Hutoba ya Ijumaa

Ubora wa maadili katika ujumbe wa Muhammad
14 Rabi`u awal 1437H. Sawa na 25 Disemba 2015 A.D

awkaf

Kwanza :Vipengele

 1. Uisilamu ni dini ya maadili mema.
 2. Kuporomoka kwa maadili ni kuporomoka kwa umma.
 3. Maadili ni matunda ya matendo sahihi.
 4. namna gani tutatukuka kupitia maadili yetu?

Pili: Dalili

Katika Kurani Tukufu:

 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema { Na hakika wewe una tabia tukufu.} Alqalam, 4.
 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili} Al aaraf, 199.
 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitae kwa Mwenyezi Mungu, na akasema: hakika mimi ni katika Waisilamu 34. Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. 35. lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.} Fuswilat 33 -35.
 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema { Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!} Alfurqaan, 63.
 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema { Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha. 19 Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.} Luqman, 17-19.
 2. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Soma ulivyofunuliwa katika kitabu, na ushike sala, hakika sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ni jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda. 46. wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu nayaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja. Na sisini wenye kusilimi kwake. } Al ankabuut, 45-46.
 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili !} Al baqarah, 197.
 1. Mwenyenzi Mungu Mtukufu anasema {Wala usimt’ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. 12. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, 13. Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. 14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto! 15. Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! 16. Tutamtia kovu juu ya pua yake.} Alqalam 10-16.

Katika hadithi za Mtume (Saw)

 1. Kutoka kwa Nawaas bin Sama`n Al-answaary (Mwenyezi Mungu amwie radhi) kwamba yeye amesema: Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) kuhusu wema na ubaya? Akasema: “wema ni tabia njema, na ubaya ni uliopoَّ ndani ya moyo wako na ukachukia watu wengine wasikione.” (Sahihi Muslim).
 1. Kutoka kwa Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ Hakuna kitu cha muumini ambacho kitakuwa kina uzito kwenye mizani yake siku ya kiyama kuliko tabia njema, na hakika ya Mwenyezi Mungu anamchukia muovu mwenye tabia chafu.” (kitabu cha Tirmidhy).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) “ Hakika mimi nimetumwa ili kutimiza matendo mema” (Imepokewa na Imam Ahmad).
 1. Kutoka kwa Abi Durrin (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) ameniambia: “ Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na fuatishia jema kwa baya ili ulifute, na ishi na watu kwa tabia njema.” (Imepokewa na Tirmidhiy).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) “Muumini aliyekamilika imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake.” (Imepokewa na Ahmad).
 1. Kutoka kwa Saa`d bin Hisham bin Amir Al answaari (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: Nilisema “ewe mama wa waumini –yaani Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), – nieleze kuhusu tabia za Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema “ kwani wewe si unasoma Kurani? Nikamwambia ndio, akasema: “Basi hakika tabia ya Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) ilikuwa ni Kurani.” (Imepokewa na Muslim).
 1. Kutoka kwa Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: “ nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ hakika ya muumini hujulikana kwa uzuri wa tabia zake na kwa vyeo vya kusimama usiku na kufunga mchana.” (Imepokewa na Abu Daudi.)
 1. Kutoka kwa Jabir (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ hakika ya nimpendae kati yenu na atakaekuwa karibu nami kwenye kikao siku ya kiama ni yule mwenye tabia njema, na hakika ya nimchukiae kati yenu na atakaekuwa mbali nami kwenye kikao siku ya kiama wenye kuropokwa, wenye kusema sana na wenye kujigamba” Masahaba wakamuuliza ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu tumekwishamuelewa ni nani mropokwaji na msema sana َlakini ni nani huyo mwenye majigambo ََ? Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akasema ni wenye kiburi.” (Amepokea Tirmidhy.)

Tatu: Maudhui

Hakuna shaka ya kuwa namna ya kuupata utukufu ndani ya uisilamu ipo za aina tofauti, na katika utukufu wake ni kuwa ni dini ya sheria na tabia, inayokusanya maadili na utu wa hali ya juu, ambau unaweka pamoja sura ya kipekee ya tabia njema. Na dini hii inatukuka kwa kuwa imekusanya njanja zote za maisha, haikuacha jema miongoni mwa mambo mema isipokuwa imekusanya na kulilingania na kuhimiza kulishikilia, wakati huo huo haikuacha ovu isipokuwa imeliweka wazi na kulitahadharisha na kuamrisha kuliepuka.

Na katika mambo mazuri ambayo yamelinganiwa na kupendezeshwa kwa kuwa nayo ni: Kujipamba na tabia njema kama subira, upole, huruma, ukweli uaminifu, kutimiza ahadi, ukarimu, haya, kunyenyekea, ushujaa, uadilifu, wema, kusaidia, kuweka macho chini, kuondoa uchafu, ubashasha wa uso, maneno mazuri, dhana nzuri, kumheshimu mkubwa, kusuluhisha kati ya watu, athari njema, kuchunga hisia za wengine na tabia njema nyenginezo. Na haya yote ni kama ilivyoashiriwa katika aya ya Kurani Tukufu {Hakika hii kuran inaongoa kwenye yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.) Al israa 9.

Na kwa jambo hili kuna aya na hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu nyingi sana, kwa mfano Mwenyezi Mungu anamuamrisha Mtume wake kwa kusema {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili} Al a`raf 199. Pia anasema {na semeni na watu kwa wema} Al baqara 83. Anaongeza kusema tena { Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa} Alnisa 144. Na aya zenye ujumbe kama huu ziko nyingi.

Na kwa kila mwenye kuzingatia aya a Kurani na akachuguza kwa kina atagundua ya kuwa muna aya nyingi sana zenye kulingania katika tabia njema na kuhimiza watu wawe nazo. Na si  kwa chochote zaidi ya kuwa tabia ni kama mizani ya kisheria yenye kumpima mtu na kumpandisha mtu daraja za ukamilifu.

Na kama hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu zilivyosisitiza juu ya umuhimu wa tabia katika maisha ya mwanadamu. Kwa kuweka wazi malipo kwa mwenye kuwa nazo, kwa mfano Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: “wema ni tabia njema” (imepokewa na Imam Muslim.) na wema ni neno lenye kumaanisha kila lililo zuri. Na hadithi nyengine ya Mtume wa Mwenyezi Mungu: “ Hakuna kitu cha muumini ambacho kitakuwa kina uzito mkubwa kwenye mizani kushinda tabia njema” na katika mapokezi mengine: “ Hakuna kitu cha muumini ambacho kitakuwa kina uzito mkubwa kwenye mizani siku ya kiyama kuliko tabia njema, na hakika ya Mwenyezi Mungu anamchukia muovu mwenye tabia chafu.” (imepokewa na Tirmidhy katika kitabu chake kutoka kwa Abi Dardai.)

Na hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akihimiza watu wawe na tabia njema, kwani baadhi ya wakati huwa anasema “Muumini aliyekamilika imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zao.” (Imepokewa na Ahmad).

Na akaulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu: “ Ni muumini gani aliye bora? Akasema: “ Mwenye tabia njema kuliko wote” (imepokewa na Ib Maajah.

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoulizwa kuhusu kitu ambacho kitawaingiza kwa wingi watu peponi akasema: “ucha Mungu na tabia njema.” (Kitabu cha Tirmidhy.)

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akafanya kuwa miongoni mwa mapenzi ya kumpenda yeye ni kuwa na tabia njemaakasema: “hakika ya nimpendae kati yenu na atakaekuwa karibu nami kwenye kikao siku ya kiama ni yule mwenye tabia njema.” (Kitabu cha Tirmidhy.)

Maadili yana nafasi yake kubwa sana ndani ya uisilamu, kwani ni kiini cha dini na johari yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) alipoulizwa: “ dini ni nini? akasema: “tabia njema” (Imepokewa na Muslim.)

Si hivyo tu bali pia Mtume wa Mwenyezi Mungu amezipa tabia umuhimu wa hali ya juu pale alipotangaza kwa kusema kuwa, lengo kuu la kutumwa kwake na la ujumbe wake ni kutimiza maadili mema akasema: “ hakika nimetumwa kwa ajili ya kutimiza tabia njema.” (Imam Buhkari.)

Na hata kabla utume watu walikuwa wakimuita mkweli muaminifu. Hizo ndizo tabia njema za kiisilamu ambazo zinakwenda sambamba na imani ya ukweli, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa ni mfano wa hali ya juu kabisa wa tabia njema, kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wake akamsifu kwa kusema {Na hakika wewe una tabia tukufu} Al qalam 4.

Na huu ni ushahidi mkubwa sana kutoka kwa Mkuu Alietukuka kwa Mtume wake (Rehma na amani zimshukie juu yake), kwa uzuri wa tabia yake na wema wa maadili yake. Hakika ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa ni mwenye tabia njema kuzidia wote, kwani tabia ya Kurani yote aliikusanya yeye na akawa anaifuatisha na kujiepusha na makatazo yake, hapo ubaora ndipo ulipojikusanya na haya yanathibitishwa na mama wa waumini Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi), alipoulizwa  kuhusu tabia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ tabia yake ilikuwa ni Kurani.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa ni mfano wa kimatendo katika kuifuata Kurani, alikuwa ni mwenye tabia bora zaidi kuliko watu wote, na pia alikuwa na upendo, huruma, ucheshi, msamaha kuzidi wote, mkweli anapozungumza, anapotoa ahadi, na mkarimu kwenye familia, na ni mfano katika unyenyekuvu pamoja ya kuwa yeye ni bwana wa viumbe,  amuonae ni lazima amtukuze, ukiungana nae basi utampenda.

