Adabu na Haki za Misingi za Jamii na athari zake katika upevukaji wa Jamii na Ujenzi wa Ustaarabu

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote. Ambaye anasema katika kitabu chake Kitukufu:

     {قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ}

Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

Na ninashuhudia kuwa hakuna Mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Yeye Pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad ni Mja na Mjumbe wake. Anasema Mtume wetu Muhammad S.A.W: Mwenyezi Mungu Mtukufu amenifunza adabu na akanifundisha vizuri.

Ewe Mola wetu, mswalie, mrehemu na umbariki Mtume wetu, na Jamaa zake na Maswahaba wake wote na kila mwenye kuwafuata kwa Wema mpaka siku ya Malipo.

Na baada ya utangulizi huu:

Hakika Uislamu umekuja kwa mfumo uliokamilika, unaopandilia uhusiano wa mwanadamu na Mola wake, na uhusiano wa watu, na uhusiano wa Ulimwengu mzima. Na Sheria ya Kiislamu imejaa taratibu na Adabu Kuu ambazo zinachangia katika kukuza Jamii na kuifanya isonge mbele kimaendelea na kuiletea maisha bora. Na miongoni mwa Adabu hizo ni: Adabu ya kuomba idhini, ambapo Uislamu umeiweka adabu hii ya kuomba idhini, na kuifanya kuwa ni katika adabu za Uislamu ambazo zinawapa watu mazingira ya kujitenganisha na wengine, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتاً غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّى تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَى أَهْلِهَا ذلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ}

Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka.

Na Mtume S.A.W ametufundisha sisi jinsi ya kuomba idhini, na kwa ajili hiyo mtu anapaswa kuanza kutoa salamu, kisha kutaja jina lake. Mtu mmoja aliomba idhini kwa Mtume S.A.W akiwa nyumbani kwake, akasema: Je ninaweza kuingia? Mtume S,A.W akamwambia mtumishi wake: Mtokee mtu huyu, na umfundishe jinsi ya kuomba idhini ya kuingia, na umwambie: Sema: Asalaamu alaikum, je niingie? Yule Mtu akamsikia na akasema: Assalaamu Alaikum. Je niingie? Na Mtume S.A.W akamwidhinisha aingie, na akaingia. Na kutoka kwa Jabir R.A, Anasema: Nilienda kwa Mtume S.A.W, na nikaugonga mlango wake, akasema: Ni nani huyu? Nikasema: Ni mimi. Akasema: Mimi mimi! Kama vile aliyachukia maneno haya.

Na miongoni mwa adabu za kuomba idhini ni kuinamisha macho, na kutouelekea mlango. Anasema Mtume S.A.W: Hakika mambo yalivyo, kuomba idhini kumewekwa kwa sababu ya macho. Na kutoka kwa Saadu bin Ubaadah R.A, anasema: Kwamba yeye aliomba idhini ya kuingi huku akiwa ameuelekea mlango, na Mtume S.A.W akamwambia: Usiombe idhini ya kuingia na wewe ukiwa umeuelekea mlango. Na imepokelewa kwamba Mtume S.A.W alikuwa pindi anapoiendea nyumba yoyote na akafika mlangoni akitaka kuomba idhini ya kuingia hakuuelekea mlango, alikuwa anaujia mlango upande wa kulia au kushoto, na anapopewa idhini ya kuingia huingia, na kama hakupewa idhini basi huondoka.

Na miongo mwa adabu kuu ambazo Uislamu umezilingania: ni adabu ya jinsi ya kuwa njiani na katika maeneo ya umma. Uislamu umeipa haki barabara ambayo lazima itekelezwe. Anasema Mtume S.A.W: Tahadharini na kukaa njiani. Wakasema Maswahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tunalazimika kuwa katika vikao vyetu vya njiani. Tunazungumza ndani yake. Mtume S.A.W akasema: Mtakapokuja katika vikao vyenu vya njiani, basi ipeni njia haki yake. Wakasema: Ni ipi hiyo haki ya njia? Akasema Mtume S.A.W: kuinamisha macho, na kuondosha kila kinacholeta maudhi, kuitikia salamu, na kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Na anasema Mtume S.A.W:  Imani ina sehemu sabini na kitu – au sitini na kitu – na sehemu iliyo bora kuliko zote ni kusema Hapana Mola mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nay a chini yake ni kuondosha maudhi njiani. Na haya ni sehemu ya Imani.

Kwa hiyo mtu anayeitumia njia au sehemu yoyote ya umma, anapaswa kutonyanyua sauti yake, au kuzungumza kwa sauti ya juu yenye kusumbua, na kutocheka kwa sauti yenye kukiuka maadili, na kutotupa uchafu hovyo njiani bali kuuweka uchafu huo katika sehemu husika, bali ni wajibu kuuondosha uchafu njiani, kama ambavyo ni lazima kutozorotesha njia, na kuwaudhi wapitao kwa kuwakodolea macho au kuwanyanyasa kwa maneno au hata kwa vitendo.

