Haki ya mtoto katika ukuaji mzuri na maisha bora na maandalizi
mazuri kwa ajili ya mustakbali
10 jamad Uwla 1437 H. Sawa na 19-2-2016 A.D.

awkaf-

 

Kwanza : Vipengele

 1. Watoto ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu inapaswa kuishukuru.
 2. Huduma ya uisilamu kwa watoto
 3. Nguzo muhimu za ukuzaji mzuri wa watoto.

  1. Kumchagulia jina zuri.
  2. Kumnyonyesha kidesturi.
  3. Kuwafanyia wema na kuacha kutumia nguvu na ukali
  4. Uadilifu na usawa kwa watoto wote.
 4. Ulazima wa kuwahakikishia watoto maisha bora.
 5. Umuhimu wa kuwa na tama maishani mwetu.

Dalili: ndani ya Kurani tukufu na hadithi

 1. Mwenyezi Mungu anasema: { Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. 50 Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza.}Ashura, 49-50.
 2. Mwenyezi Mungu anasema: { Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsiyenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana nawajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za MwenyeziMungu?} Anahl, 72.
 3. Mwenyezi Mungu anasema: { Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.}Albaqara, 233.
 4. Mwenyezi Mungu anasema: { Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katikawake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalietuwe waongozi kwa wachamngu }Alfurqan, 74.
 5. Mwenyezi Mungu anasema: { Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwaImani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na walahatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kilamtu lazima atapata alicho kichuma.}At tuur, 21.
 6. Mwenyezi Mungu anasema: {Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa. 14 Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mamayake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. 15 Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat’ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. 16 Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe yakhardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye khabari za yote. 17 Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. 18 Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha. 19 Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.}Luqman 13-19.
 7. Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenuna Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. WanausimamiaMalaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa} At tahriim, 6.

Dalili za hadithi

 1. Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rhma na amani zimshukie juu yake) amesema: nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari)
 2. Kutoka kwa Maaqil bin Yasaar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) kutoka kwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “hakuna mja ambaye Mwenyezi Mungu humpa wa kumchunga, akafariki mchungaji hali ya kuwa amefanya hadaa basi Mwenyezi Mungu atamuharamishia pepo.” (Bukharin a Muslim).
 3. Kutoka kwa Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “siku moja nilikuwa nyuma ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ ewe kijana mimi nitakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, na pale uombapo basi muombe Mwenyezi Mungu, na pale utakapo msaada basi taka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tambua kuwa lau umma utakusanyika juu ya kutaka kukunufaisha kwa kitu basi hawataweza kukunufaisha isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu. Na lau wakikusanyika juu ya kutaka kukudhuru kwa kitu basi hawataweza kukudhuru kwa kitu isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu, kalamu zishanyanyuliwa na kurasa zishakauka.” (Tirmidhi).
 4. Kutoka kwa Abdalla Bin Amru bin A`s (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “mtu inatosha kuwa na madhambi kwa kule kutomjali anaye mlea.” (Kitabu cha Hakim).
 5. Kutoka kwa Saad Bin Abi Waqas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akinitembelea mwaka wa hija ya kuagana, kutokana na maumivu yaliyonizidi, nikasema: “ nimefikwa na maumivu, nami nina mali, na hakuna atakayeirithi isipokuwa mwanangu wa kike, je nitoe sadaka thuluthi mbili za mali yangu? Akasema : “hapana,” nikasema: “nusu? Akasema: “Hapana”, kisha akasema: “ thuluthi, na thuluthi ni nyingi, kwani wewe ukiacha kizazi chako matajiri ni bora kuliko kuwaacha ni watu waombao wengine, kwani (pia) hutumii matumizi yoyote aikawa uanataka radhi za Mwenyezi Mungu isipokuwa utalipwa kwayo.” (Bukhari).
 6. Kutoka kwa Thauban (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “Dinari bora aitoayo mtu ni ile dinari anayoitoa kwa ajili ya familia yake, na dinari aitoayo kwa ajili ya kipando chake katika njia ya Mweneyzi Mungu na dinari aitoayo kwa wenzake katika njia ya Mweneyzi Mungu.” Abu Qalabah akasema “ akaanza kwa watoto, kisha akasema Abu Qilabah: na hakuna mtu mwenye kupata malipo mazuri kama Yule anayetoa kwa ajili ya watoto ili kuwazuilia wasiombe au kuwanufaisha kwa ajili ya Mweneyzi Mungu na kuwatosheleza.” (Muslim).
 7. Kutoka kwa Athman Hatabiy amesema: nimemsikia Ibn Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) akimwambia kijana: “ mfunze heshima (adabu) mwanao, kwani wewe utaulizwa juu ya mwanao, ni kitu gani umemfunza? Na yeye ataulizwa juu ya wema wako na kukutii kwako.” (Imam Albayhaqiy – Sunan Kubra).
 8. Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema mjumbe wa Mweneyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “hakika nyinyi mtaitwa siku ya kiama kwa majina yenu na majina ya baba zeni, basi majina yenu yafanyeni kuwa mazuri.” (imepokewa na Daud).
 9. Kutoka kwa Aamir, amesema: nimemsikia Nuumaan bin Bashiir (Mweneyzi Mungu awawie radhi) naye yuko juu ya membari akisema: “Baba yangu amenipa zawadi, Umrah bint Rawaha akasema: sikubali mpaka mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aishuhudie. Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akaja, akasema: “mimi nimempa mwanagu kutoka kwa Umrah bint Rawaha zawadi, akaniamrisha kuwa nikufanye wewe kuwa ndiye shahidi ewe mjumbe wa Mwenyezi mungu, akasema: “je wanao wengine umewapa kama hiki?” akasema: “ hapana.” Akasema “ muogopeni Mwenyezi Mungu na fanyeni uadilifu juu ya watoto wenu.” Akasema, akaichukua zawadi yake. (Bukhari).
 10. Kutoka kwa Umara Bin Salama (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: nilikuwa katika chumba cha mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) na mkono wangu ulikuwa ukitangatanga ndani ya sahani akaniambia “ewe kijana taja jina la Mwenyezi Mungu ( sema Bismillahi) na kula kwa mkono wako wa kulia na kula kilicho mbele yako.”

