoja anaeharakisha katika Jambo la uma, kwa namna inayoleta mgongano na uhalisia au inagongana na Sheria na Mikataba na Makubaliano ya Kiataifa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha utekelezaji wa Mikataba. Anasema Mwenyi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ ءَامَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ}

Enyi mlioamini, zitekelezeni ahadi zenu.

Kwa hivyo aya hii tukufu inakusanya kila aina ya mikataba na mambo ya kufuatwa ambao mtu analazimika kuyafuata yeye na  mtu mwingine. Na anasema Mtume S.A.W: Waislamu hufuata Masharti waliojiwekea wao wenyewe, isipokuwa Sharti inayoharamisha Halali au sharti inayohalalisha Haramu.

Tunamwona Mtume S.A.W, anamrejesha Abu Basiir R.A, baada ya Mkataba wa Hudaibiyah, kwa mujibu wa Mkataba ambo uliwekwa baina ya Mtume S.A.W, nan a Makureshi wa Makkah, pamoja na kuwepo uwezekano wa Swahaba huyu kudhurika; kwa ajili ya kulinda Mkataba aliyowekeana na Makureshi wa Makkah, na hii ni aina ya utekelezaji wa Mkataba kwa upande mmoja, na ni aina ya kutanguliza na kuweka Masilahi ya Uma mbele kwa upande wa pili.

Hakika mazungumzo kuhusu Serikali – bila ya kuwa na mzinduko, uelewa, au fahamu – hatari yake huugusa muundo kamili wa nchi na nguvu zake; na huufanya usalama wa nchi na utulivu wake wote uwe ni halali, na kichekesho, na kuongezeka kwa upuuzi na mtu kuzungumzia mambo asiyoyajua katika asiyoyaelewa. Wingi ulioje wa watu wanaoleta ufisadi ardhini na wala hawarekebishi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ana ametuamrisha tulirejeshe jambo hili kwa wahusika, akasema:

{وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَى أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا}

Na linapowafikia Jambo lolote lililohusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na kama wangelipeleka kwa Mtume na kwa wenye Mamlaka kati yao, wale wnaochunguza wangelilijua. Na kama si fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yenu na rehema yake mngelimfuata Shetani isipokuwa wachache wen utu.

Ninaisema kauli yangu hii, na nimawomba Mwenyezi Mungu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wa Viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kuwa Hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, asiye na mshirika yoyote, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetuMuhammad, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola wetu mswalie, mrehemu na umbariki Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila mwenye kuwafuata wao kwa wema mpaka siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu,

Hakika maana ya Serikali inapindukia shime ya mtu mmoja mmoja mwenye mipaka maalumu na kuelekea katika shime ya watu wote. Na kwa ajili hiyo jambo lake halijaenea kwa watu wote; bali linafanywa na wabobezi wanaotambua thamani ya jukumu walilopewa linalohusiana na Usalama wa Taifa, na maisha ya Watu wote na Masilahi yao. Nyenzo za Mataifa na hali yake ya kijimbo nay a kimataifa, na masuala yake a kisasa na kijamii na kiusalama na kielimu na kadhalika. Na wenye elimu, kama Mwenye kujitahidi miongoni mwa watu wa Jitihada na Mitazamo, anapojitahidi na katika Nyanja za ubobezi wake na akakosea basi ana ujira. Na iwapo atajitahidi na akapatia basi ana ujira wa aina mbili, na mana ya kwenda kinyume huelekea kwamba mwenye kujitahisi katika wasio na elimu na ubobezi katika kisichokuwa ubobezi wake, na katika yale asiokuwa nayo elimu nayo basi jitihada yake sio ya wanachuoni na wabobezi katika ubobezi wao, na katika asiyokuwa na elimu nayo, na iwapo atajitahidi na akapatia basi ana malipo ya kuthubutu kwake juu ya Hadithi a Fatwa katika mambo asiyokuwa na elimu nayo, na iwapo atajitahidi na akakosea, basi ana yeye malipo mawili na mzigo wa kosa lake, na mwingine wa kuthubutu kwake kutoa fatwa bila ya elimu; na hivyo ni kwa ajili ya hima ya Uislamu ya kuwaheshimu Wanachuoni na ubobezi wao, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ}

Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.

Na Ahlu Dhikri ni Wanachuoni Bobezi wa Elimu yoyote katika Elimu kwa mujibu wa Mwenye majukumu, na kwa hivyo, imekatazwa kuharakisha utoaji wa Fatwa bila ya Elimu au Egemeo lolote la kisheria. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا لِيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ إِنَّ اللَّهَ لا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ}

Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَذَا حَلَالٌ وَهَذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ * مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ}

Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu – mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa. Ni starehe ndogo, nao watapata adhabu chungu.

Na anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakayetolewa Fatwa bila ya kuwapo Elimu, basi madhambi yake yatakuwa kwa yule aliyemtolea Fatwa.

