- أوقاف أونلاين - https://foreign.awkafonline.com -

Haki ya mwanamke katika kurithi na maisha mazuri

Mokhtar-300x198

Kadhia ya urithi ni moja kati ya kadhia kubwa sana amabazo mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) ameisisitiza katika hotuba yake ya kuagana aliposema: “hakika Mwenyezi mungu amempa kila mweye haki amempa haki yake, tambueni kuwa hakuna wasia kwa anaerithi.” (Ibn Majah). Naye Mwenyezi Mungu ameweka wazi mafungu ya wanaorithi na suala hili hakumuachia yeyote katika viumbe vyake, akasema {11. Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu:Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alichokiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alichokiacha, ikiwa anaye  mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi  hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Munguni Mjuzi na Mwenye hikima.}.

Na haikuishia hapo kutaja mafungu tu, lakini pia kurani tukufu imetaja na adhabu kali mno kwa kila atakaefanya dhuluma katika haki hizi, akasema Mwenyezi Mungu mtukufu, {13. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

  1. Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.}. Na ikawakemea watu majahili kwa kule kula kwao mali za baadhi ya warithi bila ya haki, akasema {Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, 18. Wala hamhimizani kulisha masikini; 19. Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, 20. Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. 21. Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, 22. Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, 23. Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? 24. Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! 26. Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. 25. Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.}. Na mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “mwenye kukata mirathi ambayo mwenyezi Mungu na Mtume wake wamefaradhisha, basi Mwenyezi Mungu atamkatia urithi wake peponi.”

Na inasimuliwa kuwa kuna mtu alimnyima mtoto wake wa kike mirathi, akangoja hadi muda wa kufariki (kwa mzazi wake) na kukutana na Mola wake, alipoingizwa sehemu ya kuoshwa (naye mtoto wa kike) akaingia, akawa anamwangalia na kusema: “ewe Mola wangu hakika unaelewa kuwa ameninyima baadhi ya neema za dunia name nakuomba umnyime neema za akhera.”

Kasha kitendo cha kuwanyima wanawake urithi huenda ikawa kinasababishwa na tabia ovu au tamaduni na mila zilizopitwa na wakati ambazo hazina asili yoyote katika sheria, na kama kwamba Yule anayemnyima mwengine na kumpa mwengine anadhani ya kuwa amefanya jambo la masilahi kwa anayestahiki na kwa siye stahiki kwa Mola wa viumbe vyote, muumbaji wa kila kitu na Mbora wa mahakimu, na kama kwamba (anayegawa mirathi kwa dhuluma) anasema ndani ya moyo wake: “mgao wa Mwenyezi Mungu haunipendezi” au “mimi nitagawa vizuri zaidi kuliko hata Mwenyezi Mungu” –Mungu atuepushe mbali- kwani angelikuwa ni muumini wa kweli na kuamini kuwa mgao wa mwenyezi Mungu ni bora na wa haki basi mtu huyu asingelifadhilisha mwengine na kumuacha mwengine.

Ama kuhusu mwanamke kwa ujumla sawa awe ni dada,mke, mtoto wa kike au yeyote, ieleweke kuwa dini yetu imekataza kuwadhulumu na kupunja haki zao, bali ikasema kuwa uadilifu kwao na kwa watoto wa kiume ni njia nzuri ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kupata pepo yake, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema: “Yeyote atakaekuwa na mwanamke na akawa hajamzika akiwa haina wla hakumdhulumu ْna wala mzazi wake hakumpendelea zaidi ya mwengine (kamfanyia usawa) basi Mwenyezi Mungu atamuingiza peponi.” Na katika hadithi hii kuna maana kubwa na ufasaha wa hali ya juu kabisa kwani mtume amesema “yeyote” ambayo inamaanisha mjumuiko na pia akasema “mwanamke” na wala hakusema  “mtoto wa kike” kwa sababu mwanamke inakusanya jinsia ya kike sawa awe mtoto, dada,mtoto wa kike  n.k.

Na mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) ameusia kuwakirimu na kuwatendea wema wanawake katika nyanya zote, kwani katika hadithi kudisiy ambayo imepokewa na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) kutoka kwa Mola mtukufu anasema: “Niridhisheni kupitia madhaifu wawili, mwanamke na yatima.” Na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake anasema: “mwenye kuwa na watoto wa kike watatu, akawa na subira kwao, akawalisha, na kuwavisha kwa kipato chake, basi hao watakuwa kwake ni kinga ya moto siku ya kiama.” Na katika mapokezi mengine, mwenye kuwa na watoto wakike wawili au ndugu wa kike wawili. Na katika mapokezi mengine pia inasisitiza hata kama atakuwa na mtoto wa kike mmoja tu akamfundisha na kumpa malezi mema atakuwa kwake ni kinga ya moto siku ya kiama. Na alipokuwa mzee mmoja amekaa pamoja na mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akaja mtoto wake wa kiume,akamchukua na kumbusu na kumuweka mapajani mwake, kasha baadae akaja mtoto wake wa kike akamchukua na kumuweka ubavuni mwake, mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ unaonaje lau kama ungeliwafanyia uadilifu”. Hapa anakusudia kama ulivyomuweka mtoto wa kiume mapajani ilibidi pia ufanye hivyo hivyo kwa mtoto wa kike kwa kumuweka kwenye paja jengine.

Ingawa kwa wakati tulionao tunaona aina tafauti za utenganishaji usiohitajika, ndani ya nyumba moja ya familia kwa baadhi ya watu, mtoto wa kiume huwa ni bora kuliko  wa kike, na katika sekta ya elimu hushughulikiwa zaidi wavulana kuliko wasichana, kwenye mirathi –ambayo tunatoa tolea lake- ima atakuwa hapewi kabisa au atapewa lakini kwa kuridhisha tu (na si kama haki yake), nalo ni jambo lisilokubalika hata kidogo hiyo ni aina ya kumkandamiza na kutumia mabavu au unyanyasaji. Ita utakavyo isipokuwa kinachohitajika ni mirathi ya haki kwa ajili ya kumfuata sheria ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu na kwa ugawaji kama ambavyo sheria, haki, uadilifu inavyotaka.