Mama wa waumini Khadija (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amemtakasa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kumwambia: “ hakika wewe utaunga koo, utavumilia vishindo, utampata asiyekuwepo na utakuwa ni mwenye kuwarudisha watu katika haki.”

Na Mola wake pia akamsifu kwa kusema {Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea} Al imraan 159. Na kwa tabia hii basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) ameweza kuathiri nyoyo na akili.

Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) aliwalea masahaba zake katika tabia njema na kuwaamrisha kujipamba nayo na kuishikilia, na haya ni kama alivyosema kumambia Abi Dhari (Mwenyezi Mungu amwie radhi), “ mche Mwenyezi Mungu popote ulipo na fuatishia jema kwa baya ili ulifute, na ishi na watu kwa tabia njema.” Wakajifunza upole, msahama na hisani na kujiepusha na maasi na hasira wakawa ni wema na wavumilivu, wakawa pia ni mfano wa hali ya juu katika tabia na muamala na ukarimu sawa kwa mtu mmoja mmoja au kwa pamoja.

Mtume wa Mwenyezi Mungu alipohama kutoka Makka kwennda Madina na kuwaunganisha undugu kati ya muhajirina na Maanswari, Ansari alikuwa akimuunga mkono ndugu yake muhajirina kwa nusu ya mali yake, kwani tabia ya mwanadamu hujulikana kwa kadir ya utoaji wake, na kurani metupa mfano mzuri ambao haukusudii kumlenga mtu maalumu, isipokuwa ni sifa kwa waumini wote, Mwenyezi Mungu anasema {bali wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa wenyewe ni wahitaji} Al hashri 9.

Kwa ajili ya tabia hizo umma ukaongoza, ukawa unaangaliwa kuwani igezo kwa kule kushikamana na tabia njema iliyotukuka. Na watu walikuwa wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi kwa kuona tabia na muamala mzuri, na maadili mema. Ama wakati tabia zilipoanza kubadilika na maadili ya watu kuanza kupotea; kigezo chema kikatoweka na ufahamu ukabadilika, hakika amesema kweli imamu Malik (Mwenyezi Mungu amwie radhi), aliposema “Umma huu wa mwisho hautopata kuwa mzuri isipokuwa kwa kufuata umma wa mwanzo.

Maadili ni kitu bora ambayo jamii kujikinga na upotovu, na kuihifadhi na misukosuko na kupotea, amani ya umma na nguvu za ujenzi wake na kuimarika nafasi yake ipo katika maadili mema. Na kama ilivyo kuwa kuenea kwa uchafu na maovu ni kwa sababu ya kujiweka mbali na maadili mema na vitendo vizuri.

Tengeneza tabia yako kwa matendo mazuri * ijenge nafsi yako kwa maadili ili isiyumbe.

Ipe nafsi ubora naa fya njema * kwani nafsi kwa maovu huwa duni.

Kwa ajili hiyo, kuwa na hadhari juu ya kuporomoka kwa maadili ni jambo la kusisitizwa. Kutoka kwa Sahli bin Saa`d Saa`idi (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kwamba yeye amemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “ Hakika ya Mwenyezi Mungu ni Mkarimuna anawapenda wakarimu na hupenda tabia njema na huchukia mambo machafu.”

Maadili hulifanya taifa kukua na athari zake hubakia milele, na kwa kutokuwa na maadili mema taifa husambaratika na huanguka. Ni Staarabu ngapi zimeporomoka na si kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi au nguvu zake za kijeshi lakini ni kwa sababu ya kuwa na maadili maovu. Mwenyezi Mungu amrehemu kiongozi wa mashairi. Aliposema:

Hakika umma utabakia kwa kubaki maadili * wakikosa maadili basi na umma hutoweka.

Na ukizingatia ibada ndani ya kurani na hadithi za Mtume tutagundua kuwa malengo hasa makuu ni: kuijenga tbia njema ya muisilamu na kumpamba kwa maadili, hakuna ibada ambayo Mwenyezi Mungu ameiamrisha mfano; sala, saumu, zaka, na kuhiji isipokuwa ina athari ambayo inaonekana ndani ya tabia ya mtu, si hivyo tu, bali tabia hii huathiri mtu hadi jamii kwa ujumla. Uisilamu si kufanya ibada zisizo na natija ndani ya msikiti ambazo hazina mfungamano na maisha ya nje (ya msikiti), ikawa aliyesali baada ya sala atoke kisha afanye ghoshi, adanganye, amuudhi jirani yake, si hivyo. Lakini ibada zimeletwa kwenye dini zote ili mwanadamu awe na utu na tabia iwe njema. Kwa mfano sala, Mwenyezi Mungu ametuwekea wazi hekima yakusaliwa. Akasema {Soma ulivyofunuliwa katika kitabu, na ushike sala. Hakika sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndio jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.} Al ankabuut 45. kujiepusha na maovu na kujitakasa na kauli chafu na matendo mabaya hivi ndivyo sala itakiwavyo. Kutoka kwa Ibn Abass (Mwenyezi Mungu awawie radhi), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: hakika ninaikubali sala kwa anaenyenyeyekea kwa utukufu wangu, na akawa hajitukuzi mbele ya waja wangu, na wala haendelei kuniasi, na akawa naumaliza mchana wake kwa kunitaja, na kuwahurumia masikini, na wapiti njia na wajane, na kuwahurumia wenye matatizo..” (Imepokewa na Bazaz.)

Na kutoka kwa Ib Masu`ud (Mwenyezi Mungu amwie radhi): “ Yule ambaye sala yake haimuamrishi kutenda mema na wala haimkatazi kuacha mabaya hatozidishiwa kwa Mwenyezi Mungu isipouwa kutengwa mbali.” (Imepokewa na Twabari). Basi yule ambaye sala yake haimuweki mbali na maovu sawa iwe ya maneno au matendo, mtu huyu basi sala yake itakuwa haimfikishi katika lengo miongoni mwa malengo makubwa ya sala.

Na namna hiyo hiyo kwa upande wa utoaji wa zaka, kufunga, kuhiji na kwa upande wa ibada nyengine, utaona kuwa zimewekwa kwa kuitakasa nafsi na kumfanya mja atukuke kimaadili, na Mwenyezi Mungu anasema khusu zaka: {Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.} Al taubah 103.

Hivyo basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akalipambanua zaidi neno sadaka ambayo ni inampasa muisilamu kuitoa, imepokewa kwa Abi Dhari (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) “kutabasamu mbele ya uso a mwenzako ni sadaka, na kuiweka tupu ndoo yako na kuijaza ya mwenzako ni sadaka, kuamrisha mema na kukataza mabaya pia huandikiwa sadaka, kuondoa mwiba na jiwe njiani ni sadaka, kumuongoza aliyepotea njia pia ni sadaka.” (Imepokewa na Bazaz).

Na swaumu ni ibada miongoni mwa ibada alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kufanikisha uchamungu, matunda na malengo ambayo Mwenyezi Mungu anayataka yafikiwe na mja ni uchaji Mungu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu} Albaqara 183.

Kwa kupitia funga utashi wa muumini huwa na nguvu na anakuwa na uwezo wa kuidhibiti nafsi yake na matamanio yake, kwani imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “ Funga ni kinga, basi asisema maneno mabaya wala kutenda mabaya, na iwapo mtu amempiga au kumtusi basin a aseme; mimi nimefunga.” (Imepokewa na Bukhari). Hii inamaanisha kuwa funga yake inabidi imlinde na kuwa na tabia chafu na matendo maovu, funga ni lazima iache athari za tabia njema kwa muisilamu na katika maadili yake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!} Albaqara 197. Na kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake): “ atakaeijia nyumba hii akawa hajanena upuuzi, na wala kufanya uchafu basi atakuwa amerejea kama kwamba amezaliwa na mama yake”. (Imepokewa na Muslim.)

Kwa upande wa ibada ni lazima iache athari njema kwa mtu na kwa jamii, na iwapo ibada hazitoleta athari yoyote kwa mtu na maadili yake na nyenendo zake huwa haina thamani yoyote siku ya kiyama, kwa sababu matendo maovu hula zile ibada na mema kama ambavyo moto unavyokula kuni. Imepokewa na Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) amesema: “ Munamjua ni nani muflisi? Wakamjibu, mtu aliyefilisika miongoni mwetu ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na dirhamu wala starehe, akasema (Rehma na amani zimshukie juu yake) “ Mtu aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakaekuja siku ya kiama na sala zake, funga zake, na zaka zake, na atakuja hali ya kuwa kamtukana huyu, kamzulia huyu, amekula mali ya huyu na kumwaga damu ya huyu na amempiga huyu, atakaa na kupunguzwa katika mema yake, n kwa huyu yatachukuliwa mema yake, na yatakapomalizika mema yake, kabla ya kumaliza kuhesabiwa huchukuliwa madhambi yao na kupewa yeye kisha hutumbukizwa motoni.” (Imepokewa na Tirmidhy.)

