Uislamu ni utendaji na Mwenendo. Mifano itokanayo na Maisha ya Taabiina

Sifa zote njema ni zake yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote, anaesema katika Kitabu chake Kitukufu:

{وَالَّذِينَ جَاءُوا مِنْ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ}

Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, asiye na mshirika wake, na kwamba Bwana na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mola Mlezi wetu, tunakuomba umswaslie, umpe Rehema na umbariki Bwana wetu, yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote, na kila atakayewafuata kwa wema mpaka siku ya Mwisho.

Na baada ya Utangulizi huu,

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huwachagua katika waja wake, watakaoitumikia Dini yake na kuwa na moyo mkunjufu kwake na kwa Ujumbe wake. Na Mtume S.A.W, amesema kwamba chaguo la Uma huu ni Maswahaba wake R A, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia waliowafuatia Maswahaba R.A. Kutoka kwa Abdillahi bin Masoud R.A, amesema: anasema Mtume S.A.W: Watu walio bora zaidi ni wa Karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia…

Kwa hiyo hawa ndilo chagua la Mwenyezi Mungu Mtukufu waliosifika kwa Kheri nyingi, na walioibeba Amana ya Elimu, wakiisafisha kutokana na kauli za wapotoshaji na mwenendo wa walio batili, na tafsiri potofu za wajinga. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu na akawajumuisha na Maswahaba wa Mtume S.A.W, na kuwapa wasifu wa Ihsani, na akawaridhia wote, na akawaahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu Pepo yenye kupita Mito chini yake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ}

Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Muhahajirina na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Na Taabiina (waliowafuatia Maswahaba) ni Watu walio karibu zaidi na zama za Mtume S.A.W, kwani wao ni Kizazi cha Maswahaba wa Mtume R.A, na waliowafuatia wao ni Kizazi cha pili cha Waliowafuatia Maswahaba wa Mtume S.A.W, na walijifunza mikononi mwao R.A.

Na wote wamechukua elimu zao kutoka kwa Mtume S.A.W, na waliambatana na Maswahaba wa Mtume R.A, kwa fadhila na kwa elimu; na katika hili tunaupata Ushahidi wa Bin Omar R.A, kwa Saiid bin Musiib R.A, kwa kauli yake: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakika yeye ni miongoni mwa Watoa Fatwa. Na alikuwa anasema: Muulizeni Saiid bin Musiib; hakika yeye aliketi na Wema. Na Saiid bin Musiib alikuwa akitoa Fatwa na Maswahaba wakiwa hai. Na Atwaau bin Abuu Rabaah alikuwa akiketi na wavulana akiwa Makkah baada ya kufariki kwa Mtaalamu wa Uma Abdullah bin Abas R.A, na Bin Omar R.A, alipokuja Makkah wakamuuliza akasema: Enyi Watu wa Makkah mnanikusanyia mimi masuala mbalimbali wakati mnae Abu Rabaah?

Taabiina walikuwa wakijulikana mno kwa ukweli wa mapenzi yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hasanil Basriy Mola Mlezi amrehemu, alikuwa anapoizungumzia Hadithi ya Kipande cha Mti – na kumuinamia Mtume S.A.W – analia na akasema: Enyi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Kipande cha Mti kinamnyenyekea Mtume S.A.W, kwa kuwa na shauku nae, na kwa hivyo nyinyi mna haki zaidi katika hili, na muwe na shauku ya kutaka kukutana naye. Na Imamu Malik R.A, aliwahi kuulizwa: ni lini ulimsikia Ayubu Sakhtiyaaniy akizungumza?  Akasema:  Alihiji Hija mbili na mimi nikawa ninamfuatilia na wala sisikii lolote kuka kwake, isipokuwa yeye alikuwa pindi Mtume S.A.W anapotajwa hulia mpaka nikamhurmia, na alikuwa amefikia kiwango cha juu mno cha unyenyekevu wao kw Mtume SAW, wakawa wao hawaungumzii Hadithi yake isiokuwa wanapokuwa katika hali ora abisa, na wauasi wao walileleka katika malezi hayo. Anasema Abu Salamahl Jazaaii Mola amrehemu: Malik bin Anas alikuwa anapotaka kutoka kwenda haja hutawadha udhu wake kwa ajili ya Sala, na huvaa nguo nzuri zaidi, na huchana ndevu zake, na mpaka akaambiwa kuhusu jambo hilo, akasema: Ameyachukua ayo kutoka katika Hadithi ya Mtume S.A.W.

