Maana ya Shahada na daraja za Mashahidi

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَالشُّهَدَاءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ}.

na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao.

Na ninashuhudia ya kwamba hakuna mungu mwingine yoyote anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia ya kwamba Bwana Wetu na Mtume Wetu Muhammed ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu tunakuomba umswalie umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila atakayewafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.

Na baada ya Utangulizi huu:

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana waja aliyowachagua na kuwatengea Shahada, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنْكُمْ شُهَدَاءَ}

ili Mwenyezi Mungu awapambanue walio amini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi.

Na kutokana na utukufu wa jina la Shahada, basi maana zake zimekuwa nyingi, wao ni Mashahidi; kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu na Malaika wake A.S, wamewashuhudia wao kwa Pepo, na kwamba wao wako hai kwa Mola wao wanaendelea kuruzukiwa na wanashuhudia yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu katika neema, na ni wenye kuushuhudia ukweli wa ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwao, na maana nyingine nzuri za Shahidi na Kufa Shahidi ambazo zinaliongezea Utukufu na cheo, zinabainisha nafasi ya Mashahidi kwa Mola wao Mlezi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 }وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَلَنْ يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ  * سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ * وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ{ .

Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a’mali zao. Atawaongoza na awatengezee hali yao Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajulisha.

Na hakuna jambo linalomfanya mwanadamu awe na matarajio zaidi ya rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko Mtu kuitoa roho yake kwa ajili ya Nchi yake ambayo aliitetea na akafa kwa ajili hiyo. Atapata malipo ya juu ya Mashahidi nayo ni biashara isiyoharibika, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِنَّ اللهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الجَنَّةَ}

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo.

Kwa hiyo nafasi ya Ushahidi ni katika nafasi za juu zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na kufa Shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna madaraja yake; na daraja la juu zaidi ni: Kufa Shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kupambana na Adui; kwa ajili ya ulinzi wa Nchi na kwa kutafuta fadhila zake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Hakuna kilichobora zaidi kuliko matone mawili na athari mbili;  tone la machozi kwa ajili ya kumwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na tone la damu inayomwagwa katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na athari mbili; ni athari katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na athari katika faradhi Miongoni mwa faradhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 Kuna aina za Shahada ambazo hazikadiriwi kwa thamani yake ilivyo juu; na miongoni mwake ni: Kila aliyekufa shahidi katika Ulinzi wa Nchi yake au chochote katika mali za Nchi hiyo, au kwa sababu ya kazi yake ya kuiinua nchi tu yake; kama vile: askari polisi ambaye analinda misikiti na anawalinda watalii wanaokuja kuitembelea Nchi yake na yule anayeyalinda mabaki ya kale na kuyahifadhi yasiharibiwe, na akafa Shahidi kwa sababu nia yake safi katika kazi yake na kupupia kwake katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi zaidi na kila mwenye kufanya kama wafanyavyo hao basi atakuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile mfanyakazi wa serikalini ambaye Shime yake kubwa ni kuzilinda mali za umma, na akafanya akiwa katika Kazi hiyo.

 Vilevile Mtu atakayefariki dunia kwa sababu ya kujilinda yeye mwenyewe au kumlinda mtu mwingine, au kwa kuilinda heshima yake au ya mtu mwingine, au kwa kuilinda mali yake au mali ya Mtu mwingine basi huyu atakuwa amekufa Shahidi. Anasema Mtume S.A.W: Mtu yoyote atakayeuawa kwa sababu ya kuilinda mali yake basi ni Shahidi, na atakayeuawa kwa ajili ya kulinda damu yake basi atakuwa Shahidi, na atakayeuawa kwa ajili ya Dini yake basi mtu huyo ni shahidi, na atakayeuawa kwa ajili ya Watu wake basi huyo ni Shahidi. Kwa hiyo Watu wote hawa wanalinda Nchi yao na Mali zake, na wanazilinda mali zao, Nafsi zao, Heshima zao ambazo Uislamu umeharamisha kushambuliwa, na ukaamrisha kulindwa na kuhifadhiwa. Anasema Mtume S.A.W: Kila mwislamu kwa mwislamu menzake ni Haramu: Damu yake, Mali yake, na heshima yake.