Na alipoulizwa (Rehma na amani zimshukie juu yake) ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu; “ hakika ya fulani hutajwa kwa kuwa anasali sana, anafunga sana, na anatoa sadaka sana isipokuwa anawakera majirani zake kwa ulimi wake, akasema; “yeye ataingia motoni”. Akasema: “ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika ya fulani hutajwa kuwa ni mchache wa kufunga, na sadaka zake, na sala zake naye hutoa sadaka kwa, isipokuwa hawakeri majirani zake kwa ulimi wake; akasema “yeye ataingia peponi.” (Imepokewa na Ahmad).

Hakika tabia njema (maadili mema) inakusanya kwa viumbe vyote, hakuna tafauti kati ya muisilamu na asiye muisilamu, wote ni ndugu kwa ubinaadamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} Israa 70.

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliposimama lilipopitishwa, akaambiwa: ni jeneza la Myahudi, mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) “je kwani si nafsi? (imepokewa na Bukhari).

Na Mwenyezi Mungu {wala msijadiliane na watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.} Al ankabuut 46. Na kutoka kwa Mujahid, kwamba Abdallah bin Amru (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amechinjiwa mbuzi na familia yake, alipofika akasema: je mumempa jirani yetu myahudi? Je mumempa jirani yetu myahudi? Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) akisema: “ Jibrilu hakuacha kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhani kuwa anaweza kumrithi” (Imepokewa na Tirmidhy.)

Na tabia njema si kwa wanaadamu tu pekee, isipokuwa inakusanya hata wanyama pia, kwani Mwenyezi Mungu amemuingiza kijana peponi kwa sababu ya mbwa aliyemyweshelezea maji. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), “hakika ya kijana alimuona mbwa anakula mchanga kutokana na kiu, kijana akachukua khofu yake akawa anamchotea kwayo maji mpaka akamywesha, akamshukuru Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akamuingiza peponi” (Imepokewa na Bukhari). Na namna kama hiyo Mwenyezi Mungu amemuingiza mtu motoni kwa sababu ya paka, imepokewa na Ibn Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi), hakika ya Mwenyezi Mungu amesema “mwanamke ameadhibiwa kwa sababu ya paka amemfunga na wala hakumuacha huru akila masalia ya ardhini.” (Imepokewa na Bukhari).

Iwapo tunataka kujiimarisha kitabia na kuinuka kwa jamii yetu hatuna budi kufuata vigezo vyema. Vigezo ni kitendea kazi muhimu katika kujenga maadili, Mwenyezi Mungu anasema {Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana } Al Ahzab 21. Kwani mzazi anatakiwa kuwa ni kigezo kwa mwanawe, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) ametueleza kwamba ya mtoto huzaliwa katika maubile safi, maumbile ya Mwenyezi Mungu aliyowaumbia watu, kisha tena kigezo ndicho kitakachombadilisha ima kizuri au kibaya. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie juu yake) “ hakuna kizaliwacho isipokuwa huzaliwa katika  maumbile (uisilamu), ima baba yake humfanya kuwa myahudi, au mnasara au mmajusi…” Kisha akaendelea kusema Abu Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), {Basi uelekee uso wako sawasawa kwenye dini ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyoonyoka sawa.} Ruum 30. (Imepokewa na Bukhari).

Vile vile mwalimu  ni kigezo kwa wanafunzi kwa mwenendo wake na tabia zake, wanafunzi inabidi wawe kama yeye kitabia. Siku moja imam Shafii ameingia kwa Harun Rashid pamoja na kijana Siraj, akawakaribisha na kuwaambia wakae kitako mbele ya Abdul-swamad ambae ni mwalimu wa watoto wa Rashid. Siraj akasema kumwambia Shafii: ewe Abu Abdallah! Hawa ni watoto wa Amir Muuminina, naye ni wanafunzi wake, unaonaje lau kama ungeliwausia.. Imam Shafii akamwelekea Abi Abdul-swamad akamwambia, “iwe kwako ewe kiongozi wa waumini ukitaka kuwarekebisha wanao ni itakubidi kuirekebisha nafsi yako kwanza, kwani macho yao yanaangalia macho yako, zuri kwao ni lile utakalolipenda wewe, na baya kwao ni lile uliachalo…” (Kitabu cha Hilliya Awliyaa. Abi Na`im).

Na jambo lililo muhimu kukumbushia  ni kwamba, tabia za mtu binafsi ambazo hujilazimisha kuacha na kujikataza na kitu,  n.k. na kuna tabia za kifamilia kati ya mtu na mkewe na kati ya mtu na wanawe na wazazi wake na watu wa karibu nae na ukoo wake na mfano wake. Pia kuna tabia za kijamii kwa mfano katika kuuza, kununua, ujirani, urafiki, kazini, … n.k. na pia kuna tabia za kimataifa kati ya nchi na nchi, na tabia za wakati wa vita na wakati wa usalama.

Na katika mambo ambayo humsaidia mja katika kuwa na tabia njema ni: kufanya kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kuomba awe na tabia njema, na pia kujitahidi ndani ya nafsi yake ili ashinde matamanio, na kuihesabu nafsi kila siku pamoja na kuzingatia mwisho wa kuwa na tabia mbaya na kwa yaliyowafika watu walioishi kwenye jamii mbaya.

Miongoni mwa aliyokirimiwa Mtume Muhammad (Saw)
7 Rabiul awwal, 1437 H. Sawa na 18 Disemba 2015 A.D.

awkaf

Kwanza: Vipengele

 1. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) tangu mwanzo wa kuumbwa.
 2. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) kabla ya kuzaliwa.
 3. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) kwa kuwemo katika na familia njema.
 4. Kutajwa jina lake Mtume Muhammad (Saw) kunaendana sambamba na utukufu wa utume na ubora wa risala.
 5. Wajibu wa kumpenda na kumtii Mtume Muhammad (Saw).
 6. Kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (Saw) kwa kupata ulinzi utokao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
 7. Ujumbe wake ni kwa walimwengu wote.
 8. Ujumbe wake ni rehem kwa walimwengu wote.

Pili: Dalili

Dalili ndani ya Kurani Tukufu

 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia.} (Al Imraan aya ya 81).
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.} Albaqarah aya 129.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!} Assa`f aya 6.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Mwenye kumt’ii Mtume basi ndio amemt’ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi waoAl nisaa aya 80.
 2. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.} Al Imraa aya 31.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri} Al maidah aya 67.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui } Sabaa 28.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} Al anbiyaa aya107.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu } Al ahzaab 56.
 1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu} Al nuur aya 63.

Dalili ndani ya hadithi

 1. Kutoka kwa Waathila bin Asqa`a (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ hakika ya Mwenyezi Mungu amechagua Kabila la Kinana kutoka katika kizazi cha Ismaili, na akawachagua Maquraishi kuwa ndio kutoka kwa Kabila la  Kinana, na katika maquraishi ukachagulia ukoo wa bani Hashim, na katika ukoo wa bani hashim akanichaguwa mimi”. (Imepokewa na Muslim).
 1. Kutoka kwa Irbaadh bin Saariya Salamiy amesema: nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ … mimi ni kutokana na  maombi ya baba yangu Ibrahim, na bishara ya Isa kwa watu wake, na nikutokana na ndoto ya mama yangu ambaye ameona nuru imechomoza na kuangaza majumba ya Sham.” (Kitabu cha Imam Ahmad).
 1. Kutoka kwa Abi Saaed (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kutoka kwa Mtume (Saw) kwamba yeye amesema: “Jibrilu alinijia akaniambia: hakiak mola wako na mola wangu anasema: Ni namna gani nimenyanyua utajo wako? Mtume akajibu: Mwenyezi Mungu ndie ajuae: Jibrilu akasema: nitajwapo mimi nawe hutajwa pamoja nami”) (Kitabu cha Zawaed cha Imam Haytham).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema “yeyote atakaenitii mimi basi kwa hakika amemtii Mwenyezi Mungu, na atakaeniasi basi kwa hakika amemuasi Mwenyezi Mungu” (Imepokewa na Muslim na Bukhari).
 1. Kutoka kwa Anas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “hatoamini mmoja wenu mpaka niwe ananipenda zaidi kuliko wazazi wake watoto wake na watu wote.” (Imepokewa na Muslim na Bukhari).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie), “hakika mimi ni rehema yenye kuongoa” (Imepokewa na Imam Hakim katika kitabu cha Mustadrik).
 1. Kutoka kwa Jabir bin Abdi Llah (Mwenyezi Mungu awawie radhi amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie): “ nimepewa mambo matano hakuna nabii yeyote aliyepewa kabla yangu: nimepewa ushindi wa kuwahofisha maadui kwa mwendo wa mwezi, nikafanyiwa ardhi kuwa ni msikiti na ipo safi na mtu yeyote katika umma wangu akifikwa na swala basi na aswali, na nimehalalishiwa ngawira, na ilikuwa nabii akipelekwa (akitumwa) kwa watu wake maalumu, ama mimi nimetumwa kwa watu wote, na nimepewa uombezi. ((Imepokewa na Bukhari).

Tatu: Maudhui

Hakika Mwenyezi Mungu amemkirimu mtume wake, ukarimu ambao hajawahi kumpa yeyote katika waja wake, mwanzo wa kuumbwa kwake (rehma na mani ziwe juu yake), kabla ya kuzaliwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake), baada ya kuzaliwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake), dani ya maisha yake na baada ya kufariki kwake (rehma na amani ziwe juu yake).

