Kuwa na Hima ya hali ya juu ndio njia pekee ya kustaarabika kwa Mataifa

Sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote anaesema katika Qurani tukufu:

{سَابِقُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ذَلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ}

Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyo wekewa walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.

 

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad Ni Mja na Mjumbe wake.  Ewe Mola Wetu tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata mpaka siku ya Mwisho.

 

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakika Dini ya Uislamu kwa Mafundisho yake yenye hadhi ya juu, unahimiza kuwa na hima ya juu, bidii, jitihada na Ujenzi, na unazuia uzembe, uvivu na uharibifu. Na haya yamekuja katika jumbe zote za Mwenyezi Mungu Mtukufu zilizotangulia, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَى * وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّى * أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى * وَأَنْ لَيْسَ لِلْإِنْسَانِ إِلَّا مَا سَعَى * وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَى * ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَى}

Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.

Na Mtume S.A.W, amekwishabainisha uzito wa kuwa na Hima ya juu, katika kauli yake S.A.W: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mkarimu na anaupenda ukarimu na Tabia zilizo njema na anachukia Tabia mbaya.

Na Bwana wetu Omar bin Khatwaab, R.A, anasema: Msiidogeshe Hima yenu, hakika mimi sijawahi kuona kinachozuia tabia njema kuliko uchache wa Hima. Na imesemwa kwamba: miongoni mwa alama za kupevuka kwa akili ni kuwa na Hima ya hali ya juu.

Anasema Abu Twayib Mutanabiy:

 

Sijawahi kuona kitu katika kasoro za Watu

     Kama upungufu wa Wawezao kukamilisha mambo

 

Kuwa na Hima ya hali ya juu hakuishii tu katika nyanja maalumu; bali ni lazima kipatikane katika kila anayoyafanya mwanadamu katika maisha yake, na katika hayo ni: Ibada, Sheria tukufu imehimiza kuharakisha na kushindana katika uwanja wa Ibada, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَسارِعُوا إِلى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّماواتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ}

Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu, asemae Kweli, amekuwa ya malipo makubwa kwa mwenye kujihangaisha na kufanya bidii katika ibada zake, akasema S.W:

{وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَى لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَئِكَ كَانَ سَعْيُهُمْ مَشْكُورًا}

Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a’mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa.

 

Na Mtume wetu S.A.W, alikuwa mtu mwenye Hima ya hali ya juu katika mambo yote ya maisha yake ikiwemo Ibada. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alimsemesha akamwambia:

{يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ * قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا * نِصْفَهُ أَوِ انْقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا * أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا * إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا} l

Ewe uliyejifunika. Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! Nusu yake, au ipunguze kidogo. Au izidishe – na soma Qur’ani kwa utaratibu na utungo. Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito.

 

Kwa hiyo, Mtume S.A.W akawa anakesha usiku mpaka miguu yake inavimba. Na alipoulizwa juu ya jambo hilo akasema S.A.W: …kwanini mimi nisiwe Mja mwenyekushukuru?

 Na wingi ulioje wa Mtume S.A.W, kuwahimiza Maswahaba wake na Uma wake juu ya Kuwa na sifa ya kipekee na Hima ya hali ya juu. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Mnapomwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mwombeni Pepo ya Firdausi; kwani hakika hiyo ni Pepo iliyo ya kati, na ya juu katika Pepo, na juu yake kuna Arshi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutoka huko inachimbuka mito ya Peponi.

Na kutoka kwa Tabia bin Kaabi R.A, amesema: Nilikuwa nikilala na Mtume S.A.W, nikamletea chombo chake cha kutawadhia na mahitaji yake, akaniambia: Omba, nikasema: Ninakuomba niwe na wewe Peponi. Akasema: (au kuna kingine kisicho hicho) Nikasema: Ni hicho hicho. Akasema: Nisaidie mimi juu ya nafsi yako kwa wingi wa kusujudu.

