Matunda ya Imani

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote anaesema katika Qurani tukufu:

{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُمْ بِإِيمَانِهِمْ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ}

Hakika walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itakuwa inapita mito kati yao katika Mabustani yenye neema.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume wetu Muhammad Ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na jamaa zake na Maswahaba wake na kila mwenyekuwafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Na baada ya utangulizi huo.

Hakika Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake ni kujaalia kile tendo jema analolifanya mja kuwa na faida yake nzuri. Na katika matendo bora yenye kumnufaisha mtu au jamii ni kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Mtume wetu S.A.W, amebainisha ukweli wa Imani ambayo inatakiwa iwepo katika moyo wa Muumini, na hilo lilitokea pale Jiburilu A.S, alipomuuliza Mtume S.A.W, kuhusu Imani akasema: … ni kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Kasari Kheri na Shari yake. Akasema Jiburilu: Umesema kweli.

Kwa hiyo, Imani sio maneno matupu yatamkwayo kwa ulimi, bali ni Itikadi ndani ya Moyo wa Mja, na kukiri kwa ulimi na kutenda kwa viungo vya mwili mzima. Kwa hiyo Imani ya kweli ni ile iliyotulizana Moyoni na inasadikiwa na vitendo kwa kufuata Amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujiepusha na Makatazo yake.

Na imamu Hasanil Basriy Mola amrehemu, alipoulizwa: Je wewe ni Muumini? Akasema: Imani iko ya aina mbili; kama wewe unaniulizia Kumuamini  Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake na Pepo, na Kufufuliwa, na Kuhesabiwa, mimi ninaamini hivyo, na ikiwa unaniuliza kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anaposema:

{إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَاناً وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ * الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ * أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً}

Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi. 

Basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu sijui kama mimi ni miongoni mwao au hapana.

Kwa hiyo Imani ya kweli ni ile iliyojaa Moyoni na kuulizana humo na athari yake yenye nguvu ikaonekana moyoni na akilini, na kwa Mtu mmoja mmoja na kwa Jamii nzima. Na miongoni mwa matunda yake ni kwamba Imani hurithisha Tabia njema, kwani Imani na Amana viko pamoja na havitengani.

Anasema Mtume wetu S.A.W: Asiyekuwa na Imani haaminiki na hana Dini mtu aliyetekeleza ahadi zake.

 يقول الحق سبحانه: {وَمَن يُؤْمِن بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ}

Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. 

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Linashangaza Jambo la Muumini; hakika jambo lake lote ni Kheri tupu na haiwi hivyo kwa Mtu yoyote isipokuwa kwa Muumini, anapofikwa na jambo la kufurahisha hushukuru, na anapofikwa na jambo la kuchukiza huvumilia ikawa kufanya hivyo ni Kheri kwake.

Na miongoni mwake: Hakika Imani humlinda mwenye nayo kutokana na kufanya mambo yanayoangamiza. Anasema Mtume wetu S.A.W: Mzinifu hazini wakati anazini hali ya kuwa muumini. Na wala hanywi pombe wakati anakunywa pombe hali ya kuwa muumini. Na wala haibi wakati anaiba hali ya kuwa muumini. Na wala hanyang’anyi kitu cha kunyang’anywa, Watu wakamnyanyulia macho kwa kitu hicho hicho wakati anakipora hali ya kuwa yeye ni muumini.

Vile vile muumini wa kweli huiepusha nafsi yake na kila kitu kinachowaudhi Watu kihisia kama vile kuwafanyia masihara au kuwatania na kuwadhania vibaya. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَى أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَى أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ  وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ}

Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu. 

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ}

Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. 

Kwa hiyo Imani ya kweli hurithisha Amani ya Moyo. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ}

Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?

 

Na katika matunda ya Imani: Ni Uungaji mkono kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Ushindi: Kwani Imani ya kweli humfanya Mja awe pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَأَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ}

Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini. 

Na Kuwa pamoja kunakokusudiwa hapa ni Nusura Usaidizi na Uungaji mkono. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ } 

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{ إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ}

Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi. 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu.

{وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ}

Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini. 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُواْ لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً وَقَالُواْ حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ * فَانقَلَبُواْ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللّهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُواْ رِضْوَانَ اللّهِ وَاللّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ}

Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa. Basi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. 

Na katika matunda ya Imani ni Mwenyezi Mungu Mtukufu kupandikiza upendo wa Mja katika mtoto za Viumbe, mpaka ukawaona Waumini wa Kweli wakihurumiana na Kuwa wapole wao kwa wao na wanajiongezea na bila kuogopana. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَنُ وُدًّا}

Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi. 

Mja anapompokea Mola Wake Mlezi kwa Moyo wa Muumini mkweli, Mola Wake Mlezi na Mtukufu huzipokea nyoyo za Waumini. Katika Hadithi Qudsiy anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Mtukufu anapompenda mja, humwita Jiburilu na kumwambia: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda fulani basi umpende, na Jiburilu humpenda, na akanadi kwa Waja wa Mbinguni: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda fulani, basi nanyi mpendeni. Basi Waja wa Mbinguni nao wakampenda. Kisha anaandikiwa yeye Kukubalika hapa hapa Ardhini.