Ama ukarimu aliokirimiwa na Mwenyezi Mungu mwanzo wa kuumbwa ni; Mwenyezi Mungu ameuinua utajo wake kwa waliotangulia (umma wa mwanzo) na waliochelewa (umma wa mwisho), kwani hakuna Mtume yeyote aliyetumwa na Mwenyezi Mungu – kabla yake (rehma na amani ziwe juu yake) isipokuwa amechukua ahadi na utiifu iwapo atakutana na Mtume  rehma na amani ziwe juu yake) basi atamuamini na kumnusuru, Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: {Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia} (Al imraan aya 81). Mwenyezi Mungu Mtukufu akamzidishia Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake) ubora na heshima kwa ahadi hii ambayo imeshuhudiwa na Mitume wengine pia.

Na mitume waliotangulia pia walimbashiria, kutoka kwa Irbaadh bin sariyata Salamiy amesema: nimemsikia  Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “mimi ni kutokana na  maombi ya baba yangu Ibrahim, na bishara ya Issa kwa watu wake, na nikutokana na ndoto ya mama yangu ambaye ameona nuru imechomoza na kuangaza majumba ya Sham.” (Kitabu cha Imam Ahmad).

Na maombi ya sayidna Ibrahim (A.S) ni pale aliposema { Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.}  Albaqara 129. Ama bishara ya sayidna Isa (A.S) ni pale aliposema Mwenyezi Mungu { Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri}  Assa`f 6).

Na kuhusu kukirimiwa kwake Mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) na Mwenyezi Mungu kabla ya kuzaliwa kwake, ni kule kuitwa Muhammad. Amina bint Wahab alipokuwa akielezea namna alivyomzaa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake). Nimewasikia waliokuwa wakimbwambia; “ wewe umebeba mamba ya bwana wa umma huu, utakapomzaa tu basi sema: ninamrudisha kwa aliye Mmoja na aepukane na kila shari ya mwenye husuda, kisha umpe jina la Muhammad, kwani jina lake ndani ya kitabu cha Taurati ni Ahmad, atashukuriwa na wakazi wa ardhini na wa mbinguni. Na jina lake ndani ya kitabu cha Injili ni Ahmad atashukuriwa na wakazi wa ardhini na wa mbinguni.. na jina lake ndani ya Kurani ni Muhamad basi umwite kwa jina hilo. (Imam Bayhaqiy).

Hivyo basi, ukoo wake katika koo njema zaidi ya koo nyengine, kwani yeye rehma na amani ziwe juu yake) ni katika kizazi cha familia iliyo bora zaidi, imesemwa hayo na Mwenyezi Mungu { Na mageuko yako kati ya wanao sujudu } Ashuaraa aya 219, amesema Ibn Abbas, kinachokusudiwa ni katika migongo ya mababu, Sayidna Adam (A.S), Sayidna Nuh (A.S) na Sayidna Ibrahim (A.S) mpaka akazaliwa mtume wetu rehma na amani ziwe juu yake). (Tafsiri Ibn kathir).

Familia yake ni bora, na ni nyumba njema katika nyumba za waarabu, kwani Mwenyezi Mungu ameihifadhi na maovu ya kijahilia, na akamtoa katika migongo mitukufu mpaka kwenye tumbo jema kutoka kizazi hadi kizazi.  Mwenyezi Mungu amechagua  Kabila la Kinana kutoka katika kizazi cha Ismaili, na akawachagua Maquraishi kuwa ndio kutoka Kinana, na katika maquraishi ukachaguliwa ukoo wa bani Hashim, naye Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni katika uchaguzi ulio bora na mwema. Imepokewa na Waathila bin Asqa`a (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: nimemsikia  Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “ hakika ya Mwenyezi Mungu amechagua Kabila la  Kinana kutoka katika kizazi cha Ismaili, na akawachagua Maquraishi kuwa ndio kutoka Kinana, na katika maquraishi ukachagulia ukoo wa bani Hashim, na katika ukoo wa bani hashim akanichaguwa mimi”. (Imepokewa na Muslim).

Ama kukirimiwa kwake na Mwenyezi Mungu katika maisha yake rehma na amani ziwe juu yake). Jina na utajo wake umenyayuliwa duniani na akhera, kwani jina la Mwenyezi Mungu huwa halitajwi isipokuwa na jina la Mtume rehma na amani ziwe juu yake) hutajwa pamoja nae. Hakika amesema kweli Mwenyezi Mungu: {tukaunyajua utajo wako}.

Kutoka kwa Abi Saaed (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kutoka kwa Mtume (Saw) kwamba yeye amesema: “Jibrilu alinijia akaniambia: hakika mola wako na mola wangu anasema: Ni namna gani nimenyanyua utajo wako? Mtume akajibu: Mwenyezi Mungu ndie ajuae: Jibrilu akasema: nitajwapo mimi nawe hutajwa pamoja nami”) (Kitabu cha Zawaed cha Imam Haytham).

Na Mwenyezi Mungu ameliweka pamoja jina lake na jina la Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake) katika sehemu nyingi, kwani hata shahada ya anaesilimu huwa haikubaliwi mpaka amshuhudie kuwa yeye ni mjumbe mtume na upweke wa Mwenyezi Mungu.

Amesema Hassan bin Thabit (Mwenyezi Mungu amwie radhi):

Jina la Mwenyezi Mungu lipo na la mtume * pindi Muadhini akisoma adhana.

Hutaja jina hilo kwa utukufu * kwenye arshi ni Mahmud na huyu hapa ni Ahmad.

Jina la Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) hutajwa atajwapo Mwenyezi Mungu kwenye shahada mbili, kwenye hutuba ya Ijumaa, ndani ya Kurani Tukufu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka sambamba utiifu wa mtume kua ndio utiifu wa Mwenyezi Mungu, akasema: {Mwenye kumt’ii Mtume basi ndio amemt’ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao} Al nisaa 80.

Ibnu Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) alikuwa akisema: Aya tatu zimeteremshwa na kuambatana sambamba na aya tatu, hakuna aya hata moja yenye kukubalika bila ya aya nyengine (iliyo sambamba nae).

Ya  kwanza: { Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanao inama } Albaqarah 43.

Ya pili : { Nishukuru Mimi na wazazi wako} Luqman 14.

Ya tatu: {Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume} Al nisaa 59. kwani atakaemtii Mwenyezi Mungu na kuacha kumtii Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) mtu huyo haikubaliwi ibada yake.

Pia Mwenyezi Mungu ameweka sambamba uteuzi (uchaguzi) wa kumteua mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kuwa sana na kumteua Yeye Mwenyezi Mungu. Amesema {Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu.} Al fathi aya 10.  a kufanya kuwa, kumtii Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kuwa ni moja ya mafanikio ya kuingia peponi, akasema { Na anaye mt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.} Al ahzaab aya 71. Na aya nyenginezo.

Na imekuja katika hadithi kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake) amesema: “ watu wote katika umma wangu wataingia peponi isipokuwa atakaekataa”, akaulizwa: na ni nani atakaekataa ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “ atakaenitii mimi ndie atakaeingia peponi, na atakaeniasi mimi huyo ndie aliyekataa.” ( imepokewa na Bukhari).

Na hadithi ya Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi), wakati alipoliendea jiwe jeusi na kulibusu akasema: “hakika mimi ninaelewa wazi kuwa hili ni jiwe halidhuru wala halinufaishi, na lau kama nisingelimuona Mtume anakubusu basi nisingelikubusu”. (Imepokewa na Bukhari). Utiifu kwa Mwenyezi Mungu hautokamilika katu isipokuwa kwa kumtii mtume wake (rehma na amani ziwe juu yake).

Na vile vile katika kukirimiwa kwake Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) na Mwenyezi Mungu ni kufanywa mapenzi yake kuwa ni sehemu ya imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu, namapenzi a Mwenyezi Mungu ni mapenzi ya Mtume wake (rehma na amani ziwe juu yake). Kumfuata Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni alama ya upendo kwake, Mwenyezi Mungu amesema: { Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. } Al Imraan 31. Kumpenda mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni jambo la lazima kwa kila muisilamu. Imekuja katika hadithi Kutoka kwa Anas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie) “hatoamini mmoja wenu mpaka niwe ananipenda zaidi kuliko wazazi wake watoto wake na watu wote.” (Imepokewa na Muslim na Bukhari).

Si hivyo tu, bali hata imani ya mja huwa ni pungufu ndani ya moyo wake iwapo hatotanguliza mapenzi ya Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) zaidi ya nafsi yake, wazazi wake, na watu wote kwa ujumla.

Imepokewa na Abdallah Bin Hisham (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema: “ tulikuwa pamoja na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)naye ameushika mkono wa Umar bin Khatwab akasema kumwambia Umar: ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wewe ninakupenda sana isipokuwa nafsi yangu ninaipenda zaidi, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) akasema: “ hapana, naapa kwa yule ambae nafsi yangu ipo mikononi mwake mpaka niwe unanipenda kuliko nafsi yako”. Umar kamwambia Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) “ hakika kuanzia hivi sasa na ninaapa kuwa wewe ninakupenda zaidi kuliko nafsi yangu, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) akamwambia: “ Hivi sasa ewe Umar.” (Imepokewa na Bukhari).

