Wito wa Manabii na Mitume katika urekebishaji kwa mtazamo wa kurani tukufu
12 Rabiu Akhar 1437H. 22 Januari 2016A.

awkaf-

 Kwanza: Vipengele

 1. Uisilamu ni dini ya wema na marekebisho
 2. mifano ya ulinganio wa Manabii na mitume katika kurekebisha kwa kupitia Kurani Tukufu
 3. Umuhimu wa kuzirekebisha nafsi zetu kwanza.
 4. Athari ya marekebisho kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii
 5. Madhara ya kuacha kujirekebisha.

Pili: Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika} [Al anaam; 48]
 2. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kwa kupitia ulimi wa Nabii Shuaib ( Rehema na amani zimshukie juu yake) {Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayo kukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea} [Hud; 88]
 3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kwa kupitia ulimi wa Nabii Shuaib ( Rehema na amani zimshukie juu yake) { Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.Na pimeni kwa haki iliyo nyooka; 183. Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi} [Ashuaraa; 181-183]
 4. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema.} [Alaaraf; 56]
 5. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu} [Al aaraf; 142]
 6. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilin} [Al anaam; 151]
 7. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema } [Hud; 117]
 8. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Na Mola wako Mlezi haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu awasomee Ishara zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhaalimu.} [Al qasas; 59]
 9. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi.} [Hud; 61]
 10. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa} [Nisaa; 114]
 11. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema {Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini} [Al anfaal; 1]

Dalili kwa hadithi za Mtume ( Rehema na amani zimshukie juu yake)

 Kutoka kwa Zayd Bin Milha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika ya mtume ( Rehema na amani zimshukie juu yake) amesema: (… hakika ya dini imeanza ngeni na itarudi hali ya kuwa ni ngeni, basi uzuri ulioje kwa wageni (nao ni) ambao wanarekebisha yale waliyoyaharibu watu baada yangu katika mwenendo wangu (sunna zangu). (Tirmidhiy)

 1. Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake), “Je nikuelezeni lililo bora kuliko thawabu za kufunga na s;a na sadaka? Wakasema: “Ndio, akasema, kuwarekebisha jamaa , kwani kuharibika kwa jamaaa ni kuifuta dini miongoni mwa watu . (Tirmidhy)
 2. kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akisema: “ewe Mola nirekebishie dini yangu ambayo ni hifadhi ya mambo yangu, na unirekebishie dunia yangu ambayo ni maisha yangu, na unirekebishie akhera yangu ambayo ni mareleo yangu, na nifanyie maisha kuwa na kila la kheri, na nifanyie umauti wangu yawe ni starehe kwa kila ovu.” (Muslim).
 3. kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema; amesema mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) kila kiungo cha mwanadamu kina sadaka, kila siku ichomozayo jua, akipatanisha kati ya watu waili ni sadaka, kumsaidia mtu katika kumpandisha kipando cha mnyama wake ni sadaka au kumsaidia mtu kupandisha mzigo wake juu ya mnyama ni sadaka,  neno zuri ni sadaka, na kila hatua apigayo kwenda kusali ni sadaka, kuondoa uchafu njiani ni sadaka.” (Bukhari na Muslim)
 4. Kutoka kwa Ubada Bin Umayr Bin Auf, amesema, Abu Ayubu (Mwenyezi Mungu amwie radhi) aliniambia: Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliniambia ewe Aba Ayubu, je nikujuulishe sadaka ambayo Mwenyezi Mungu na mtume wake wanaipenda? Suluhisha kati ya watu wakikasirikiana na kuharibiana.” (Muujam kabiir, Twabarani)
 5. Kutoka kwa Anas Bina Malik amesema: amesema mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “ iwapo kiama kitasimama na kwenye mkono wa mmoja wenu ana mbegu basi akiweza kuipanda na aipande.” (Bukhari)

Tatu: Maudhui

 Miongoni mwa maadili ya uisilamu ambayo dini yetu imehimiza na kulingania sana ni maadili ya wema na usuluhishaji (urekebishaji). Kwani ni tabia njema ambayo nafsi ya mtu hupenda na kuitamani. Ni maadili ambayo kila mtu inapasa awe nayo kwa ajili ya kuimarisha ulimwengu. Na ni kitu kitakiwacho katika sheria kwa kuwa kinaondosha sababu za ufisadi na mipasuko, huharakisha uwepo wa ukaribu kati ya watu kwa lengo la  kuleta usawa wa hali zao ndani ya maisha.