Tatu: Maudhui

Miongoni mwa neema kubwa sana ambazo Mweneyezi Mungu amemneemesha mwanadamu baada ya imani ya Mweneyezi Mungu Mtukufu ni neema ya mtoto ambayo huhifadhi kizazi na hutuliza moyo. Watoto ni neema ya Mwenyezi Mungu, ni zawadi kutoka kwake humpa amtakae katika waja wake, Mwenyezi Mungu anasema: { Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. 50 Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza }Ashuura, 49-50. Watoto huyafanya maisha kuwa ni ya furaha na ucheshi, huondoa kiza ndani ya nyumba na huingiza mwanga, wao ni taa za nyumba, utulivu wa macho na ni vipenzi vya nyoyo, wao ni pambo la maisha ya dunia, kama alivyosema Mola wetu ndani ya Kuran Tukufu {Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na memayanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwamalipo, na bora kwa matumaini.} Kahf 46.

Hivyo basi, neema hii – ya watoto – inapasa kushukuriwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kipenzi cha Mwenyezi Mungu mtume Ibrahim (rehma na amani zimshukie juu yake) baaya ya kupewa mwana na Mwenyezi Mungu alisema: {Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi. 40. Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Sala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu.} Ibrahim 39-40.  Kuishukuru neema ni kuihifadhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema  { Na alipo tangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru nitakuzidishieni; na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali } Ibrahim, 7. Na inapasa kuwahudumia ili akue katika kizazi kitakachomtambua Mwenyezi Mungu, kujua haki za wazazi wake, haki za jamii na taifa.

Uisilamu umetoa huduma kubwa sana kwa watoto na kwa kuwalea vyema basi hupatikana furaha duniani na akhera kwa watoto na wazazi. Uisilamu ukamjali mtoto kabla hata ya kuja duniani ukamtaka mwenye kutaka kuoa achague mke mwema, kwani nyumba itakapokuwa imezingirwa na mazingira ya imani athari zake njema huenea kwa waliomo, na hivi ni kama alivyosema Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliposema: “ ..mchague aliye na dini  mikono yako ipate kubarikiwa” (Muslim).. na uisilamu umejali mtoto kabla ya hata kuanzishwa kwa taasisi za kimataifa zeneye kujali haki za watoto, kwa kuwa kipindi hiki ni hatari na chenye misukosuko katika maisha ya mwanadamu. Utoto ni kipindi kigumu na uhimu ambacho kila mtu ni lazima apitie kisha apitea ujana. Hivyo, uisilamu ukajali sana utoto ili wawe ongezeko zuri  na chanzo chenye kuwa na faida katika jamii. Ukawapa hukumu (sheria) nyingi kuhusu wao ambazo zinarudi kwa mtoto, familia, kisha jamii kwa manufaa na faida njema.