Na Hima ya hali ya juu katika Ibada hupelekea uzuri wa kuitekeleza ibada hiyo na kudhihirisha athari yake katika mwenendo wa mtu, na katika tabia yake. Hasemi uongo, hawi mhazini, na wala hadanganyi katika bidhaa (hapigi kunga), na hali mali za Watu kwa njia isiyo ya halali, na kwa hiyo utekelezaji wa Ibada unaenda sambamba na lengo lake, na hapo ndipo unapojitokeza unyoofu ambao ndio msingi wa Dini hoi iliyonyooka.

 

Na miongoni mwa nyanja muhimu za kuwa na Hima ya hali ya juu ni: Elimu. Mtume S.A.W, ametuamrisha tumwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu Elimu yenye manufaa ambayo manufaa yake yanarejea kwa viumbe Wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume wetu S.A.W: Mwombeni Mwenyezi Mungu Mtukufu Elimu yenye manufaa, na mjikinge kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Elimu isiyo na manufaa.

Na miongoni mwa dua zake Mtume wetu S.A.W, Ewe Mola Wangu, hakika mimi ninajikinga kwako na Elimu..

Kwa hiyo Elimu inayofaa ni silaha ya kweli inayozipa nguvu Nchi, na kwayo Mataifa husonga mbele, na hakuna taifa lolote lililosonga mbele isipokuwa kwa elimu, na hakuna taifa lolote lililochelewa kimaendeleo isipokuwa kwa kuzembea na kuchelewa kwake katika nyanja mbalimbali za elimu.

Na Maswahaba wake Mtume S.A.W, na waliwafuatia R.A, walikuwa na Hima ya hali ya juu katika kutafuta elimu, tunamwona Bwana Wetu Abu Huraira R.A, alikuwa na Hima ya hali ya juu katika kutafuta Hadithi za Mtume S.A.W. Na alikuwa akisema: sikuwa ninashughulishwa na upandaji wa miti jangwani au kuweka mikataba ya biashara sokoni, na kumwacha Mtume S.A.W, bali nilikuwa nilikuwa ninamwomba Mtume S.A.W, neno anifundishe…

Akasema Bin Omar R.A: Ewe Abu Huraira wewe ulikuwa na Mtume S.A.W, zaidi yetu na ulikuwa mjuzi zaidi yetu wa Hadithi za Mtume S.A.W. Na anasema Bwana Wetu Abdullahi bin Abas R.A: …nilikuwa ninaletewa Hadithi kutoka kwa Mtu, ninakuona akiwa anasema, ninatengeneza mto kwa kuweka nguo yangu juu ya mlango wake, na upepo unavumisha mchanga usoni mwangu, kisha anatoka na kuniona na kusema: Ewe Mtoto wa ami yake Mtume, ni kipi kilichokuleta hapa? Si ungenitumia ujumbe mimi nikakujia uliko? Na mimi ninasema: Hapana, mimi nina haki zaidi ya kukujia wewe. Kisha ninamuuliza kuhusu Hadithi.

Nae Ismail bin Yahya amesema: Nimemsikia Shafi Mola amrehemu, anasema: Nimehifadhi Qurani nikiwa mtoto wa miaka saba, na nikahifadhi Kitabu cha Hadithi kiitwacho Muwatwau nikiwa na umri wa miaka kumi, na Imamu Ahmad Mola amrehemu, alikuwa anahifadhi Hadithi laki moja. Na inasemekana pia Imamu Nawawiy alikuwa akihudhuria kwa siku darasa kumi na mbili.

Vilevile Wanachuoni Wetu wa zamani walikuwa na bidii kubwa katika ubebaji wa Amana ya Elimu katika kila nyanja zake, na wakaufikisha Ujumbe kwa Watu ukiwa kama ulivyo, na kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa ajili ya kuwanufaisha Watu wote. Wao waliyaorodhesha majina yao na Hima yao ya hali ya juu, kwa kazi yao hiyo, kwa herufi za nuru kwenye kumbukumbu ya Historia. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ}.

Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi.

 

Na katika nyanja za kuwa na Hima ya hali ya juu ni: Katika Kazi. Sheria tukufu imetangaza uzito wa kazi na kuinyanyua hadhi yake, ambapo Qurani tukufu umefungamanisha baina ya Ibada na Kazi na kujaalia ziambatane. Na katika hili anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّهِ وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيراً لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}

Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.

 

 

Na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuahidi Mtu atakaeitekeleza kazi yake ipasavyo, atakuwa na maisha mazuri Duniani na atakuwa na neema ya Makazi mazuri Siku ya Kiama.

 

 Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ}

Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.

 

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلاً}.

Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi.

 

Na hakuna kinachothibitisha zaidi utukufu wa kazi kuliko Mitume A.S, ambao wote walikuwa wanafanya kazi. Adam A.S, Ibrahim A.S, na Luti A.S, walikuwa wakulima. Nuhu A.S, alikuwa fundi seremala, na Idrissa alikuwa fundi cherehani (mshonaji wa nguo), Swalehe A.S, alikuwa mfanyabiashara, na Daudi A.S, alikuwa mhunzi.

 

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ * أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ}

Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, (tukasema): Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia. Na tukamlainishia chuma. (Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayo yatenda.

 

Kwa hiyo thamani ya Mtu hupanda juu kwa kufanya kazi, akaweza kusimamia vizuri kile anachokiweza. Kazi ni bora kuliko kuomba omba Watu. Anasema Mtume S.A.W: Ni bora Mtu akaenda kukata mzigo wa kuni na kuubeba (ili auuze) kuliko kuomba omba mtu, anaweza akampa au akamnyima.

Na haimaanishi tu kazi bali kuifanya kazi hiyo ipasavyo. Anasema Mtume wetu S.A.W: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda pindi mmoja wenu anapofanya kazi basi aitekeleze ipasavyo.

Na Mtume S.A.W, alikuwa anapupia kila mtu awe na kazi nzuri inayomnufaisha yeye na wengine. Anasema Mtume wetu S.A.W: Kila Mwislamu ana jukumu la kutoa Sadaka. Wakasema: Ewe Mtume Wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama mtu hakupata kitu cha kutoa sadaka je? Akasema: afanye kazi kwa mikono yake ili ajinufaishe yeye mwenyewe na atoe sadaka. Wakasema: Na kama hakupata je? Akasema: amsaidie mwenye shida kubwa. Wakasema: na ikiwa hakuweza kufanya hivyo je? Akasema: basi afanye mema na ajizuie na kila aina ya Shari, kwani kufanya hivyo kwake yeye ni Sadaka. Mtume S.A.W, alihimiza kwa yule aliyeshindwa kufanya kazi ajizuie kuwadhuru Watu na akakifanya kitendo hicho kuwa ni cha kulipwa thawabu kwani yeye atakuwa amewakinga Watu na shari na madhara yake.

Na miongoni mwa daraja za juu za Hima ni: Hima ya kusaida Jamii na kumsaidia mnyonge na kumwokoa mwenye huzuni ya kupoteza mali na kukidhi mahitaji ya wenye kuhitaji, na Ushujaa wa kupambana vitani na Utukufu wa nafsi. Mtu mmoja alienda kwa Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume Wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni nani anapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu? Na matendo yepi yanayompendeza zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu? Mtume S.A.W, akasema: Anaependwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni yule anaewanufaisha Watu, na katika matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuingiza furaha mwislamu au kumtatulia jambo zito, au kumlipia deni, au kumwondoshea njaa (kumlisha chakula), na ni bora kwangu mimi kutembea na ndugu yangu katika kumtatulia jambo lake kuliko kukaa itikafu katika Msikiti huu. Kwa maana ya msikiti wa Madina kwa muda wa mwezi mmoja. Na yoyote atakayeizuia hasira yake basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri uchi wake. Na mtu yeyote atakayezuia ghadhabu zake na hata kama angelitaka kuitumia ghadhabu yake hiyo alikuwa na uwezo wa kuitumia, Mwenyezi Mungu Mtukufu ataujaza moyo wake amani Siku ya Kiama. Na mtu yeyote atakaye tembea na nduguye katika kumtatulia jambo lake mpaka akamtatulia, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ataiweka miguu yake katika Njia ya Swiratwa Siku ya Kiama ambayo miguu itatoka kwenye njia hiyo.

