Usamehevu Kiakida na na Kimwenendo

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ}

Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito.

 

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, aliye peke yake na wala hana mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake, anaesema: Nimetumwa kwa Dini yenye Usamehevu. Ewe Mola wetu tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata kwa wema hadi siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Mtume S.A.W, alikuja na Risala ya Kimataifa iliyoufanya Usamehevu uwepesishaji viwe Mfumo wa Maisha. Hakuna mazito yoyote katika Dini, wala hakuna Uzito wowote katika kuyabeba majukumu, hakuna shida au ugumu wowote, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ}

Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini.

 

Anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Dini ni nyepesi. Na hakuna mtu yeyote atakayefanya nzito isipokuwa humshindi. Basi ongozaneni, jongeleaneni, peaneni habari njema, saidianeni asubuhi na mchana ( mnapokuwaa safarini), na sehemu ya usiku.

Kwa hiyo, Usamehevu katika Sheria ya Uislamu sio neno linalotamkwa tu, au alama inayonyanyuliwa juu; bali ni Akida wanayoiishi Waislamu wote na wakaifanya ikawa Mfumo wao wa Maisha. Lakini pia, ni Msingi miongoni mwa misingi aliyoiamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake, watangamane kwayo, na akaijaalia ikawa sababu ya kuzipata radhi na msamaha wake pamoja na rehma zake, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا أَلا تُحِبُّونَ أَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَكُمْ}

Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni?

 

Ni kwamba tunachojitahidi ni Kuufanya Usamehevu uwe mwenendo wetu kimaisha, kwani Ulinganiaji wa Uislamu wa Usamehevu ni Ulinganiaji wa kiutendaji na kiutekelezaji. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametoa wito kwa Waja wake akiwataka wawasamehe waliowakosea na wawe wasamehevu, na wito huu umekuja katika sehemu nyingi ndani ya Qurani Tukufu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ}

Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.

 

Na Mtume S.A.W, aliutekeleza Usamehevu kivitendo akiwa na Watu. Mtume S.A.W, akawa mfano mzuri wa kuigwa kwa Uma wake na kwa Utu kwa ujumla, ambapo anasema Mtume S.A.W: Hakika mambo yalivyo, miki rehma iongozayo. Na anasema Mama wa Waumini Bi Aisha R.A: Hakuwahi Mtume S.A.W, kuchagulishwa baina ya vitu viwili isipokuwa alichagua chepesi kama hakikusababisha dhambi, na kama kisababisha dhambi, basi yeye alijiweka mbali nacho…

Na hapa kuna swali ambalo lazima kila mmoja wetu anapaswa ajiulize wazi wazi na bila kificho nalo ni kama lifuatavyo: Je? Sisi tunatekeleza Akida hii katika mienendo yetu? Na je? Tumeifanya ikawa ni Mfumo wa kutangamana baina yetu na baina yetu na Wengine wote? Usamehevu ni Mwenendo mzuri ambao lazima utekelezwe na kila mwislamu katika nyanja zote za maisha yake. Na kwa hivyo, tunaona Usamehevu baina ya mke na mume wake, nao ni Uhusiano wenye hadhi ya juu mno katika mahusiano ya Wanadamu. Na ni moja kati ya alama za utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha wazi kwamba Uhusiano wa wanandoa unajengeka kwa Mapenzi,vRehma na Mtangamano Mwema. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً}

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu.

 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَى أَن تَكْرَهُواْ شَيْئاً وَيَجْعَلَ اللّهُ فِيهِ خَيْراً كَثِـيرًا}

Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake

 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ}

Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao

 

Kwa maana ya kwamba; wanawake wana wao uzuri wa kusuhubiana nao kwa Wema na wanaume wao kama vile ambavyo wao wa anavyopaswa kuwafanyia vivyo hivyo Waume zao. Anasema Mtume S.A.W: Mbora wenu ni yule aliye Mbora kwa Watu wake wa Nyumbani, na Mimi ni Mbora wenu kwa Watu wangu wa Nyumbani. Na Mtume S.A.W, ameusia sana kuwatendea wema Wanawake, ambapo anasema S.A.W: Mume asimchukie Mke wake, na (atambue) akichukia kitu chochote kile katika tabia za mke wake atambue kwamba Mtu mwingine anaweza kukipenda.

Na Wasia wa Mwisho wa Mtume S.A.W, ulikuwa juu ya Wanawake, kabla ya kufa kwake, ambapo alisema S.A.W: Usianeni kuwatendea wema Wanawake.