Uisilamu umechunga kuhusu watoto tokea yupo tumboni mwa mama yake, ukaweka hukumu na sheria zenye kumkinga na kumlinda uanadamu wake katika kumchunga na kumpa malezi yote anayostahiki., hiki ni kipindi cha mwanzo ambacho pia anastahiki kutunzwa na kuchungwa. Kwa maana hiyo, uisilamu umedhamini haki ya maisha yake hali ya kuwa bado yu tumboni mwa mama yake. Ukaharamisha utoaji wa mimba kwa makusudi, na kuwajibisha kutunzwa kwa mama mja mzito, na ukaruhusu kwa mama mja mzito kutofunga katika mwezi wa Ramadhani pindi akihofia mtoto wake tumboni, mpaka akue kama kawaida. Kutoka kwa Anas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake amesema: “ hakika ya Mweneyzi Mungu ameondosha kwa msafiri nusu sala na funga na kwa mja mzito na mwenye kunyonyesha.” (Nisai).

Vilevile katika yanayohusu kutunzwa kwa watoto: kumchagulia jina zuri, wazazi waliotangulia walikuwa wakijilazimisha kuwachagulia wana wao majina mazuri watakayoitwa, kwani jina zuri huleta furaha nyoyoni na utulivu tafauti na jina baya. Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema mjumbe wa Mweneyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) “hakika nyinyi mtaitwa siku ya kiama kwa majina yenu na majina ya baba zenu, basi majina yenu yafanyeni kuwa mazuri.” (imepokewa na Daud). Wazazi wawili wanaporuzukiwa mwana basi wameamrishwa wamchagulie jina zuri, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema “mtoto anakuwa katika rehani kwa akika yake, atachinyiwa siku ya saba, atapewa jina, na kunyolewa kichwa chake.” (Tirmidhi).

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amependelea kwa umma wake wachague majina ayapendayo Mwenyezi Mungu, kutoka kwa Naafi`, kutoka kwa Ibn Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “ majina yapendwayo na Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdulrahman.” (Abu Daudi). Nakatika mapokezi ya imamu Muslim, kutoka kwa Umar, amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake): “ hakika majina yenu yapendwayo sana na Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdulrahman.” Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akikataza kuwaita wana majina mabaya, akasema “ usimwite mtoto wako jina la Rabaha wala Yasara wala Aflaha wala Naafia` (Muslim).

Na sababu ya kukatazwa kuitwa majina mabaya ni kwa upande wa nafsi ya mtoto, ili isije kumsababishia aina Fulani ya makero ya nafsi. Mzee mmoja alikuja kwa Umar bin Khatwab (Mwenyezi Mungu amwie radhi) akimshtakia kuhusu mwanawe, Umar akawita mzazi na mwanawe na kumlaumu mwana juu ya haki ya mzazi wake na kwa kusahau kwake haki hizo, mtoto akasema, ewe kiongozi wa waumini, kwani mtoto hana haki kwa wazazi wake? Akasema: “anazo.” Akamuuliza: “ ni zipi haki zenyewe? Akasema Umar: “ ni kuwa mwema mama yake, kumchagulia jina zuri, kumfundisha kitabu (kurani). Mtoto akasema: “ewe kiongozi wa waumini hakika baba yangu hakufanya hata moja katika hayo, mama yangu alikuwa mtu mweusi aliyekuwa akimilikiwa na mwenye kuabudu moto na ameniita kombamwiko (mbawakawa) na wala hakunifundisha hata herufi moja ndani ya kitabu. Umar akamgeukia mzee akamwambia, “wewe umekuja kwangu kumshtakia mwanao juu ya haki yako, lakini wewe umekeuka haki zake kabla ya yeye kukeuka haki zako na umemtendea sivyo kabla ya yeye kukutendea sivyo.” (Malezi ya watoto katika uisilamu).

Sufyan Thauri amesema: “ haki ya mtoto kwa wazazi wake ni kuitwa jina zuri, kumuoza pindi akibaleghe, na kumfunza heshima (adabu) njema.” Kwani kumchagulia jina zuri humsaidia katika kuishi maisha mazuri atakayoweza kuepukana na kutaniwa na kufanyiwa kujeli, pia atapata raha na utulivu wa nafsi pale atakapoitwa kwa jina lake, jina ni kitambulisho cha mtu.