Na katika Hadithi Qudsiy nyingine, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mja Wangu anaendelea kujikurubisha kwangu kwa sala za Sunna mpaka nikampenda, na ninapompenda Mimi huwa masikio anayosikia kwayo na macho yake anayoona kwayo, na mkono anaoutumia na mguu anaoutembelea na kama angeniuliza kitu chochote ningempa na kama angeliniomba nimkinge na mabaya ningemkinga.

Na miongoni mwa Faida, ni kwamba Imani ni sababu ya kuondoshewa matatizo na balaa pamoja na ugumu wowote. Anasema Mtume wetu S.A.W: Je nikujulisheni pindi mmoja wenu anapofikwa na janga au tatizo lolote miongoni mwa matatizo ya Dunia aombe na aombe kwayo na Mwenyezi Mungu Mtukufu atamwondoshea matatizo hayo? Akaambiwa: ndio. Akaisoma dua ya Dhu Nuun:

{لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ}

Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. 

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ وَكَذَلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ}

Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini. 

Na hayo ni kwa Waumini wote kwa ujumla.

Ninaisema kauli yangu hoi na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na nyinyi. 

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume wetu Muhammad Ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata mpaka Siku ya Malipo.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika miongoni mwa Matunda mazuri zaidi ya kuwa na Imani, ni kwamba Imani huleta Usalama na Amani Kijamii. Muumini wa kweli anapokuwa na Imani ya kweli moyoni mwake huwa chanzo cha Usalama, Matumaini na Utulivu. Na Watu wanasalimika wao na roho zao na mali zao. Anasema Mtume wetu S.A.W: Mwislamu ni yule ambaye Waislamu wamesalimika na Ulimi na Mkono wake, na Muumini wa kweli ni yule anayeaminiwa na Watu kwa mali na heshima zao.   

Kwa hiyo, sio katika Maadili ya Muumini kuwatisha Waumini au kuwafanyia uadui, hata kama wangelikuwa sio Waislamu. Anasema Mtume wetu S.A.W: Mtu yoyote atakayemuua mtu aliye chini ya mikataba nasi, basi hatainusa harufu ya Pepo, na hakika harufu ya Pepo inapatikana umbali wa miaka arubaini.

Na Mtume wetu S.A.W, ameweka wazi kwa kuukana ukamilifu wa Imani kwa yule anayemuudhi jirani yake au anayelala hali ya kuwa jirani yake ana njaa na yeye anajua kuwa jirani yake ana njaa, akasema S.A.W: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hawi muumini wa kweli, Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hawi muumini wa kweli, Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hawi muumini wa kweli. Ikasema: ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Akasema: Ni yule ambaye Jirani yake hasalimiki na Shari zake.

Na anasema Mtume wetu S.A.W: Atakuwa hajaniamini Mimi yule atakaelala hali ya kuwa ameshiba na jirani yake ana njaa, na yuko karibu yake na yeye anajua kuwa jirani yake ana njaa.

Kwa hiyo, Imani ya kweli ni ile inayofanywa muhusika awe mtu wa kufanya mema yenye kheri nyingi na kuwasaidia wengine, na Imani ya kweli ndiyo inayo nyoosha maadili ya Mtu mwenye Imani hiyo na athari zake kuonekana katika Mwenendo wake na vitendo vyake vyote na mihangaiko yake yote ya Duniani, na jinsi anavyoshirikiana na viumbe wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kuwaonea huruma Watu, Wanyama na Vitu kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَى حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا * إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنْكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا}. 

Anasema msemaji:

Imani inapopotea basi hakuna usalama,

                                 na hakuna Dunia kwa asiyeihuisha Dini

Na mwenyekuridhika na maisha bila ya Dini

                           Basi ameyafanya maangamizi yawe mwenza. 

Na hakika zawadi iliyo bora zaidi ya kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu ni malipo makubwa na Pepo, Siku ya Mwisho ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia waja wake waliomwamini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 { إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ}

Hakika walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itakuwa inapita mito kati yao katika Mabustani yenye neema. 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ}

Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake… 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ}

Na wale walio amini na wakatenda mema, hao ndio watu wa Peponi, humo watadumu. 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا}

Hakika wale walio amini na wakatenda mema – hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema. 

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا * خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا}

Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. Watadumu humo; hawatataka kuondoka. 

Na katika Hadithi Qudsiy, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Nimewaandalia waja Wangu wema kile ambacho macho hayajawahi kukiona, wala masikio hayajawahi kukisikia, na wala hakijawahi kufikirika katika nafsi ya mwanadamu, kisha Mtume S.A.W, akasoma:

{ فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ }

Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho – ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda. 

Tunapaswa sisi tuwe na uhakika wa Imani kiitikadi, kivitendo, na kwa kauli, na kupelekea kuenea kwa hali ya Kuhurumiana, kushirikiana, Kuwa Wakweli, kuwa na Haya, Kuishi kwa furaha, Kutosheka, na kujiepusha na uongo, udanganyifu, Hiana, Kusengenya, Umbea, Uzinzi, Dhuluma, na kushambulia heshima za Watu, na tunapaswa kuzilinda heshima za Nafsi zetu, na mali kuzipa haki yake, na Mataifa kuyapa fadhila na hadhi yake. 

Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, tunakuomba uipendezeshe Imani katika nyoyo zetu, na usifanye nyoyo zetu ziuchukie ukafiri, Ufuska, na Uasi, na utujaalie tuwe ni wenye kuongoka, uzilinde Nchi zetu na Nchi zote Duniani.