Kwani Shahada ni Tuzo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Viumbe walio bora zaidi baada ya Mitume na Manabii, kwani wao wako katika daraja bora zaidi Siku ya Malipo. Na miongoni mwa Matunda ya Shahada: ni kwamba Mashahidi hawahisi Mauti na Ukali wake. Anasema Mtume Wetu S.A.W: Shahidi hahisi chochote wakati wa kufa kwake isipokuwa ni kama anavyohisi mtu aliyefinywa. Na Mashahidi wao husalimika na adhabu ya kaburini na fitina yake. Kuna Mtu mmoja alimwambia Mtume S.A.W: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikoje hali ya Waumini wanofitinishwa makaburini mwao isipokuwa Shahidi? Akasema Mtume S.A.W: umeremetaji wa mapanga unamtosha kichwani mwake. Na wala matendo yao mema hayakatiki milele: Anasema Mtume Wetu S.A.W: Kila maiti hupigwa mihuri katika matendo yake isipokuwa yule aliyefia vitani katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika yeye matendo yake mema yanaendelea kukuzwa mpaka siku ya Kiama, na ataepushwa na fitna ya Kaburini na Watu hawa wana Malipo makubwa mno na watapewa kila wakitakacho kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwingi wa kutoa. Kwa hiyo Shahidi Husamehewa pale pale mwanzo wa tone la damu yake linapomwagika na huoneshwa Makao yake ya Peponi, na huepushwa na adhabu ya Kaburini na huwekwa mbali na Mafadhaiko Mkubwa.

  Vilevile Shahidi hufufuliwa siku ya Kiama akiwa ni mwenye kuheshimika akitoa harufu ya miski mwilini mwake. Anasema Mtume S.A.W: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye nafsi yako iko mikononi mwake hajeruhiwi Mtu yoyote miongoni mwenu katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu – na Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua aliyejeruhiwa vitani katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu – isipokuwa Mtu huyu huja Siku ya Kiama na rangi yake ikiwa ni rangi ya Damu na harufu ya Miski.

Ninaisema kauli yangu hii na ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu anisamehe mimi na akusameheni nyinyi.

* * *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote na rehma na amani zimfikie Mtume wa mwisho katika Mitume na Manabii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; Bwana Wetu Muhammad na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na watakaowafuata.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika Mashahidi wema wataendelea kudumu katika kumbukumbu za umma; kama ruwaza ya kujitolea, ushupavu pamoja na utukufu na nguvu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaka kuwapa Maisha ya Kweli ya Milele yasiyo na kifani, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ*فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِمْ مِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ * يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ}

Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.

Na anasema Mtume Wetu S.A.W: Roho zao ziko katika midomo ya ndege wa kijana walio ndani ya Pepo, wana viota vyao vilivyotundikwa katika Arshi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndege hao wanaenda popote watakapo ndani ya Pepo kisha wanarejea katika viota vyao, na Mola wao anawaangalia kisha anasema: Je kuna kitu chochote mnachokitamani? Watasema: Tutamani kitu gani sisi Wakati twaenda popote tutakapo ndani ya Pepo? Atawauliza hivyo hivyo mara tatu, na wanapoona hawataachwa bila ya kuulizwa, watasema: Ewe Mola Wetu Mlezi tunataka uturejeshee roho zetu katika miili yetu ili tuuawe tena katika njia yako. Na anapoona kuwa wao hawana haja yoyote basi huachwa.

Ni kwamba atakayemwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa Shahidi kwa Ukweli na nia safi basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamfikisha katika daraja hilo. Na anasema Mtume wetu S.A.W: Mtu yoyote atakayemwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Shahada kwa ukweli na Usafi wa nia basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamfikisha katika daraja hilo la Mashahidi, hata kama Mtu huyu atafia kitandani.

Kwa hiyo mtu yeyote atakaye kuwa na shauku kubwa ya kuilinda Dini na Nchi yake pamoja na kulinda Mali za umma na akafia katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu basi yeye ni Shahidi.

Kongole nyingi kwa wale aliyowachagua Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya kuwa Mashahidi. Na amewakirimu kwa kuwa karibu na Manabii, Wasema kweli na Wema, na akawaneemesha kwa ukaribu huu, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا} .

Na wenye kumt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!

Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba uwarehemu Mashahidi Wetu, na Uilinde Nchi yetu na Nchi zote za Duniani. Amin.