 Hapana shaka kuwa wema na usuluhishaji ni upeo utakiwao kwa waja katika ibada zao na katika kazi zao, bila ya wema ibada haikubaliki, kwa hivyo,  hakuna budi kwa mwanadamu awe mwema katika nafsi yake kimatendo na kimaneno mwenye kusuluhisha matatizo ya wengine na kutenda kwa ajili ya kuwarekebisha.

Na mwenye kuzingatia aya za Kurani Tukufu ataona kuwa zimeweka mkazo mkubwa sana katika suala hili – la maadili ya urekebishaji-. Neno kurekebisha limetajwa ndani ya Kurani Tukufu karibuni mara mia moja na sabini, n kila kinapotajwa kitu kwa wingi huwa ni dalili ya  umuhimu wake na ukubwa na nafasi yake. Hivyo neno hili (urekebishaji – usuluhishaji) limkuja kwa maana tafauti na katika mana zote hizi inajulisha kuwa uisilamu ina lengo kusawaziha wanadamu katika itikadi zao, ibada zao, matendo yao na nyanja nyengine za maisha yao.

Kurani Tukufu imeweka sambamba kati ya imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kurekebisha – kusuluhisha, katika aya nyingi, kama ni ishara ya mja kuwa na imani ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema {Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika} [Al anaam; 48] na amesema Mwenyezi Mungu {Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini} [Al anfaal;1]

Vile vile Kurani Tukufu imeweka sambamba kati ya uchaji Mungu na kurekebisha – kusuluhisha, Mwenyezi Mungu amesema {basi watakao mchamngu na wakatengenea haitakuwa khofu kwao, wala hawatahuzunika} [Al aaraf; 35]. Na pia kufungamanisha kati ya kutubu na kurekebisha – kusuluhisha akasema Mwenyezi Mungu { Ila wale walio tubu na wakatengeneza na wakabainisha,} [Al baqara; 160]. Na pia akasema { Na wakitubia wakatengenea }[Anisaa; 16]. Na akasema pia { Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu} [Anuur; 5]. Hivyo basi, kurekebisha – kusuluhisha ni matunda ya imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na uchaji na ni toba ya kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote.

Na Kurani Tukufu imependezesha kurekebisha – kusuluhisha kwa kuwa kuna malipo makubwa, Mwenyezi Mungu anasema { Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa} [Anisaa; 114].

Na tukifuatilia habari za manabii na mitume pamoja na watu wao tutaona kuwa wametumwa kwa lengo la kurekebisha yale waliyoyaharibu watu katika dunia. Na kwa ajili hiyo ujumbe wa kila nabii ulikuwa ni mmoja, nao ni kurekebisha ulimwengu kutokana na maasi na magonjwa ambayo yameenea kati yao, na kila mtume akapelekwa kwa watu wake ili kuondoa ufisadi ambao umeenea katika zama zake, Mwenyezi Mungu akawatuma kwa waja wake ili wawe wabashiria mema na waonyaji wa itikadi na sheria pamoja na maadili ya kuisawazisha nafsi na kuiepusha na uchafu wa ushirikina. Mwenyezi Mungu anasema {Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.} [Al anbiya; 25] na wito wao mitume umekuja kwa ajili ya kuwarekebisha waja duniani ili wakapate radhi za Mola wao huko akhera.

Mfano sayidna Nuh (rehma na amani zimshukie juu yake) hakika aliwalingania watu wake kwa ajili ya kuwarekebisha ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu ili wapate kumuabudu Yeye (Mwenyezi Mungu) na wasimshirikishe na chochote na waachane na ibada ya masanamu ambayo hayadhuru wala hayanufaishi, Mwenyezi Mungu anasema { Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa’ wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra 24. Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.} [Nuh; 23-24]. Na akawa anawapenezeshea katika kujirekebisha ili wapate riziki nyingi, na Mwenyezi Mungu awaneemeshe kwa mali na watoto. Mwenyezi Mungu anasema {Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. 11. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. 12. Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito. 13. Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?} [Nuh;10-13]

