- أوقاف أونلاين - https://foreign.awkafonline.com -

Umuhimu wa juhudi za pamoja

أ.د/ محمد مختار جمعة وزير الأوقاف

D / Mukhtar Mohamed Juma Waziri wa Awqaf

Jamii yetu imeingiliwa na fatwa ngeni pamoja na rai zisizo sahihi na baadhi ya wenye husuda na wasio na ujuzi na wenye nafsi dhaifu ambao wanawaingilia maulamaa, kwa madhumuni ya kupata umaarufu, vyeo na kutaka kuonekana tu, wakazitumia rai zote zisizo sahihi na zilizo ngeni ili wapate kuonekanwa na kwa ajili ya masilahi yao pamoja na makundi yao.

Na kwa kutokana na wingi wa kadhia pamoja na matukio mapya yanayojiri na kugawanyika kwake na vuguvugu lake pamoja na kutowafikiana kwa baadhi yake katika rai za wanazuoni na wasomi waliotangulia ambao wao walitoa fatwa kwa mujibu wa zama zao na wakati wao pamoja na sehemu zao. Ukizidisha na ujinga wa wasio wasomi wa fani hiyo ambao hawana ujuzi wa kuchambua na kufanya uhakiki, pia kuacha kutendea baadhi ya hukumu bila ya vigezo, na hii ni kwa sababu ya ujinga wa tukio pia ujinga wa kutofahamu sharti za vipimo sahihi. Kwa sababu hizi ndio imepelekea kuwepo kwa ulazima wa upatikanaji wa juhudi za pamoja.

Kwa ajili hiyo. Huu ukawa ndio wito wa Imamu Mkuu Prof. Ahmed Twayyib, kiongozi wa Al Azhar Shariyf, katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano wa Kikao kikuu cha masuala ya Waisilamu, uliofanyika katika mji wa Luxur, wenye anuani: “Mtazamo wa viongozi na maulamaa katika kurekebisha hotuba za dini, na kutengua fikira zisizo sahihi,” na kuwepo juhudi ya pamoja ambayo itawaita wasomi wakubwa katika nchi tafauti ulimwenguni, na kwa kila mwenye kuwa na hisia juu ya umma na matatizo yake, ili wapinge kwa ushujaa wao wote masuala yaliyopo kwa mfano; ugaidi, ufahamu wa hukumu juu ya pahala pa  kiisilamu, kujiunga na makundi ya kigaidi yenye kutumia silaha, kuacha kuwa pamoja na wanajamii na kuwachukia, kuhalalisha damu za raia wasio na hatia kwa kuwaua au kwa kuwaripua, au kila chenye kuhusika na haki za kibinadamu na uhuru, na kila lenye kuhusika katika masuala ya kijamii kwa mfano, suala lenye kupewa kipaumbele ni masuala ya mwanamke, kuanza kujua mwezi upi wa kiarabu ndio unaotangulia kwa kupitia makadirio ya falaki, masuala ya Hijja na hasa katika kuanza kuhirimia Jiddah kwa wale waendao (kuhiji) kwa kupitia vyombo vya anga au kwa vyombo vya bahari, pia kulenga mawe katika nyakati zote nyengine , na masuala mengineyo ambayo yanashikana na haki za nchi, na yanashikana na wakati na pia mahitajio ya watu.

Na ili umma uinuke inapasa kutoa fat-wa zenye kuwezekana kutendeka na zenye kuharamisha kujibweteka na  uvivu, na hii ni kwa masharti isije ikatolewa fat-wa yenye kuhitaji mazingatio ya kina kwa kuitolea fat-wa iliyokuja kwa ujumla na kwa maelezo ya ujumla ambayo hayaendani na uhalisi uliopo na ambazo pia hazitaweza kutoa jibu juu ya masuala au hata kubadilisha kilichopo.

Na bila shaka juhudi za pamoja zitasaidia sehemu kubwa na zitaweka wazi sana ili kufuta rai zisizo sahihi, na kwa ajili ya kuondosha sababu za uasi, Kikao kikuu cha masuala ya Waisilamu katika mkutano wake wa mwisho kimezungumzia mambo muhimu, nayo ni:-

  1. Kufunga, kuzuia, na kuacha kufuata bila ya mwelekeo, na kuweka wazi ufahamu wa kuyafasiri maelezo kama yalivyo katika asili yake na kujiepusha na uelewa wa matukio ambayo matokeo ya fat-wa yake hayatafanana na tukio, na kutofahamu misingi ya sheria kiujumla (pasi na kujua asili yake), pia kuwapa nafasi wasio na elimu katika kueneza ulinganio.
  2. Baadhi ya watu kuitumia dini kama biashara, na kuitumia kwa malengo ya kisiasa na kwa vikundi vya vyama, pia kwa kujipatia faida katika vikundi na miasasa yao kwa jina la dini na taifa, na kujifanya watendaji wa dini lakini kwa mtazamo wa nje na wa kisiasa badala ya kuitendea dini kwa ajili yake Mwenyezi Mungu pekee.
  3. Kufanikiwa kwa baadhi ya watawala katika kuwatumia vibaraka wao katika nchi nyingi za kiarabu na za kiisilamu, sawa kama ni kwa ajili ya kubadilishana masilahi, au kupewa ahadi za uongo kwa baadhi ya makundi, au kwa njia ya kununuliwa na kuwa kama watumishi.

Ikifanyika juhudi ya pamoja basi itapelekea kufikia lengo kubwa hasa katika upande wa kuwepo pamoja kwa wasomi, na sababu nyingi za mtengamano zitaondoka, na hii itapelekea, bila shaka, umma kuwa kitu kimoja, na hasa hasa katika kupambana na fikira zisizo sahihi, za uasi na zenye kupotosha.