 

Na ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. NaNa ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad Ni Mja na Mjumbe wake.  Ewe Mola Wetu tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata mpaka siku ya Mwisho

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika kwa ajili ya nyanja ambazo tunapaswa kushindania sisi sote na tuwe na hima ya hali ya juu: Ni kuitumikia Nchi. Utumishi kwa ajili ya Nchi ni katika Imani; na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tushindane katika uwanja wa heri na Manufaa ambayo athari zake zinarejea kwa Taifa, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ إِلَى اللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ}

Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.

 

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu waja wake wanakimbilia kuwasaidia Watu mambo mazuri, na anabainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba heri hiyo humnufaisha muhusika Duniani na Akhera.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّهُمْ كانُوا يُسارِعُونَ فِي الْخَيْراتِ وَيَدْعُونَنا رَغَباً وَرَهَبًا وَكانُوا لَنا خاشِعِينَ}

Hakika wao walikuwa wepesi wa kutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea.

 

Na kwa kuwa na Hima ya hali ya juu, na utashi wa kuwanufaisha Watu, na kuwa na ukamilifu wa Imani juu ya fadhila zake Mwenyezi Mungu Mtukufu na Taufiki yake.

Na katika kuwa na Hima ya juu: Ni Hima ya kuzijenga Nchi na kubeba majukumu ya kijamii na kushindana katika mambo ya wema; kama vile kukarabati misikiti, kujenga shule, kununua vifaa vya mahospitalini na kuwatibu wagonjwa, yote haya na mengine kama haya ni Sadaka endelevu, ambapo anasema Mtume wetu S.A.W: Mambo saba ujira wa Mja utaendelea kutolewa baada ya kufa kwake akiwa kaburini kwake: Mtu atakaefundisha elimu yoyote, au akazibua mto,  au akachimba kisima, au akapanda mtende, au akajenga Msikiti au akarithisha Qurani, au akaacha Mtoto anayemwombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya kufa kwake.

 

 ni wa kuitumikia Nchi yetu ambayo sote tunaishi ndani yake, na heri inarejea kwa wananchi wake wote, na tukayafikia hayo kwa mshikamano na umoja Wetu, kwa Mzinduko na Kuhurumiana na kunyoosha mkono wa kumsaidia kila mtu kwani nchi ni ya kwetu sote, na inasonga mbele ikiwa na sisi sote , na sisi sio Watu wenye utashi duni au nguvu duni au juhudi duni kuliko wengine, kwani Sisi ni Watu wenye Ustaarabu , Asili na Historia. Na hapana budi tutambue kwamba kupatikana kwa maendeleo na kuwa juu kunahitaji kupambana na magumu yote na kwa hiyo ni kujikana kwa ajili ya kuwatumia wengine, kwani Maadili mema hupatikana kwa tabu, na masilahi na kheri hazifikiwi isipokuwa kwa juhudi na uzito mkubwa. Anasema Abu Tamaam katika kauli yake:

 

Nimeiangalia raha kuu sijaiona

inapatikana ila kwa njia ngumu

 

Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba uturuzuku Hima za hali ya juu tutakazozitupatia katika Ushindani, Fadhila, Kusonga mbele, na Kuimarika katika mambo yanayotufaa Duniani na Akhera, na uilinde nchi yetu na Nchi zote Duniani.