Na mfano mwengine ni nabii Shuaibu (rehma na amani zimshukie juu yake) anatibu ufisadi wa itikadi na kila lililoambatana na uharibifu wa uchumi kwa watu wake, akawa anawalingania waache kupunguza vipimo na mizani, na tabia hii mbaya ilikuwa imeenea sana kati ya watu wake, akaja kuwalingania katika marekebisho ya kuhifadhi haki ya muuzaji na mnunuzi. Mwenyezi Mungu anasema kwa ulimi wa nabii Shuaib (rehma na amani zimshukie juu yake) { Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua’ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni. 85. Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwakhini watu vitu vyao; wala msieneze uovu katika nchi mkafanya uharibifu.}  [Hud; 84-85]. Kisha akawawekea wazi kuwa lengo la ulinganio wake ni kurekebisha akasema { Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea.} [Hud;88]. Na katika sehemu nyengine anasema kuwa dhumuni ni kurekebisha tabia mbovu ya watu ya kupunguza mizani na vipimo akawa anawaambia {Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. 182. Na pimeni kwa haki iliyo nyooka; 183. Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisad.} [Ashuaraa; 181-183].

Na tuzingatie kitu muhimu sana pale Sayidna Shuaib (rehma na amani zimshukie juu yake) aliposema wakati anawalingania watu wake {Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea} [Hud; 88]. Hapa amebainisha kuwa pana dhumuni kubwa ambalo hapana budi kuchungwa kwa kila mwenye kutaka kurekebisha, nalo ni kufanya marekebisho kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee.

Nayo marekebisho hayahitaji masilahi na wala mapendekezo ya mtu binafsi, ni marekebisho yenye kurekjelea manufaa yake kwa wana jamii wote na kwa kila mtu.

Mfano mwengine ni Nabii Saleh (rehma na amani zimshukie juu yake) anawaita watu wake kwa kusema {Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit’iini mimi. 151. Wala msit’ii amri za walio pindukia mipaka, 152. Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi} [Ashuaraa 150-152]

Na wakati sayidna Mussa (rehma na amani zimshukie juu yake) alipomachilia madaraka mdogo wake sayidna Harun (rehma na amani zimshukie juu yake) juu ya watu wake alimuusia kuwarekebisha na kuacha kufuata njia za waharibifu. Mwenyezi Mungu amesema {Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.}[Al aaraf 142].

Kisha akaja mtume wa waisilamu (rehma na amani zimshukie juu yake) kukamilisha marekebisho katika nyanja zote za maisha ya kidunia, kijamii kiuchumi na kisiasa ambayo hata watume waliomtangulia walilingania pia. Na kwa kutazama kwa undani kabisa kuhusu maisha yake tutaona kuwa mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ametengeneza tamaduni za kiisilamu zenye kushikamana na maadili na tabia. Baada ya kuwa jamii ilikuwa imejaa uharibifu wa kitabia kama uzinifu, wizi, mauaji, riba, kula mali za watu kwa dhuluma na kula mali za mayatima na mengineyo katika maovu na mambo ya kuchukiza. Lakini mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliyakabili haya yote kwa mfumo wa kuyarekebisha, na wito wake ukawa ni wito wa urekebishaji wa mtu na jamii. Mwenyezi Mungu anasema {Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.}[Al anfaal 24]. Na kwa upande wa dini, ulinganio wake umekuja kwa kuirekebisha nafsi kupitia dini, akaweka wazi ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na hana mshirika, na akasimamisha dalili za kumpwekesha. Na pia kwa upande wa kurekebisha tabia alilingania kuwa na tabii njema ambayo ndio chimbuko la ulinganiaji. Imepokewa kutoka kwa Al bayhaqi (Mwenyezi Mungu amwie radhi) katika kitabu chake kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ hakika mimi nimetumwa kuja kukamilisha tabia njema.”

 Na kama ambavyo mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alilingania katika misingi ya maadili mema ya kiutu ambayo kwayo jamii hutengenea, na huhifadhi umoja wake na nguvu zake pia mshikamano wake kwa ajili ya kushi maisha yaliyo salama na mazuri, yasiyo na machafuko wala mipasuko wala fujo na matendo ya kigaidi kinyume na tuonavyo hivi sasa kuhusu mambo ya  uharibifu, mauaji na ubomoaji.

Na katika maadili ambayo sheria ya mbinguni imekusaya kuhusu urekebishaji ni uadilifu, usamehevu, kutelekeza ahadi, kutimiza amana, ukweli katika maneno na matendo, kuwafanyia wema wazazi wawili, kuacha mali ya mayatima, kuchunga haki za jirani na maneno mazuri hii ni kwa sababu chimbuko la sheria za mbinguni ni moja, na kwa ajili hii mtume (rehma na amani zimshukie juu yake)amesema: “ manabii ni ndugu kwa aila za mama tafauti (lakini) dini yao ni moja.”  (Bukhari).