Na inatosha kwa ampendae Mtume (rehma na amani ziwe juu yake)

Kuwa na ubora na bahati ya kufufulia pamoja nae mpenzi wake Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) siku ya kiama, na nii ni fadhila kubwa sana na ukarimu wa hali ya juu. Imepokewa na Anas Ibn Malik (rehma na amani ziwe juu yake) amesema: “tulipokuwa mimi na Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) tunatoka msikitini tukakutana na mtu kwenye mlango wa msikitini, akasema: ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kiama kitakuwa lini? Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) akasema “ je umejiandaa nacho? Kama kwamba yule mtu alikuwa amejawa na unyenyekevu  “kisha akasema: ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu sikujiandaa kwa kufunga sana, wala kwa swala, wala kwa sadaka lakini mimi ninampena mwenyezi mungu na Mtume wake, akasema: ‘ wewe basi utakuwa na umpendae”. (Imepokewa na Bukhari).

Na katika hali ya juu zaidi ya kukirimiwa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni kuwa Mwenyezi Mungu anapomzungumzia huwa hamtaji jina lake kikawaida kama anavyowataja mitume wengine wa kabla yake. Mitume wengine walikuwa wakiitwa majina yao kikawaida tu, mfano kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: { Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani,} Al baqarah 35.

{Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu,} Al Imraan aya 55.

{Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu } Hud aya 48.

{Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote } Al qaswas 30.

{ Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu!} Maryam 12.

{ Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa! 12. Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T’uwa.} Taha 11-12.

{ Tulimwita: Ewe Ibrahim! 105. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. } Aswaafat 104-105.

{(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.}  Maryam aya 7.

Lakini anapomzungumzia mtume wa mwisho (rehma na amani ziwe juu yake) anamtaja kwa cheo chenye kujuulisha utukufu wake na nafasi yake na ukubwa wa risala yake, Mwenyezi Mungu anasema {Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji,} Al ahzaab 45.

Pia anasema {Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri} Al maidah aya 67.

Si hivyo tu, bali pia Mwenyezi Mungu amewakataza wafuasi wa umma huu kutomwita jina lake kikawaida kama walivyokuwa wakiita wafuasi wa umma ziliizopita  mitume yao. Na akaahidi kumpa adhabu kali atakaehalifu agizo hili. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu { Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu. } Al nuur aya 63.

Vile vile kukirimiwa kwa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) ni wajibu wa kumfanya kuwa ni kigezo, Mwenyezi Mungu amesema { Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana } Al ahzaab 21.

Aya hii ina umuhimu mkubwa sana kwani chimbuko la wajibu wa kumfuata Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kimaneno, kivitendo na kihali, je, tunamfuata na kuigiza kama alivyokuwa (rehma na amani ziwe juu yake).?

Na pia katika kukirimiwa kwake na Mwenyezi Mungu ni kuwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtakia rehema ndani ya kitabu chake pia na malaika wakamtakia rehema na kuwahimiza waumini nao wamswalie (wamuombee rehma), Mwenyezi Mungu amesema { Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu} Al ahzaab aya 56.

Na pia katika kukirimiwa kwake ni kwamba Mwenyezi Mungu mwenyewe  ndie aliyeshika jukumu la kumlinda (rehma na amani ziwe juu yake), tna mitume wengine, wao ilikuwa  wakituhumiwa kwa tuhuma sizo huwa wanajitetea wenyewe, mfano nabii Nuh (A.S.), watu wake wamemtuhumu kwa upotofu kama inavyosimulia Kurani Tukufu, inasema {Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotofu ulio dhaahiri.} Al aaraf 60. Naye anajitete mwenyewe kwa kusema {Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 62. Nakufikishieni Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na ninakunasihini; na ninayajua kwa Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi} Al aaraf 61-62.

Mfano mwengine nabii Hud (A.S.) watu wake walimtuhumu kwa uzembe na wendawzimu na uongo walipomwambia {Wakasema watukufu wa wale walio kufuru katika kaumu yake: Sisi tunakuona umo katika upumbavu, na hakika sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo} Al aaraf aya 66. Naye anajitetea mwenyewe kwa kusema. {Akasema: Enyi watu wangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliye toka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 68 Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kukunasihini, muaminifu} Al aaraf 67-68.

Lakini kwa mtume wa mwisho (rehma na amani ziwe juu yake) kila anaposingiziwa uongo na kumzushia uzushi Mwenyezi Mungu ndiye anaesimama kumtetea, watu wake walimtuhumu kuwa yeye ni mshairi, { Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.} Al anbiya 5. Mwenyezi Mungu akawarudi kwa kusema { Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur’ani inayo bainisha} Yasin 69.

Wakamwambia kuwa yeye ni kuhani, anayasema aambiayo na shetani… Mwenyezi Mungu akawarudikwa kusema { Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.} Al Twuur 29.

Na Mwenyezi Mungu anaapa kiapo – na hakuna kiapo kikuba kkuliko cha Mwenyezi Mungu –  kwa ajili ya kumlinda mtume wake (rehma na amani ziwe juu yake) na kuthibitisha ukweli wa wahyi na kurani na kuvunja hoja na uzushi wao, Mwenyezi Mungu anasema { Basi naapa kwa mnavyo viona 39. Na msivyo viona, 40. Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. 41. Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. 42. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. 43. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.} Al haqah aya 38-43.

Baadhi ya nyakati walikuwa wakimwambia kuwa yeye ni mchawi. Mwenyezi Mungu akawajibu { Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.} Al dhariyaat 52. Na baadhi ya nyakati walikuwa wakimwambia amerogwa, Mwenyezi Mungu akawajibu aliposema { Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale katika hiyo? Wakasema madhaalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliye rogwa 9. Tazama jinsi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea, wala hawataiweza Njia.} Al furqan 8-9.

Wakasema ni mwendawazimu, nae Mwenyezi Mungu akawarudi kwa kusema {Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki.} Al muuminuun aya 70. Na kauli yake aliposema { Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo. 2. Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. 3. Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. 4. Na hakika wewe una tabia tukufu.} Al qalam aya 1-4.

Wakamtuhumu kwa upotofu na kuchanganyikiwa , naye Mwenyezi Mungu akawajibu, aliposema  {1. Naapa kwa nyota inapo tua . 2. Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. 3. Wala hatamki kwa matamanio. 4. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa.} An najm 1-4.

Si hivyo tu bali Mwenyezi Mungu amejitolea kumkinga na kumlinda juu ya washirikina, akasema, {Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.} Al maidah 67.

Na vile vile katika kukirimiwa kwa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) kwa kule kupewa ujumbe kwa walimwengu wote na si kwa kizazi maalumu au watu maalumu, ulinganio wake ni kwa watu wote. Kwani Mwenyezi Mungu aliwatuma kila mtume kwa watu wake ama Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) yeye ni kwa watu wote. Kurani tukufu imeweka wazi jambo hili, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema { Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui} Saba`a 28.

Na Kutoka kwa Jabir bin Abdi Llah (Mwenyezi Mungu awawie radhi amesema: amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie): “ nimepewa mambo matano hakuna nabii yeyote aliyepewa kabla yangu: nimepewa ushindi wa kuwahofisha maadui kwa mwendo wa mwezi, nikafanyiwa ardhi kuwa ni msikiti na ipo safi na mtu yeyote katika umma wangu akifikwa na swala basi na aswali, na nimehalalishiwa ngawira, na ilikuwa nabii akipelekwa (akitumwa) kwa watu wake maalumu, ama mimi nimetumwa  kwa watu wote, na nimepewa uombezi. ((Imepokewa na Bukhari).

Na miongoni mwa kukirimiwa ni kufadhilishwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake) na Mwenyezi Mungu zaidi ya mitume wengine, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) amepewa ubora zaidi na hii ni kama ilivyoeleza Kurani Tukufu { MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo} Al baqara aya 253. Na kama walivyoeleza baadhi wa wafasiri pale aliposema { Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo..} anaekusudiwa hapa ni mtume wetu (rehma na amani ziwe juu yake), kwani yeye ndie mwenye vyeo vya juu, na ni mwenye mwujiza wa kudumu nayo ni Kurani Tukufu na ni mwenye risala iliyokusanya mambo yote mazuri yaliyotajwa katika umma zilizotangulia.

Na katika hadithi ambayo imepokewa na imam Muslim na Tirmidhy kutoka kwa hadithi ya Abu Hurayra, kwamba Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) amesema, “ nimefadhilishwa zaidi ya mitume wengine kwa mambo sita: nimepowa ufupisho wa maneno, nimenusuriwa kwa kuwapa hofu maadui – na katika mapokezi ya ya Bukhari: nimpewa nusura ya kuwaogopesha maadui kwa mwendo wa mwezi – na nimehalalishiwa ngawira, na ardhi ikafanywa kwangu kuwa ni msikiti na ni safi, n nimetumwa kwa viumbe wote na unabii ukaishia kwangu.”

