Amana ya neno na majukumu yake
1 Rajab 1437H. sawa na Aprili 2016 A.D

awkaf-

Kwanza: vipengele:

 1. Nafasi ya neno katika uisilamu.
 2. Kuhifadhi ulimi ni katika dalili za kuwa na imani.
 3. Amana ya neno na majukumu yake ni jambo la lazima kisheria na kimaadili.
 4. Hatari ya neno na athari zake kwa mtu na kwa jamii.

Pili:Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa 71. Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt’ii MwenyeziMungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.} (Al ahzab. 70-71)
 2. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {.. na semeni na watu kwa wema, } (Albaqara. 83)
 3. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet’ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet’an ini adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu } (Israa. 53)
 4. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa liliojema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.} (Fussilat. 34)
 5. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {Arrah’man, Mwingi wa Rehema 2. Amefundisha Qur’ani. 4. Akamfundisha kubaini. 3. Amemuumba mwanaadamu,} (Arahman.1-4)
 6. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara,na matawi yake yako mbinguni. 25. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka. 26. Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong’olewa juu ya ardhi. Hauna imara.} (Ibrahim.24-26)
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole } (Albaqara. 263)
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : { Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu:Hichi halali, na hichi haramu – mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.} (Anahl.116)
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {. Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka. 44. Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.} (Taha.43-44)

Dalili ndani ya hadithi

 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “hakika ya mja hunena neno la kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humnaynyua kupitia neno hilo daraja. Na hakika ya mja hunena neno la kumkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia basi huingia kupitia neno hilo katika moto wa jahannamu.” (Bukhari na Muslim).
 2. kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie) “ kila salamu ni sadaka, kila siku ichomezewayo jua akawa anafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na kumsaidia mtu katika kipando au kumsaidia kupandisha mzigo juu ya kipando ni sadaka. Neno zuri ni sadaka. Na hatua aipigayo kuelekea msikinitini ni sadaka. Na uchafu auondoshao njiani ni sadaka.” (Bukhari na Muslim)
 3. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) hakika ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie) amesema: “ dalili za mtu mnafiki ni tatu, asemapo huongopo. Akiahidi hatimizi ahadi. Na akiaminiwa hufanya khiyana.”
 4. Kutoka kwa Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie ):“ anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi asimuudhi jirani yake. Na anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake. anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi aseme neno zuri au anyamaze.” (Bukhari na Muslim)
 5. Kutoka kwa Ibn Abass ((radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) kuna mtu nguo (shuka) yake ilipeperushwa kwa upepo katika zama za Mtume (rehema na amani zimshukie ) akaulaani upepo. Mtume (rehema na amani zimshukie ) akamwambia: “ usiulaani kwani umetumwa, kwani yeyote mwenye kukilaani kitu pasi na haki basi laana ile humrudia mwenyewe.” (Abu Daudi)
 6. Kutoka kwa Muadh bin Jabal (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)  amesema: nilikuwa safarini na Mtume (rehema na amani zimshukie )nikawa karibu naye … kasha akasema: “je, nikueleze juu ya umiliki wa hayo yote? Akasema: “ nikasema:  “ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: akaashiria katika ulimi wake na kusema: “jizuie na huu”. Nikasema: “ kwani sisi tunahesabiwa kwa  tukisemacho? Akasema: “ ewe Muadhi,mama yako akupotea hivyo unadhani watu wataingia motoni kwa sababu ya nyuso zao –au amesema- kwa pua zao – huoni kuwa wataingia motoni kwa sababu ya ndimi zao..” (Tirmidhiy)

Tatu: Maudhui

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemneemesha mwanadamu kwa neema nyingi zisizohesabika akasema: { Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira,Mwenye kurehemu.} (Anahl.18) Na miongoni mwa neema kubwa sana ni ulimi akasema {Kwani hatukumpa macho mawili? 9. Na ulimi, na midomo miwili?} (albalad.8-9) na kasha akaupa ulimi neema nyengine nayo ni kuweza kutamka ambayo humtenganisha mwanadamu na viumbe wengine, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema : {Arrah’man, Mwingi wa Rehema 2. Amefundisha Qur’ani. 4. Akamfundisha kubaini. 3. Amemuumba mwanaadamu,} (Arahman.1-4).

Neno ni anuani ya ulimi na ni njia ya kuwasiliana na mwengine na kupitia maneno maisha huendelea, na hakuna sheria yoyote iliyojali neno kama sheria ya kiisilamu, imejali kwa hali zote sawa iwe kweli au matani. Kuna maneno hufutahisha watu na mengine hukasirisha, na kwa neno heshima na umwagaji wa damu huhifadhika.