Na katika matunzo ya uislamu kwa mtoto: inatakiwa kumyonyesha iwe ni haki yake inayotambulika, Mwenyezi Mungu anasema: { Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.}Albaqara, 233. Katika aya hizi tukufu wazazi wa kike wameamrishwa kama kwamba wameambiwa. “enyi wazazi wanyonyesheni watoto wenu kwa miaka miwili kamili, kani mtoto kipindi hiki huwa anahitaji maangalizi muhimu ya chakula ambayo yatamsaidia katika kukuza mwili wake na hakuna chakula kilicho bora kama maziwa ya mama yake ambayo Mwenyezi Mungu ameyaandaa kwa ajili hiyo. Na amesema kweli Mwenyezi Mungu: { Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenyekhabari?} Almulk 14. Ama iwapo mama ana matatizo ambayo kisheria ameruhusika kutonyonyesha au mtoto kajizuilia kunyonya au mzazi kufariki basi hapa sheria ya kiisilamu imelazimisha kwa mzazi wa kiume kumtafuta myonyeshaji wa huyu mwana kwa malipo ili mwana apate usalama wake.

Na elimu za kiafya na nafsi zimethibitisha kuwa kipindi cha kunyonyesha mtoto kilichotajwa kisheria cha miaka miwili ni lazima kwa ajili ya ukuaji wa mtoto ukuaji unaohitajika nayo ni kwa pande mbili:- kisiha na kinafsi. Na kumkuza mtoto katika mazingira ya upendo, utulivu na amani nayo haya yote hayapatikani isipokuwa kwa mama ambaye atamsaidia mwana kukua katika ukuaji bora na kumfanya aishi maisha mazuri.

Na miongoni mwa misingi ya ukuzaji wa mtoto: kumtendea wema na kuacha kutumia nguvu na ukali. Kwani hujulikana kisheria kuwa  upendo hauleti isipokuwa jema. Kutoka kwa mama wa waumini Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ewe Aisha Mwenyezi Mungu ni mpole naye hupenda upole, humpa mwenye mpole kile ambacho hampi (humnyima) asiyekuwa na upole (mwenye kutumia mabavu) na kile ambacho hawapi wengineo.” (Muslim). Nguvu na ukakamavu katika malezi na kutumia mabavu katika malezi hupelekea kumfanya mtoto mara nyingi kuharibika kitabia na kumfanya amchukie mzazi wake (mlezi) na kutosikia maneno yake.

Imepokewa katika hadithi tukufu kwa mba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akimbeba Hassan na Hussein (Mwenyezi Mungu awawie radhi) juu ya mabega yake na akicheza nao. Na katika misingi aliyotumia mtume mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ilikuwa ni upole na ulaini. Kutoka kwa Burayda kapokea kutoka kwa baba yake amesema: “mtume alipokuwa juu ya mimbari akihutubia, mara Hassan na Hussein wakaingia hali ya kusota na walikuwa wamevaa nguo nyekundu, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akashuka akawabeba kisha akasema: “Mwenyezi Mungu amesema kweli { Hakika mali yenu na watoto wenu ni jaribio} Ataghaabun,15. Nami nimewona hawa wakitembea na kusota sikuweza kusubirio bali nikashuka na kuwabeba (Nisai).

Mlezi mwema- sawa ni mzazi au mwalimu – yeye ndie achungae misingi hii mikubwa ya malezi nayo ni matendo ya upole na laini. Na kujiepusha na maguvu na ukakamavu, hutibu tatizo kwa hekima na upole, maguvu husababisha hofu ndani ya nyoyo ya mtoto na woga ukiachana na wasiwasi wa kinafsi na kuona haya na kutojiamini. Ahnaf bin Qiys amesema katika moja ya nasaha zake: “ usiwe kwao kufuli ili wasije wakatamani kifo chako na wakachukia kukuona upo karibu nao na kuyachukia maisha yako.” Kuwatendea upole haina maana kuwa usitumie adhabu wakati inapobidi, lakini ni lazima tukumbushe kuwa adhabu ni lazima iwe kwa hekima na wala isiwe kwa kila kosa alikosalo (alitendalo).