Na katika kukirimiwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake) ni kuwa Mwenyezi Mungu akiapa basi huapa kwa kupitia jina lake na wala hatumii jina la viumbe vyake, na Mwenyezi Mungu akiapia juu ya vitu basi ni kwa kuvitilia mkazo, na anaapia vitu vingi mbali mbali, kama visivyo na uhai, wanyama, malaika, maeneo, nyakati, na hali ya kilimwengu. Mwenyezi Mungu hakupa ndani ya Kurani kumuapia mwanadamu isipokuwa Mtume (rehma na amani ziwe juu yake), aliposema { Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo} Al hajar 72. akikusudia,  kupitia uhai wako ewe Muhamad hakika wao wamo katika upotofu mkubwa, na wamo katika kutojua njia wala haki wala uongofu… Na washirikina waliposema kuwa Mwenyezi Mungu amemuacha mkono Mtume Mtume (rehma na amani ziwe juu yake), na amemtenga, Mwenyezi Mungu Mtukufu akapa kuwa yeye hakumuacha na wala hakumuacha mkono, akasema {1. Naapa kwa mchana! 2. Na kwa usiku unapo tanda! 3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. 4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. 5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.} Adhuha 1-5.

Na kwa upande wa kukirimiwa kwake (rehma na amani ziwe juu yake) baaya ya kufariki, ni kuwa Mwenyezi Mungu amempa uombeaji mkubwa siku ya kiama. Kwani katika hadithi mbayo ameipokea Bukhari na Muslim kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), hakika mtume (rehma na amani ziwe juu yake) amesema, “ mimi ni bwana kati ya watoto wa Adam siku ya kiama, na ni wa mwanzo atakaepasukiwa na kaburi na ni mwombezi wa mwanzo na wa mwanzo atakae ekubaliwa maomi yake.”

Na katika aya tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu  amemfanya (rehma na amani ziwe juu yake) kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, amesema { Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.} Al anbiyaa 107.

Kutoka  kwa  Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani zimshukie), “hakika mimi ni rehema yenye kuongoa”. Na katika mapokezi mengine nimetumwa kuwa ni rehema yenye kuongoa.

Hatari za ulinganio potofu na umuhimu wa kuuzuia kwa ajili ya
upatikanaji wa amani na utulivu
29 Safar 1437 H.
Sawa na 11 Disemba 2015 A.D

awkaf

Kwanza: Mambo muhimu

 1. Neema ya amani na utulivu.
 2. Utulivu wa nchi ni katika mambo ya lazima kisheria na kitaifa.
 3. Vitendea kazi vya utulivu katika taifa.
 1. Raia kuipenda nchi yake.
 2. Kueneza upendo na msaada kati ya watu.
 3. Kuwasikiliza na kuwatii viongozi wa nchi kwa lile atakalo Mwenyezi Mungu, na kulitumikia taifa.

 

 1. Kujiepusha na fitina.
 2. Hatari ya ulinganio potofu kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii.
 3. Ulazima wa kuzuia ulinganio huu.

Pili: Dalili

Ndani ya Kurani Tukufu

 1. Mwenyezi Mungu anasema : { Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda.. } Albaqara aya ya 126.
 2. Mwenyezi Mungu anasema : { Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu.} Ibrahim aya ya 35.
 3. Mwenyezi Mungu anasema : {Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma – hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka. } Al an aam aya ya 82.
 4. Mwenyezi Mungu anasema : {1. Kwa walivyo zoea Maqureshi. Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto. 3 Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii, 4. Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.} Quraish aya ya 1-4.
 5. Mwenyezi Mungu anasema : { Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.} Al qaswas aya ya 57.
 6. Mwenyezi Mungu anasema : { Je! Hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani zao? Je! Wanaamini upotovu, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikataa? } Al ankabuut aya ya 67.
 7. Mwenyezi Mungu anasema : { Na baina yao na miji mingine tuliyo ibariki tuliweka miji iliyo dhaahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani } Sabaa aya 18.
 8. Mwenyezi Mungu anasema : { Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa } Al imraan 173.
 9. Mwenyezi Mungu anasema : { Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. } Al anfaa aya 25.
 10. Mwenyezi Mungu anasema : { Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.} Al nuur aya 19.
 11. Mwenyezi Mungu anasema : { Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.} Al nisaa 59.
 12. Mwenyezi Mungu anasema : {Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet’ani ila wachache wenu tu.} Al nisaa 83.

Hadithi za Mtume (Saw)

 

 1. Kutoka kwa Ibnu Ubayd llah bin Mehsan Al-hatmiy, kutoka kwa baba yake, amesema, amesema Mtume (Saw): “ atakaeamka hali ya kuwa yupo salama katika nafsi yake, ana siha katika mwili wake, na ana chakula cha siku yake basi kama kamba amemilikishwa dunia”. (Imepokewa na Tirmidhy).
 1. Kutoka kwa Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu amwie radhi), amesema, amemsikia Mtume (Saw) anasema: “ macho mawili hayataguswa na moto; jicho lililolia kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na jicho lililokesha kulinda kwenye njia ya Mwenyezi Mungu”.
 1. Kutoka kwa Abdullah bin Ady bin Hamraa, amesema: nimemuona Mtume (Saw) amesimama katika eneo la Haz-wara akasema: “ hakika eneo hili ni eneo bora katika maeneo ya ardhi ya Mwenyezi Mungu, na eneo lipendwalo na Mwenyezi Mungu, na lau kama nisingelikuwa nimefukuzwa hapa, basi nisingelitoka”. (Kitabu cha Ahmed na Tirmidhy). Haz-wara hili ni eneo lililopo nchini Makka.
 1. Kutoka kwa ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: amesema Mtume (Saw) kuhusu Makka: “Mji bora ulioje na niupendao na lau kama watu wangu hawakunifukuza basi nisingelikaa katika mji mwengine” (Imepokewa na Tirmidhy).
 1. Kutoka kwa Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: Mtume (Saw) amesema: “Ewe (Mwenyezi Mungu tupendezeshe kuupenda mji wa Madina kama ulivyotupendezesha kuupenda mji wa Makka. (Imepokewa na Bukhari).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amemsikia Mtume (Saw) akisema: “atakaenitii mimi basi hakika amemtii Mwenyezi Mungu, na atakaeniasi basi hakika amemuasi Mwenyezi Mungu, na atakaemtii kiongozi basi amenitii mimi, na atakaemuasi kiongozi basi ameniasi mimi, kwani kiongozi ni kizuizi hupambana kwa ajili yao na humuogopa Mwenyezi Mungu kwa ajili yao, na pindi akiamrisha kumtii Mwenyezi Mungu na kufanya uadilifu atapata malipo mema kwa hilo, na iwapo atakuwa kinyume na hivyo basi mzigo huwa ni wake. (Imepokewa na Bukhari).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi), kutoka kwa Mtume (Saw) amesema: “atakaejitoa katika utiifu na kuachana na kundi (umoja) kisha akafariki, basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia, na yeyote atakaepigana chini ya bendera ya upofu, hukasirika kwa ajili ya koo yake au huendeleza chuki au kutaka ushindi kwa koo yake kisha akafariki, basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia. Na yeyote katika umma wangu akatoka akawa anawapiga wema na waovu na wala hakuna anaesalimika nae na wala hatimizi ahadi kwa wenye ahadi ya ulinzi, basi huyo si katika mimi na mimi si katika yeye. (Imepokewa na Muslim).
 1. Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: “amesema Mtume (Saw): “ Itakujakuwa fitina kiasi ambacho fitina ya aliyekaa ni bora kuliko fitina ya aliyesimama. na fitina ya aliyesimama ni bora kuliko ya anaetembea. na fitina ya anaetembea ni bora kuliko fitina ya anaeieneza. Yoyote mwenye kutafuta utukufu kutokana na fitina hiyo basi ataupata. Na mwenye kupata kimbilio basi ajilinde kwa kimbilio hilo. (Imepokewa na Bukhari na Muslim).

Tatu: Maudhui

 

Hakika miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu ni neema ya usalama na utulivu, bila ya hizo akili na nafsi ya mwanadamu hautulizani, na katu hatopata furaha ulimwenguni hata kama atakuwa anamiliki dunia na vilivyomo, kwani bila shaka furaha na neema ya ulimwengu ni kuwepo kwa amani na utulivu, kwani katika hadithi ya Mtume (Saw) : “ atakaeamka hali ya kuwa yupo salama katika nafsi yake, ana siha katika mwili wake, na ana chakula cha siku yake basi kama kwamba amemilikishwa dunia”. (Imepokewa na Tirmidhy).

Neema ya amani na utulivu ni matakwa ya kila kiumbe ulimwenguni, hata nabii ibrahim (amani iwe juu yake) aliwaombea watu wake aliposema. {Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.} Albaqara aya 126.

Hapa nabii Ibrahim (amani iwe juu yake) anamuomba Mwenyezi Mungu aibariki Makka kwa amani na pato (rizki), na katanguliza kuomba amani kabla ya rizki kwa sababu rizki haitokuwa na utamu wake pindi ikikosekana amani, kupitia amani mwanadamu hupata utulivu na anahisi umuhimu wa maisha. Naye Mwenyezi Mungu akamuitikia mtume wake na kipenzi chake kwa kuifanya Makka kuwa ni sehemu tulivu kwa uwezo wake na utashi wake, na kuifanya nchi ya uisilamu, na hii yote ni kwa baraka za maombi ya nabii Ibrahim (amani iwe juu yake). Si hivyo tu bali nabii Ibrahim (amani iwe juu yake) ametanguliza neema ya usalama –amani – kabla ya tauhidi, akasema {Na Ibrahim alipo sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu.} Ibrahim aya 35.

Na kama Mwenyezi Mungu mtukufu alivyowaneemesha makuraish kwa neema hii kubwa, akawapa maisha mazuri na utulivu katika nchi, Mwenyezi Mungu amesema :{3.Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii. 4. Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.} Quraesh aya 3-4.

