Miji mikuu, mipaka na ujenzi wa taifa

Mokhtar-300x198

Uhusiano kati ya miji mikuu na mipaka yake ni uhusiano wa kukamilishani na si wa kugombana na wala haitakikani iwe hivyo, kwa kuwa hakuna taifa lolote ambalo linaweza kujitosheleza kufanya kuwa mji mkuu ndio kitovu na kusahau pande nyengine za taifa kwani bila ya mipaka taifa haliwezi kusonga, isipokuwa tu mataifa mengi huifanya miji mikuu kuwa ni kituo kikubwa walichokipa kipaumbele na mifano ya kihistoria inaweka wazi ushahidi wa jambo hili. Isipokuwa kuna tafauti kati ya mataifa yaliyoendelea na mataifa yasiyoendelea katika kutoa umuhimu wa miji mikuu. Mataifa yaliyoendelea haiwezekani kuzembea hata kidogo kuhusu hata kipande cha ardhi, jengo au sehemu na kuiacha ikiharibika au kufanyia uharibifu au hata fikira tu za kutaka kujitenga (kama ni maeneo). Mshairi mmoja alikwenda kwa Umar bin Abdul Aziz (Mungu amwie radhi) akamsomea shairi akasema: Iwapo unahifadhi unaowamiliki basi elewa Wafanyakazi wa ardhi yako ni mbwa mwitu Hawajaitikia wito wako uliowaita Mpaka wapigwe viboko na kukatwa shingo Na kwa kuwa ukuaji wa maeneo na sehemu za mipakani si jukumu la serikali pekee au viongozi wa kisiasa, kwani hifadhi na umuhimu pamoja na kazi za ukuzaji ni jukumu linalokusanya taasisi zote za nchi, sawa na iwe taasisi rasmi au mashirika ya kijamii, wafanyabiashara, watega uchumi, sekta za elimu, sekta za afya, za ujenzi, za tamaduni, wizara ya wakfu, na wizara nyengine na mashirika pia, pamoja na jumuiya za huduma za kijamii. 2 Wote hawa inabidi watilie umuhimu mkubwa na hasa maeneo ya mipaka. Na walipe kipaumbele na kuona kuwa ni suala linalohusu usalama wa taifa kwa upande mmoja na la ukuzaji kwa upande wa mwengine. Na inatakikana sote kwa pamoja tuyageuze maeneo ya mipakani iwe ni maeneo ya kuvutia na si ya kukimbiwa. Na inapotokezea taifa kutojali maeneo haya basi huwa ni nafasi kwa makundi kufika katika maeneo haya na kufanya kambi zao na kusababisha msongamano usio wa kawaida kwa vituo vya huduma za kijamii na kupatikana uwepo wa ujenzi wa kiholela, na hata kusababisha kukuwepo kwa maisha ya kitabaka, maradhi na matatizo mengine ya kijamii ambayo yatahitaji udhibiti usio wa kawaida ili kuyatatua. Ama kwa upande wa taifa kujali na kutoa umuhimu wa maeneo haya ya mipakani kwa upande wa vitega uchumi, ni kule kuweka huduma za lazima kwa wananchi wake: makazi, afya, elimu, utamaduni, na huduma nyenginezo ambazo zinahitajika kuendeleza maisha katika ardhi yao. Pamoja na kuwepo kwa nafasi za kazi na uzalishaji. Hayo yote yatapelekea kwa wananchi kuipenda ardhi yao (taifa lao) na kuhifadhi chembe ndogo ya mchanga ili isipotee pamoja na kuwafanya wawe wazalendo. Na panapokuwepo kwa vivutio na ushajiishaji wa kazi katika maeneo haya na kuwepo kwa vitega uchumi madhubuti kama nchi inayotilia mkazo ilivyo hivi sasa katika maeneo ya Sinai, Matruh na Ismailia mpya, Halayib, Shalatin na Wadi Jadid, na maeneo mengine kama yale ya jangwani. Maeneo haya karibuni yatabadilika na kuwa ya kuvutia. Kitu ambacho kitapelekea kuwepo kwa ugawaji sawa wa kijiografia, kimakazi na pia utawezesha kuwepo kwa maisha mazuri kwa wananchi wa maeneo hayo. Na kupunguza msongamano wa utoaji wa huduma kwa wakazi wa maeneo hayo, au kupatikana huduma kama zile zipatikanazo katika miji sawa huduma za kisiasa au za kiuchumi. Na kuwepo kwa vivutiaji vitakavyowezesha kuvutia watalii na kuushangaza ulimwengu na kuonyesha ukubwa na upevu wa wanachi wa ukuaji wao.