Sheria zinaweza kutafautiana katika ibada na namna ya kuifanya kwa mujibu wa zama na nyakati, lakini maadili na tabia za kiutu ambazo ni msingi wa kuishi hizi huwa hazitafautiani katika sheria yoyote. Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) “ katika yale waliyopata watu katika maneno ya mitume wa mwanzoni ni kuwa utakapokuwa huna haya basi fanya utakacho.” Basi ni sheria gani iliyohalalisha kuua nafsi  ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha kuuliwa isipokuwa kwa haki au imehalalisha kuwatenga wazazi wawili, au kula haramu au kula mali ya mayatima au kula mali za wafanyakazi?

Na ni sheria gani iliyohalalisha uongo, kuvunja ahadi, khiana, au kulipa mabaya kwa wema?  Yote haya ni kinyume, kwani sheria za mbinguni zimelingana na kujikita katika maadili ya kiutu, na yeyote ambae ataziacha tabia hizi basi huwa hajatoka tu katika sheria bali pia atakuwa ametoka katika mzunguko mzima wa maadili na kujivua maumbile ya uanadamu wake ambayo Mwenyezi Mungu amemuumbia.

Kwa ajili hiyo, Ibn Abas (rehma na amani ziwashukie juu yao) amesema kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu {Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. 152. Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka 153. Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu} [Al anaam 151-153]. Aya zenye kuzungumzia hukumu hazikufuta chochote katika vitabu vyote, kwani nimambo yaliyoharamishwa ka watu wote, nayo ni asili ya maandiko, yeyote atakayetenda kwa mujibu wa aya hizo basi ataingia peponi na mwenye kuacha ataingia motoni.

Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ametupigia mfano wa hali ya juu katika kurekebisha – kusuluhisha kimaneno na kimatendo, na dua yake ilikuwa ni kutaka marekebisho katika kila jambo, alikuwa akiomba ““ewe Mola nirekebishie dini yangu ambayo ni  hifadhi ya mambo yangu, na unirekebishie dunia yangu ambayo ni maisha yangu, na unirekebishie akhera yangu ambayo ni mareleo yangu, na nifanyie maisha kuwa na kila la kheri, na nifanyie umauti wangu yawe ni starehe kwa kila ovu.” (Muslim).

Na alikuwa akisuluhisha kati ya watu, pia alikuwa na pupa ya kuondosha fitina na hitilafu. Imepokewa kutoka kwa Sahli bin Saad (rehma na amani zimshukie juu yake) “ kuwa watu wa Kubaa walipigana nakurembeana kwa mawe, mtume akaelezwa jambo hilo, basi akasema: nipelekeni ili nikawasuluhishe.” (Bukhari)

Hakika ya wema na usuluhishaji ni nguzo madhubuti za kubaki kwa jamii na kuendelea kwake, nasi tuna haja ya kurekebisha nafsi zetu kwanza na kuzisafisha katika nyanja zote za kimasiha kama za kisiasa, kijamii kiuchumi na kielimu pia. Kuirekebisha nafsi ni jambo litakiwalo na sheria na ni wajibu wa kidini, na hasa katika wakati huu tulionao ambao imani imekuwa ni dhaifu na uharibifu wa tabia na kupotea kwa haki na wajinu, watu wengi wakawa hawaelewi haki ya mkubwa wala za jamaa, wazazi na za taifa.

Na katika kurekebisha ni kujichunga mtu juu ya haki yake na za wenzake, asifnye uadui katika haki za wengine, na kila mtu aelewe wajibu wake na autekeleze ipasavyo, kwani kufanya hivyo ni kutekeleza maadili mazuri na kujiweka mbali na uharibifu na ufisadi katika ardhi na dhuluma na kuujaza moyo chuki na hasada. Kwani hiki ni kiini cha urekebishaji, kila mtu ajirekebishe yeye mwenyewe kwa ajili ya Mola wake na kwa ajili ya wenzake na kwa ulimwengu mzima, kufanya hivyo atakuwa mtu mwema mwenye kuweza kurekebisha na mwengine. Yaani kama kwamba kujirekebisha ni kuitakasa nafsi kwa kuipamba kwa tabia njema na kuizuia na dhuluma na madhambi na kutenda yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu, na kuiimarisha ardhi pia kutoa hazina na siri zake ambazo manufa yake huwa kwa wote.