Na kama alivyowaneemesha kwa kuifanya Al kaaba kuwa ni mahala pa utulivu, Mwenyezi Mungu anasema {Je! Hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani zao? Je! Wanaamini upotovu, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikataa?} Al ankabuut 67.

Kupitia amani na utulivu taifa hukua na watu hupata utulivu wa maisha yao na utafutaji wa riziki zao, taifa nalo huendelea pamoja na jamii, uchumi pia hukua, na haya tayari Mwenyezi Mungu ameshayaeleza katika Kurani tukufu wakati alipowaneemeha watu wa Saba-a kwa neema ya amani na utulivu, akasema {Na baina yao na miji mingine tuliyo ibariki tuliweka miji iliyo dhaahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.} Saba-a aya 18.

Hakuna taifa lililotangulia miongoni mwa mataifa, na wala jamii miongoni mwa jamii isipokuwa amani na utulivu upo kwa raia zake.

Kuyumba kwa amani na utulivu huathiri pakubwa taifa na raia hata katika ibada – ambayo ni lengo kuu la kuumbwa wanadamu – kwa ajili hiyo, hata sala isaliwayo wakati wa wasiwasi (sala ya hofu) ipo tafauti na sala isaliwayo wakati wa amani kimuundo na kimatendo. Na hata ibada ya kuhiji pia inashurutishwa kuwepo na amani njiani, na kama njia itakuwa haina amani basi ibada ya hijja huwa si lazima kuitimiza, hapa tunafahamu kuwa, hata ibada haitokamilika kama itakiwavyo pindi tu pakiwa na ukosefu wa amani na utulivu.

Amani na utulivu ukiwepo katika taifa na ikawa kila mmoja yupo salama yeye mwenyewe, mali zake, heshima yake, bila shaka jamii hii wataishi katika utulivu wa hali ya juu kabisa, pasi na hofu wala wasiwasi, na jamii itanufaika kwa maendeleo na ukuaji, na maendeleo ni vitu vya lazima kisheria na ni matakwa ya taifa pia ni lengo kuu na muhimu miongoni mwa malengo ya dini tukufu.

Vitendea kazi vya kuleta utulivu: raia inamlazimu aipende nchi yake ambayo anaishi kwa uhuru unaokubalika, na ahisi umuhimu wa taifa ambalo amekulia katika mchanga wake, na hivi ndivyo alivyopiga mfano Mtume (Saw) kivitendo, wakati anahama Makka Tukufu na kuhamia Madina Munawara,  kwani Mtume (Saw) ametufundisha mapenzi ya taifa na ubora wa kujifaharisha nalo, na mapenzi yake (Saw) juu ya nchi yake ya Makka na hisia zake juu ya taifa hilo ilikuwa ni jambo kubwa, pamoja na ubaya wa watu wake, akasema ingawa ameathirika kuliacha: {Hakika hii ni ardhi bora ya Mwenyezi Mungu na ni ardhi ya Mwenyezi Mungu niipendayo na lau kama watu wangu hawakunifukuza basi nisingelitoka.” (Kitabu cha Ahmad na Tirmidhy).

Na katika mapokezi ya Ibni Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi) amesema: amesema Mtume (Saw) kuhusu Makka” (“ Mji bora ulioje na niupendao na lau kama watu wangu hawakunifukuza basi nisingelikaa katika mji mwengine” (Imepokewa na Tirmidhy).

Na alipohamia Mtume (Saw) katika mji wa Madina akaanza kujenga taifa la kisasa kwa lengo la kuwafundisha masahaba zake na ulimwengu kwa ujumla ya kuwa taifa halijengwi isipokuwa kwa wale wenye kulipenda, na dua yake kubwa ilikuwa kama ilivyokuja kutoka kwa mama wa waumini Aisha (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: amesema Mtume (Saw) “ Ewe Mwenyezi Mungu tupendezeshee mji wa Madina kama ulivyotupendezeshea mji wa Makka au zaidi”. (Imepokewa na Bukhari)

Na Mtume (Saw) hakuwa akitaka kuonesha upendo wa taifa isipokuwa kutaka kuwepo kwa amani na utulivu ili kila mmoja awe na usalama.

Kwa ajili hiyo ni lazima kwa kila raia ahifadhi taifa lake na alipende na alilinde pia alitetee, na asimamie wajibu wake na majukumu yake kwa ajili ya taifa. Taifa kwa mtazamo wa kiisilamu ni kitu kikubwa sana na kuzembea kuhusu haki ya taifa ni hatari sana, kwa ajili hiyo, Mtume (Saw) amempa cheo kila ambae atahifadhi utulivu wa taifa lake na kujitolea muhanga kwa ajili yake, kwani Mwenyezi Mungu hatomuadhibu na wala moto hautogusa macho yake, kwani malipo huwa sana na matendo.

Imepokewa na Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi amesema: nimemsikia Mtume (Saw) akisema; “ macho mawili hayataguswa na moto; jicho lililolia kwa ajili ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na jicho lililokesha kulinda kwenye njia ya Mwenyezi Mungu”. (Imepokewa na Tirmidhy).

Kulipenda taifa ni katika mambo muhimu sana yaletayo utulivu nchini kwa jamii yoyote, kwani mtu akilipenda taifa lake na akihisi jukumu lake la kuhifadhi amani na utulivu na wala hayuko pamoja na wanaoliharibu katika  wenye kuhubiri, kwani mwanadamu akipata utulivu ndani ya nchi yake basi pia utulivu wa nafsi yake utakuwepo na ataleta mafanikio katika kazi zake na chumo lake.

Na katika vitendea kazi vya utulivu: ni kueneza upendo, ushirikiano kati ya watu, Mtume (Saw) anasema “ Muumini kwa muumini mwenziwe ni sawa na jengo hushikana wenyewe kwa wenyewe na kisha akagandisha vidole vyake” (imepokewa na Bukhari na Muslim).

Na kujiepusha na tofauti na migongano, kwani hiyo ni shari inayowapelekea kwenye mgawanyiko na upotevu, Mwenyezi Mungu anasema (Na mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri) Al anfaal 46.

Tujiepushe sana na ushabiki au vikundi vikundi kwani hivyo ni shari ipelekeayo kusambaratika kwa jamii, na inapasa kuunga jamii na kuwepo ushirikiano ili amani na utulivu uwepo na hivi ndivyo alivyoamrisha Mwenyezi Mungu {Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. } Almaaidah aya 2.

Na katika mambo muhimu ambayo husaidia kuleta utulivu nchini: ni kuwatii wenye madaraka bila ya kuasi Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu anasema {Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema} Alnisaa 59.

Kwani wenye madaraka ni kama kivuli cha Mwenyezi Mungu katika ardhi, kama alivyosema Mtume (Saw) “viongozi ni kivuli cha Mwenyezi Mungu katika ardhi, yeyote atakaewakarimu naye atakirimiwa na Mwenyezi Mungu na atakaewadhalilisha, nae atadhalilishwa na Mwenyezi Mungu”. Imepokewa na Tabariy na Bayhaqiy.

Na pia Mtume (Saw) amesema, “yeyote atakaemkirimu kiongozi atendae kwa ajili ya Mwenyezi Mungu duniani, basi naye Mwenyezi Mungu atamkirimu siku ya kiyama, na yeyote atakaemdhalilisha kiongozi atendae kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi naye atadhalilishwa siku ya kiyama”. (Imepokewa na Ahmad)

Hakika kumtii kiongozi ni kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kwa masilahi ya taifa na kwa imani ya waisilamu, na kiongozi akimrisha au kukataza itapasa kumtii pindi tu si katika maasi ya Mwenyezi Mungu. Imepokewa na Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema, amemsikia Mtume (Saw): “ yeyote atakaenitii mimi basi amemtii Mwenyezi Mungu, na yeyote atakaeniasi basi amemuasi Mwenyezi Mungu, na yeyote atakaemtii kiongozi basi amenitii mimi, na yeyote atakae muasi kiongozi basi ameniasi mimi, kwani kiongozi ni kizuizi hupambana kwa ajili yao na humuogopa Mwenyezi Mungu kwa ajili yao, na pindi akiamrisha kumtii Mwenyezi Mungu na kufanya uadilifu atapata malipo mema kwa hilo, na iwapo atakuwa kinyume na hivyo basi mzigo huwa ni wake.” (Imepokewa na Bukhari). Kinachokusudiwa ni kumtii kiongozi bila ya kumuasi Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutengeneza dini na dunia.

Kwa ajili hiyo ni wajibu wa raia kusikia na kutii viongozi, na wala asitengane na kundi la waisilamu, imepokewa kutoka kwa Abi Hurayra, kutoka kwa Mtume (Saw) kwamba yeye amesema: “atakaejitoa katika utiifu na kuachana na kundi (umoja) kisha akafariki, basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia, na yeyote atakaepigana chini ya bendera ya upofu, hukasirika kwa ajili ya koo yake au huendeleza chuki au kutaka ushindi kwa koo yake kisha akafariki, basi huwa kafariki katika kifo cha kijahilia. Na yeyote katika umma wangu akatoka akawa anawapiga wema na waovu na wala hakuna anaesalimika nae na wala hatimizi ahadi kwa wenye ahadi ya ulinzi, basi huyo si katika mimi na mimi si katika yeye. (Imepokewa na Muslim).