Na vilevile miongoni mwa malezi bora kwa watoto: ni uadilifu na usawa kati yao. Uadilifu kwa viumbe vyote ni haki ya lazima katika sheria ya kiisilamu, Mwenyezi Mungu anasema {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mnona uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika MwenyeziMungu anazo khabari za mnayo yatenda}Almaida, 8. Na jambo hili linapasa kwanza lianze kwa mzazi na watoto wake.

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) ameelekeza wazazi wa kike na wa kiume misingi ya lazima ambayo ni lazima waifuate, si hivyo tum bali pia ameambatanisha na uchaji wa Mungu Mtukufu,  kutoka kwa Amir, Kutoka kwa Aamir, amesema: nimemsikia Nuumaan bin Bashiir (Mweneyzi Mungu awawie radhi) naye yuko juu ya membari akisema: “Baba yangu amenipa zawadi, Umrah bint Rawaha akasema: sikubali mpaka mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aishuhudie. Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akaja, akasema: “mimi nimempa mwanagu kutoka kwa Umrah bint Rawaha zawadi, akaniamrisha kuwa nikufanye wewe kuwa ndiye shahidi ewe mjumbe wa Mwenyezi mungu, akasema: “je wanao wengine umewapa kama hiki?” akasema: “ hapana.” Akasema “ muogopeni Mwenyezi Mungu na fanyeni uadilifu juu ya watoto wenu.” Akasema, akaichukua zawadi yake. (Bukhari). Na imepokewa na Abdulrazaak katika kitabu chake kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alimuita kijana mmoja wa kianswar, akaja (mbele ya mtume) kisha mtoto wake wa kiume akaja na akambusu na kumbeba na kumkumbatia na kukaa nae, kisha (baadae) akaja mtoto wake wa kike akamshika mkono akammkalisha chini, mtume rehma na amani zimshukie juu yake) “lau ungeliwafanyia uadilifu ingelikuwa ni bora kwako, jikurubisheni kwa watoto wenu hata pale munapowabusu.”

Na katika kufanya uadilifu kwa wote kuna faida kubwa mno na huwasaidia ndugu kusaidiana katika mema na pia huwasaidia katika kutengeneza kizazi chema ndani ya jamii kama inavyosaidia kujenga undugu wa ukweli kati ya jamaa.

Kinyume na haya tunaona mtafaruku kati ya wanandugu ambayo ni sababu kubwa sana ya kuasi wazazi, kuwakimbia na kuwachukia na pia ni sababu ya kupandikiza chuki kati ya wanandugu.

Baadhi ya matukio ya wanaelimu ya nafsi yamethibitisha kuwa mtoto mara nyingi humili kuhisi kufanya  mabaya kwa sababu ya dhuluma na kutotendewa usawa ndani ya familia. Na mfano mzuri sana ni kisa cha nabii Yussuf (rehma na amani ziwe juu yake) kwa kuboreshwa kwake zaidi yao, Mwenyezi mungu anasema {Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwawanao uliza 8.Pale walipo sema: Hakika Yusuf na nduguyewanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, hali sisini kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa dhaahiri. 9. Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wababa yenu ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya mtakuwawatu wema.} Yusuf 7-9.

Vilevile katika misingi ambayo uisilamu umeiweka kwa ajili ya kudhibiti ukuaji bora wa mtoto: ni malezi na mafundisho ya sheria. Mwenyezi Mungu mtukufu amewamrisha wazazi wa kike na wa kiume ndani ya kurani tukufu umuhimu wa kuikinga nafsi na jamaa ili wasiingia katika maangamizi, akasema {Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenuna Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. WanausimamiaMalaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa}At tahrim, 6. Na kumlea mtoto na kumfundisha adabu ni misingi itakiwayo na sheria nazo pia ni haki miongoni mwa haki za mtoto kwa wazazi wake. Kutoka kwa Ibn Abass (mwenyezi Mungu awawie radhi) wamesema: ewe mjumbe wa Mweneyzi Mungu, tumekwisha elewa haki ya mzazi kwa mwanawe, lakini ni zipi haki za mwana kwa mzazi? Akasema; “kumfundisha adabu njema na kumlea vizuri.” (Sehemu ya imani. Kitabu cha Bayhaqiy) na amepokea Tirmidhi katika kitabu chake kwamba mtume (rehma na amani zimshukie juu yake amesema: “hakuna wema autendao mzazi kwa mwana kuliko wema wa kumlea malezi mema.”