Na miongoni mwa adabu, ni adamu ya Usafi. Uislamu unauzingatia usafi kamili wa mwili, nguo na eneo kama ni kitu kisichotenganishwa na shria, kwa namna inayoendana na umuhimu wake kama mwenendo wa kibinadamu, na thamani ya kistaarabu; na kwa hivyo, Uislamu umetuasa tufuate na kutekeleza mjumuiko wa adabu mbali mbali zinazomfanya mwanadamu awe na mwonekano mzuri, watu hawachukizwi naye. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu waumini wenye kupupia usafi wa miili yao, na kujisafisha kwa nje na ndani yao, akasema:

 {إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}

Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojisafisha.

Na Mtume S.A.W anasema: Hakika Mwenyezi Mungu anaupenda uzuri, naye ni msafi anaupenda usafi…

Na anasema Mtume S.A.W: Usafi ni sehemu ya Imani… Na mtume S.A.W alimwona mtu mmoja akiwa amejawa na vumbi – nywele zake zimetawanyika – akasema Mtume S.A.W: Je Mtu huyu hakupata kitu cha kuziweka sawa nywele zake? Na amlimwona mtu mwingine aliyevaa nguo chafu, akasema S.A.W: je mtu huyu hajapata kitu cha kusafishia nguo zake?

Mtume S.A.W ametuasa pia juu ya usafi wa meno, na amefanya hivyo kwa sababu ya kupupia usafi na uzuri wa harufu yam domo, na kutowaudhi watu kwa harufu mbaya yenye kukera ambayo inaweza kuwafanya watu wamkimbie. Anasema Mtume S.A.W: Kama nisingeuhofia Umma wangu – au watu wote – basi ningewaamrisha kupiga mswaki katika kila swala.

Na miongoni mwa adabu za Uislamu, ni adabu ya Mazungumzo. Mazungumzo ni katika njia za kutambuana na kurekebisha makosa. Na Uislamu umeufungua mlango wa mazungumzo baina ya watu wote; mpaka kufikia uongofu wa ukweli, bila ya uzito wowote au vikwazo. Lakini mazungumzo yanapaswa yawe mbali na kuwasema vibaya watu wengine, au kuwadharau au hata kuwadhalilisha. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ}

Na ujadiliane nao kwa njia iliyo bora.

Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَقُلْ لِعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ..}

Na Waambie waja wangu waseme maneno mazuri…

Na anasema Mtume S.A.W: Muislamu sio wa kuwasema wengine vibaya, au kuwalaani au kutoa kauli chafu au maneno ya kukera.

Kwa hivyo, mazungumzo yanatakiwa yawe mazuri yenye kufuata misingi ya elimu na kutotoka nje ya lengo kuu pamoja na kuchunga mazingira. Na katika misingi hiyo ya kielimu ni kuwa na uhakika na maelezo yanayotolewa pamoja na kutoharakisha katika kunukulu.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ}

Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenyekujuta kwa mliyoyatenda.

Na anasema Mtume S.A.W: kufanya mambo kwa utulivu kunatokana na Mwenyezi Mungu, na kufanya mambo kwa haraka haraka kunatokana na Shetani.

Na anasema Mtume S.A.W:  Kufanya mambo kwa utulivu kunatakiwa katika kila jambo isipokuwa kazi ya Akhera tu.

Na anasema Mtume S.A.W: Inamtosha Mtu kuwa mwongo kwa kukizungumzia kila anachokisikia. Na miongoni mwa adabu za mazungumzo:  ni kutokariri mara kwa mara vumi au kuzizungumzia kwa kina; kwani mwenye kufanya hivyo anachangia kuzitangaza na kuzisambaza. Vumi huvuma na kuenea zaidi zinapopata ndimi za kuzikariri na msikio ya kuzisikiliza na nafsi zinazozikubali na kuzipitisha.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُمْ مَا لَيْسَ لَكُمْ بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِنْدَ اللَّهِ عَظِيمٌ}

Mlipo yapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.

Na anasema Mtume S.A.W: Mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, asimuudhi jirani yake, na mtu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake amkirimu Mgeni wake, na mtu Mwenyekumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na aseme maneno mazuri au anyamaze.

Na katika adabu kuu zilizokuja katika Uislamu: ni kupunguza sauti; na maana yake ni mtu kutoinyanyua sauti yake kuliko kiwango kilichozoeleka na hasa katika uwepo wa aliye juu yake kihadhi. Na Katika Qurani Tukufu kuna wasia wa Luqman kwa mwanae ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ إِنَّ أَنْكَرَ الْأَصْواتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ﴾ [لقمان: 19].

Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.

Na Mwenyezi Mungu amewasifu wale wanaopunguza sauti zao na hasa katika uwepo wa Mtume S.A.W.

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ أُولَئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَى لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ﴾ [الحجرات: 3].

Kwa hakika wanao teremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.

Na miongoni mwa adabu: ni kumwongoza aliyepotea na kumrejesha katika njia iliyo sawa, kwa kumwelekeza.

Anasema Mtume S.A.W:  Tahadharini na ukaaji wa njiani. Wakasema Maswahaba; sisi hatuna budi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa katika vikao vyetu tunazungumza kwenye vikao hivyo. Akasema: Na mtakapovijia vikao vyenu basi ipeni njia haki yake. Wakasema: Ni ipi haki hiyo ya njia? Akasema: ni kuinamisha macho, kuondosha maudhi, kujibu salamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya, na kumwongoza aliyepotea.

Ninasema kauli yangu hii na ninamwomba Msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili yangu na kwa ajili yenu

*        *        *

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa viumbe vyote. Na ninashuhudia kuwa hakuna mungu mwingine anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye peke yake na hana mshirika wake, na ninshuhudia kuwa Bwana wetu na Mtume wetu Muhammad S.A.W, ni Mja wake na ni Mjumbe wake. Ewe Mola wangu swalie, mpe rehma na umbariki yeye, na jamaa zake na maswahaba wake wote.

Ndugu zangu waislamu: kuna adabu kuu zingine zenye umuhimu mkubwa ambazo hapana budi tujipambe nazo kama waislamu. Miongoni mwazo ni: Kumsaidia mwenye matatizo: Uislamu umeijaalia adabu hii kama ni moja ya matendo mema mno yanayomkurubisha mja kwa Mola wake. Kutoka kwa Abu Dhari R.A: kwamba Mtume S.A.W anasema: Haina nafsi ya mwanadamu isipokuwa wajibu wa kutoa sadaka kila siku inayochomozewa na jua. Ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tutapata wapi sadaka hiyo tutakayoitoa? Akasema: Hakika milango ya kheri ni mingi: Kumsabihi Mwenyezi Mungu, na kutoa takbiira na kusema laailaaha illa laahu, na kuamrisha mema na kukataza mabaya, na kuondosha maudhi njiani, na kumsikilizia kiziwi, na kumwongoza kipofu na kumwelekeza mwenye kutaka kuelekezwa haja yake na kuhangaika kwa nguvu zote iwezekanavyo kwa kuichosha mikono yako kwa ajili ya kumsaidia mnyonge, yote haya ni sadaka kutoka katika nafsi yako na kwa ajili ya nafsi yako. Sahiihu bnu Habbaan.

Na miongoni mwa sadaka nyingine:  ni kuwasaidia wanyonge na wenye mahitaji maalumu kwa ajili ya kuleta mlingano katika maisha yetu, kwa ushahidi wa kauli ya Imamu Ali R.A: “Mwenyezi Mungu amefaradhisha katika mali za matajiri vyakula vya mafukara isipokuwa panapokuwapo uchoyo wa tajiri na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawauliza Matajiri kwa hili”. Na malezi haya yanahesabika kama nyongeza kubwa ya pato la kitaifa kwamba kuwalea watu ni haki na wajibu wa jamii. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu yukaribu na mwenyekuvunjika moyo wake, ni Mpole anayewahurumia waja wake. Hadharau chochote katika wema hata kama ni neno zuri; anasema Mtume S.A.W: Usidharau chochote katika wema, hata kama unakutana na nduguyo na uso mkunjufu.

Na anasema Mtume S.A.W: na hakika nyinyi mna nusuriwa na kupewa riziki kwa ajili ya walio wanyonge katika nyinyi! Na Mwenyezi Mungu humsaidia Mja anayeendelea kumsaidia nduguye.

Na katika adabu: ni kumuheshimu mkubwa na kumnyenyekea pamoja na kuwa mpole kwake na kutomnyanyulia maneno, na kwa hiyo uchungwe utu uzima wake na utangu wake katika Uislamu, na hadhi yake itambulike pamoja na nafasi yake. Na mkubwa pia anaamrishwa kuwaonea huruma wadogo na kuwa mpole na laini kwao. Anasema Mtume S.A.W: Hakuna Mwislamu yoyote anayemkirimu mwenye mvi isipokuwa Mwenyezi Mungu atamlipa yeye kwa kumpa mtu atakayemkirimu katika umri wake wa uzeeni.