Na huenda sababu ya kulazimika kuwatii na kuwasikiliza viongozi ni kwa vile iwapo wataacha mema basi  hapo ndipo italazimu kutowatii kwani kufanya hivyo kutapelekea kuzidi uasi, na kitakiwacho ni kunasihiana ambako kuko kwa njia tofauti zilizo salama na za kidemokrasia, na hii ni kwa ajili ya kufanya neno la umma liwe ni moja, na kuzuia mipasuko na makundi, ambayo huenda yakasababisha mauaji, umwagaji wa damu, kuvunjiana heshima, kufanya yaliyoharamishwa, kuangamiza taifa, kupoteza mali, kudhoofisha ushirikiano na haya yote yapo wazi kwa kila mtu kwa sababu ya  matatizo yaliyosababishwa kwa kutowasikiliza viongozi.

Na katika mambo makubwa yanayoondosha utulivu wa taifa: ni kueneza fitina ambazo zinapelekea kuondoka kwa neema na kuleta maafa, na kukata ushirikiano kati ya mataifa na mengine, na kueneza machafu na kuondosha mazuri, na kutangaza roho ya uadui na chuki na kuacha kueneza roho ya upendo na undugu.

Fitina ni moto wenye kuangamiza kikavu na kibichi, yenye kutenganisha kati ya mtu na mwengine, mama na mwanawe, mtu na mkewe, na inampelekea mja kuacha kumtii Mola wake. Na yeyote anaechochea fitina ni amelaanika, na muenezaji wake ni mtu fitina mwenye kuharibu hali njema na kuzifanya kuwa mbaya, ama muuaji na aliyeuliwa wote watafikia motoni na ni makazi mabaya yaliyoje.

Kwa ajili hiyo, uisilamu umefanya pupa kubwa zaidi ili kuepukana na fitina, na Mtume (Saw) ametuelekeza maelekezo ya kuweza kuepukana na fitina, na kumfundisha muisilamu ni namna gani ataweza kutaamali na fitina. Kwani imepokewa kutoka kwa Abdallah Bin Amru bin Al-as (Mwenyezi Mungu awawie radhi), hakika ya Mtume (Saw) amesema: “ itakuwaje pindi mukifikwa na wakati, ambao watu watapetwa na wakabaki wabaya kati yao wametimizi  ahadi zao na amana zao, kisha wakahitilafiana hata wakawa kama hivi” akakutanisha vidole vyake, masahaba wakasema, unatuamrisha nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “ Kichukueni mukijuacho kuwa ni haki, na kiacheni mukichukiacho, na mukubali jambo mulionalo ndilo na kuacha mambo (mabaya) yatendwayo na wengi.

Shime tena shime kuhifadhi umoja wa taifa. Na tahadhari kisha tahadhari na fitina zilizo wazi na zilizo jificha, kwani hata Mwenyezi Mungu ametuhadharisha nazo katika sehemu nyingi ndani ya Kurani, na katika hizo ni kama alivyosema kuwa fitina ikifika mahala huwa haibagui katia ya aiungae mkono na aipingae, akasema { Na jikingeni na Fitina ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.} Al anfaal 25.

Pia naye Mtume (Saw) ametuhadharisha sana, imepokewa kutoka kwa hudhaifa (Mwenyezi Mungu amwie radhi, amesema, amemsikia Mtume (Saw) akisema: “ fitina hupita nyoyoni kama nyoyo za mkeka wenye nyuzi nyuzi wazi, nyoyo yoyote itakayoikubali, basi huwekewa kidoto cheusi na nyoyo yoyote itakayoikataa huwekewa kidoto cheupe hata huwa cheupe mfano wa almasi, mtu huyo hatodhuriwa na fitina kwa muda wote wa kuwepo mbingu na ardhi. (Imepokewa na Muslim)

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: “amesema Mtume (Saw): “ Itakujakuwa fitina kiasi ambacho fitina ya aliyekaa ni bora kuliko fitina ya aliyesimama. na fitina ya aliyesimama ni bora kuliko ya anaetembea. na fitina ya anaetembea ni bora kuliko fitina ya anaeieneza. Yoyote mwenye kutafuta utukufu kutokana na fitina hiyo basi ataupata. Na mwenye kupata kimbilio basi ajilinde kwa kimbilio hilo.  (Imepokewa na Bukhari na Muslim).

Hakika ni wajibu kwa mwisilamu mwenye akili ajiepushe na fitina na kiali lenye kupelekea fitina, na ataamali na fitina kwa hadhari sana, kwani imepokewa na Anas (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema; amesema Mtume (Saw) kuwambia Maanswari: “ Mutakuja kuona baada yangu athari, basi kuweni na subira mpaka mutakapokutana nami, na ahadi yenu ni kunywa katika hodhi. Hapa Mtume (Saw) anakusudia kuwa wataona athari za mambo ya kuliwaza ya kidunia, na wasio wema watafadhilishwa zaidi wa walio wema,na hawatokuwa na nafasi.

Kufunga njia zinazopelekea katika fitina na kujikinga nazo ni kitu kitakiwacho kwa muisilamu ambae anataka kufanikiwa duniani na akhera, na hivyo ndivyo Mtume (Saw) anamsifia anaechukua hadhari na kujiepusha kuzama katika fitina kadiri ya uwezo wake.

Kutoka kwa Abi Hurayra (Mwenyezi Mungu amwie radhi) amesema: “amesema Mtume (Saw): “ Itakujakuwa fitina kiasi ambacho fitina ya aliyekaa ni bora kuliko fitina ya aliyesimama, na fitina ya aliyesimama ni bora kuliko ya anaetembea, na fitina ya anaetembea ni bora kuliko fitina ya anaeieneza, yoyote mwenye kutafuta utukufu kutokana na fitina hiyo basi ataupata, Na mwenye kupata kimbilio basi ajilinde kwa kimbilio hilo.  (Imepokewa na Bukhari na Muslim).

Na kujikinga na fitina kutatokana na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na maamrisho ya Mtume wake (Saw), na kuwa pamoja na jamaa na kuwatii viongozi kwa wema. Na kwa ajili ya masilahi ya taifa, hivyo basi, Mwenyezi Mungu amemtahadharisha mwenye kuacha jamaa na kuzama katika fitina duniani ya kuwa atakumbana na adhabu iliyo kali. Mwenyezi Mungu anasema {Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu} Alnuur 63.

Ni wajibu wa kila mmoja wetu kusaidiana kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu lilobarikiwa, kujitahidi kulitukuza kwa kufaya juhudi na kuhifadhi mali zake na kuzingatia tabia na maadili yake, kanuni na sheria zake ili tupate kujiinua kwa kuhifadhi usalama wetu na utulivu wetu. Raia mwema ni yule mwenye kujenga nchi yake na kuleta utulivu na kuuhifadhi na wala hawi pamoja na watu wenye nyoyo za msilahi yao ya kibinafsi, na wenye ulinganio potofu wenye kubomoa na ambao wanafanya kazi ya kuliharibu taifa na kueneza fujo.

 Mwenyezi Mungu anasema, {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.} Al imran aya ya 103.

Na miongoni mwa fitina kubwa zenye kupoteza amani na utulivu ndani ya jamii: ni ulinganio potofu ambao unaotolewa na wenye imani dhaifu, ambao hawana upendo na taifa lao na wenye misimamo mikali ambao kazi yao ni kuhakikisha kuisambaratisha jamii na kuleta hali ya misukosuko ndani yake, na kubomoa nguzo zake na kuharibu vyanzo vyake. Na pia hawatosheki na mipango yao miovu ya kuangamiza ambayo lengo kuu ni kuliangusha taifa na kupoteza utulivu wake.

Na hatari kubwa iliyoje ndani ya taifa ambayo hupelekea kuwepo mtafaruku ni kule kuitumia dini vibaya, na kuzidisha yasiyokuwemo na matumizi mabaya ya ulinganio usio na malengo au kwa hutuba za midomoni tu au kwa majadiliano mengi yasiyo na matokeo yoyote muhimu. Na hivi karibuni sauti nyingi potofu na zenye kuharibu zimesikika ambazo zinaita bila ya hata haya kuharibu taifa, kumwaga damu, na kuwahofisha walio katika usalama na kueneza machafu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika kitabu chake kitukufu {Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.} Al nuur 19.

Ulinganio huu potofu ambao wenye wana malengo ya kuiharibu jamii na kueneza fujo na kupoteza umuhimu wa kuwepo kwa sheria ni moja wapo ya hatari kubwa tena sana za kupoteza usalama ndani ya taifa, na ni moja wapo wa umuhimu wa kuamsha moto za kuwepo vitndo vya kigaidi, na huifanya jamii isifike kwa sifa zisizostahiki. Hakika ulinganio huo ambao wanaoueneza unapelekea kuwepo fitina kubwa ambayo itayumbisha taifa na waja pia kwa kuwepo mauaji, uharibifu, kuyumbisha hali ya usalama kati ya mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima, na kuna mifano ya kuanguka na kuporomoka mataifa mbali mbali kutokana na hali ya kukosa usalama. Dini yetu tukufu ya kiisilamu inalingani yote yaletayo usalama na utulivu na kupinga vikali aina zote za uadui na ugaidi