Na miongoni mwa misingi muhimu ya ukuzaji watoto ni kuwaelekeza na kuwalea malezi bora, malezi na maelekezo yanatakikana yawe kwa utaratibu na si mbele ya wengine, na hivi ndivyo alivyokuwa akifanya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) Kutoka kwa Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: “siku moja nilikuwa nyuma ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ ewe kijana mimi nitakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, na pale uombapo basi muombe Mwenyezi Mungu, na pale utakapo msaada basi taka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tambua kuwa lau umma utakusanyika juu ya kutaka kukunufaisha kwa kitu basi hawataweza kukunufaisha isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu. Na lau wakikusanyika juu ya kutaka kukudhuru kwa kitu basi hawataweza kukudhuru kwa kitu isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu, kalamu zishanyanyuliwa na kurasa zishakauka.” (Tirmidhi).

Kisha tena mtume (rehma na amani zimshukie juu yake analea na kufunza na kuelekeza adabu njema kwa kupigia mifano mizuri juu ya mtoto, imepokewa Kutoka kwa Umara Bin Salama (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: nilikuwa katika chumba cha mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) na mkono wangu ulikuwa ukitangatanga ndani ya sahani akaniambia “ewe kijana taja jina la Mwenyezi Mungu ( sema Bismillahi) na kula kwa mkono wako wa kulia na kula kilicho mbele yako.”(Muslim). Imam ghazali (Mweyezi Mungu amrehemu) “mtoto ni amana mbele ya wazazi wake, moyo wake uko safi suio na dosari, pindi ukizoweshwa mazuri na kufundishwa mema basi atafurahia duniani na akhera.”

Juu ya mlezi awe kiongozi kwa watoto wake, ajiweke katika tabia njema kabla ya kuwaamrisha, kwani watoto huiga.

Ana haki aliyesema:

Watoto wetu hukuwa kutoka kwetu * kama vile wazazi wake walivyomzowesha

Na la msingi kulitaja ni kuwa, malezi hayawi kwa wazazi peke yaolakini pia kwa mwalimu. Mwalimu ni sehemu katika jamii na ana umuhimu na ulazima wa kukuza kizazi kwa kuzingatia tamaduni za jamii anayoishi. Watoto niamana inayobebwa na jamii kwa ujumla na ni jukumu lililo katika shingo zao, na inapasa kuwalea ipasavyo.wote pamoja wafahamu jukumukubwa walilolibeba kuhusu watoto, na hakuna mfano wa wazi zaidi ya kauli ya mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari)

Dini ya kiisilamu inambebesha mzigo wazazi wa kuhifadhi watoto kwani imepokewa Kutoka kwa Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: hakika yaMweneyzi Mungu atamuuliza kila mchungaji kwa kile alichokichunga je amekihifadhi au amezembea, mpaka atamuuliza pia mume juu ya watu wa nyumba yake.” (imepokewa na Ibn Haban.) na tumuangaliapo mtoto basi tumuangalia kama mtu aliyekamilika na kuwa na haki zote za kimwili, kinafsi, kimali, kielimu, na malezi na ni wajibu kuzihifadhi ili awe na maisha mema na bora na ili jamii iwe na ustaarabu na kuenea upendo, mapenzi na huruma.

Na tunasisitiza umuhimu wa kuwa na tama juu ya watoto wetu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuishi bila ya tama. Hakuna maisha iwapo tamaa haipo, na ikikosekana tamaa maisha hupotea. Wasomi wameeleza ya kuwa “kukata tamaa ni  kuchanganyikiwa na kujichanganya huwa ni katika makosa makubwa.” Abdallah Bin Abass (Mweneyzi Mungu awawie radhi) anasema: “kuna kijana kasema: “ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni yepi madhambi makubwa: akasema: “kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kupoteza matumaini kwa Mweneyzi Mungu. kukata tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu, na atakaeepushwa na Mwenyezi Mungu na hayo basi amedhaminiwa kuingia peponi.”

nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye ataulizwa juu ya alichokichunga.” Mpokezi akasema nadhani alisema: “kijana ni mchungaji wa mali ya baba yake naye ataulizwa juu ya alichokichunga, nyote ni wachungaji na mutaulizwa juu ya mulichokichunga.” (Bukhari)