Na huu ni katika mwonekano wa utukufu wa Uislamu, rehma na usamehevu wake, uadilifu na utoaji wa haki pamoja na ari ya kumkirimu mwanadamu. Na Mtume S.A.W ametufundisha tuwe na adabu kwa Mwenye mvi, mwenyekuhifadhi Qurani Tukufu, Kiongozi Mwadilifu, kama ni sura miongoni mwa sura za kumtukuza Mwenyezi Mungu aliyetukuka, ambapo anasema S.A.W: Hakika katika kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumkirimu mwenye mvi aliye mwislamu, na Mwenyekuihifadhi Qurani Tukufu asiyejikweza au kutoijali, na kumheshimu kiongozi mwadilifu. Anasema Mtume S.A.W: Sio katika sisi mtu asiyemhurumia mdogo kati yetu, na anayemdharau mkubwa kati yetu. Na akaamrisha mema na akakataza mabaya.

Hakika uelewa mzuri wa Usamehevu wa Uislamu haushurutishi mwenye mvi awe mwislamu. Imepokelewa kuwa Mtume S.A.W alitoa sadaka yake kwa watu wa nyumba ya myahudu, kwani jambo hili linafanyika kwao. Na huyu hapa Bwana wetu Omar bin Abdul Aziiz R.A: anamwandikia mfanya kazi wake huko Basra akisema: angalia katika watu wa Dhima yule aliyezeeka, nguvu zimemwishia, na hawezi tena kuzalisha mali, basi mtolee kutoka katika Nyumba ya Mali ya Waislamu kiasi kinachomsaidia.

     Na miongoni mwa haki za Jamii kwa watoto wake kuchunga masilahi makuu ya nchi, hata kama tutachukua mfano wa suala la ongezeko la wakazi, hakika sisi tunathibitisha kuwa kuna mambo mawili. La kwanza: Kwamba baadhi ya watu wanajiangalia wao wenyewe ikiwa wanao uwezo na ni matajiri, na uwezo sio tu uwezo wa kifedha, bali ni uwezo wa kifedha nakimalezi, na kila kinachojumuisha kila upande wa matunzo na malezi, na wala sio uwezo wa mtu tu, isipokuwa ni jambo linalopindukia nyenzo za mtu mmoja mmoja na kuelekea katika nyenzo za mataifa katika kutoka huduma bora ambazo mtu peke yake hawezi kuzitoa huduma hizo, na kuanzia hapo, hali na nyenzo za mataifa ni moja ya sababu muhimu ambazo lazima ziwekwe katika zingatio kwenye kila upande wa mchakato wa idadi ya wakazi

Mtu anaeishi kwa ajili ya ke binafsi hakustahili kuzaliwa. Kwa hiyo ongezeko la wakazi lisilodhibitika halioneshi athari yake kwa mtu mmoja mmoja au kwa familia tu, bali bali linajenga madhara makubwa mno kwa nchi zisizofuata njia za kielimu katika kutibu masuala ya wakazi na kwamba upana na ufinyu katika Suala hili havipimwi kwa vipimo vya mtu mmoja mmoja katika kujitenga na hali za Mataifa na nyenzo zake kuu.

Pili: Kwamba uchache wenye nguvu ni bora kuliko wingi ulio mnyonge na dhalili ambao ameuzungumzia Mtume S.A.W kwamba ni wingi unaofafa na wa sungusungu, kwani hali za aina yake ambazo baadhi ya Mataifa yanazipitia katika mazingira yasiyoziwezesha kujipatia nyenzo za kimsingi katika afya, elimu na miundo mbinu katika hali ya uwingi unaodhibitika, na kwa namna inayopelekea kuwa wingi huo ni sawa na uwingi wa sungusungu. Hakika mtu yoyote mwenye akili anatambua kwamba panapotokea ukinzani baina ya Ubora na uwingi basi hakika zingatio la kweli huwa katika ubora na wala sio uwingi na hapo ndipo uchache wenye nguvu unapokuwa bora mara elfu moja kuliko uwingi wenye unyonge na Udhaifu.

Na hii ni kwa kuwa wingi unarithisha unyonge, au ujinga au ukengeukaji wa gurudumu la ustaarabu, na ambako huwa ni upuuzi mzito ambao hauhimiliki au hauyafikii matakwa ya vyanzo vya dola na nyenzo zake, huo ni wingi aliousifu Mtume wetu S.A.W, kama wingi unaofanana na wingi wa sungusungu ambao hauna faida yoyote bali ni uwingi unaodhuru na wala haunufaishi.

Ewe Mola wetu tuongoe tuwe na tabia njema zaidi, kwani hakuna wa kutuongoza katika tabia njema zaidi isipokuwa Wewe, na utuondoshee kila baya, kwani hakuna wa kuondosha mabaya isipokuwa Wewe, na utujaalie tuwe katika waja wako wenye nia safi.