Kwa hiyo, Usamehevu unatakiwa uwe mwenendo wa wanandoa wawili, na iwe Sheria ya Kibinadamu inayoyapangilia Maisha yao. Uzuri ulioje wa maneno ya Abu Dardaa-a, R.A, alipomwambia Mke wake R.A: Utakaponiona nimekasirika basi niridhishe,  na ninapokuonesha hasira zangu huwa ninaridhika, katika Mtangamano Mwema wa kibinadamu uliosimamishwa na misingi ya Uadilifu pamoja na Usamehevu.

 

Vile vile kuna Usamehevu na Jirani:  anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَى وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنْبِ}

Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia.

Wingi ulioje wa Usia wa Mtume S.A.W juu ya jirani! Anasema Mtume S.A.W: Jiburilu aliendelea kuniusia juu ya Jirani mpaka nikadhani atanirithisha.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Anayemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuiamini Siku ya Mwisho, amkirimu Jirani yake.

Na anasema Mtume S.A.W: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, haamini Mtu yoyote, Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, haamini Mtu yoyote, Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, haamini Mtu yoyote; akaulizwa: Ni Mtu gani huyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema: Mtu huyo ni yule ambaye Jirani yake hasalimiki na Shari zake.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Mbora zaidi wa Marafiki mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni yule aliye Mbora kwa mwenzake, na Jirani Mbora zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni yule Mbora wao kwa jirani yake.

Na anasema Mtume S.A.W: Muumini sio yule anaelala wakati Jirani yake aliye karibu naye ana Njaa.

Usamehevu unatakiwa vile vile uenee baina ya mtu na wafanyakazi wenzake, na katika vyuo vikuu na katika shule mbalimbali, na sehemu zingine zote. Na Qurani Tukufu imeimarisha Uhusiano baina ya Watu wote, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ}

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.

 

Mtume wetu S.A.W, alikuwa Mbora zaidi katika Watu kitabia kwa Watu wote na kwa Maswahaba wake, akawa S.A.W, anawatendea wema, anamtembelea mgonjwa wao, na anawatembelea mara kwa mara, anatoa sadaka kuwapa Mafukara wao, na kuwalipia Madeni yao na kuwatimizia haja zao, na alikuwa anawasamehe makosa yao. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّهِ لِنتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ}

Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo.

 

Usamehevu barabarani na katika vyombo vya Usafirishaji: Mtu anaweza kuudhiwa vyovyote iwavyo au kuwaudhi wengine, kwani Watu wapo wa aina nyingi. Kuna mwenye hasira, kuna mkali, na kuna msamehevu, kuna mwenye nguvu, kuna mnyonge, kuna asiyevumilika. Uzuri ulioje wa kukutana na Watu wote hao kwa Upole na Usamehevu! Na majibu ya Mtu yakawa kwa Ulaini na adabu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَعِبَادُ الرَّحْمَنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا}

Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!

 

Na Mtume wetu S.A.W, anasema: Hamtaingia Peponi mpaka muamini. Na hamtaamini mpaka mmpendane. Je nikujulisheni kitu ambacho mkikifanya mtapendana? Peaneni salamu baina yenu.

 

Vilevile ni lazima kufuata taratibu zilizowekwa barabarani na kwa ajili ya vyombo vya usafiri kama vile kuwaachia watu wazima na wanyonge na wanawake viti wakae, na kuchunga hisia za Watu na kuwa nao kirafiki. Anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Upole hauwi katika kitu chochote isipokuwa hukipendezesha, na wala hauondoshwi katika kitu chochote kile isipokuwa hukifanya kiwe kibaya.

Na miongoni mwa alama za Usamehevu ni Usamehevu wa Nafsi, kwani kutoa ni Dalili ya kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake. Na ni dalili ya mtu kutengenekewa mambo yake na kuwa na Msimamo, kwayo Muumini hujulikana, na nyoyo huwa pamoja, na kwayo mja hupata thawabu za wema Wake.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ}

Hamtoipata Pepo mpaka mtoe mnavyovipenda.

 

Kutoa na kuwapa Mafakiri na Masikini ni dalili ya Usamehevu wa Nafsi na Maadili yake Mema. Anasema Mtume wetu S.A.W: Mtoaji yuko karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, yuko karibu na Pepo, yuko karibu na Watu na yuko mbali na Moto.