Na katika Taabiina, wapo ambao Mtume S.A.W aliwataja kwa wema, kama vile Uweisil Qarniy ambaye alikuwa akimtendea wema mama yake, na Mtume S,A,W, amemtaja  na  akawaambia Maswahaba kuwa Dua yake ni yenye kupokelewa. Kutoka kwa Omar bin Khatwab R.A, amesma: hakika mimi nimemsikia Mtume S,A,Wm , anasema: Hakika Mbora wa Taabiina ni Mwanaume mmoja anaitwa Uweis, na ana mzazi wake wa kike  na alikuwa na uweupe basi mwamrisheni akuombeeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Na Omar alipowaendea watu wa Yemen akawa anamuulizia mtu huyo na alipomwona mwambia: Niombee, akasema: Wewe kwakweli ndio wa kuniombea mimi. Wewe ni Swahaba wa Mtume S.A.W. Omar aliendelea kumwomba hivyo hivyo mpaka Uweis akamwombea Dua Omar…

Na Taabiina walijifunza Dini sahihi kutoka kwa Maswahaba wa Mtume S.A.W.  aliyeijua Dini vizuri. Na tunaona ya kwamba Imamu Hasanil Basriy Mwenyezi Mungu amrehemu, yeye ni katika Taabiina wakubwa, aliulizwa: Je? Wewe ni Muumini? Akasema: Imani ipo ya aina mbili; ikiwa wewe unaniuliza mimi kuhusu kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake, na Pepo, na kufufuliwa, na Malipo, basi mimi ni Muumini, na ikiwa unaniuliza kuhusu Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

{إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَاناً وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ * الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ * أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً}

Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi.

Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba mimi sijui kama ni miongoni mwao au sivyo. Amesema Baihaqiy akitoa maelezo juu ya jambo hili: Haani hakusita katika asili a maniyake hapo hapo, bali alisimamia katia ukamilifu wake ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaahidi watu wa weponi katika Kauli yake Tukufu:

 {لَهُمْ دَرَجَاتٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ}

Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi

     Vile vile wao waliujua vyme wepesi na wakautekeleza ipasavyo karika maisha yao. Anasema Sifiyani Thauriy Mola amrehemu: Hakika Mambo yalivyo, Elimu kwetu sisi ni kibali cha uaminifu, na ama ukali wa mambo kila mmoja wetu anauweza. Na Azraq bin Qais akasema: Tulikuwa katika kingo za Mto huko Ahwaaz na majili yalikuwa yamejaa akaja Abou Barzat akiwa juu ya farasi akawa anasali na akamwacha farasi wake, na Yule farasi akaondoka, Yule bwana akaiacha sala yake na akamfuata farasi wake mpaka akamfikia alipo akamchukua kisha akarejea na kuilipa sala yake. Na kuna mtu mmoja aliyekuwa nasi aliyeona tukio hilo, akaja na akasema: Mwangalieni huyu Sheikh, ameiacha sala yake kwa ajili ya Farasi wake! Akaja na akasema: Hakuna mtu yoyote aliyenikanya tangu Mtume S.A.W, afariki Dunia, na akasema: Hakika nafasi yangu inaniruhusu, kama ningelimwacha farasi wangu nisingeliwafikia watu wangu isipokuwa Usiku. Na hakika Mtu huyu alifunza jambo hilo kutoka kwa Mtume S.A.W, ambaye hakuwahi kuchagulishwa baina ya mambo mawili isipokuwa alichagua lililo jepesi kati ya mawili hayo kama halikuwa na dhambi yoyote kwa kulifanya kwake. Na Mtume S.A.W, anasema: Rahisisheni mambo na wala msiyatie ugumu, na mpeane habari njema na wala msipeane habari mbaya. Na kauli yake Mtume S.A.W: Hakika upole ahuwi katika kitu chochote isipokuwa hukipendezesha, na hauondoshwi katika kitu chochote isipokuwa hukifanya kiwe kibaya.