Maswahaba wakubwa na  Taabiina (waliokuja baada yao) walikuwa R.A, walikuwa wanaogopa kutoa Fatwa, huwenda ni kutokana na hatari yake; na tunamwona Abu Bakar Swidik R.A, anasema: Ni Mbingu gani itakayoniwekea kivuli mimi? Na ni Ardhi gani intakayonibeba mimi? Iwapo nitasema kuhusu Kitabu cha Mwenyezi Mungu bila ya Elimu?

Na Shaabiyu aliulizwa kuhusu jambo akasema: Mimi sio mzuri katika hilo, na Maswahaba wakamwambia: Tumekuonea aibu, akasema: Lakini Malaika hakuona haya aliposema:

{لَا عِلْم لَنَا إلَّا مَا عَلَّمْتنَا}

Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliotufunza wewe.

Na Abdulrahan bin Abii Laila, amesema: Nimewadiriki Maswahaba mia moja na ishirini miongoni mwa Maanswar (Maswahaba wa Madina) miongoni mwa Maswahaba wa Mtume S.A.W, mmoja wao anaulizwa suala, na analirejesha kwa huyu, na huyu analirejesha kwa huyu, mpaka linarejea kwa Swahaba wa kwanza.

Na ulinzi wa nchi kwa ujumla wake, ni jukumu la pamoja, kila mmoja kwa nafasi yake na nyenzo zake. Anasema Mtume wetu S.A.W: Nyinyi Nyote ni wachunga, na kila mmoja ataulizwa juu ya anachokichunga; Imamu ni Mchunga nae ataulizwa Kuhusu wale anaowachunga. Na Mwanaume ni mchunga kwa Watu wake nae ataulizwa Kuhusu anaowachunga. Na Mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mume wake na ataulizwa Kuhusu anaowachunga. Na mtumishi ni mchunga wa mali ya mwajiri wake na ataulizwa Kuhusu anachokichunga.

Huwenda Watu wengi wakawa wanadharau yale wanayoyazungumza au wanayoyaandika au wanayoyasambaza katika mitandao ya kijamii. Bali baadhi ya Watu wanaweza wakayaona kuwa ni sehemu moja ya burudani kwao na wala hawatambui kuwa utengenezaji wa maneno ya kuyavumisha na kuyaeneza baina ya watu ni njia mojawapo ya kubomoa inayotumiwa na Watu wa batili katika mapambano yao na Watu wa Haki. Unauona Uma kama mwili mmoja unajishuku wenyewe kwa wenyewe, na kufanyiana khiana wenyewe kwa wenyewe; na kwa ajili hiyo, anasema Mtume S.A.W: Inamtosha Mtu kusema uongo kwa kukizungumzia kila anachkisikia.

Ikiwa Mtu kuzungumzia kila anachokisikia ni aina miongoni mwa aina za uongo, anayefanya hivyo kuadhibiwa adhabu kali huko Akhera, inakuwaje kwa mwenyekuyazungumzia asiyoyaona au kuyasikia na wala hayajui, anazungumza kama uzushi upotoshaji? Na ni maneno mangapi ya uongo yanayovuma, yakawa sababu ya muhusika kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu Siku ya Kiama. Anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Mja anaweza kuzungumza neno linalomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, akawa halizingatii, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamnyanyua kwalo daraja za juu. Na kwamba Mja anaweza kuzungumza neno linalomkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambalo yeye halizingatii, akaingia kwa neno hilo Moto wa Jahanamu.

Tunayakiwa tuwe makini, tuchukue tahadhari na tupime akilini, na kutojiingiza katika mambo tusioyajua, au kufutu bila ya Elimu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuwe na msimamo na kutowafuata Waharibifu, na kupata uhakika wa Habari zote zinazotufikia ambapo anasema:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ}

Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda

Na Mtume wetu S.A.W, anasema: Kufanya Mambo kwa utulivu kunatokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kufanya Mambo haraka haraka kutokana na Shetani. Na anasema Mtume wetu S.A.W:

Kufanya mambo kwa utulivu ni katika kila kitu isipokuwa kazi ya Akhera.

Tutambue kwamba tunahitaji mno kuijua thamani ya Serikali na kuyatanguliza Masilahi Makuu ya Nchi na kuzijua hatari zinazokuzunguka na ambazo tunakusudiwa kutumbukia ndani yake kama walivyotumbukia wengine na tukapitwa na fursa na zikawaendea maadui wa Dini na Nchi yetu. Na tuendelee kuwa na msimamo tukiwa tumeungana kwa ajili ya Haki, ili tusiangukie katika vitimbi vya Maadui zetu wanaotuwinda, na tueneze hali ya kujiamini baina yetu, na tushirikiane katika kila jambo la kheri ambalo matunda yake yanarejea kwa watu wote.

Ewe Mola wetu Mlezi tunakuomba utuwafikishe katika kutekeleza Haki za Nchi yetu, na uwalinde wananchi wote na viongozi wetu na Jeshi letu la Polisi na la Ulinzi, na Uijaalie Nchi yetu tukufu amani na usalama, maisha bora na utajiri, pamoja na nchi zote Duniani.