 

Vile vile Usamehevu katika kuuziana na katika kudai Deni lake: Anasema Mtume wetu S.A.W: Mwenyezi Mungu Mtukufu anamrehemu mtu anaekuwa msamehevu pindi anapouza, anaponunua na anapodai alipwe Deni lake. Na kutoka kwa Al-irbaadhi bin Saariya R.A,  amesema: Nilimuuzia Mtume S.A.W, msokoto wa kamba nikamjia na kudai anilipe, nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nilipe pesa zangu thamani ya msokoto wa kamba niliyokuuzia. Akasema Mtume wetu S.A.W: Sawa, nitakulipa. Sitakulipa isipokuwa kwa dirhamu mpya zinazong’aa kwa weupe wake. Akasema yule Mtu: Mtume akanilipa kwa malipo Mazuri zaidi. Na Mtume S.A.W, aliwahi kujiwa na bedui mmoja, akamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nilipe deni langu. Mtume S.A.W, akampa ngamia aliyepevuka kiumri, na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Malipo haya ni mazuri zaidi ya bidhaa yangu. Mtume S.A.W, akasema: Hakika Uma bora ni wale walio bora katika kulipa madeni yao.

Na hakika Mtume S.A.W, aliwahimiza watu kila jambo linalopelekea Usamehevu na Wepesi na likaleta maana ya udugu wa kibinadamu na Mjongeleano baina ya watu wote, kama vile kuwasamehe madeni wale wasiojiweza au kuwapa muda zaidi. Anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakayempa muda zaidi anaemdai mwenye matatizo, au akaamua kumfutia madeni yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu atampa kivuli katika Kivuli chake. Na anasema Mtume wetu S.A.W: Mtu mmoja alikuwa anawadai Watu, akamwambia kijana wake: Utakapoenda kwa mtu ambaye mambo yake ni magumu, basi msamehe, huwenda Mwenyezi Mungu Mtukufu atetusamehe na sisi, Mtu huyo akafariki dunia na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamsamehe.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

***

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kwamba hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, aliye peke yake na wala hana mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe   Mola wetu tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata kwa wema hadi siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu.

 

Hakika miongoni wa alama zenye hadhi ya juu za Usamehevu na zilizo nyepesi pia ni maneno mazuri.

 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا}

na semeni na watu kwa wema

 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَقُلْ لِعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ}

Waambie waja wangu waseme maneno mazuri,

 

Na maneno mazuri yanakuwa kwa Watu wote, bila kujali tofauti zao za rangi, jinsia na Imani zao. Na jambo hili kama linamaananisha kitu basi litakuwa linamaanisha Ubora wa Malezi na Tabia njema

 Na imesemwa kuwa: Uzuri wa Tabia ni kitu chepesi; ni uso mkunjufu, na maneno laini na mazuri.

 Mungu Mtukufu amemwamrisha Bwana wetu Musa A.S, amsemeshe Firauni kwa maneno mazuri, pamoja na kiburi na ubishi wake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{اذْهَبَا إِلَى فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَى* فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَيِّنًا لَعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَى}

Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.

 

Tunapaswa tujiepushe na Mambo ya Upuuzi ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ}

Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,

 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا}

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa.

 

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ* تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا وَيَضْرِبُ اللَّهُ الأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ}

Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka.

 

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Mja anaweza kuzungumza neno katika yanayoridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu bila kukusudia, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamnyanyua hadhi za juu. Na hakika Mja anaweza kuzungumza neno katika yanayomchukiza Mwenyezi Mungu Mtukufu bila kukusudia na likampeleka neno hilo Motoni.

Ni wajibu vile kujiepusha na kila aina ya Maneno Machafu, kwa Kauli yake Mtume S.A.W: Hakika ya Muumini sio katika kulaani au kukashifu, au kutoa kauli zisizopendeza.

Hakika Usamehevu ni ukati wa baina ya Viwili vinavyokinzana; Ukali, na kupuuzia, vyote hivyo ni ukali ulio mbali mfumo wa Uislamu wa kati na kati, ambao unakusanya aina mbalimbali za usamehevu na urahisishaji na Huruma ambavyo humaliza aina zote za Siasa kali na kujikweza kidini, na kupindukia pamoja na kupotosha watu.

 

Tunakuomba ewe Mola wetu Mtukufu uturuzuku Usamehevu katika kauli zetu, katika vitendo vyetu, katika Mtangamano wetu na katika mambo yetu yote. Na utusuluhishie tulichosigana, na Uilinde Nchi yetu na Nchi zote Duniani.