Taabiina pia walitekeleza katika maisha yao, tabia ya Upole na Kuleana na kuwahisi wengine, kwa vitendo. Tunaona kwamba Ali bin Huseina bin Ali, R.A, alikuwa akiwasaidia Mafukara wengi mno kwa siri, na hakuna mtu aliyekuwa akijua/ na alipofariki Dunia walimkosa wa kuwasaidia, na walipomkosha walikuta mgongoni mwake na begani mwake athari za kuwabebea mizigo wanawake waliofiwa na waume zao na masikini na kuwafikishia majumbano mwao, na wakati huo wakajua kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiwajia nyakati za usiku kwa vitu alivyokuwa akiwaletea. Na inasemekana kwamba: alikuwa akiwalea mana Ahlu baiti, huko Madina. Na kuhurumiana na kuleana hakuishii kwa Waislamu tu, bali kunawakusanya pia waislamu na wasio waislamu. Tunaona kwamba Bwana wetu Omara bin Abul-Aziiz, R.A, anamwandikia mfanyakazi wake huko Basrah akisema: Na umwaangalie alie kabla yako miongoni mwa Watu wa Dhimma, hakika mama huyo amezeeka sana, na hana nguvu tena, na hana tena uwezo wa kujitafutia riziki, kwa hiyo uwe unampa kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu kile kinachonfaa. Na hapo Bwana wetu Omar anaiga mfano wa Bwana wetu Omarl Khatwaab R.A, alipomwona mtu aliyezeeka miongoni mwa Watu wa Kitabu anawaomba omba watu, akasema: Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hatukumtendea haki mtu huyu, kwani tumeutumia ujana wake na tukampoteza katika uzee wake. Kisha akawa anampa kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu kiasi kinachomtoshelezea mahitaji yake. Na vile vile tuna mfano mwingine wa Bwana wetu Khalid bin Walid R.A, katika mkataba wake kwa ajili ya watu wa Alheerah:

Na nimewaandalia wao, pale mtu anapozeeka na kukosa nguvu za kufanya kazi, na anapopatwa na janga lolote miongoni mwa majanga, au alikuwa tajiri kasha akafilisika, nimemwandalia usaidizi kutoka katika Hazina ya Mali ya Waislamu. Na wote hao, walikuwa wakimfuata Mtume S.A.W, na walikuwa wakiitekeleza Dini sahihi ya Uislamu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{لا ينهاكم اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ}

Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.

Huruma hii haikuishia kwa Watu tu bali iliwajumuisha pia Wanyama na Ndege na viumbe wengine. Omar bin Abdul-Aziiz, Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu, alimwandikia Mfanyakazi wake wa Misri akimuusia kuwahurumia ngamia, akasema: Hakika nimefikiwa na habari ya kwamba Misri kuna ngamia wabeba mizigo, na kwamba ngamia hubebshwa mizigo mizito mno ya ratili elfu moja, ukifikiwa na ujumbe wangu huu, basi sitaki kujua kuwa ngamia wanabebeshwa zaidi ya kiwango cha mzigo wa ratili mia sita. Vile vile aliusia kuwahurumia ngamia bila kulipuuzia jambo hili, wala wasipigwe pigwe. Na alijifunza jambo hili kutoka kwa Mtume S.A.W, pale alipomuusia mwenye ngamia kwa kusema: Je huwezi kumcha Mwenyezi Mungu na kumuogopa kwa ajili ya ngamia huyu ambaye umeruzukiwa naye? Hakika ngamia huyu amenilalamikia ya kwamba wewe unamnyima chakula na unamtesa.

Ninaisema Kauli yangu hii na ninamwomba msamaha Mwenyezi Mungu na kukuombeeni nyinyi.

* * *

     Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye pekee asiye na mshirika yoyote. Na ninashuhudia ya kuwa Bwana wetu Muhammad na Mtume wetu, ni Mja na Mjumbe wake. Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu, mswalie na umrehemu na umbariki yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake wote.

Ndugu zangu Waislamu:

Hakika sifa za kipekee walizokuwa nazo Taabiina, ni Usamehevu kwa kwatu wote. Na kuwa wapole kwao. Walikuwa ni watu wenye usamehevu wa ali ya juu sana na ulaini pia katika kuishi na watu. Kutoka kwa Qataadah, amesema: Tuliingia kwa Hasanul Basriy, hali ya kuwa akiwa amelala, na kichwani kwake kuna kikapu, tukakivuta kikapu kile, tukakuta kuna mkate na tunda, na tukawa tunakula. Kasha yeye akazinduka, na akatuona, na akafurahishwa na kitendo kile, akatabasamu hali ya kuwa anaisoma kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {أَوْ صَدِيقِكُمْ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ}

Au rafiki yenu basi hapana ubaya wowote juu yenu…

            Na kutoka kwa Jurair bin Haazim R.A, amesema: Tulikuwa kwa Hasan, na ilikuwa katikati ya mchana, mwanae akasema: Mpumzisheni Sheikhe kwani hakika nyinyi mmemtaabisha mno, kwani yeye hajala wala hajanywa, akasema Hasan: Waache. Hakika mimi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu hakuna kitu kinachoyatuliza macho yangu kama kuwaona wao.