Na kutokana na hatari ya neno Mwenyezi Mungu Mtukufu ameleta amri ya kutaka ulimi uhifadhiwe, na kuacha kutamka lenye kuondoa heshima za watu, na kuzungumzia yasiyohusu wala yasiyo na faida, akasema { Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari } (Qaf.18).  viungo vyote vya mwanadamu vimeshikamana na ulimi, ulimi ukiwa mwema navyo huwa vilevile na ukiwa mbaya navyo huwa vibaya. Kutoka kwa Abi Said Alkhudriy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: mwanadamu afikapo asubuhi viungo vyote husemeza ulimi na kuuambia: muogope Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili yetu kwani ukiwa sawa nasi tutakuwa sawa  na kama utapinda nasi tutapinda.” (Tirmidhi).

Na Mtume (rehema na amani zimshukie ) ameweka wazi kwa kumwambia Muadh kuwa ulimi ni sababu ya kumfanya mtu aingie peponi au motoni. Akasema : nilikuwa safarini na Mtume (rehema na amani zimshukie )nikawa karibu naye … kasha akasema: “je, nikueleze juu ya umiliki wa hayo yote? Akasema: “ nikasema:  “Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: akaashiria katika ulimi wake na kusema: “jizuie na huu”. Nikasema: “ kwani sisi tunahesabiwa kwa  tukisemacho? Akasema: “ Mama yako  akupotea ewe Muadhi,  hivyo unadhani watu wataingia motoni kwa sababu ya nyuso zao –au amesema- kwa pua zao – huoni kuwa wataingia motoni kwa sababu ya ndimi zao..” (Tirmidhiy)

Neno ni amana na inabidi kwa atamkaye amuogope Mwenyezi Mungu Mtukufu kwalo, kwani lina madhara na hatari kubwa pia lina faida na mafanikio mengi. Imepokewa kutoka kwa  Abi Hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema: “ hakika ya mja hunena neno la kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humnaynyua kupitia neno hilo daraja. Na hakika ya mja hunena neno la kumkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa hajalizingatia basi huingia kupitia neno hilo katika moto wa jahannamu.” (Bukhari na Muslim).

Na ilivyokuwa neno zuri ni dalili ya imani ya mtamkaji kama alivyotueleza Mtume (rehema na amani zimshukie) pale aliposema: “anaeamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na siku ya mwisho basi aseme neno zuri au anyamaze.” Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha kusema neno la kweli kwa yeyote bila ya kutafautisha na wala tusitamke isipokuwa tamshi jema ambalo hujenga na wala halibomoi, huimarisha na si kuporomosha, akasema (na semeni na watu kwa wema, } (Albaqara. 83). Pia akasema {Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet’ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet’ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu } (Israa. 53)na akasema pia {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa 71. Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.} (Al ahzab. 70-71). Kutengemea kwa matendo na kupata msamaha wa madhambi upo kupitia matamshi mema na kwa maneno mazuri. Kwa ajili hiyo maelekezo ya uisilamu ni kuchunguza na kuwa na uhakika wa ukisemacho, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {. Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.}(Alhujuraat.6).

Kwa ajili hiyo itafahamika kuwa kuhifadhi ilimi ni dalili ya imani, na ni katika uisilamu mzuri na ni njia ya kufikia pepo ya Firdausi ya juu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasmea  { Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,} Almuuminuun.3) mpaka aliposema {Hao ndio warithi,11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.} (Almuuminuun10.11). na kutoka kwa Saad bin Muadh (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume (rehema na amani zimshukie) amesema: “yeyote atakayenipa dhamana ya kuhifadhi kilichopo kati ya ulimi wake na kilichopo kati ya miguu yake miwili basi nami ninampa dhamana ya kuingia peponi.” (Bukhari).

Na amana ya neno na majukumu yake ni jambo la lazima kwa upande wa sheria na kimaadili, kwani huufanya umma uwe pamoja na kuwa na nguvu na kuweza kumbadilisha adui kuwa rafiki na chuki kuifanya kuwa ni upendo na kuondoa matendo na vitimbi vya shetani, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {34 Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa liliojema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.} (fussilat.34). na kama ilivyokuwa neno zuri hukutanisha nyoyo na kurekebisha nafsi na kuondosha huzuni na hasira na kufanya kuhisi kuridhia na furaha hasa hasa linapoambatanishwa na tabasamu. Imepokewa kutoka kwa  Abi Dhari (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)amesema:  amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehma na amani zimshukie) “kutabasamu katika uso wa ndugu yako ni sadaka.” (Bukhari).

