Kisa cha masanamu na ubomoaji wa ustaarabu

Mokhtar-300x198

Kwa kuanzia, hakuna muisilamu duniani mwenye kuabudu sanamu. Au hata kuamini jambo hilo pia hata kulingani kuabudiwa au kufikiria tu jambo hilo, si muisilamu tu mwenye kuamini hivi lakini pia hata wale wa dini zilizoteremshwa. Na iwapo uisilamu umekataza kutengeneza masanamu mwanzoni mwa uisilamu basi hili lilikuwa kwa sababu mbili; Ya kwanza. Watu walikuwa bado ni wapya katika uisilamu na walikuwa wameacha kuabudu masanamu kwa muda mchache (tangu kuingia kwao katika uisilamu) kwa kudhania kuwa yanawaweka karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu. Kama iliyoeleza kurani tukufu kwa ndimi zao pale Mwenyezi Mungu aliposema { Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu }. Sababu ya pili:Iwapo masanamu haya hutengenezwa kwa ajili ya kuabudiwa au kutengenezwa kwake ni kwa ajili ya kumfananisha na Mwenyezi Mungu. Na kati ya yenye kuthibitisha hayo na kuwa tukiachilia mbali kuondosha masanamu yaliyokuwa yakiabudiwa ndani ya Alkaaba kwa ajili ya kuisafisha haikuthibiti kuwa kuna sahaba yeyote aliyevunja sanamu au athari yoyote ile ya sanamu katika nchi yoyote katika zile walizozifungua. Hii ni kwa kuwa walifahamu malengo ya makusudio ya uisilamu ufahamu ulio sawa na wala hawakusita kusimamia ufasiri wa aya kijuujuu. Lakini waliangalia kwa undani zaidi juu ya makusudio na malengo kwa dalili ya kuwa walijua madhumini ya aya, hata sayidna umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) pale alipozuia fungu la sadaka kwa wale wanaozoweshwa nyoyo zao 2 katika uisilamu pamoja na kuwa imethibiti ndani ya kurani, Mwenyezi Mungu aliposema { Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika njia ya Mwenyezi Mungu,) na alipoulizwa Umar( Mwenyezi Mungu amwie radhi) iweje unasimamisha fungu ambalo Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akilitoa? Akasema: “ tulikuwa tukiwapa na uisilamu ni dhaifu na kwa lengo la kuwazowesha lakini sasa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameupa nguvu uisilamu kwa fadhila zake kwa ajili hili fungu hili halina kazi tena. Na zaidi ya haya, alizuia kutimizwa hukumu ya wizi katika mwaka wa njaa pale alipomwandkia mmoja wa wafanya kazi wake, utafanya nini akikujia mwizi (mtu kaiba)? Akasema: nitamkata mkono wake.” Akasema: “ mimi akinijia mwenye njaa basi nitaukata mkono wako. Isipokuwa umma wetu wa kiisilamu umefikwa na mitihani mikubwa akili za watu wake zikasimama wakaanza kuhalalisha na kuharamisha bila ya elimu, ufahamu na wala kujua, wakajidhatiti kwa nafsi zao na za wanafunzi na wafuasi wao kwa yale wasiyo kuwa na elimu nayo kwa kutoa fatwa, wakapotea na kupoteza wengine, pia kufungua mlango mpana wa kuwapa mwanya watawala na mabeberu kufuta athari za ustaarabu wetu sawa ustaarabu wa kiarabu, kiisilamu, kikiristu, kifirauni, kiashuri, kibabeli, kiyunani, kirumi na ustaarabu mwengine. Hii ni kwa kufuta utajo wa waarabu na pia ustaarabu wake na ustaarabu wa kiisilamu na pia wa kikiristu. Kwa kuwa wao ni wajinga wa tabia na 3 wasio na dini na wala maadili. Kwao wao ni kufikia malengo yao pasi na kutizama sababu na hata kama kuangamiza wanadamu na majengo na kila kikavu na kibichi pia hata kubomoa ustaarabu wa kibinaadamu. Mbaya zaidi ni kuwa haya yanatendeka kwa jina la dini na baadhi ya watu huidhania dini vibaya na kuona ni ya kiadui kumbe dini ipo mbali sana na mambo haya. Na hata kama watajidanganya wenyewe na kuwahadaa wahanga wao (wafuasi wao) katika vijana wenye kujiunga nao kwamba wao wapo sawa. Hao ni kama wale aliosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, {na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu. Kwa hakika hao waliwafanya mashet’ani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka} na anasema {Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri} {. Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu. 205. Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.} Na kiongozi mkuu wa Al Azhar Profesa Ahmad Al-Twayib amesisitiza kama alivyosisitiza waziri wa wakfu na Dar Al-Iftaa ya Misri, kuwa haifai kuharibu alama hizi za ustaarabu kwa namna yoyote ile sawa iwe kwa kuzivunja, kuziharibu 4 mkuziuza, kuziiba au kuzibomoa na kuziharibu ni sawa na kuharibu ustaarabu wa mwanadamu. Na katika jambo lenye kuhitaji mazingatio na lenye kuleta hisia na mshangao na kuleta masuala mengi ni msimamo wa nchi za magharibi na mashirika ya kimataifa juu ya kimya chao kikubwa juu ya makosa haya ambayo lau kama yangelitokea sehemu yoyote hapa ulimwenguni ukiachilia mbali eneo la mashariki ya kati (ukanda wa kiarabu) basi ulimwengu wote ungelijua. Basi hii ndio tabia ya maadui zetu ambao wanatushajiisha katika vita visivyo vya sheria, na lenye kuuma zaidi ni zile Fatwa ambazo hutilia mkazo matendo ya aina hii, hivyo basi tunahakikisha na kuthibitisha tena na tena kuwa kuna haja kubwa ya kuweka sheria ambazo zitazingatia utoaji wa Fatwa kwa kutolewa na wale tu wenye ujuzi nazo na si wengine.