Na katika haya ndani yake kuna kujikana na kutambua uzito wa elimu na kuiheshimu na kubainisha cheo cha Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Nafsi za watu. Na huwenda likawa hilo ni somo kwa mwenyekujitanguliza kwa watu ili aizungumzie Dini ya Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na Elimu nayo, akapotoka na akawapotosha watu. Anasema Mtume S.A.W: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu haondoshi Elimu kwa kuiondosha kwa Waja wake, bali huindosha Elimu kwa kuwaondosha Wanachuoni, mpaka asibakie hata mwanachuoni mmoja, na hapo watu wakawafanya wajinga kuwa viongozi wao, wakaulizwa na wkatoa fatwa bila ya kuwa na Elimu, wakapotea na wakawapoteza watu.

Hakika Tabiina walikuwa Ruwaza njema kwa waliokuja baada yao miongoni mwa Maimamu. Tunaona kwamba Imamu Malik bin Anas R.A – naye ni miongoni mwa waliowafuatia Taabiina – anaombwa na Abu Jaafarl Mansour Mwenyezi Mungu amrehemu, akisambaze kitabu chake cha Muwatwau katika Miji mbali mbali ya Kiislamu, akisema: Mimi nimekusudia kuamrisha vitabu vyako hivi ulivyoviandika – kwa maana ya Muwatwau –  vichapishwe kwa wingi kasha nipeleke  chapa moja moja  katika kila mji miongoni mwa miji yote ya Waislamu, niwaamrishe wayafanyie kazi yaliyomo ndani yake, na wasikikwepe na kuelekea katika kingine na wakalingania kinyume na hayo kwa elimu hii iliyozuka. Kwani hakika mimi nimeliona Chimbuko la Elimu hii ni Mapokezi ya watu wa Madina n Elimu yao. Akasema Imamu Malik: Ewe Amiri wa Waumini, usifanye hivyo. Hakika watu wametanguliwa na maneno mengi, na wamesikia Hadithi nyingi, na wamepokea Riwaya nyingi, na kila watu wamechukua kutoka kwao kwa yale yaliyowafikia hapo kabla, na wakayafanyia kazi, na wakayajongelea kwayo kutokana na hitilafu za watu na wengine wao, na hakika kuwarudi kwa yale waliyokwishayaamini ni kuwalazimisha, kwa hivyo waache watu na hali zao walizo nazo, na walichokichagua watu wa kila mji miongoni mwao kwa ajili yao. Akasema: hakika ninaapa, kama ungeliniunga mkono katika jambo hili basi ningeliamrisha litekelezwe.

Na katika unyenyekevu wenye ukarimu na ufahamu mkubwa na Elimu ya Fiqhi, ni tukio la Imamu Shafi aliposigana na Mwanafunzi wake Yunus bin Abdul Aalaa, na akasimama hai ya kuwa na hasira, na ulipofika Usiku, Yunus akasikia mtu anagonga mlango wa nyumba yake, akasema: ni nani aliye mlangoni? Akasema: Muhammad bin Idris, Yunus akasema: nikawa ninafikiria kila mtu anayeitwa kwa jina hilo la Muhammad Idris nikakuta ni Imamu Shafi peke yake, akasema: Na nipoufungua Mlango nikakutana nae uso kwa uso akasema: Ewe Yunus, mamia ya masuala yanatukutanisha pamoja na suala moja linatutenganisha?! Ewe Yunus, usijaribu kushinda katika hitilafu zetu zote, kwani baadhi ya nyakati kujipatia ushindi wa nyoyo ni bora kuliko kujipatia ushindi wa Mambo mbali mbali, Ewe Yunus, usiyabomoe madaraja uliyokwishayajenga na kuyavuka, kwani huwenda siku moja ukayahitaji kwa ajili ya kaurejea, daima lichukie kosa lakini usimchukie mkosa, na uyachukie maasi kwa moyo wako wote, lakini msamehe na umhurumie Mtu aliyemwasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, Ewe Yunus, ikosoe kauli ya mtu, lkini muheshimu msemaji, kwani jukumu letu sisi ni kuyaangamiza maradhi na sio mgonjwa.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu Imamu Shafi kwa kauli yake hii:

Ninawapenda Wema nami si katika wao

huwenda nikaupata uombezi wao

Na ninamchukia ambaye biashara yake ni maasi

Hata kama bidhaa zetu zinalingana.

Na Wanachuoni wetu watukufu wakaufuata Mwenendo huo huo na wakawa Ruwaza njema kwetu sisi katika kuibeba Amana ya Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ya Uislamu na kuielewa kwa mweleweko sahihi, na kujipamba na Tabia zake pamoja na uzuri wa kuufikisha kwa Watu, kwa hekima na Mawaidha Mazuri.

Ewe Mola wetu tujaalie tuwe miongoni mwa wenye kuisikia Kauli na wakaifuata iliyo bora zaidi, haowee ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaongoa na haowee ndio wenye kuzingatia.