Na kama ilivyokuwa amana ya neno linahitaji kwa msemaji kuwa asiseme isipokuwa kwa kheri na ukweli, asiseme uongo wala kwa hadaa au kwa kutoa ushahidi wa uongo na kugeuza ukweli na wala asizungumze bila ya kujua. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu – mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.} (Anahl.116).

Pia katika amana za neno ni kutoa nasaha na ushauri mwema, kwani dini ni kushauriana kama alivyotueleza Mkweli Muaminifu (rehema na amani zimshukie) kutoka kwa Tamim Aldaramiy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kuwa Mutume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie ) amesema: “ dini ni nasaha”. Tukasema: “ ni kwa nani.? Akasema: “ ni kwa (ajili) ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake na kwa viongozi wa waumini na wengineo.” (Muslim). Na kutoka kwa Abi hurayra (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie ) “mweney kutaka ushauri basi amesalimika.” (Daudi).  Hivyo basi, nasaha na ushauri wa ukweli mambo mengi hutengemea ikiwemo amani na , upendo katika taifa.

Neno ni silaha ya hatari sana yenye pande mbili, linaweza kuwa ni sababu ya kuimarika kwa taifa pindi ni zuri na la ukweli na linaweza pia kuwa ni sababu ya kuporomoka, ufisadi na uharibifu pindi liwapo si la ukweli. neno si kitu kidogo lina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya watu, na kwa yale wafanyiayo mfano wa kuuziana, ahadi na makubaliano na mifano mwngine yenye kuhitaji ukweli katika mazungumzo.

Haifichikani kuwa neno zuri lina athari nzuri kati ya watu, wema kwa jirani kupitia neno zuri huenda ikawa ndio sababu ya kuingia peponi, na ubaya wake kwao ikawa ndio sababu ya kuingia motoni. Imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra amesema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu (rehema na amani zimshukie ) aliambiwa: “ ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna mwanamke Fulani anasali usiku na kufunga mchana, na hufanya (mema) na hutoa sadaka na huwakera majirani zake kwa ulimi. Mtume (rehema na amani zimshukie ) akasema: hana jema huyo yeye ni katika watu wa motoni.” Akaambiwa:“na kuna mwanamke fulani husali sala za lazima tu na hutoa sadak ، lakini hamkeri mtu. Mtume (rehema na amani zimshukie ) akasema yeye nikatika watu wa peponi.” (Bukhari).

Vilevile neno lina athari kubwa katika mahusiano kati ya muisilamu na asiyekuwa muisilamu, hata pamoja na maadui zetu Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuseme nao kwa maneno mazuri, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka. 44. Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.} (Taha. 43-44)

 Na katika jambo la msingi kulitaja hapa ni kuwa neno lililoandikwa linaweza kuwa na maafa na madhara makubwa ya kuangamiza taifa na halina tafauti na neno litamkwalo, aina zote hizi ni amana, na ni wajibu wa kila ashikae kalamu aipe haki yake kama itakiwavyo na awe na pupa na kujiepusha na makosa kwani ni kalamu ndio itakayomuweka wazi juu ya misimamo yake na inahitajika aitumie kwa kunusuri haki na kuilingania pia.  Imam Jahidh anasema “kalamu ni ndimi mbili nayo ni yenye kubakisha athari.” Si hivyo tu bali ni upanga mkali sana na weney nguvu na unafika mbali kuliko hata upanga wenyewe.

Kwa ajili hiyo kila mwandishi amuogope Mwenyezi Mungu Mtukufu aache kueneza habari za uongo na kuupotosha ukweli pia kuzungumzia heshima za watu na kuacha kabisa kila lenye kuleta madhara kwa jamii kwani jambo hili huwa ni khiyana ya neno.

Mshairi anasema:

Mwandishi yeyote atatoweka * na alichokiabdika kitabakia

Basi mkono wako usiandike  kitu isipokuwa * siku ya kiama ukikiona utafurahi

Kila mtu aelewe jukumu la neno na kuwa atasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na mbele ya dhamira yake kwa kila alichokizungumza, ili isije ikawa ndio sababu  ya kutengana na kukimbiana kati ya wanajamii na mtu na mwengine na kutengana kati ya mwanfamilia na kuharibu mahusiano kati ya watu.

Tunahitajia sana maneno mazuri ya kweli kati ya watu na jamii ili kueneza mapenzi na ukaribu na kuondosha mtengamano na mfarakano. Neno zuri lina athari nzuri na yenye kuleta masilahi mazuri na pia huleta msamaha wa makosa. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawa sawa 71. Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt’ii MwenyeziMungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.} (Al ahzab. 70-71).