Uzuri, furaha na hisia njema

Mokhtar-300x198

Uisilamu ni dini ya ustaarabu na upendo, dini ya furaha na maelezo yake na njia zake zote zinathibitisha hili na hata kurani tukufu na hadithi za mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) pia zinathibitisha hili. Mwenyezi Mungu anasema katika kurani { Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. 6. Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na mnapo-   wapeleka malishoni asubuhi.}

 Na anasema pia { Ambaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na akakupitishieni humo njia, na akakuteremshieni kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za mimema.} na kuendelea kusema { na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.} {, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.} na kusema pia {17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?19. Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?} na anasema pia { Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema.}ama kuhusu mbingu zilizo juu anasema { na tumezipamba kwa wenye kuangalia.} { Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa,}

Kurani tukufu imetuamrisha kujipamba kwa mapambo mazuri na tuchukue mapambo yetu kila tuendapo misikitini (tusalipo). Mwenyezi Mungu anasema { Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu 32. Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.} Na Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) aliposema: “ haingii peponi mtu mwenye chembe ndogo ya kiburi (dharau). Mtu mmoja akasema: “kuna mtu hupendelea nguo yake iwe nzuri na viatu vizuri.” Mtume akasema: “ Mwenyezi Mungu ni mzuri hupenda uzuri, kiburi ni kukana ukweli na kudharau watu.” (muslim). Na sayidna Mughira bin Shuuba (Mungu awie radhi) alipomueleza kuwa yeye amemchumbia mwanamke, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akamwambia: “mwangalie kwani itapelekea kudumu kati yenu.” (Tirmidhiy).

Mtume (rehma na amani zimshukie alikuwa kipenda uzuri, na alilingania pia uso wa bashasha akasema: “jambo jema lolote usilidharau hata kama utakutana na mwenzio basi iwe kwa uso wa bashasha.” (Muslim). Na  kusema kuwa kuingiza furaha kwa watu ni kitu kimuwekacho mtu karibu na Mwenyezi Mungu akasema: “ mwenye kuingiza furaha katika nyoyo ya muisilamu basi ni haki ya Mwenyezi Mungu kumridhisha siku ya kiyama.” Na akasema “ amali zipendwazo sana na Mwenyezi Mungu ni furaha uiingizayo kwa muisilamu.” Na akawataka masahaba zake kuvaa nguo nzuri wakati wanapokutana na katika sherehe na minasaba

Pamoja na kuwa uzuri wa kweli haupo katika mandhari ya muonekano na uzuri wa vitu lakini unavuka mipaka zaidi nao ni uzuri tabia na mwuonekano. Mustafa Saadiq Rafii (Mungu amrehemu) anasema: “ mwanamke mbora ni yule mwenye sura nzuri kama tabia zake na akili yake ikawa uzuri wake wa tatu. Mwanamke huyu akiwa na mwanamke mwenye kuendana nae basi atamfurahisha na kumfurahisha na kumfurahisha. Mshairi anasema

Mtu iwapo hajalaumiwa kwa heshima yake

Basi nguo yoyote aivaayo huwa nzuri

Tunaelewa kuwa kidogo huwa ni kingi

Nikasema kuwa ukarimu huona kidogo

Sikudhurika kwa kidogo na jirani yetu

aliye mwema ni mwenye nguvu

na jirani mwenye wengi ni  dhalili

Inatulazimu sote kujipamba kwa tabia za kiisilamu katika muonekano wetu, mazingira yetu, mashule yetu, vhuo vyetu, bustanini mwetu, matembezini mwetu na katika sehemu zote. Na wala tusifanye yenye kuondosha  furaha na ucheshi.

Na katika alama kubwa sana za ucheshi na ziletazo furaha ni neno zuri lililo jema, sayidna Umar bin Khatab (Mungu amwie radhi) alipita kwa watu waliokuwa wakiota moto akachukia kuwasalimia kwa kusema “amani iwe juu yenu enyi watu wa motoni” isipokuwa akasema”  amani iwe kwenu enyi watu wa kivulini”. Na kama ulivyotulingania uisilamu kuwa tuchague majina yenye maana nzuri na kujiepusha na majina mabaya yasiyoendana na hisia za kiutu, kwani kurani imetuamrisha kufanya kila lililo zuri na jema na kusema kila lililo jema. Mwenyezi Mungu anasema { nasemeni na watu kwa wema,} Albaqara 83. Na akasema { Waambie waja wangu waseme maneno mazuri,} Israa 53. Basi kauli mbiu yetu ni “hisia njema na uzuri”. Hisia nzuri ni kigezo cha kujua uzuri na kuueneza kwa waliotuzunguka katika wanajamii.