Kurekebisha huwa kwa mshikamano na si kwa mgawanyiko nao ni ule unaolinganiwa na Kurani Tukufu, wema na usuluhishaji huakisi upendo na usamehevu kati ya wana jamii kisha kwa umma mzima, na kwa kupitia marekebisho vyanzo vya ugomvi hutoweka na chuki pamoja na husuda.

Nayo marekebisho hayana wakati maalumu, lakini mtu huwa hana budi kuendeleza suluhisho hadi mwisho wa uhai wake na kwa ajili hiyo mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ameashiria katika hadithi aliyoipokea Anas bin Malik (Mwenyezi Mungu amwie radhi) “iwapo kiama kitasimama na kwenye mkono wa mmoja wenu ana mbegu basi akiweza kuipanda na aipande.” (Bukhari)

Na la muhimu kulitaja hapa ni kuwa suluhisho – marekebisho hayawezi kuonekana mattund yake mpaka mtu aanze yeye mwenyewe kisha ndani ya familia yake na kwa jamii yake. Marekebisho ni kitu cha lazima ili jamii iwe sawa n taifa linufaike kwa usalama na kwa kazi na maendeleo na kueneza upendo kati ya watu. Na yeyote afanyae juhudi kwa mali yake ili asuluhishe kati ya watu waliohaimiana ajue kuwa mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ameshamuombea dua akasema “hakika ya dini imeanza ngeni na itarudi hali ya kuwa ni ngeni, basi uzuri ulioje kwa wageni (nao ni) ambao wanarekebisha yale waliyoyaharibu watu baada yangu katika mwenendo wangu (sunna zangu). (Tirmidhiy).

Suluhisho lina athari kubwa sana kwa mtu na kwa jamii, nazo: kuwezesha maisha mazuri, Mwenyezi Mungu anasema {Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.} [Anahl; 97]

Pia, kuokoka na maangamizo na uharibifu, Mwenyezi Mungu anasema { Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema} [Hud 117].

Na pia kuirithi ardhi, kwani kuirithi kwake kumeshartishwa kwanza kuweko namarekebisho, Mwenyezi Mungu anasema {Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema} [al anbiya 105].

Vile vile kuwepo uongozi wa Mwenyezi Mungu na hifadhi yake kwa yule aliyeshikamana na misingi sahihi ya marekebisho, Mwenyezi Mungu amesema {Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu aliye teremsha Kitabu. Naye ndiye awalindae walio wema} [Al aaraf 196].

Pia kuna kuhifadhi kizazi, Mwenyezi Mungu {Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako khazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria}[Kahf; 82], kisa cha kujengwa ukuta wa watoto waili mayatima kwenye kisa cha nabii Mussa (rehma na amani zimshukie juu yake) kisa hiki kinajulikana, na kazi ya kujenga haikuya ya bure lakini ilikuwa na athari ya wema ya mzazi wao. Imepokewa kutoka kwa Abbas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) ilikuwa ni kwa sababu ya wema wa mzazi wao lakini haukutajwa wema wa watoto hao.

Pia suluhisho huleta usalama wa kutoogopa dunia na akhera, Mwenyezi Mungu anasema { Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.} [Al anaam; 48] pia huleta msamaha na upendo, Mwenyezi Mungu anasema {. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu} [Anisaa; 129]

  Marekebisho yakifanyika juu ya kitu basi huwa kimepambika na ni tabia ipendwayo na Mwenyezi Mungu na mtume wake (rehma na amani zimshukie juu yake) kwani kupitia hayo maisha huenda itakiwavyo, na umma unakuwa umeshikamana, myonge huwa na nguvu, waisilamu huwa wamoja na neno lao huwa moja na huondosha mgawanyiko, na kueneza upendo nayo ni dalili ya imani, mwenyezi mungu anasema {Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe. }[Alhujraat; 10].

Na tukosapo thamani ya suluhisho basi umma utaharibika, familia zitaporomoka, fujo zitaenea, ufisadi nao utashika nafasi na haki za Mwenyezi Mungu zitavyunywa, maovu yatatendwa hapo ndipo jamii, taifa na ustaarabu utakaposambaratika, kuacha kusuluhisha hupelekea kuenea kwa adhabu hapa duniani na maangamizo ya kinafsi kama ufakiri, udhalili na fedheha.